Kona ya Urembo.

JE WAJUA JINSI YA KUONDOA CHUNUSI/MAPELE KWA NJIA YA ASILI BILA KEMIKALI?

Monday, October 31, 2016 naomimwakanyamale 0 Comments

Chunusi  hutokea pale oil glands ambazo zipo chini ya ngozi zinaposhambuliwa na vijidudu viharibifu {bacteria} na kusababisha zivimbe na kutengeneza usaha. Mara nyingi chunusi hutokea, usoni, shingoni, mgongoni, mabegani na kwa wengine mpaka  kifuani.

*Zipo lotion, creams au dawa zakuondoa chunusi lakini kwa njia ya asili ni nzuri, rahisi na huondoa chunusi kwa haraka bila kuingiza kemikali mwilini.

* Hivi ni baadhi ya vitu unavyoweza kuvipata kwa urahisi na kuvitengeneza mwenyewe nyumbani kwako.



1. Limao

Limao lina Vitamini C kwa wingi, inaweza kuwa ni njia mojawapo ya  inayoweza kukausha chunusi kwa haraka.
Jinsi ya kutumia:-
*Chukua pamba iloweke au chomvya kwenye juisi ya limao kisha, paka moja kwa moja kwenye eneo lililo athirika kabla ya kulala.
*Chukua kijiko kimoja cha juisi ya limao, changanya na kijiko kimoja cha Cinnamon, kisha paka kwenye eneo lililo athirika, kwa usiku kucha.

2. Kitunguu Swaumu

Kitunguu Swaumu kina madini ya Salfa ambayo mbali na kusaidia kuponyesha chunusi,  pia husaidia kupambana na bakteria waharibifu mwilini. Jinsi ya kutumia:-
Menya kitunguu chako, kitwange mpaka kiwe laini kabisa, kisha weka kwenye eneo lililo athirika moja kwa moja kwa muda usiopungua dakika tano, kisha osha kwa maji vuguvugu. Waweza rudia kadiri upendavyo kwa siku.

Pia nivizuri kula punje moja ya kitunguu swaumu kwa siku, kwa ajili yakusafisha damu. Lakini usizidishe kwani vyaweza kukuchafua tumbo.

3. Tree tea oil.

Mafuta haya yanavirutubisho ambavyo vinauwezo wa kupambana na wadudu waharibifu wanao haribu ngozi kwa chunusi. Ni mazuri kwa kuondoa chunusi na makovu pia.Jinsi ya Kutumia:-
* Chomvya pamba yako kwenye mafuta haya, kisha paka kwenye eneo lililo athirika. Acha kwa muda wa dakika 15 mpaka 20, ndipo uoshe.
* Waweza kuchanganya matone machache ya Tree tea oil na kijiko kimoja cha chai cha Aloe Vera kisha pakaa kwenye chunusi. Acha kwa muda wa dakika 15 mpaka 20 ndipo uoshe.

4. Unga wa dengu
Unga wa dengu una uwezo mkubwa wakuvyonza mafuta au uchafu uliopo kwenye ngozi.
Jinsi ya Kutumia:-
Changanya unga wako wa dengu na maji au juisi ya limao, {Isiwe nzito sana}, kisha paka eneo lenye chunusi. Acha mpaka ikauke kabisa ndipo uoshe.
 

 

6. Barafu {Ice Cube}:-
Barafu inatumika kupunguza wekundu na uvimbe wa chunusi. Inasaidia kuongeza mzunguko wa damu katika eneo lile lililo athirika na kuondoa uchafu na mafuta yaliyojikusanya pale na kutengeneza chunusi.
Jinsi ya Kutumia:-
* Funga na kitambaa kipande chako cha barafu, waweza kukisagasaga pia ili kupata vipande vidogo vya barafu, kisha funga kwenye kitambaa laini, weka kwenye eneo lililo athirika kwa sekunde chache, kisha rudia tena na tena.

KARIBU UONGEZEE NJIA NYINGINE HAPO CHINI ZINAZOWEZA KUTUSAIDIA KUONDOA CHUNUSI.



0 comments: