Healthy,
Jinsi Ya Kupunguza Uzito kwa Kutumia Kinywaji cha Tangawizi.
Vipo vinywaji
vingi sana vyenye sifa za kupunguza uzito au kukata mafuta mwilini. Lakini kama
nilivyoonyesha kwenye nakala yangu nyingine juu ya “Nguvu ya
Tangawizi mwilini”, leo nitakupa siri ya kutumia Tangawizi Kupunguza Uzito.
Mahitaji.
*Maji
*Tangawizi
* Limao {Ukipenda}
Uandaaji.
Chemsha Maji yako, kisha ongeza Tangawizi ambayo utakuwa umetwanga. Acha ichemke kwa muda, kisha uitoe
jikoni. Waweza kuinywa kama chai, bado ikiwa ya moto bila ya kuongeza Sukari. Na kuweka maji ya Limao kiasi, kama utapenda.
Hakikisha unaweka Tangawizi ya kutosha. Ladha
ya Tangawizi isikike kwenye Maji.
Wakati Gani wa Kuinywa?
*Usiku Wakati wa Kwenda
kulala :- Kwa
kuwa Tangawizi
inasaidia kusaga chakula mwilini huku ikiyeyusha mafuta,
ni vyema kinywaji hicho kukinywa wakati unakwenda kulala, ili isikufanye
ukasikia njaa, na kushawishika kula tena. Cha msingi ni kulala ukiwa unauhakika
wa chakula ulichokula kwa siku nzima, kitasagwa na kutolewa uchafu wote ambao
hautahitajika mwilini. Na
*Asubuhi kabla ya Kifungua kinywa :- Soma
faida ya Tangawizi kwenye nakala yangu iliyopita. {Je, Wajua Nguvu Ya Tangawizi?}
0 comments: