Lifestyles,

KUWA MAKINI NA KILA UNACHOTAMKA. MANENO YANA NGUVU

Friday, November 13, 2015 naomimwakanyamale 0 Comments


Kwa neno tu, Mungu aliumba Dunia iliyokuwa tupu na katika hali isiyoeleweka. Kwa kutamka tu akatengeneza kila kitu kinachoonekana leo, hata wanadamu wanaojaribu kumpinga pia aliwaumba. Isipokuwa kwa wanadamu alitenda kitu cha ziada. Alimtengeneza MWANADAMU kwa mfano wake. Akaweka nguvu, yaani ile hali ya kiungu ndani yake. Ndio maana kila Mwanadamu anapotoa NENO lake ni lazima liumbe kitu. Kiwe KIZURI au KIBAYA. Lazima tuwe waangalifu sana na maneno tunayotoa, hata kama ni ya utani. Hata kama ni kwa watoto wadogo sana. Awe wako au wajirani. Fikiri kabla hujaongea kitu. Hata kama umekasirika, zoeza kinywa chako kutamka maneno uliyo yakusudia kuyatoa. Huwa inagarimu sana kutoa sumu ya maneno ndani ya moyo wa mtu. Kama huna jambo jema lakuongea. Ni heri kunyamaza kabisa.


0 comments: