Healthy
JINSI YA KUONDOA HARUFU MBAYA.
Piga mswaki angalau mara mbili kwa siku. Asubuhi na usiku wakati wakwenda kulala.
Nivizuri kusafisha katikati ya meno yako angalau mara moja kwa siku. Wengine hupendelea asubuhi au usiku kabla ya kulala, ili kuwa na kinywa safi walalapo.
Hii ni njia ambayo yaweza kukushangaza, lakini husaidia sana. Ni mojawapo ya njia aliyonipa mama yangu mzazi, zamani sana, kwa ajili ya rafiki yangu kipenzi. na ilimsaidia sana. ALIPONA.
NJIA YAKUONDOA HARUFU MBAYA KINYWANI.
Je umeshakumbana na mtu mwenye tatizo la kunuka mdomo? Au una tatizo hilo? Usijali, zipo njia rahisi sana zakutibu tatizo hilo, tena kwa gharama ndogo sana au kwa kutumia vitu vya ASILI vinavyotuzunguka.
Kwanza lazima kujua sababu kubwa ya tatizo lakunuka kwa mdomo ni kutokana na vijidudu, {bacteria} kujijenga nyuma ya ulimi au katikati ya meno.
JINSI YA KUONDOA HARUFU MBAYA.
*PIGA MSWAKI:-
*Floss:-
*Tongue Scraping:-
*Kunywa Maji:-
1. Mdalasini, {Cinnamon}
Ni rahisi kudhani kuwa kusugua ulimi kwa mswaki pekee, inatosha. Lakini mswaki husugua sehemu ya mbele ya ulimi zaidi kuliko "SCRAPING" ambayo hukusanya na kuondoa kabisa vijidudu vyote kwenye ulimi, kisha nje ya mdomo kabisa.
Unywaji wa maji ya kutosha, mfululizo kwa siku nzima, husaidia kuondoa harufu mbaya kinywani, kwani hufanya kinywa kuwa na unyevunyevu wakutosha, na kuzuia vijidudu hivyo kutokujijenga. Pia baada ya kila mlo, sukutua kinywa kwa sekunde kadhaa, ili kuondoa mabaki ya chakula yaliyosalia kwenye meno.
VIPO VITU VYA ASILI UNAVYOWEZA KUJITENGENEZEA MWENYEWE KUSAIDIA KUFANYA KINYWA CHAKO KUWA NA HARUFU NZURI.
Mdalasini una mafuta ya cinnamic aldehyde ambayo si kwamba itatoa tu harufu mbaya kinywani, bali itapunguza pia vijidudu hivyo.
- Changanya maji kikombe kimoja cha chai na kijiko kimoja cha chai cha unga wako wa cinnamon, kisha chemsha.
- Waweza ongeza na hiliki kidogo.
- Chuja, kisha waweza tumia kusukutulia/kusuuza kinywa kama aina nyingine tu za "Mouth Wash".
2. Cloves {Karafuu}.
Mbali ya kukipa kinywa harufu nzuri, pia karafuu kusaidia kuua vijidudu hivyo vinavyo sababisha harufu mbaya.
- Waweza tafuna karafuu hizo, ambazo zitaondoa harufu mbaya mara moja.
- Au waweza tengeneza chai yake. Chemsha karafuu yako ya unga kwa dakika 5 mpaka 10. Kisha kunywa au tumia kusukutua kinywa.
3. Juisi ya Limao.
Asidi iliyomo kwenye limao husaidia kuzuia kuongezeka
*Changanya kijiko cha chai cha juisi hiyo ya limao na maji kikombe kimoja, kisha sukutua. Waweza pia kuchanganya na chumvi.
MCHANGANYIKO HUO, PIA WAWEZA KUSAIDIA TATIZO LA KINYWA KIKAVU, AMBAYO NDIO SABABU KUBWA YAKUFANYA KUNUKA KWA KINYWA.
4. Majani makavu ya Mgomba.
*Tafuna majani hayo kila siku asubuhi kila uamkapo, kabla yakupiga mswaki. Hakikisha umeyatafuna majani hayo makavu ya mgomba, mpaka yamelainika kinywani. Kisha suuza kinywa chako na kupiga mswaki.
HIZO NI BAADHI TU YA NJIA ZA KUONDOA HARUFU MBAYA YA KINYWA. KARIBU UTUSHIRIKISHE NYINGINE.
Wapare tena kwa dawa. Ila imenishangaza iyo njia ya jani kavu la mgomba. Asante kwa maarifa
ReplyDelete