Lifestyles,

Just Faith....

Friday, September 11, 2015 naomimwakanyamale 0 Comments

Ni lazima kujiwekea msingi imara katika Maisha. Namaanisha MSINGI sio MISINGI. Ambao hauta yumbishwa na matukio. Na juu ya huo msingi ni lazima kuendelea kujenga kwa IMANI. Wengi wetu tunajua nini tunataka katika Maisha. Lakini tunatofautiana jinsi ya kufikia ndoto zetu. Inatakiwa kufahamu kwa hakika, SIO RAHISI HATA KIDOGO kufikia malengo yaliyo mazuri. Kuna mapito mengi tena magumu huwa tunapitia yasiyoendana hata kidogo na ndoto zetu, lakini haimaanishi tulichokusudia sio sahihi, hapana. Kila ndoto uliyonayo ni sahihi. Ipo nguvu ndani ya mwanadamu iliyotoka kwa aliyemuumba mwanadamu, wakati wote husema kwa sauti ya chini kukusukuma kufanya kitu Fulani, kamwe usipuuze. Huyo ndiye wewe halisi, Kwamwe usikatishwe tamaa na mazingira yako au jinsi wakuonavyo watu au ujionavyo kwa nje. Songa mbele weka mawazo chanya, pambana mpaka mwisho, utafika tu.

0 comments: