HealthySABABU 10 ZA KUNYWA MAJI KWA WINGI.
Hivi wajua kuwa pindi usikiapo tu kiu, ni kwamba, mwili wako unapiga kelele kukutaarifu kuwa ulishaishiwa maji?
|
Asilimia 60 ya mwili wako umebeba, au umetengenezwa na maji. Kwa hiyo pale unapokuwa umeishiwa na maji mwilini inamaanishwa mwili wako unashindwa kufanya kazi ipasavyo.
Je hiyo inamaanisha nini? Kwa nini tunatakiwa kunywa maji?
1. Usipokunywa maji, utakufa:- Tunaweza kuishi kwa muda mrefu zaidi bila kula chakula, lakini si maji. Kwa hiyo yatupasa kunywa maji zaidi ya tunavyokunywa sasa.
2. Husaidi kupunguza uzito:- *Unapokuwa unakunywa maji hasa ya baridi, mwili wako unatumia nguvu ya ziada kubadili lile joto la yale maji yaiyoingia mwilini kuwa sawa na joto la mwili wako. Kwa hiyo una burn more calories kwa kunywa maji tu.... {Authority Nutrition.} *Wakati mwingine tunachanganya kiu na njaa. Unafikiri una njaa, kumbe ukweli ni kiu. Unywaji wa maji wa kutosha husaidia kupunguza hamu ya kula, na inakufanya usisikie njaa au usile sana. Kwa hiyo.. {a}. Kunywa maji kabla yachakula, husaidia kupunguza njaa na kukufanya ujihisi umeshiba kwa hiyo itakusaidia kupunguza chakula unachoingiza mwilini. {b}. Badili unywaji wa vinywaji vinavyoweza kukunenepesha, mfano:- soda, bia, juice au vinywaji vinavyotengenezwa na sukari nyingi, na ongeza unywaji wa maji.
3. Huzuia Kansa:- Uchunguzi umeonyesha unywaji wa maji yakutosha unaweza kuzuia kansa ya utumbo kwa asilimia 45, kansa ya kibofu kwa asilimia 50 na pia inaweza kupunguza athari ya kansa ya ziwa.
4. Hupunguza hasira:- Uchunguzi umeonyesha pia unywaji maji kwa wingi hupunguza msongamano wa mawazo. Hukufanya ufikirie vizuri, na kukupunguzia hasira za hapa na pale. Kunywa maji.
5. Kufanya mazoezi bora:- Unywaji maji wakutosha husaidia kuongeza ufanyaji mzuri wa mazoezi. Misuli yetu ina asilimia 75 ya maji. Upungufu wa maji mwilini unaweza kusababisha udhaifu, uchovu, kizunguzungu na upungufu wa virutubisho mwilini. Maji hupa misuli nguvu ya kufanya kazi zaidi. Kunywa maji kwa mazoezi bora na fanisi.
6. Punguza maumivu ya viungo:- Maji ya kunywa yanaweza kupunguza maumivu katika viungo vyako kwa kufanya cartilage kuwa laini na nyevunyevu.
7. Husaidia kutoa uchafu mwilini na vijidudu:- Maji husaidia mmeng'enyo wa chakula mwilini na huondoa taka mwilini kwa njia ya mkojo na jasho. Usipokunywa maji yakutosha, waweza pata matatizo mengi ikiwepo maumivu ya tumbo yanayosababishwa na kukosa haja kubwa.
8. Kukinga na maumivu ya kichwa:- Wakati mwingine kichwa huuma sababu ya ukosefu wa maji mwilini. Unapoumwa na kichwa, jaribu kunywa maji mengi kwa wingi, kama huduma yako ya kwanza. Yaweza saidia.
9. Hufanya ngozi yako kuwa nzuri:- Unywaji wa maji kwa wingi husaidia utengenezwaji wa cells mpya, hivyo huongeza muonekana mzuri wa ngozi na kukupa rangi nzuri. Maji husaidia ngozi kufanya kazi yake yakutoa jasho kwa rahisi, kwa hiyo inapunguza pia athari ya kuotwa na mapele.
10. Kulisha mwili wako:- Maji husaidia kuzungusha virutumisho mwilini na kufika katika kila kiungo. Ukosefu wa maji yakutosha mwilini kusababisha kutosambaa kwa virutubisho mwilini.
KABLA HUJAFIKIRIA KUKIMBILIA HOSPITALINI KWA MATIBABU, KUNYWA MAJI KWA WINGI. |
About author
Writer ,Journalist, Fashonista ,Entrepreneur ,Storyteller, Mother , Wife.
0 comments: