Story
“Nini kimevurugika?” “Kila kitu. Naomba Mungu asaidie tu, nikimaliza shule, nipate kazi, maisha yaanze.” “Unampango wakuishi wapi? Namaanisha utatafuta kazi maeneo gani?” Geb aliendelea kudadisi. Nanaa alitulia kidogo kama anafikiria. Akajibu kwa upole. “Popote pale nitakwenda kufanya kazi au nitatafuta kazi, isipokuwa Moshi na Arusha.” Geb aliweka uso wa kuuliza kidogo kisha akatupia swali jingine. “Kwa nini hupataki Moshi na Arusha?” Nanaa akanyamaza, akabaki anafikiria.
“Eti Nanaa?” Geb akauliza tena. Alikuwa na sauti nzuri iliyotulia na kumfanya mtu yeyote apende kumsikiliza. Labda ni Nanaa tu. Lakini alijisikia vizuri kuwa karibu na Geb. “Hiyo mikoa sitamani kuja kurudi tena. Imebeba historia mbaya tupu ya maisha yangu” “Ikitokea unapata kazi huko, je? Tena kwa ahadi ya pesa nyingi.” “Mmmh! Sitakwenda.” Nanaa akajibu kwa hisia za majonzi akiwa ameinama kama amekumbushwa mbali. “Kweli umepachukia.” Kwa muonekano ule, Geb mwenyewe akaamini kuwa Nanaa amekusudia kutorudi.
“Lakini si unajua ukishindwa hiki unapanga tena mipango mingine? Usiache kujiwekea malengo, kwa kuvunjika kwa malengo uliyokuwa umejiwekea zamani.” Geb alishauri. “Wakati mwingine unakata tamaa au unajishuku labda unaweka malengo yasiyowezekanika maishani. Unaamua kuacha tu. Usubiri litokee lakutokea, upambane nalo mbele ya safari. Kuliko kuumia kila wakati.” “Pole. Lakini ipo siku nitataka uniambie hiyo mipango iliyogoma kutimia.” Nanaa alicheka kidogo, akainama kama anayefikiria.
“Nilikuudhi nini?” Geb aliuliza kwa kubembeleza. “Hapana. Hakuna ulipokuwa umekosea. Ni mimi mwenyewe tu. Naomba unisamehe.” Nanaa alimwangalia tena. Angemuudhi mtu yeyote, lakini sio Geb. Kijana mgeni kwake, lakini akajikuta ameshateka moyo na fahamu zake.
“Siweze kusamehe kama sifahamu kosa, Nanaa. Kama nikitu cha kurekebisha, si niafadhali tujue turekebishe ili isitokee tena?” Nanaa akanyamaza. “Eti mchumba wa Fili? Au Jeff ameshamzidi mahesabu?” Nanaa alijikuta akicheka kwa sauti. “Kumbe na wewe mchokozi hivyo?” Geb alicheka. “Mimi sio mchokozi. Najiandaa kwa harusi.” “Kwani na wewe ulisikia mazungumzo yangu na Jeff?” Nanaa aliuliza kwa aibu sana huku akicheka. Geb alibaki akitabasamu tu. Nanaa akapata jibu lake moja kwa moja.
“Usiniambie kama na wewe ulisikia!” “Mlikuja kuongea nyuma yetu. Tena Danny alikuwa akionyesha kitu alichokuwa akifanya Fili. Wakawa wamepingiana pesa na Zinda. Kuna mtoto mmoja hivi, bonge kidogo.” “Ni Tyrii?” Nanaa akauliza. “Ehee! Umeshawajua!?” “Kumbuka nilicheza nao muda wote.” Wakacheka.
“Sasa Tyrii alimsukuma kwa makusudi Fili. Wote tukaona. Fili akakasirika sana. Zinda akasema nilazima Fili atampiga ngumi. Danny akasema mwanae sio mgomvi kabisa. Zinda akambishia. Ndio Danny akasema tunyamaze kimya tuone kama mwanae atamrudishia au la. Wakapingiana dau. Tukakubaliana tunyamaze kimya tuangalie tuone. Kwa hiyo wote tulikuwa kimya tukifuatilia tukio zima. Na wakamwambia mama yake asiende kuwaingilia. Sasa wakati tunawaangalia watoto, na nyinyi mkaja nyuma ya ule uzio mkaanza kuongea. Basi tukawa tunaangalia watoto, huku tunawasikiliza.” Nanaa akaziba uso huku anacheka kwa aibu.
“Mungu wangu! Kwa hiyo mkasikia kila kitu?” Nanaa akauliza tena huku ameficha uso. “Naona jamaa amekazana na Fili naye yupo na mipango iliyokamilika. Mahari mpaka sehemu ya kukuweka. Sasa sijui nani ataibuka na mke!?” Nanaa akacheka tena. “Naona safari hii nimebahatika. Nimempata mchumba Fili anayenipenda, na kujivunia mbele za watu.” Geb akamtizama, na kuuliza, “Kwani safari zingine hukubahatika?” Nanaa alipooza usoni, akatingisha kichwa kukataa. Cheko likaisha. Huzuni ikamjaa kadiri alipokumbuka wanaume aliokwisha kuwa nao kwenye mahusiano ndivyo furaha iliendelea kupotea mpaka usoni akaonyesha.
Taratibu Geb aliona machozi yanachirizika pembeni ya mashavu ya Nanaa. Akayafuta kwa haraka na kurudisha tabasamu lake la kumtuliza tu. Lakini wazi alionekana kuna huzuni nyuma ya hilo tabasamu. “Pole Nanaa. Basi safari hii, tutahakikisha Fili anakufikisha kanisani.” Nanaa akacheka tena. “Geb wewe ni mchokozi bwana, kama Danny!” “Mimi nakwambia ukweli, sikuchokozi.” “Haya bwana.” Geb alimtizama kidogo, nakuangalia pembeni huku akitabasamu.
“Unacheka nini sasa?” Nanaa akamuuliza pale alipomuona anatabasamu. “Ukicheka unapendeza. Una dimpozi nzuri sana, Nanaa.” Geb alimgeukia na kumtizama wakati anamsifia. Nanaa alibabaika kidogo, akajishika machavuni. “Zipo hapa bwana. Unajishika wapi huko?” Geb aliweka kidole chake kwenye kishimo kilichopo kwenye shavu la kulia la Nanaa, Nanaa akacheka. “Ewaa! Hapo ndio zimetokea vizuri.” Geb akasifia tena. Kule kushikwa tu na Geb, Nanaa alijisikia vizuri sana.
“Sijui hata nafanana na nani?” Nanaa alijiongelesha. “Najua mama yako alifariki, lakini hukuwahi hata kuona picha zake?” Geb alimfanya Nanaa amwangalie kwa mshangao. “Umejuaje!?” Nanaa akauliza kwa mshangao. “Kaka yako anakupenda sana, Nanaa. Huwa akizungumzia habari za ndugu zake, haachi kukutaja na wewe. Kwa hiyo nakufahamu kwa kiasi.” Nanaa alibaki hajui aseme nini. Kwa kuwa hakujua Geb anamfahamu kwa lipi.
“Ninazo picha za zamani za mama yangu. Lakini sifanani naye hata kidogo. Sasa sijui kwa kuwa alifariki akiwa bado mtoto mdogo!? Lakini hatufanani kabisa hata sifanani na ndugu zake. Labda hii rangi kama ya kaka. Lakini nipo watofauti kabisa. Nimejaribu kujifananisha hata na bibi, lakini sijioni kabisa kwake. Isipokuwa rangi tu. Bibi mzaa mama anarangi kali sana. Ndio maana wote mpaka kina Viola, mtoto wake, kaka, mimi, kina mama zetu. Wote tumechukua rangi ya bibi. Lakini sioni kingine. Nahisi nitakuwa nafanana na upande wa baba yangu.” “Ulifanikiwa kumuona baba yako?” Geb akauliza.
“Kwa nini yeye hakuta kukulea mwenyewe!?” Geb akauliza kwa kumuhurumia. Nanaa akanyamaza kidogo, akainama kama kuzuia machozi. “Tokea nazaliwa mpaka leo, mume wake hakuwahi kunipenda. Alihesabu mimi ni mzigo mzito ambao hakutaka kujihusisha nao, na wakati huo na wao walikuwa na mtoto mdogo Viola. Kwa hiyo baada yakushindwa pakunipeleka, ndio nikaishia kwao. Kwa kifupi mpaka hivi leo, hatukuwahi kujua baba yangu ni nani.” Nanaa alitoa tabasamu lililoonyesha limejaa maumivu.
Alimpokea mtoto kutoka kwa shemeji yake, Nanaa akaaga kwa kaka yake, wakaondoka. Njiani kulikuwa na utulivu kidogo. Lakini ukimya huu haukuwa kama ule wa mwanzoni. Grace aliwakatisha mazungumzo yaliyoibua hisia za huzuni katikati yao. Nanaa alijiegemeza vizuri kwenye kiti, akabaki akiangalia nje ya dirisha. Geb alimtupia macho mara kadhaa kama anayetaka kuongea kitu, akajikuta anakwama, hajui aongee nini.
“Hivyo hatukuongea.” “Basi huwezi kuwa umeishiwa maneno. Bado nasubiri maelezo.” “Lakini si umeshasamehe?” “Mpaka nijue sababu.” “Haya bwana. Muwe na usiku mwema.” Geb alikuwa akimtizama na tabasamu lililomfanya Nanaa azidi kufurahia na kusahau hata kama dunia inazunguka. Kwamba masaa yanasogea. Alitamani kuendelea kuwepo na Geb. Kitu ambacho hakuwahi kusikia kabla, na wala hakuwa tayari. Lakini akajikuta inamtokea “Na wewe pia. Usiku mwema.” Nanaa akashuka akiwa na furaha moyoni. Akasubiri afungue mlango, akaingia ndani bila ya kugeuka nyuma tena, ndipo Geb alipoondoka.
Geb aliondoka pale akielekea kwao njiani akikumbuka dimpozi za Nanaa. Akacheka. “She is nice!” Akasifia moyoni na kucheka. Akakumbuka kicheko kizuri cha Nanaa. Kuna wakati alicheka huku machozi yakimtoka. Pia Geb akavutiwa zaidi. “Well, not only nice but also beu…” Geb akatulia kwanza.
Akakumbuka mazungumzo kati ya Nanaa na Jeff. Akavuta pumzi kwa nguvu. “Lakini hamna kitu. Sina haja yakutilia shaka.” Akajiliwaza. Lakini akakumbuka vile Jeff alivyong’ang’ania na kurudi kuomba namba ya simu. Isitoshe akapiga. Geb akakumbuka ni kama kwenye mazungumzo aliyosikia yakiendelea ndani ya gari, Nanaa aliahidi kupiga kesho yake. “Tena ni kama Jeff amesema kabla ya lunch ili asishindwe kula naye dinner. Sikumsikia Nanaa akikataa. Infact…” Geb aliendelea kuwaza.
“Hataki kunipa pesa yangu.” Fili alizidi kulia. Geb akaenda kumbemba. “Nyamaza mtoto mzuri.” Geb akaendelea kumbembeleza. “Hivi baba yake yuko njiani. Nimemwambia aje, amuelezee mwanae vizuri, aelewe. Maana yeye ndio ameyataka yote haya.” Grace aliendelea, kidogo wakamsikia Danny ameingia anaongea. “Yuko wapi Dume langu?” “Njoo huku ofisini kwa muhasibu.” Grace alimwita mumewe.
is mine - ni Wangu! Part 1, Sehemu ya 9
Nanaa na
Geb.
"Tukae hapa.” Geb alitafuta mahali akakaa, Nanaa naye
akaenda kukaa pembeni yake, wakatulia kidogo. “Vipi
shule lakini?” Geb akauliza. “Tupo field, kwa sasa. Tukirudi ndio mwaka wa tatu na wa mwisho,
tunamaliza.” Nanaa akajibu. “Unampango
wa kuendelea kusoma?” Geb
akauliza tena. “Mimi sio mpenda shule.” Geb akacheka. “Kweli tena. Hata hapa
nilipofika ni kwa sababu ya kaka James. Sasa kuja kurudi tena kusoma shahada ya
pili! Hapana kwa kweli.” “Utataka kufanya nini ukimaliza?” “Hata
sijui. Nilikuwa na mipango mingii, lakini yote imevurugika. Nahisi nitajua
mbele ya safari.” Geb akamwangalia.
“Nini kimevurugika?” “Kila kitu. Naomba Mungu asaidie tu, nikimaliza shule, nipate kazi, maisha yaanze.” “Unampango wakuishi wapi? Namaanisha utatafuta kazi maeneo gani?” Geb aliendelea kudadisi. Nanaa alitulia kidogo kama anafikiria. Akajibu kwa upole. “Popote pale nitakwenda kufanya kazi au nitatafuta kazi, isipokuwa Moshi na Arusha.” Geb aliweka uso wa kuuliza kidogo kisha akatupia swali jingine. “Kwa nini hupataki Moshi na Arusha?” Nanaa akanyamaza, akabaki anafikiria.
“Eti Nanaa?” Geb akauliza tena. Alikuwa na sauti nzuri iliyotulia na kumfanya mtu yeyote apende kumsikiliza. Labda ni Nanaa tu. Lakini alijisikia vizuri kuwa karibu na Geb. “Hiyo mikoa sitamani kuja kurudi tena. Imebeba historia mbaya tupu ya maisha yangu” “Ikitokea unapata kazi huko, je? Tena kwa ahadi ya pesa nyingi.” “Mmmh! Sitakwenda.” Nanaa akajibu kwa hisia za majonzi akiwa ameinama kama amekumbushwa mbali. “Kweli umepachukia.” Kwa muonekano ule, Geb mwenyewe akaamini kuwa Nanaa amekusudia kutorudi.
“Lakini si unajua ukishindwa hiki unapanga tena mipango mingine? Usiache kujiwekea malengo, kwa kuvunjika kwa malengo uliyokuwa umejiwekea zamani.” Geb alishauri. “Wakati mwingine unakata tamaa au unajishuku labda unaweka malengo yasiyowezekanika maishani. Unaamua kuacha tu. Usubiri litokee lakutokea, upambane nalo mbele ya safari. Kuliko kuumia kila wakati.” “Pole. Lakini ipo siku nitataka uniambie hiyo mipango iliyogoma kutimia.” Nanaa alicheka kidogo, akainama kama anayefikiria.
“Wewe mipango
yako yote inatimia?” Safari hii Nanaa naye akauliza swali nakumfanya
Geb acheke huku akifikiria kidogo. “Daah! Swali
zuri sana. Japokuwa sikuwahi kuulizwa kabla na na..” Geb akababaika
kidogo. “Lakini labda niwe muwazi.” Akaendelea. “Siwezi kulalamika. Ni
mambo madogo madogo tu ambayo naweza kurekebisha. Yapo ndani ya uwezo wangu.
Siwezi kulaumu. Namshukuru Mungu kwa hilo.” “Hongera.” Geb alicheka akamwangalia. “Natakiwa
hongera eeh?” “Kabisa. Niwachache sana wanaoweza kufikia ndoto zao.” Geb alitabasamu. “Asante. Namshukuru Mungu
kwakweli.” Alijibu na kunyamaza. Ukimya wa muda ukapita tena.
“Unafurahia
kufanya kazi na Grace?” Geb
akauliza tena. “Ukweli hana shida. Ilimradi ufanye tu
majukumu yako. Kwanza anachoka kuongea na kusikiliza maneno mengi. Mpole kama
wewe.” Nanaa alijibu na
kumfanya Geb acheke. “Umejuaje kama
mimi mpole? Au kwa kuwa sijalalamika kwa kutojibu ujumbe wangu?” Nanaa akacheka kwa
aibu nakujificha uso. “Eti Nanaa?”
“Samahani.” “Kabla yakuomba msamaha, niambie kwa nini hukunijibu.”
Nanaa alinyamaza kama anafikiria.
“Eti Nanaa?”
“Ni habari ndefu. Lakini unisamehe tu.”
Walijikuta wakiangaliana. Nanaa alijaribu kukwepesha macho lakini
akakuta bado Geb akimwangalia kwa utulivu. “Ni mambo mengi,
Geb.” Nanaa
alijilalamisha kwa upole. “Yanayohusiana
na ule ujumbe niliokutumia au ni kitu kingine? Maana nilitaka kujua
unaendeleaje na kama ulifika nyumbani salama. Basi. Nikaona umesoma ujumbe
wangu, halafu kimya. Hukurudisha majibu Nanaa.” Nanaa akainama.
“Ukweli
niliiingiwa na wasiwasi. Ikabidi kukufuata nyumbani kujua unaendeleaje. Tena
wala hukunisalimia mimi. Au kuna kitu nilikuudhi tulipokuwa wote pale ofisini?” Nanaa akajisikia vibaya sana
moyoni. Japokuwa siku ile usiku walipoenda kumtizama nyumbani baada yakuondoka
ofisini bila kuaga na kumuacha Geb haelewi, aliyezungumza ni Grace na Danny tu.
Geb alikuwa kimya. Kumbe yeye ndio aliyekuwa na safari ya kwenda kumuona. Grace
na mumewe walikuwa wasindikizaji tu!
“Nilikuudhi nini?” Geb aliuliza kwa kubembeleza. “Hapana. Hakuna ulipokuwa umekosea. Ni mimi mwenyewe tu. Naomba unisamehe.” Nanaa alimwangalia tena. Angemuudhi mtu yeyote, lakini sio Geb. Kijana mgeni kwake, lakini akajikuta ameshateka moyo na fahamu zake.
“Siweze kusamehe kama sifahamu kosa, Nanaa. Kama nikitu cha kurekebisha, si niafadhali tujue turekebishe ili isitokee tena?” Nanaa akanyamaza. “Eti mchumba wa Fili? Au Jeff ameshamzidi mahesabu?” Nanaa alijikuta akicheka kwa sauti. “Kumbe na wewe mchokozi hivyo?” Geb alicheka. “Mimi sio mchokozi. Najiandaa kwa harusi.” “Kwani na wewe ulisikia mazungumzo yangu na Jeff?” Nanaa aliuliza kwa aibu sana huku akicheka. Geb alibaki akitabasamu tu. Nanaa akapata jibu lake moja kwa moja.
“Usiniambie kama na wewe ulisikia!” “Mlikuja kuongea nyuma yetu. Tena Danny alikuwa akionyesha kitu alichokuwa akifanya Fili. Wakawa wamepingiana pesa na Zinda. Kuna mtoto mmoja hivi, bonge kidogo.” “Ni Tyrii?” Nanaa akauliza. “Ehee! Umeshawajua!?” “Kumbuka nilicheza nao muda wote.” Wakacheka.
“Sasa Tyrii alimsukuma kwa makusudi Fili. Wote tukaona. Fili akakasirika sana. Zinda akasema nilazima Fili atampiga ngumi. Danny akasema mwanae sio mgomvi kabisa. Zinda akambishia. Ndio Danny akasema tunyamaze kimya tuone kama mwanae atamrudishia au la. Wakapingiana dau. Tukakubaliana tunyamaze kimya tuangalie tuone. Kwa hiyo wote tulikuwa kimya tukifuatilia tukio zima. Na wakamwambia mama yake asiende kuwaingilia. Sasa wakati tunawaangalia watoto, na nyinyi mkaja nyuma ya ule uzio mkaanza kuongea. Basi tukawa tunaangalia watoto, huku tunawasikiliza.” Nanaa akaziba uso huku anacheka kwa aibu.
“Mungu wangu! Kwa hiyo mkasikia kila kitu?” Nanaa akauliza tena huku ameficha uso. “Naona jamaa amekazana na Fili naye yupo na mipango iliyokamilika. Mahari mpaka sehemu ya kukuweka. Sasa sijui nani ataibuka na mke!?” Nanaa akacheka tena. “Naona safari hii nimebahatika. Nimempata mchumba Fili anayenipenda, na kujivunia mbele za watu.” Geb akamtizama, na kuuliza, “Kwani safari zingine hukubahatika?” Nanaa alipooza usoni, akatingisha kichwa kukataa. Cheko likaisha. Huzuni ikamjaa kadiri alipokumbuka wanaume aliokwisha kuwa nao kwenye mahusiano ndivyo furaha iliendelea kupotea mpaka usoni akaonyesha.
Taratibu Geb aliona machozi yanachirizika pembeni ya mashavu ya Nanaa. Akayafuta kwa haraka na kurudisha tabasamu lake la kumtuliza tu. Lakini wazi alionekana kuna huzuni nyuma ya hilo tabasamu. “Pole Nanaa. Basi safari hii, tutahakikisha Fili anakufikisha kanisani.” Nanaa akacheka tena. “Geb wewe ni mchokozi bwana, kama Danny!” “Mimi nakwambia ukweli, sikuchokozi.” “Haya bwana.” Geb alimtizama kidogo, nakuangalia pembeni huku akitabasamu.
“Unacheka nini sasa?” Nanaa akamuuliza pale alipomuona anatabasamu. “Ukicheka unapendeza. Una dimpozi nzuri sana, Nanaa.” Geb alimgeukia na kumtizama wakati anamsifia. Nanaa alibabaika kidogo, akajishika machavuni. “Zipo hapa bwana. Unajishika wapi huko?” Geb aliweka kidole chake kwenye kishimo kilichopo kwenye shavu la kulia la Nanaa, Nanaa akacheka. “Ewaa! Hapo ndio zimetokea vizuri.” Geb akasifia tena. Kule kushikwa tu na Geb, Nanaa alijisikia vizuri sana.
*************************************
“Sijui hata nafanana na nani?” Nanaa alijiongelesha. “Najua mama yako alifariki, lakini hukuwahi hata kuona picha zake?” Geb alimfanya Nanaa amwangalie kwa mshangao. “Umejuaje!?” Nanaa akauliza kwa mshangao. “Kaka yako anakupenda sana, Nanaa. Huwa akizungumzia habari za ndugu zake, haachi kukutaja na wewe. Kwa hiyo nakufahamu kwa kiasi.” Nanaa alibaki hajui aseme nini. Kwa kuwa hakujua Geb anamfahamu kwa lipi.
“Ninazo picha za zamani za mama yangu. Lakini sifanani naye hata kidogo. Sasa sijui kwa kuwa alifariki akiwa bado mtoto mdogo!? Lakini hatufanani kabisa hata sifanani na ndugu zake. Labda hii rangi kama ya kaka. Lakini nipo watofauti kabisa. Nimejaribu kujifananisha hata na bibi, lakini sijioni kabisa kwake. Isipokuwa rangi tu. Bibi mzaa mama anarangi kali sana. Ndio maana wote mpaka kina Viola, mtoto wake, kaka, mimi, kina mama zetu. Wote tumechukua rangi ya bibi. Lakini sioni kingine. Nahisi nitakuwa nafanana na upande wa baba yangu.” “Ulifanikiwa kumuona baba yako?” Geb akauliza.
“Kuna kipindi
nilitamani kumtafuta, lakini mama mkubwa aliniambia sio jambo sahihi, kwa kuwa
alikana mimba yangu, na hata wazazi wake walimfukuza mama yangu na kumuonya
asiwahi kurudi tena. Na hapo mama alikuwa amefukuzwa nyumbani kwao. Mama mkubwa
anasema mama alipofukuzwa kule nyumbani kwao, na kwa huyo mwanaume, akawa hajui
pa kwenda. Ndio akamchukua yeye. Lakini alipomuuliza zaidi juu ya baba yangu,
mama alishindwa kueleza zaidi alikuwa akilia tu. Akasubiri labda akijifungua
ndipo anaweza kumuuliza tena, lakini wala hakutoka kwenye chumba cha
kujifungulia. Akafa bila kueleza zaidi juu ya baba yangu. Sasa kwa kuwa bado
mama hakuwa namawasiliano mazuri na wazazi wake, au niseme zaidi bibi ambaye
ndiye aliyekuwa mzazi wa pekee aliyekuwa akiwalea kina mama. Bado alikuwa na
hasira na mama, hata baada ya mazishi, bibi alinikataa kabisaa. Hakutaka hata
nirudishwe kule kijijini, nyumbani kwake. Akamwambia mama mkubwa kwa kuwa yeye
alifanya kosa lakumpokea mama, yeye ndio anipeleke kwa baba yangu, sio pale.” Nanaa
akaendelea.
“Anasema
aliponirudisha kule kwa upande wa aliodhania ndio baba yangu, na wao
walinikataa kabisa. Wakamfukuza mama mkubwa akiwa na mimi. Hata hivyo mtoto
wao, yaani yule baba ambaye ni mwanaume aliyekuwa ametajwa na marehemu mama, mwanzoni
wakati mama mkubwa alipoenda na mama akiwa mjamzito, alisema mama alikuwa na
wanaume zaidi yake. Sasa kwa nini achaguliwe yeye kupewa huo mzigo, ambao ni
mimi? Ndio mama mkubwa akakosa nguvu ya kuniacha pale, anasema akahangaika sana
kutafuta mtu anayetaka mtoto wakati ule, akakosa. Akatafuta hata kunipeleka kwenye
vituo vya watoto yatima, akashindwa. Walimwambia kwa wakati ule kituo hicho
kilikuwa kimejaa, na hawana fedha, na mimi sio kwamba ni yatima nisiye na
ndugu. Nipelekwe kwa ndugu zangu.” Geb akashangaa.
“Kwa nini yeye hakuta kukulea mwenyewe!?” Geb akauliza kwa kumuhurumia. Nanaa akanyamaza kidogo, akainama kama kuzuia machozi. “Tokea nazaliwa mpaka leo, mume wake hakuwahi kunipenda. Alihesabu mimi ni mzigo mzito ambao hakutaka kujihusisha nao, na wakati huo na wao walikuwa na mtoto mdogo Viola. Kwa hiyo baada yakushindwa pakunipeleka, ndio nikaishia kwao. Kwa kifupi mpaka hivi leo, hatukuwahi kujua baba yangu ni nani.” Nanaa alitoa tabasamu lililoonyesha limejaa maumivu.
“Pole sana. Sikuwa nikijua kwa undani
hivyo.” “Ndio hivyo. Sasa imekuwa kama ni roho chafu nilizaliwa nayo. Nakuwa
nakataliwa na kila mtu. Kila ninaposhika, hapashikiki. Nimebakiwa na kaka tu.
Inaniingizia hofu ya kuendelea kukaribisha watu karibu yangu. Nimeona hata
nikiwakaribisha kwenye maisha yangu, nawachefua kwa haraka sana.” Geb alimuhurumia asisadiki
anayosema Nanaa. Yeye asingechefukwa kama angebahatika kuwa karibu yake.
Aliwaza Geb.
Kabla hajaongea kitu, wakasikia Geb akiitwa. “Geb!”
Wakashtukia Grace anakuja huku anaita. “Vipi?”
“Mpeleke mwanangu akalale bwana. Danny anazidi kuongea hataki turudi nyumbani.
Mbu watamng’ata.”
Wakasimama. “Mnisamehe
kama nimewakatisha.” “Hamna shida. Hata mimi naona niombe lifti tu kwa Geb.
Nataka nikapumzike.” Nanaa
alijibu kiustarabu tu. Alikuwa kwenye wakati mzuri sana. Geb alionyesha yupo tayari
kumsikiliza. Pole za hapa na pale zilikuwa zikimliwaza Nanaa. Na kufurahia kuwa
karibu yake, asitamani watoke pale.
“Sasa Geb?” Ilibidi Grace amuulize Geb aliyekuwa ni kama
yupo njia panda. Amepokonywa tonge mdomoni, hakujua ajibu nini kwa haraka. Ni
kama alitaka kuendelea kuwepo pale. “Tafadhali
Geb!” Grace
akajaribu kubembeleza. “Hamna neno. Ngoja nikamchukue. Vipi
mama?” “Naona ana kazi yakucheka tu. Si unamjua anavyopenda porojo za Danny?
Sasa wamekutana na James. Zinda ameshalewa! Na wengine ndio wanazidi kuagiza,
naona tutakesha leo.” “Basi namuacha. Nitamshusha Nanaa nyumbani kwao, ndipo
niende nikamlaze Fili. Nimuogeshe kwanza kabla yakumbadilisha nguo?”
Walianza kuondoka kurudi ndani hotelini. “Fanya chochote utakachoweza. Maana
amejaa michanga mpaka kichwani.” “Uzuri akilala huwa haamki, nitamuosha
kidogo.” Walikuwa wametangulia
Grace na Geb, Nanaa akiwafuata nyuma taratibu. Ukweli Grace alivutia
kumwangalia. Nanaa alikubaliana na kaka yake, James.
*************************************
Alimpokea mtoto kutoka kwa shemeji yake, Nanaa akaaga kwa kaka yake, wakaondoka. Njiani kulikuwa na utulivu kidogo. Lakini ukimya huu haukuwa kama ule wa mwanzoni. Grace aliwakatisha mazungumzo yaliyoibua hisia za huzuni katikati yao. Nanaa alijiegemeza vizuri kwenye kiti, akabaki akiangalia nje ya dirisha. Geb alimtupia macho mara kadhaa kama anayetaka kuongea kitu, akajikuta anakwama, hajui aongee nini.
Simu ya kwanza ya Jeff kwa Nanaa.
Akiwa amepotelea mawazoni kwenye gari hilo ambalo
Geb ni dereva, simu yake ikaanza kuita. Nanaa akaingalia kwa muda, akaipokea. “Ni mimi Jeff!”
“Nilihisi tu.” Nanaa akacheka
kidogo. “Vipi?
Ulishatoka kwenye sherehe au nikufuate?” “Asante kwa kujali Jeff. Lakini
nimepata lift. Hapa nipo njiani narudishwa nyumbani.” “Ulikuwa na wakati mzuri
huko?” Jeff aliendelea
kudadisi taratibu. “Siyo mbaya. Nimefurahia.” “Ulikula?” Nanaa akacheka. “Ulikataa kula mchana. Ndio maana
nauliza.” “Hapana Jeff. Sikula. Bado nilihisi tumbo limejaa. Mchana nilikula
chakula kingi. Na mbaya zaidi ilikuwa ugenini. Kila nikifikiria hivi
nilivyoshiba mpaka sasa, nahisi nilitia aibu huko ugenini. Sijui kama wenyeji
wangu walishiba.” Akamsikia
Jeff anacheka na yeye. “Inawezekana una tumbo lenye shukurani tu.” “Haya bwana. Nipe moyo
tu.” Wakatulia kidogo.
“Jeff!” Nanaa akaita. “Nipo Nanaa.” “Nilifikiri umekata.”
“Bila kukuaga?” Nanaa
akacheka. “Siwezi kufanya hivyo.” Geb alikuwa akiwasikiliza maongezi
yao. Lakini alikuwa kimya kabisa. Wala hakuonyesha kama yuko pale. “Asante kwa
kupiga.” Nanaa
akashukuru. “Mbona kama unaniaga?” “Hapana.” Nanaa alijibu kiungwana.
Lakini alijua wazi mazungumzo ya muda mrefu akiwa na Geb pale kwenye geri, sio
ustaarabu. “Unaweza kuendelea kuzungumza?” “Naomba nikupigie kesho.” “Upo
sehemu ambayo huwezi kuongea?” Nanaa akatulia kidogo.
“Unakumbuka nilikwambia nimepewa lift? Sasa tupo njiani ndio
narudishwa nyumbani.” “Oooh! Sawa. Basi nitasubiri simu yako kwa hamu.” “Lakini
unakumbuka nilisema kesho?” Jeff
akacheka. “Sawa Nanaa.” “Muda gani ni mzuri?” Nanaa akauliza tena. “Iwe tu kabla ya lunch. Ili usije
ukashiba sana, ukashindwa kula na mimi dinner.” Nanaa akacheka. “Sawa. Nitafanya hivyo. Usiku mwema.”
“Asante. Na wewe Nanaa.” “Asante.” Akakata simu.
******************************************
Hakuna aliyemuongelesha mwenzake tena pale ndani
ya gari. Hata hivyo walikuwa wamekaribia kufika nyumbani kwa James. Geb
alisogeza gari karibu kabisa na nyumba. “Nashukuru kwa
lifti na kunisikiliza. Samahani kama nilikwambia mambo yasiyokuhusu.” “Hata
kidogo. Na mimi nimefurahia wakati mfupi, tuliokuwa nao.” Nanaa
akacheka. “Sio mfupi hivyo. Nimeongea vyote hivyo!
Mpaka nimeishiwa maneno.” “Mmmh!” Geb alijifanya kama anafikiria. “Nini?” “Sikumbuki kusikia
maelezo ya kutojibiwa ujumbe wangu.” Nanaa alicheka tena.
“Hivyo hatukuongea.” “Basi huwezi kuwa umeishiwa maneno. Bado nasubiri maelezo.” “Lakini si umeshasamehe?” “Mpaka nijue sababu.” “Haya bwana. Muwe na usiku mwema.” Geb alikuwa akimtizama na tabasamu lililomfanya Nanaa azidi kufurahia na kusahau hata kama dunia inazunguka. Kwamba masaa yanasogea. Alitamani kuendelea kuwepo na Geb. Kitu ambacho hakuwahi kusikia kabla, na wala hakuwa tayari. Lakini akajikuta inamtokea “Na wewe pia. Usiku mwema.” Nanaa akashuka akiwa na furaha moyoni. Akasubiri afungue mlango, akaingia ndani bila ya kugeuka nyuma tena, ndipo Geb alipoondoka.
*************************************************
Hakutaka kuharibu ile furaha na chochote. Akaoga
haraka haraka akakimbilia kitandani huku anacheka. “Sasa
nacheka nini?”
Nanaa akajiuliza kwa sauti. “Furaha hii ni
ya Geb!? Mmmh! Acha kabisa Nanaa. Mchumba wa mtu huyo! Labda Jeff. Lakini Jeff
anaonekana muungwana. Mmmh! Ni wale wale. Kuona pipi kwenye karatasi, wanataka
kufungua waonje ladha. Sidhani. Nimpe nafasi nione? Lakini mbona nilipokuwa
naye sijajisikia hali niliyojisikia wakati nipo na Geb? Labda Jeff ndio
amenifanya nianze kujisikia vizuri hata nilipokuwa na Geb nikafurahia kwa
sababu tayari Jeff aliku…” Nanaa
aliendelea kuwaza.
*************************************************
Geb aliondoka pale akielekea kwao njiani akikumbuka dimpozi za Nanaa. Akacheka. “She is nice!” Akasifia moyoni na kucheka. Akakumbuka kicheko kizuri cha Nanaa. Kuna wakati alicheka huku machozi yakimtoka. Pia Geb akavutiwa zaidi. “Well, not only nice but also beu…” Geb akatulia kwanza.
Akakumbuka mazungumzo kati ya Nanaa na Jeff. Akavuta pumzi kwa nguvu. “Lakini hamna kitu. Sina haja yakutilia shaka.” Akajiliwaza. Lakini akakumbuka vile Jeff alivyong’ang’ania na kurudi kuomba namba ya simu. Isitoshe akapiga. Geb akakumbuka ni kama kwenye mazungumzo aliyosikia yakiendelea ndani ya gari, Nanaa aliahidi kupiga kesho yake. “Tena ni kama Jeff amesema kabla ya lunch ili asishindwe kula naye dinner. Sikumsikia Nanaa akikataa. Infact…” Geb aliendelea kuwaza.
Siku ya
Jumapili baada ya birthday ya Fili.
Walimuona Geb anaingiza simu yake mfukoni na
kuitoa kila mara. Mama yake akaona, akanyamaza. Grace naye akaona, mwanzoni
akanyamaza. Alipoona na hasira zinaanza. Hata muda wa kula ukaanza kusogezwa
mbele, Grace akamfuata mama yake chumbani kwake. “Kwani
leo vipi?” “Mimi mwenyewe nimejibiwa majibu mafupi. Nimeona ninyamaze tu, nije
kujituliza kitandani kwangu. Kwani Liz anakuja saa ngapi?” Mama yao akauliza. “Leo jumapili mama. Unajua Liz anatumia siku ya
leo na familia yake. Labda kuwe na dharula.” “Naona inakaribia kuwa dharula.”
Grace akacheka na kuondoka.
*************************************************
“Mbona ni kama alifurahia kuwa na mimi?” Geb alijiuliza. “Au ni mawazo yangu tu? Nini kilichonipelekea kudhani
alifurahia mazungumzo yetu!?” Geb alianza kujisuta. Lakini akakumbuka
vile Nanaa anavyomtizama na kucheka kila alipokuwa naye. “Mmh! Labda nimewaza kwa haraka.
Nilimsikia akicheka hata na Jeff. Kwa asili, Nanaa anapenda kucheka.” Geb alizidi kunyong’onyea kila alipokuwa
akiitazama simu yake na kukosa jumbe za Nanaa. Alitoa sauti kwenye simu yake
ili kama Nanaa akituma ujumbe mtu asijue. Lakini tena akaona aweke tu sauti ili
Nanaa akimtafuta hata kwa kuomba radhi na kutoa maelezo ya kwa nini hakujibu
ujumbe wakujuliwa hali siku ile, asichelewe kujibu. Akabaki anahangaika na simu
yake.
“Tokea enzi za
Frida, tena nikiwa mtoto, mpaka sasa, Nanaa ndio msichana pekee
amenipuuza kwa kiasi hichi! Angejua msafara wa wanawake wanaotaka hata kupata
namba yangu ya simu, hakika angeshukuru hata kupata ujumbe kutoka kwangu.” Geb aliendelea kuwaza.
“Hamna haja yakujiumiza
kichwa. Sina sababu yakusubiria simu yake. Naachana naye kabisa. Siwezi
kujikosesha raha bure. Kwanza ilikuwa nafanya kiuungwana tu. Kwa kuwa aliondoka
akisema hajisikii vizuri nikiwa naye. Kama anaona hamna umuhimu wakuwasiliana
na mimi, basi. Ulazima unaletwa na nini?” Geb aliendelea
kujiuliza, kujifariji, kujitia moyo na kujiwekea mikakati ya kupuuza majibu
kutoka kwa Nanaa. Lakini hakuacha kutupia jicho kwenye simu yake kila mara.
Alikumbuka wakati mfupi aliopata na Nanaa.
Cheka na dimpozi zilizokuwa zikitokea mashavuni kwake. Akakumbuka vile
alivyokuwa akimtizama wakati anacheza na watoto. Akajikuta anacheka peke yake
na kutoa tena simu na kuangalia kama alimtafuta hata kwa salamu. Shauku
yakutaka kumuona tena ikaongezeka.
*************************************************
Nanaa akaamka na kuandaa kifungua kinywa chake na
kaka yake. Kwa kuwa aliona kaka yake bado amelala, akaona aue ndege wawili kwa
jiwe moja. Akatengeneza chapati za kusukuma. Akapasha moto mchuzi wa nyama ya
kuku na njegere vilivyokuwa kwenye friji. Akaweka kwenye hotpots. Alitengeneza
chai nzuri ya tangawizi, hiliki na mdalasini. Akaweka kwenye chupa ya chai,
akampangia kaka yake mezani.
Alirudi kuoga, akabaki amekaa kitandani anajipaka
mafuta huku anawaza na kucheka. “Geb!”
Wazo likamjia. “Natamani
ningempigia. Lakini naanzia wapi!? Heri ningekuwa nimemjibu ujumbe wa kwanza.
Au jana ningemalizana naye juu ya kwa nini sikumjibu ujumbe wake. Pengine leo
ningekuwa huru hata kumuulizia hali. Ningejidai kumuuliza kama walifika
nyumbani salama na mtoto.” Nanaa
akaendelea kuwaza. “Ni kama nimeshakuwa na
hamu naye tayari!” Nanaa akajicheka na kujisuta.
*************************************************
Ujumbe kutoka kwa Jeff ukaingia. “Oooh
Jeff!” Nanaa akakumbuka wakati ameshika simu yake akitaka
kusoma. “Nimemsahau kaka wa watu wakati nilimuahidi
kumpigia. Ngoja nisome.” Nanaa
akafungua ule ujumbe. ‘Uliamka salama?’ Nanaa
akasoma na kubaki hajui kama amjibu au apige tu. “Sipo tayari.”
Akajiambia.
Jeff akapiga, akapokea. “Nimeona umesoma ujumbe wangu.”
Nanaa akacheka. “Ndio nilikua nafikiria nijibu nini?” “Umeshajua?” “Najiona sipo
tayari kutoka, Jeff. Moyo wangu umesita kabisa.” “Kwa nini usije kunisikiliza
tu? Nipe nafasi ya kunisikiliza. Ndipo ukatae.” “Basi naomba isiwe leo.”
“Lini?” “Weekend ijayo. Jumamosi.” “Kweli?” Nanaa akanyamaza huku akiuma meno.
“Nanaa?” “Kweli.” “Usinidanganye.” “Nitakutafuta Jeff.” “Sio
kunitafuta kwa kunipigia simu tu, tunatoka.” “Basi nitakupigia kwa uhakika kama
itawezekana au la.” “Nanaa! Mbona tunaenda mbele na kurudi nyuma!?” “Kwa kuwa
sipo tayari Jeff. Kweli sipo tayari hata kidogo. Sitaki.” “Basi. Naomba
nisikulazimishe.” Alisikika akiongea kwa sauti ya kukata tamaa. “Utakapokuwa
tayari, naomba unikumbuke.” “Sawa, asante.” Nanaa akakata kwa haraka
bila kupoteza muda.
Alimuhurumia, lakini akaamua ajipe nafasi.
Anachojisikia kwa Geb, hakijawahi kutokea kabla maishani mwake. “Sitaki
kujichanganya. Nikaanza huku, kumbe moyo wangu haupo. Hata hivyo sina haraka.
Akitaka kusubiri, anisubiri. Kama hawezi basi.” Nanaa akakubaliana na wazo lake. Akatupa simu
pembeni. Akaendelea na shuguli zake.
*************************************************
Ilipofika mchana Grace akamuhurumia mdogo wake.
Akaamua kumpigia simu Liz ili kumfanya aje hapo nyumbani, amtulize Geb. Asijue
yanayomsibu pacha wake. “Vipi?” “Nipo na familia Grace. Tumetoka kanisani, tumekuja hapa Sea
Cliff, kupata chakula cha mchana.” Liz aliongea sauti yakutotaka
kusumbuliwa. “Ninahamu na Samaki wa kuchomwa!” Grace alipata sababu ya haraka. “Basi nitakununulia. Nikuletee. Lakini
naweza kuchelewa.” “Hamna shida.” Grace akashukuru mtego wake
umefanikiwa.
Kitu kisicho cha kawaida, Geb alirudi chumbani
kulala. “Umekunywa hata uji?” Grace akamuuliza mama yake. “Kanywa kidogo. Anaonekana kuna kitu kinamsumbua.
Vipi huko kazini?” “Kila kitu kipo sawa.” Grace akajibu. “Sasa ni nini?” Mama yake akahoji tena. “Labda ni vile Liz
alivyomuacha jana pale kwenye sherehe ya Fili. Nimezungumza naye, amesema
anakuja.” “Afadhali aje, watu tucheke. Khaa!” Grace akatoka chumbani kwa mama yake.
*************************************************
Ilipofika mida ya saa 9 mchana, Liz akaingia na
samaki wa kuchoma. Danny akampokea na kuanza kula na mkewe pale pale sebleni. “Geb yuko wapi?” Liz akauliza. “Kamwangalie
chumbani kwake, amelala.” Grace alishukuru Mungu. “Naona nimuache tu, nisimsumbue.” “Kwa nini?”
Grace aliuliza kwa mshtuko kwani lengo ni Liz aje pale, amtulize mdogo wake.
Liz akafikiria kidogo. Akamwomba Grace watoke nae nje.
“Kwani vipi?”
“Kwani huko kazini mambo yakoje?” Liz
akauliza swali kama la mama yake. “Kwema tu.
Kwani vipi?” Grace akauliza kutaka kujua zaidi. “Mmmh! Geb amebadilika kidogo. Week hii nzima
nimekuwa nikimbembelezea mapenzi. Ananipa sababu. Sasa jumamosi jana,
akanipigia simu nije. Nikakataa kwa kuwa nimechoka. Lakini akasisitiza nije tu.
Nikaja nikiwa natumaini angalau nitaambulia kitu. Nimeingia kuoga, natoka, Geb
amelala kitu ambacho si kawaida yake. Tumeamka, kabla hata muda wa shuguli
kuanza. Nimemshika, unajua alinikatalia. Akasema hajisikii. Nikambembeleza,
akasema labda kwa kuwa hajala vizuri. Tujaribu baadaye. Tumekuja pale kwenye
shuguli pia ameshindwa kula. Namuuliza mbona hali? Kama unavyomjua Geb, kujibu
anapojisikia. Hakunijibu Grace. Namuaga kuwa nakwenda sehemu usiku ule, hata
kuonyesha kujali wakati mchana wake au week nzima nimekuwa nikimbembelezea
mapenzi. Mtu anayejali si angekuwa na wasiwasi labda nakwenda kwa mwanaume
mwingine? Naona nimuache kidogo.” Grace
akatulia.
“Au
unashaurije?” Liz alimtaka
shoga yake ushauri. Grace akabaki akiwaza kidogo. “Wewe Grace?”
“Si ndio nawaza?” “Sasa unawaza nini wakati ni mdogo wako, unamjua vizuri?” Hilo ndilo lilikuwa tatizo. Grace alimjua
vizuri sana Geb. Akaogopa kumpa ushauri kwa vile anavyomfahamu mdogo wake. “Naona kweli umpe muda. Labda mgonjwa au
uchovu. Au kuna kitu anapanga kichwani, kinashindana na pesa yake. Na Geb
akianza mipango yake mikubwa, kichwa chake huwa akiwi sawa.” “Afadhali
kunituliza. Nilianza kuhisi ananikwepa.”
Grace na yeye alijua hivyo hivyo. Lakini hakutaka yeye ndio amuumize
Liz. Akaona amtulize tu, watajua mbele ya safari.
*************************************************
Uzalendo ukamshinda mtoto wa kike. Akaonelea
aingie tu chumbani kwa Geb. Akamkuta ndio anatoka. Wala hakuonyesha dalili
yakumtaka arudi naye ndani. “Umependeza sana Liz.” Geb akamsifia. “Asante. Jumapili yako ikoje?” “Nimeshinda
kitandani tu.” “Kwema?” Liz
akauliza. “Yeah! Kwema tu. Twende.” “Wapi?”
“Sebleni. Nataka nikale. Sijala.” Liz
akapooza sana. Hakutegemea kuitiwa sebleni na si kitandani. “Leo ni jumapili Geb. Nipo hapa. Chumbani
kwako. Unafikiri nimekuja kuzungumza na kina Grace kweli? Niambie ni nini
kinaendelea Geb.” “Mbona kila kitu kipo sawa tu! Kwa nini unafikiri hivyo?”
“Unanikwepa kimapenzi.” Geb
aliinama na kuanza kumbusu. Alimvutia kitandani akaandelea kumbusu.
Alimbusu kwa muda kisha akamuweka sawa, na
kumuuliza. “Umefurahi sasa?” “Nakutaka zaidi Geb.
Please.” Liz alibembeleza. “Please Geb.” Isivyo ya kawaida, alimuona akivuta pumzi kwa nguvu kama
anayejishauri. Akamvua nguo na kufanya naye mapenzi. Haikuwa kama alivyozoea
Liz, lakini angalau alishukuru. Geb alimfanikishia yeye tu, akaacha.
“Mbona unatoka
kitandani wakati haujamaliza?” “Unakumbuka nilikwambia sijala? Nataka kwenda
kula.” “Kuna kitu nimekuudhi?” Liz akauliza kinyonge. “Hapana Liz. Acha kuwaza hivyo. Ni njaa tu.
Wewe umefurahia?” Liz alitoa tabasamu la kuridhika. “Nashukuru kwa kidogo ulichonipa.” “Utaniua
Liz.” Kidogo
wakacheka. Walizungumza kidogo, angalau ile hali ya wasiwasi kupita kiasi
ikampungua Liz hata na Geb. Wakatoka wote wametulia.
Siku ya Jumatatu yake.
Asubuhi kama kawaida yake, akawahi ofisini.
Kwenye saa mbili na nusu, Grace akaingia na habari za kuwa Fili ameanza shule
rasmi. Akamuonyesha Nanaa picha alizompiga mwanae. Akiwa anatoka nyumbani mpaka
yupo darasani. “Mchumba amependeza.” Nanaa akasifia,
Grace akacheka. “Alikuwa akiimba njia
nzima. Amefurahi kweli.” Wakaongea
kidogo. Grace akarudi ofisini kwake.
Ilipofika mchana, wakati kazi zimechanganya,
Grace akapigiwa simu shuleni kwa kina Fili. Nanaa akashtukia Grace
amemsimamia ofisini kwake, akiwa hana raha. “Vipi?” Nanaa akauliza. “Fili
huyo! Yaani leo ndio ameanza shule, siku ya kwanza, hata masaa saba hayajaisha
tangia awepo hapo shuleni, tayari nimepigiwa simu natakiwa niende.” Nanaa akacheka. “Amefanyaje?” “Sikutaka hata kujua. Naona
niende tu, nitajua huko huko.” “Pole.” “Sitakawia kurudi.” Grace akatoka
kwa haraka ili akajue kinachoendelea huko shuleni kwa mwanae.
Baada ya muda wakarudi. Yeye anacheka, mwanae
analia. “Wamemfanyaje tena?” Nanaa
akauliza kwa wasiwasi. Lakini Grace alishindwa hata kuongea kwa kucheka. “Nyamaza mwanangu, eeh!” Kila Grace alipokuwa akimwangalia Fili alizidi
kucheka. “Njoo Fili mtoto mzuri.” Nanaa alisimama akenda kumchukua akampakata.
Akasikia mlango unafunguliwa bila hodi.
Alikuwa Geb, aliingia huku nayeye anacheka kama
dada yake. “Muone alivyopooza. Kama sio yeye.” Geb aliongea huku cheko limemjaa. Walizidi
kucheka yeye na dada yake wakati Fili analia. “Nimekuletea
ice cream yako na ya Nanaa. Njoo uchukue.” Geb alimwita Fili. Lakini Fili akakataa.
***********************************************
“Kwani analia
nini?” Nanaa akauliza tena.
Hakuwa amepewa jibu tokea wanaingia. Grace na Geb walikuwa wakimcheka Fili. “Si Danny huyo. Kamwambia mtoto ataende shule,
atasoma sana, atapata pesa nyingii, halafu atamlipa anko James, amchukue Nanaa,
aende naye kwake. Sasa mwalimu wake anasema tangia amefika shule, hataki
kucheza wala kuimba, anataka afundishwe kusoma tu. Mwalimu anamwambia sio muda
wakusoma, atoke nje acheze na wenzake, hataki. Kakataa mpaka kula. Sasa mwalimu anasema tangia afike, hajafanya kitu
chochote yeye anasoma tu vitabu. Imefika
mchana wanatakiwa kulala, amekataa anasema apewe hela yake.” Nanaa
nayeye akaanza kucheka akawa ameshaelewa.
Wote wakajikuta wanacheka bila kujizuia, lakini
sio Fili. “Sasa
mwalimu anamuuliza pesa gani? Fili amekazana, dad amemwambia akisoma sana,
atapata pesa nyingi sana, kwa hiyo yeye ameshasoma, anataka apewe pesa nyingi
sana, hataki kulala. Yeye mchana analala na Bibi Fili na usiku analala na Mama
Fili. Hajaenda pale kulala wala kucheza au kula. Yeye ameenda kusoma na kupata
pesa, basi. Kama ni chakula amemwambia yule mwalimu kuwa Bibi Fili anampikia
uji mzuri na dad amemkataza kula kwa watu. Na kama ni michezo yeye anamichezo
mingi sana nyumbani kwao na anachezea timu ya mpira wa kikapu ya anko Geb. Yeye
amekwenda pale kusoma na kupata pesa. Sasa ashasoma, apewe pesa yake nyingi,
aondoke.” Geb na Nanaa walikuwa wakicheka mpaka machozi.
“Hataki kunipa pesa yangu.” Fili alizidi kulia. Geb akaenda kumbemba. “Nyamaza mtoto mzuri.” Geb akaendelea kumbembeleza. “Hivi baba yake yuko njiani. Nimemwambia aje, amuelezee mwanae vizuri, aelewe. Maana yeye ndio ameyataka yote haya.” Grace aliendelea, kidogo wakamsikia Danny ameingia anaongea. “Yuko wapi Dume langu?” “Njoo huku ofisini kwa muhasibu.” Grace alimwita mumewe.
Danny aliingia tu na kuanza kucheka. “Pole mwanangu. Njoo.” Danny alimpokea kutoka kwa Geb, huku anacheka.
“Usilie sasa na wewe. Wanaume huwa hatulii.” Danny akamkoromea mwanae. “Amekataa kunipa pesa nyingi, wakati
mimi nilishasoma sana.” Walizidi kucheka. “Sasa anko Geb ameniambia amekuletea ice cream
yako. Chukua ice cream kutoka kwa anko, halafu twende tukazungumze ofisini
kwangu. Anko James anakusubiri. Anataka tukakueleweshe vizuri kwa vitendo. Una
akili sana Fili, najua utazidi kuelewa. Sawa?” Fili
alitingisha kichwa kukubali.
“Kwa hiyo
unaondoka naye?” Grace
akamuuliza mumewe. “Anavyosubiriwa huko, kama shujaa. Kila
mtu anataka kumuona Fili, Dume langu.” “Hapo atakuwa amesimulia kila mtu. Danny
jamani!” “Dume langu hili. Kwanza anamsikiliza dad wake, pili akiweka malengo
anahakikisha yanatimia, haruhusu vitu vya kijinga viingilie malengo yake.
Wanataka kumdanganya mwanangu kwa uji na michezo wakati kwao vyote vipo!? Sasa
leo lazima upate zawadi. Sawa?” Danny
alitoka akiwa amembeba mtoto wake, huku akijaribu kumtuliza.
Akawaacha wote wanacheka. “Huko
ofisini wataenda kukoma. Wakutane nao hao wawili! Itakuwa ni stori tupu leo,
hawatafanya kazi mpaka muda wakufunga ofisi ufike. Ngoja na mimi nikamalizie
nilichokuwa nafanya.” Grace
alinyanyuka akatoka pale, akamuacha Nanaa na Geb.
****************************************************
Furaha ilimjaa Nanaa, asijue ni nini. “Nimekuletea Ice cream yako. Uliisahau siku ile
ya birthday ya Fili.” Nanaa akacheka. “Nilisahau
hata kama niliagiza Ice cream. Asante. Lakini usingesumbuka kuleta.” “Grace
alinipigia simu akanielezea kisa cha Fili. Akasema wapo njiani na bado analia.
Nikaona nimtulize kwa ice cream, ndio nikaamua nikuchukulie na wewe pamoja na
chakula. Najua hujala.” “Na chakula!?” “Mbona huamini?”
“Sikutegemea. Asante kwa kunifikiria. Nashukuru sana.” Nanaa alifurahi mpaka akatamani kuruka ruka.
*************************************************
Labda hujaelewa. Chakula kimeletwa na Geb!
Wakajikuta hawajui waseme nini tena. Nanaa alijawa na furaha akabaki na tabasamu
usoni huku akiangalia vile vitu alivyoletewa. Kiliwekwa kwenye boksi zuri, lunch box, na kubebwa kwenye
mfuko wa maana. Kwa hiyo akajua ni chakula kilichotolewa kwenye mgahawa
wamaana. Sio kibandani. Inamaana imefanyika juhudi za makusudi, kununuliwa na
kuletwa pale kwake.
*************************************************
“Vipi kazi lakini? Mambo yanaenda?” Akabadili mazungumzo. “Hivyo
hivyo nakazana.” “Taratibu utaelewe tu.” “Naogopa kuharibu nikamuuzi Grace,
akashindwa kunipa kazi nikimaliza shule.” Geb akacheka kidogo. “Basi ndio
ukazane ili usiharibu soko.” “Samahani. Nimefurahi mpaka nimeshindwa
kukupokea!” Geb
akacheka.
“Karibu ukae
hata kidogo. Ule ndio urudi kazini.” Nanaa akampokea kile chakula na
ice cream. Akaweka mezani. “Nina haraka
natakiwa niwahi sehemu. Tutawasiliana.” “Nakushukuru sana. Asante.” Nanaa
alishindwa kujizuia. Alihisi asante pekee haitoshi. Alibaki akichekacheka
nakushukuru. “Nimefurahi. Asante.” Akarudia tena. Geb akacheka na yeye. “Karibu.” Hakika Geb aliona furaha ya Nanaa
usoni. Hakujua kama furaha ile ni ya chakula tu, au alikuwa na furaha yake
tokea mwanzo. Akatabasamu. “Kazi njema.”
Geb akamuaga. “Na wewe pia.” Geb akatoka na kuacha Nanaa anafuraha sana
moyoni, asiamini kama bado Geb alikuwa akifikiria anachokipenda. Alileta aina
ya Ice cream ile ile ya ‘Vanilla’
aliyomwambia anaipenda. Halafu akamletea na chakula! Nanaa alitamani kupiga
mayowe kwa furaha. Alibaki akicheka cheka tu.
*************************************************
Si kwamba Grace hakuona chakula alicholetewa
Nanaa. Aliona na harufu ya kuku wa kuchoma ilienea ofisi nzima. Watu wakaanza
kulalamika kuumizwa pua. Grace mwenyewe akabaki na mshangao. “Geb!”
Grace alikaa ofisini kwake akawaza. “Geb Magesa,
anakwenda kununua chakula na kumletea Nanaa! Mmmmh!” Grace
alifikiria kidogo. Akataka kumpigia simu mama yake ampe umbea. Akaona anyamaze
kwanza mpaka aelewe vizuri. Maana hata yeye mwenyewe hakuwa ameletewa kitu
chochote chakula. “Halafu na mabadiliko Liz aliyoyaona
je!? Inawezekana Nanaa ndio sababu!?” Grace akajiuliza. Akapiga mahesabu ya siku alizokutana Nanaa na
Geb, akagundua ndio muda ambao Liz alimwambia Geb amembadilikia. “Mmmmhhh!” Grace akaguna huku
akimfikiria pacha wake.
*************************************************
Nini
kitaendelea kati ya Nanaa na Geb?
Usikose Sehemu ya 10.
0 comments: