Healthy
*KAHAWA*
Upenzi wa kahawa, umenipelekea kufanya utafiti zaidi, hasa baada ya kusikia na kusoma madhara yake badala ya faida. Huku kinywaji hiki kikitumika kwa wingi sana nchi za Magharibi, na kusifika nchini China, kuwa ni mojawapo ya tiba zao, inayofanya wasiugue, waishi kwa muda mrefu huku wakifanya kazi kwa bidii. Ilinifanya kuwa na shauku kubwa ya kufanyia utafiti juu ya kinywaji hiki cha kahawa.
PATA SIRI YA KAHAWA.
*KAHAWA*
Upenzi wa kahawa, umenipelekea kufanya utafiti zaidi, hasa baada ya kusikia na kusoma madhara yake badala ya faida. Huku kinywaji hiki kikitumika kwa wingi sana nchi za Magharibi, na kusifika nchini China, kuwa ni mojawapo ya tiba zao, inayofanya wasiugue, waishi kwa muda mrefu huku wakifanya kazi kwa bidii. Ilinifanya kuwa na shauku kubwa ya kufanyia utafiti juu ya kinywaji hiki cha kahawa.
Watafiti wameonyesha kuwa mbali na Kahawa kuwa na Caffeine ambayo wengi wameonyesha madhara yake tu, bila faida zake mwilini, pia Kahawa imebeba Vitamini B2, B5 na Madini ya potassium, manganese n.k Vyote hivyo huitajiaka au ni muhimu kwenye mwili wa mwanadamu. Angalia baadhi ya faida za kahawa.
*Hufanya kufikiri zaidi na kuupa mwili nguvu*
Wengi wamekuwa wakitumia kinywaji hiki kama kifungua kinywa tu. Kwa mazoea. Lakini tafiti zimeonyesha kuwa, utumiaji wa Kahawa unaweza kukufanya kuwa smart.
Caffeine ambayo ipo kwenye kahawa inakwenda kwenye ubongo na kufanya ubongo ufikiri vizuri. Kwa maelezo zaidi tembelea {onlinelibrary.wiley.com}
Caffeine ambayo ipo kwenye kahawa inakwenda kwenye ubongo na kufanya ubongo ufikiri vizuri. Kwa maelezo zaidi tembelea {onlinelibrary.wiley.com}
*Kahawa inaweza kusaidia kuyeyusha mafuta yaletayo madhara mwilini*
Ukiwa makini kuangalia kila "Fat burning Supplements" lazima utakuta Caffeine ndani yake. hii ni kwa sababu Caffeine inaongeza mmengenyo wa chakula mwilini na kumfanya mtu kujisikia kuwa na nguvu na kuondoa uchovu au usingizi mwilini.
Hivyo hufanya mtumiaji wa kinywaji hiki kufanya kazi kwa muda mrefu bila kuchoka, na kama ni yupo kwenye mazoezi, anauwezo wa kufanya mazoezi kwa muda mrefu bila kuchoka, kwa hiyo anauwezo wa ku "burn more fat" mwilini...Kwa maelezo zaidi..{onlinelibrary.wiley.com}
*Kahawa inaweza kupunguza madhara yakupata kisukari, {Type 2 Diabetes}*
Japokuwa wengine wamejenga mazoea ya kupata angalau kikombe kimoja tu kwa siku ili kupata ladha ya kahawa, Lakini tafiti zimeonyesha, wanyaji wa kinywaji hiki wanaweza kuepuka maradhi ya kisukari, ambayo kusababishwa na mwili kushindwa kutengeneza INSULINE.......{jamanetwork.com}
*Kahawa inaweza kuepusha maradhi mengi mwilini yakiwepo ya ubongo, hasa kipindi ufikiapo utu uzima*
Nyakati za jioni, unaweza kuwakuta wazee wapo pamoja wakicheza Bao, Karata au Mazungumzo yao tu, huku wakipata kinywaji hiki. Mbali ya kuwa ni kiburudisho kwao, lakini utafiti umeonyesha Kahawa ambayo si inasaidia kuwa smart kwa muda mfupi unapokuwa ukiitumia na kukufanya ufikiri vizuri tu, pia inalinda ubongo na maradhi ya Alzheimer's ambayo yanaleta Dementia.
Ugonjwa huu wa akili, unaofanya mtu kusahu au kuchanganyikiwa, mara nyingi huwapata watu wengi duniani mara waingiapo kwenye umri wa utu uzima.{onlinelibrary.wiley.com} . Pia watafiti wamegundua Kahawa inaweza kuepusha madhara yaletayo magonjwa ya INI na baadhi ya aina ya za kanser kama Kanser ya Ini..{www.who.int}
*Virutubisho vilivyopo kwenye Kahawa ni muhimu mwilini*
Mbali na utafiti uliofanya mwaka 2005 na chuo cha Harvard, na kugundulika kwamba Kahawa ndiyo yenye Antioxidant kubwa kuliko matunda na mboga mboga nyingi, pia Kahawa imebeba virutubisho kama Vitamini B2 & B5, Manganese, Potassium, Magnesium na Niacin. Vyote hivyo husaidia na kulinda cells zinazopambana na magonjwa mwilini...{nutritiondata.self.com}
ANGALIZO.
Japokuwa kahawa ina faida nzuri kwenye mwili wa mwanadamu, lakini pia huweza kuleta madhara makubwa kama isipotumiwa kwa kiasi. Kunywa kahawa kwa afya. Wapo watu ambao tayari wanasumbuliwa na maradhi tofauti tofauti, kwa hiyo ongezeko la Caffeine ndani ya miili yao, inaweza kusababisha madhara zaidi. Kuwa makini katika hilo. Na kwa kuwa Kahawa inakaa mwilini kwa masaa 2-6, kama unasumbuliwa na kukosa usingizi kipindi cha usiku sababu wa unywaji wa Kahawa, wataalamu wameshauri, kuacha kunywa kinywaji kichi baada ya saa 8 mchana, ili kuweza kupata usingizi wa kutosha usiku hasa baada ya kazi nyingi nyakati za mchana. Kuwa makini na kulinda afya yako.
"Too Much of Everything Is Hamful."
0 comments: