Kona ya Mahanjumati.
MAHITAJI:-
UPIKWAJI:-
JIONGEZE KWENYE PISHI LAKO LA MUHOGO.
MAHITAJI:-
Muhogo mbichi, kitunguu, kitunguu swaumu, Nazi, Karanga za kutwanga, au Peanut butter ya kopo, Nyanya, Hoho, karoti, Nyama unayotaka kulia muhogo wako, chumvi na viungo vingine ulivyozoea kuweka kwenye rosti yako, iwe Cilantro ya kutupia juu ya chakula chako, pilipili manga, binzari n.k
UPIKWAJI:-
*Chemsha mihogo yako vizuri, weka pembeni,
*Chemsha nyama yako vizuri, weka pembeni ikiwa na supu yake.
*Chukua sufuria yako unayojua haiunguzi kwa haraka, Kaanga vitunguu, karoti, hoho na nyanya.
*Vikisha iva weka karanga kutengeneza uji mzito,
*Kisha weka mihogo uliyokwisha chemsha bila maji. Yaani mikavu. Changanya na rosti yako jikoni.
*Kisha weka nyama yako sasa, endelea kuchanganya huku ukiangalia moto, kwakuwa karanga ni rahisi sana kuunguza chakula na kufanya kinuke.
* Mwishoni weka kiasi cha rojo/ mchuzi unaotaka kwenye mchanganyiko wako. Nazi na ile supu uliyopata wakati unachemsha nyama yako.
*Kama unakula na Nyama ya kukaanga au kuchoma. Nazi pekee inatosha kufanya chakula chako kiwe na rosti nzuri na tamu.
Jaribu kisha tushirikishe matokeo yake. Ni chakula kizuri sana kwa kuliwa mara moja moja kwa hamu.
0 comments: