Kona ya Urembo.

NJIA YA ASILI YA KUFANYA MENO YAKO KUWA MEUPE.

Thursday, November 03, 2016 naomimwakanyamale 0 Comments




Kabla ya kujua jinsi ya kufanya meno yako kuwa meupe, kwanza tujue sababu inayofanya meno kuwa ya njano. Zipo sababu nyingi zinazosababisha meno kuwa njano. Yaweza kuwa ni aina ya vyakula ulavyo, au vinywaji unywavyo mara kwa mara, au ni maumbile yako. Yaani jinsi ulivyo ubwa.

Hizi ni baadhi ya vitu vya asili, ambavyo waweza kujitengenezea nyumbani kwako kwa rahisi tu.

1. Baking Soda na Juisi ya limao au Maji:-


Changanya baking soda, na juisi ya limao au maji. Fanya

mchanganyiko huo kuwa mzito kama dawa ya mswaki ya kawaida. Kausha meno yako hata na kitaulo kisafi au paper towel.

Kisha weka mchanganyiko wako kwenye mswaki, kisha sugua meno yako.
Acha mchanganyiko wako kwenye meno kwa dakika moja, kisha osha. Kama unatumia limao, ni vema usizidishe dakika moja ili kuzuia acid iliyopo kwenye limao, kuharimu Enamel. Lakini kama mchanganyiko wako ni wa maji, basi waweza acha kwa muda wa dakika tatu, kisha suuza kinywa chako.

2. Strawberry 1-3, Chumvi{kiasi kidogo} na Baking Soda{1/2 kijiko cha chai}:-

Strawberry ina madini mengi ya Vitamini C, ambayo yanaweza kuondoa ule utando wa njano ulioganda kwenye meno.

Chukua Strawberry yako, isage, changanya na Chumvi kidogo na  Baking Soda. Kausha mate kwenye meno kwa kitaulo kisafi au paper towel, ili yasiwe na unyevunyevu.

Kisha weka mchanganyiko wako kwenye Mswaki, kisha sugua taratibu usiumize fizi, kisha uache  mchanganyiko huo kwenye meno kwa dakika 5, kisha suuza kinywa. Vizuri ufanye usiku baada ya kula, wakati wakwenda kulala.

3. Suuza kinywa kwa mafuta ya nazi {1 kiji cha chakula}:-

Hii unaweza usiikubali, lakini hata mimi niliposoma, ilibidi nifanyie utafiti kama kweli yawezekana. Lakini utafiti unaonyesha mafuta ya nazi yana Lauric acid ambayo inauwezo wakuua bacteria wabaya wanao sababisha meno yako kuwa ya njano na pia inasaidia kufanya fizi kuwa imara zaidi na kufanya kinywa kiwe na harufu nzuri zaidi.

Asubuhi kabla yakupiga mswaki, sukutua kinywa chako vizuri, na mafuta hayo ya nazi kwa dakika 10 mpaka 15, ukizungusha ndani ya meno yako, kisha suuza na maji ndipo upige mswaki.


JIWEKEE UTARATIBU WAKUDUMU WA KUNG'ARISHA MENO YAKO, NA HAKIKISHA UNAFUATILIA KWA MATOKEO MAZURI.



 *Waweza kuongeza njia nyingine ili wote tujifunze pamoja.*


0 comments: