JINSI YAKUONDOA {STRETCH MARKS} MWILINI.

Monday, November 07, 2016 naomimwakanyamale 0 Comments



*Strech marks ni michirizi au alama zinazojitokeza kiunoni, mapajani, kwenye makalio, kwenye matiti na mikononi. Na hii huwapata mara nyingi kina mama kipindi wapo wajawazito, pale mwili unapotanuka, mabadiliko ya homorne, au kipindi cha kupevuka nahata kipindi mtu anaponenepa. 
*Wakati mwingine  hutokana na madhara ya kunywa madawa ya aina fulani, au ukipaka mafuta, au krimu fulani kali kwenye ngozi, pia zinaweza changia uharibifu wa ngozi na kusababisha michirizi hiyo {Stretch marks}. Uzuri ni kuwa, huu si ugonjwa. Waweza kuondoa michirizi hiyo au kupunguza kwa asilimia kubwa muonekano wake.

Yapo mafuta au lotion ambazo zimeshatengeneza maalumu kwa ajili ya kuondoa stretch marks, 
Bio-oil



Au waweza kutengeneza wewe mwenyewe tiba ya asilia nyumbani kwa kutumia:-

 1. Aloe Vera:-
Aloe Vera ina uwezo mkubwa sana wa kutibu matatizo ya ngozi.
* Waweza paka Aloe Vera gel, kwenye sehemu iliyo athirika, na kuiacha hapo kwa dakika 15 kisha osha na maji ya vuguvugu.
*Njia nyingine, waweza changanya 
-Aloe Vera gel 1/4 cup, 
-Kamulia vidonge 10 vya mafuta ya 
   Vitamini E
-Na ongeza  na vidonge 5 vya Vitamini A




2. Lemon Juice:-
Njia nyingine rahisi ya kuondoa stretch marks ni kutumia juisi ya limao. Juisi ya limao ina acid ambayo inauwezo wa kuondoa au kupunguza kwa asilimia kubwa michirizi hiyo, na makovu mengine.
*Pakaa juisi hiyo katika eneo lililoathirika kwa circular motions. Acha juisi hiyo ikae kwa angalau dakika 10 kabla ya kusuuza na maji ya vuguvugu.
*Njia nyingine ni kuchanganya juisi ya tango na juisi limao kwa kiasi sawa{nusu kwa nusu}

, kisha pakaa na kusuuza baada ya dakika 15.


3. Sukari:-
 * Changanya Sukari nyeupe, na Almond oil, na juisi ya limao kidogo, kisha pakaa katika eneo lililo athirika kwa dakika kadhaa, kila siku kabla ya kuoga.
FANYA HIVYO KWA MUDA WA MWEZI MMOJA. UTAONA MATOKEO.


4. Cocoa Butter:-
CoCoa Butter ni nzuri sana kwa stretch Marks, pakaa eneo lililo athririka angalau mara mbili kwa siku.

NI SAWA NA HAYO-------}


5. Olive oil:-
Mafuta haya yana uwezo mkubwa sana wakutibu marathi mengi ya ngozi.
* Masaji taratibu eneo lililo athirika na mafuta ya "Extra Virgin Olive Oil". Hiyo itasaidia mzunguko wa damu katika eneo hilo na kuondoa stretch marks.
* Acha hapo kwa muda wa nusu saa kuruhusu madini ya Vitamini A, D, na E kupenya kwenye ngozi.


6. Maji:-
 Kunywa maji mengi yakutosha. hakikisha unakunywa angalau glasi 8 mpaka 10 kwa siku kulingana na mwili wako{Ukubwa/uzito}. Maji yakutosha mwilini, husaidia kufanya ngozi kuwa laini, hivyo kupunguza muonekano mkubwa wa michirizi hiyo.


JIPE MUDA WAKUTOSHA KATIKA MATIBABU HAYO. USIKATE TAMAA MAPEMA.

Karibu utuongezee njia nyingine.

0 comments: