Healthy

Why Banana Good For You?

Tuesday, August 22, 2017 naomimwakanyamale 0 Comments

Faida Za Ndizi.

Mbali na madini mengi yaliyomo ndani ya ndizi kama nilivyoorodhesha hapo chini, lakini inajulikana kama ni tunda lililo na ladha ya sukari ambayo inahitajika mwilini si kwa wanamazoezi tu ambao hutumia sana ndizi kabla na baada ya mazoezi, bali ndizi ni muhimu kwa kila mtu. Imebeba asilimia kubwa ya madini ya Potassium, Magnesium, fiber ambayo huhitajika mwilini
 Inaweza ikawa tunda zuri lakini si kwa kila mtu hasa wale wenye ugonjwa wa Kisukari.

Virutubisho Vilivyomo Kwenye Ndizi.
  • 110 calories
  • .5 grams of fat
  • 27 grams of carbohydrates
  • 14 grams of sugar
  • 3 grams of fiber
  • 1 gram of protein
  • 25% vitamin B6
  • 16% manganese
  • 14% vitamin C
  • 12% potassium
  • 12% fiber
  • 10% copper
  • 10% biotin
  • 8% magnesium


Faida Za Ndizi.

1. Huongeza Nguvu:-


Sukari iliyopo ndani ya Ndizi husaidia kuongeza nguvu mwilini. Pia inashauriwa kutumiwa baada ya mazoezi ili kutibu na kujenga misuli, na kukuongezea nguvu zaidi.








2. Ina Madini Muhimu Ya Potassium:- 
Madini haya ni muhimu sana mwili kwa ajili ya kuzuia magonjwa mbalimbali ikiwemo magonjwa ya moyo, iwe high or low blood pressure. Pia Potassium inasaidia utunzwaji wa maji mwilini, kujenga na kuponya muscles {Misuli}, pia Potassium ni madini yanayotumika kusaidia kuponya magonjwa ya Kidney StonesGoutMaumivu ya mgongo, Maumivu ya Kichwa, na mengineyo.






3. Husaidia Usagaji wa Chakula Tumboni:-
Ndizi moja imebeba 3 grams za Fibes {Nyuzi nyuzi} zinazo saidia sana usagaji wa chakula tumboni. Itakupunguzia kuvimbiwa, kujawa na gesi tumboni, itakusaidia kupata haja kubwa. Fibes hizi zinasaidia kusafisha utumbo wako kwa kutoa uchafu wote kwenye utumbo mkubwa. Pia wataalamu wameongezea umuhimu wa fiber kuwa inalinda magonjwa yanayonyemelea moyo, cardiac arrest, and stroke.
Kwa wanaotaka kupungua, Fiber hizo zilizopo kwenye ndizi zinauwezo wa kukupunguzia njaa ya mara kwa mara.


4. Kukufanya Uwe Mwenye Furaha:- 


Ndizi ina Amino Acid ambayo huenda 
moja kwa moja na kuathiri “Happy 
Hormones” ambayo inakufanya unakuwa 
na furaha na kukuondolea simanzi. Itakuongezea nguvu kwa kuondoa uchovu, kwa kutumia  antioxidants zilizopo kwenye ndizi.













5.Ina Madini Ya Manganese ;-


Madini hayo yanasaidia sana kuendelea kujenga na kuboresha 
Ubongo, Mifupa na Ngozi. Kukufanya kuendelea kuonekana 

kijana.







6. Affordable, Portable, Low in Calorie Snack Choice ;-

Mbali na Snack nyingine nyingi ambazo kwanza zimebeba Calories nyingi, Ndizi imebeba Calories 100-110 inategemeana na ukubwa wake, ipo Healthy inakupa virutubisho ambavyo mwili unahitaji kwa siku, rahisi kubeba popote uendapo, na pia bei yake pia ni rahisi kulinganisha na aina nyingine za Snack.





TUTAKULETEA MAPISHI YA MKATE MZURI WA NDIZI

0 comments: