SIMULIZI
Nilipotea! - Sehemu ya 3.
Baada yakumaliza darasa la saba.
K
|
wa
mshituko wa maisha, na yele anayofanyiwa kila wakati bila mama yake hata
kuhisi. Huku akiendelea kutumiwa kwa vile yule baba atakavyo, ndio Tunda
alipotea kabisa kwenye ulimwengu wa masomo. Hata ungemkuta sehemu, ungemkuta
ametulia kama ameduaa. Mambo aliyokuwa akifanyiwa, au kufanya kwa yule baba,
yalianza kuharibu akili yake. Alitamani hata siku moja wafumaniwe, lakini baba
Tom alikuwa na akili ya aina yake. Alihakikisha anawapanga vizuri watu wa
nyumbani kwake, na kuhakikisha hata Tunda mwenyewe hawi na maumivu. Maisha ya
kunywa dawa za maumivu kikawa kitu cha kawaida sana kwa Tunda. Alikuwa akipewa
azinywe, kama pipi.
Tunda alifanya vibaya
kwenye mitihani yake ya darasa la saba
kitu kilichomuudhi sana mama yake. Lakini baba yake wa kambo alimtetea na kumuahidi
yeye mwenyewe atamsomesha shule ya kulipia. Hilo lilimpa moyo mama yake na
kumshukuru sana mumewe aliyekuwa akijisifu kwa mashoga zake, kuwa ni mume
ambaye hana mpango na wanawake wengine ila yeye tu. Na ni kweli, baba Tom
alikuwa mtu wakuwahi kurudi nyumbani sana. Asubuhi alitoka na watoto, na jioni
alirudi nyumbani moja kwa moja bila kupitia hata baa. Utamkuta nyumbani mbele
ya tv akisubiria taarifa ya habari. Hapakuwahi hata kuwa na fununu ya mwanamke
wa nje. Mwanaume wakuheshimiwa sana kwenye jamii. Usingemkuta kwenye mambo
mabaya. Muungwana kwa majirani na mchapakazi kazini. Alitunza familia yake, na
heshima yake iliongezeka hata ukweni kwa kumpokea Tunda na kumtunza bila
malalamiko. Misaada kwa wakweze ikaongezeka, hapakuwa na ubaya kwa baba Tom.
Manda
alimpenda na kumthamini zaidi mumewe kwa moyo wake wa uvumilivu kwake na
heshima aliyomuwekea kwenye jamii. Tokea apate matatizo ya mgongo mara baada ya
kujifungua, mahusiano yao ya kimapenzi kama wanandoa, hayakuwa kama zamani.
Tendo la ndoa ilikuwa mara chache sana. Lakini mumewe hakuwahi kulalamikia
zaidi ya kumfariji akimwambia asiwe na wasiwasi, anaridhishwa na kidogo
anachopewa. Hata hivyo alimpongeza kwa kumzalia watoto hao wawili na juhudi
zake za kusaka pesa.
Kwa
kuwa alikuwepo tu nyumbani akisubiri kwenda kidato cha kwanza, Tunda akageuka
kuwa mlezi mkuu wa mdogo wake, Aneti. Alipewa na aliambiwa afuate masharti yote
ya malezi. Manda alimfundisha kuanzia kumuogesha huyo mtoto, kumlisha, kumbeba
na matunzo yote kwa ujumla. Kazi pekee ya Tunda ikawa mtoto. Na kwa kuwa mama
yake alikuwa mkali sana kwake, wakati wote ungemkuta Tunda na huyo mtoto
akifanya kazi za huyo mtoto tu, tena kwa makini. Kuanzia asubuhi akimka, mama
yake akitoka hapo ndani mpaka usiku huyo mtoto akienda kulala. Msafi muda wote,
na wala usingemkuta nje akicheza au akifanya kazi nyingine. Wakati wote yupo
ndani na mtoto kama yeye ndio mzazi. Na hapo ndipo baba Tom alipopata sababu ya
kumnunulia simu nzuri sana.
“Mbona simu yenyewe ya garama
hivyo!?” Manda alimlalamikia mumewe.
“Huoni anavyomtunza mtoto vizuri?
Anastahili hiyo simu.” “Basi ngoja nibadilishane naye. Nimpe yangu.” “Hapana
bwana. Mwachie mtoto. Tunda anastahili hii simu. Ametulia sana. Muda wote yupo
na mtoto. Aneti ni safi wakati wote. Afya yake nzuri. Ameokoa garama kubwa
ambayo tungemlipa mtu wa kumuhudumia Aneti, na pengine tusingepata huduma nzuri
kama Tunda anayompa mtoto. Hiyo simu itakuwa njia moja wapo yakumtia moyo na
kumuonyesha tunathamini anachokifanya.” Manda hakuwa na jinsi. Mnunuaji
alikuwa ni mumewe. Na mumewe huwa akipanga kitu na kukisimamia, huwa sio mtu
wakubadilika. Ikabidi awe mpole tu. Tunda akaitwa na kukabidhiwa ile simu huku
akipongezwa.
Hiyo
ndio ikawa njia nzuri sana ya mawasiliano kati ya baba Tom na Tunda. Ratiba
haikubadilika sana. Kipindi hicho cha mwanzoni aliporudi kazini, Manda alikuwa
akiingia asubuhi kazini na kuwahi kutoka kwenda kunyonyesha. Lakini kwa kuwa
alikuwa nesi na msafi sana, alijua jinsi yakutunza maziwa yake. Alikamua na
kuyaweka kwenye friji vizuri. Akamfundisha Tunda jinsi ya kupasha moto na kumpa
mtoto. Yeye akawa anatoka asubuhi, nakurudi jioni au usiku. Akitoka kazini,
anapitia kwenye miradi yake ambayo ilisimama kwa miezi michache nyuma,
alipofikisha miezi 8 ya ujauzito na mgongo kuanza kusumbua, daktari alimshauri
apunguze shuguli, kwa hiyo akaacha ufugaji. Aliuza kuku wote. Kuanzia wa mayai
na nyama. Akawa anakwenda kazini tu na kurudi, bila hata biashara mpaka
alipokwenda kujifungua. Aliporudi sasa, ndipo akafufua miradi yote kwa nguvu
zote, na kumuacha Tunda kama mlezi wa katoto hako kachanga.
Tom
yeye aliendelea kwenda shule kama kawaida. Kutoka asubuhi na baba yake,
anashushwa shuleni, baba yake anakwenda kazini mpaka jioni anapokwenda
kumchukua. Dada wa kazi, kazi zake zile zile. Hajihusishi na mtoto. Akimaliza
shuguli zake asubuhi wenye nyumba wakiondoka, anaingia mtaani mpaka mida ya
jioni, anarudi kupika chakula cha usiku na kumsubiria Tom arudi kutoka shule
ampe chakula na kumuhimiza kuoga, na kumuhudumia mama mwenye nyuma wake usiku
anaporudi. Alikuwa na uhuru wote sio kama Tunda aliyekuwa akilea, hawezi kutoka
kwenda popote sababu ya mtoto. Labda siku za jumapili, Manda akiwepo nyumbani,
ndipo Tunda alikwenda kutengeneza nywele, sio katikati ya week. Na hiyo ndio
ikawa nafuu ya baba Tom.
Mawasiliano
kati ya mkewe na Tunda yakawa ya kila wakati. Wakati wote baba Tom alitaka
kujua mkewe yupo wapi na anafanya nini. Simu za mara kwa mara kwa mkewe
akimjulia hali yake hazikuisha. Manda alikuwa akifurahia sana ile hali
yakujaliwa, asijue nia ya mumewe akitaka kujua alipo, ili akapate muda na Tunda
nyumbani. Kila alipojua mkewe yupo kazini muda wa mchana au kwenye miradi yake,
yeye alirudi nyumbani kwa kisingizio cha kumuona mtoto au kupeleka mahitaji ya
mtoto nyumbani. Na hapo pia akajikuta anapata muda mfupi, lakini mzuri na
Tunda. Ili akimbizane vizuri na muda na asichelewe kote kote. Hapo nyumbani na
kazini, alikuwa akimtumia ujumbe Tunda, aandae mazingira mazuri ili akifika
amkute huru. Kama aanze kumbembeleza mtoto mpaka alale, na yeye awe ameoga vizuri,
awe tayari tayari akimngojea. Na akikaribia nyumbani, atampigia tena simu,
amkute chumbani kwake, na ahakikishe mtoto amelala kitandani kwake.
Kwa
kuwa msichana wa kazi na yeye alikuwa mzurulaji, na kama endapo akimkuta hapo
nyumbani, basi anaweza kumtuma kitu cha mtoto ambacho anajua wazi hawezi
kukipata kwenye maduka ya hapo mtaani. Na atamwambia ahakikishe anakipata. Basi
msichana wa kazi atatoka hapo na furaha zote akijua anakwenda kuzurula, na
kumuachia Tunda. Na wala baba Tom hakuhitaji muda mwingi sana na Tunda pale
chumbani. Kwa kuwa alikuwa akimkuta Tunda yupo tayari akimsubiria, kwa hiyo
alifanya naye mapenzi haraka haraka nakutoka kurudi kazini. Na kama akishindwa
mida hiyo ya mchana akiwa na kazi nyingi ofisini kwake, au labda Manda akiwepo
usiku nyumbani, basi atarudi jioni na kisingizio chochote cha maana sana.
Atamchukua Tunda akidai anakwenda kununua mahitaji ya mtoto huyo mchanga ambayo
labda Tunda alimuagiza hajaelewa au ya Tunda mwenyewe. Na huko njiani
alihakikisha anatimiza haja zake kabla hajamrudisha Tunda nyumbani.
Zawadi
za hapa na pale kwa Tunda hazikukoma. Iwe ni mchana anaporudi nyumbani au
jioni. Hakuacha kumletea vitu vizuri kumfurahisha Tunda. Chochote alichotaka
Tunda, aliletewa. Tunda hakuwahi kutoa siri hiyo kwa mtu yeyote. Na baba Tom
alijitahidi sana kuwa makini ili mkewe asiwahi hata kuhisi. Mara zote alimpigia
simu Tunda sio ujumbe ili isijetokea hizo jumbe zinakamatwa. Maisha ya amani na
utulivu yakaendelea ndani ya ile nyumba. Baba Tom akipata anachotaka, bila shida
na bila matatizo, kwa kuwa baada ya muda Tunda akazoea na kuelewa kufanya
mapenzi na baba huyo. Maumivu yaliisha kabisa, basi alifanya jukumu hilo kwa
wepesi bila shida. Amani na vitisho kutoka kwa baba huyo vikakoma. Tunda akawa
binti anayependwa na kusifiwa kila mahali. Akamuanzishia kumpa na pesa zake za
matumizi mbele ya mama yake. Manda hakuona tatizo. Alimwambia zitamsaidia
kwenye matumizi yake madogo madogo. Lakini hizo pesa alizokuwa akipewa mbele ya
mama yake ilikuwa gelesha tu. Wakiwa peke yao, alimpa Tunda pesa zakutosha hata
Tunda mwenyewe hakuwa akijua azifanyie nini zaidi ya kumtuma dada wa kazi,
wajinunulie chips, kuku na kula hapo
ndani kama chakula chao cha mchana, wazazi hao wanapokuwa kazini.
Kwa
kuwa pesa ilikuwepo, akaanza kubadili hata aina ya nywele anazotengenezwa. Kila
ijumaa anapewa pesa nzuri tu ya kubadilisha nywele na kutengeneza kucha.
Jumapili ndio ikawa siku yake ya mapumziko. Anaenda kutengenezwa nywele nzuri,
na kutengeneza kucha za mikono na miguu. Mavazi mengi aliletewa na baba Tom
kama anavyomnunulia Tom na mkewe. Akaanza na
yeye kuletewa pafyume, mafuta na lotion nzuri za kueleweka kama mama
yake. Tunda aliyekuwa amechukua na maumbile ya kwao, urefu, akaanza kujazia
vizuri na kupendeza. Chips, kuku na yai kwa kila siku, huwa haziongopi kwa
yeyote. Lazima unenepe tu. Tunda akawa binti, na ndio kipindi hicho hicho cha
likizo ya darasa la saba ndipo alipovunja ungo. Akaanza kuonekana binti
aliyekomaa vizuri. Ni kweli alikuwa mweusi asiye na swali. Lakini kwa kuwa
alikuwa akitunzwa vizuri, mtoto wa kukaa ndani kwenye geti. Hana shida. Chips
yai na kuku kila siku. Fanta yake kila wakati. Zawadi za hapa na pale. Sifa
kila akimridhisha baba huyo, hapakuwa na sababu ya Tunda kutonawili. Akawa na
ngozi yakuteleza, inang’aa na vile alivyojazia na kutengeneza umbo la kike,
ungependa kumtizama tu.
Sekondari!
A
|
kaanza
kidato chake cha kwanza katika shule nzuri yakulipia ya sekondari, akiwa sio tu
amefeli darasa la saba, ila hajui lolote lile ila kuumba herufi vizuri na
kuongea kingereza kizuri kana kwamba ametokea Britain. Lakini pesa ya baba Tom
iliongea. Tunda akapata nafasi huko kwenye hiyo shule bila kusumbuka au
mtihani.
Ratiba za shule zikaanza tena kwa Tunda ambaye
amebadilika, sio mtoto tena. Akili na mwili vilishakomazwa. Kila kitu cha Tunda
mwilini mwake kilikuwa kizuri na cha thamani. Kuanzia nguo za ndani alizokuwa
akiletewa kila mara tena nzuri na za kisichana, mpaka nguo zake za nje. Baba
Tom zawadi yake kubwa ya mara kwa mara kwa binti huyo ilikuwa chupi, nguo nzuri
za kulalia na mataulo yale mazuri na ya thamani kwa Tunda. Lakini zaidi chupi
alizokuwa akimletea za kila namna. Ilikuwa ni zawadi aliyopendelea kwa kuwa
haikuwa ikionekana kwa urahisi kila avaapo, kwa hiyo hata maswali kwa mama yake
hayakuwepo. Hiyo ndio ikawa ni zawadi aliyozoezwa na baba huyo. Alizijua kwa
majina ya madizaina. Akiwa na umri huo mdogo, Tunda alishajua madizaina mbali
mbali na alikuwa akivaa nguo zao, akijua mtengenezaji ni nani na yupi
anatengeneza nzuri. Kuanzia nguo, mafuta na pafyumu alijua watengenezaji wake.
Ukweli alijitahidi sana kumtunza Tunda, na alihakikisha Tunda anajua
anamuhangaikia. Hakuacha kumwambia ili kuzidi kumleta karibu na kumtawala.
Zaidi kifikira. Akamfanya Tunda kuwa mateka wake kweli kweli.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Sasa
shule zilipoanza, ilibidi kubuni njia nyingi tofauti tofauti za kukutana nje ya
pale nyumbani. Baba Tom akaja na hoja nyingine ya nguvu. Ili kumsaidia
kimasomo, baba huyo alimwambia mkewe Manda, lazima Tunda awe na masomo ya jioni
ya ziada. Akamwambia yeye mwenyewe atamtafutia mwalimu, baada ya kutoka shule,
atampeleka kwa huyo mwalimu, atarudi ofisini kwake, na kumsubiria mpaka amalize
kufundishwa, ili akamchukue na kumrudisha nyumbani. Wazo likazidi kuvutia
zaidi. Manda akakubali bila shida. Kwanza mumewe alionyesha kumchunga sana
Tunda. Alikuwa akimwambia Manda hataki vijana wa mjini wamchezee binti yao,
anataka Tunda atulie. Na kwa kuwa tamaa kwa Tunda iliongezeka, ni kweli
alimchunga Tunda. Hakutaka Tunda awasiliane na mwanaume yeyote yule. Manda
alikuwa akimuona jinsi mumewe anavyomuhoji mambo ya msingi kama binti yake na
kumkaripia akimtaka atulie. Alikuwa akimwambia Tunda mbele ya mama yake, tena
kwa kurudia rudia, kuliko kuwa na tamaa huko nje, ni heri awaambie wao wazazi,
chochote anachotaka, watampa, ilimradi tu atulie asiwe na mambo ya wanaume.
Manda naye alikuwa akiweka msisitizo kila akimsikia mumewe akizungumza na
Tunda, akitaka amsikilize kwa makini baba yake. Tom akaanza kutumia basi la
shule kwa usafiri wa jioni kurudishwa nyumbani. Ratiba za masomo ya ziada kwa
Tunda siku za shule zikashika kasi. Hapakuwa na masomo ya ziada ila mapenzi
matupu.
Baba
huyo akawa anapata nafasi yakutosha na Tunda kila siku jioni. Ofisini wakazoea
kuwa Tunda akitoka shule mara nyingine huwa anakwenda ofisini kwa baba yake
kujisomea. Baba Tom, mtu wakuheshimiwa kazini, alikuwa na wadhifa mkubwa tu
kazini kwake, na alikuwa na ofisi yake na sekretari wake pia. Ilipokuwa ikifika
saa 10 jioni, wafanyakazi wengine wakiondoka pale ofisini, basi ilikuwa kazi ya
Tunda sasa kuingia kazini kumuhudumia baba huyo aliyekuwa dad. Watakaa ofisini
hapo na dad wake, mapazia yameshushwa, mlango umefungwa mpaka aridhike ndipo
wanarudi nyumbani.
Tuition
zikachanganya na kukolea. Ikaongezeka na siku za jumamosi pia. Baba Tom
akaongeza ratiba nyingine ya Tunda ya kutoka pale nyumbani siku za jumamosi saa
nne asubuhi kwa ajili ya kwenda tuition. Lakini lengo kubwa ni kumtoa Tunda
pale nyumbani na kupata naye muda. Siku nyingine za jumamosi, walitoka nje
kidogo ya mji. Baba Toma alijitahidi katika hilo kuwa makini pia. Walitoka mida
tofauti. Wakati mwingine alianza kutoka yeye saa mbili asubuhi, kisha baada ya
masaa mawili mbeleni, anafuata Tunda. Hakuna siku waliyochelewa kurudi. Tena
wakati mwingine, Tunda alifika nyumbani lisaa limoja kabla ya baba Tom kurudi
nyumbani. Baba Tom atapiga simu nyumbani au kwa mkewe kuulizia mahitaji ya hapo
nyumbani. Basi, Tunda atarudi na madaftari, baba Tom atarudi na mahitaji ya
nyumbani.
Ki
ukweli, kwa upande wa baba Tom, masomo haikuwa kipaumbele kabisa kwa Tunda.
Hata walipokuwa wawili na Tunda, hakumuhimiza kabisa mambo ya shule. Kwanza
hata hawakuzungumzia masomo. Yalikuwa mapenzi na kumtaka afikirie juu ya maisha
yao kana kwamba ni mkewe. Alitaka binti huyo kuwa mbunifu kwa wanachokifanya
ili kila wanapokuwa amuongezee furaha. Wakati mwingine wanapokutana huko,
anaanza kwa kumuonyesha picha za ngono, na kumtaka Tunda ajifunze na wajaribu.
Basi na yeye akawa mtu wa shukurani sana kwa Tunda. Alimsifia kwa kila
anachomfanyia. Ilimradi tu, kumfanya Tunda aendelee kuwa chini ya hemaya yake.
Matokeo
mabaya ya hapo sekondari nayo hayakukawia. Tunda ambaye ni kama hakusoma shule
ya msingi, au ni kama aliyeishia darasa la pili la kijijini kwa bibi yake,
akazidi kufeli zaidi na zaidi. Hakuna aliyejua hayo, kwa kuwa baba Tom ndiye
aliyekuwa akifuatilia mambo ya shuleni, na ripoti zote alikuwa akipokea yeye
mwenyewe kama mlipa ada. Hata alipokuwa akiitwa shuleni, kwa ajili ya masomo ya
Tunda, alijuwa kupooza walimu. Ili kupunguza makali shuleni, akazua na ugonjwa.
Akawataarifu shuleni kuwa Tunda anamatatizo kiafya, alizaliwa akiwa na
matatizo. Hata uelewa wake sio kama watoto wengine. Akaomba wamvumilie tu, kwa
kuwa ni mtoto wa kike, basi, wasaidiane kumsukuma tu, amalize hata hicho kidato
cha nne. Hilo likaeleweka, basi akaongeza na siku za kumtoa Tunda katikati ya
masomo ili kumpeleka kwa daktari kwa huo ugonjwa ambao hata Tunda mwenyewe
hakuwa akiweza kutamka jina la huo ugonjwa.
Manda
hakuwa na taarifa zozote juu ya maendeleo ya Tunda. Alibaki akihangaika na
mambo yake na watoto wake. Tunda
aliyekuwa akimlelea mtoto, hakuwepo tena nyumbani. Msichana wake wa kazi ndio
hakuzoea majukumu. Akaanza kuachiwa jukumu la mtoto kwa ahadi ya kuongezewa mshahara!
Hakufurahia wala kuzoea. Yule msichana alikuwa mtu wa kuzurula mtaani na kwa
wanaume zake. Kushinda nyumbani akibembeleza mtoto kama Tunda, ikawa ngumu.
Akaanza kumsumbua sana Manda. Mara mtoto apate maradhi haya au yale kwa uchafu.
Zaidi UTI ugonjwa unaonyesha mtoto hakuwa akisafishwa vizuri au akiachwa na
kinyesi muda mrefu. Aneti akapungua na kubadilika kiafya kwa kukosa matunzo
mazuri. Maradhi ya hapa na pale yakaanza kumlazimu Manda kubaki nyumbani akilea
wakati biashara zake nazo zinamsumbua.
Haya,
Tom naye ikawa shida nyingine kwa Manda. Muda wa kwenda kumpokea Tom kituo cha
basi akitoka shule, ukawa mgumu kwa msicha huyo wa kazi. Tom akawa anashushwa
na basi hilo la shule, lakini hamna mtu wa kumpokea, dada yupo kwa wanaume
akiwa ametoka nyumbani masaa, anadai kwenda dukani. Hilo nalo likawa aghueni
kwa Tom. Asipopokelewa kituoni ili arudishe nyumbani, na yeye anaingia mtaani
kucheza mpira na marafiki zake, mpaka majirani wamvushe barabara wamrudishe
nyumbani, au Manda mwenyewe akiona muda umepita, Tom hajarudi na msichana wa
kazi hajarudi kutoka huko dukani, inabidi ambebe na Aneti, aingie mtaani
akamsake mtoto wake. Ikawa ni shuguli nzito kwa Manda na hao watoto wake
wawili, pamoja ni miradi yake pia. Hakuna jinsi ungemwambia amfuatilie na Tunda
naye, akaweza.
Kwanza hakuona sababu na haikuwa desturi yake
kumfuatilia Tunda. Hawakuwahi kuwa na mahusiano ya kaaribu, halafu akaona
mumewe anammudu huyo Tunda. Alikuwepo nyumbani wakati wote, na akitoka hapo
basi mumewe alijua alipo na siku za shule alihakikisha anarudi naye nyumbani,
hampi mwanya wa kuwa karibu na wanaume. Na vile alivyomuona mumewe anakuwa
mkali kwa Tunda, ndio akaachana kabisa na Tunda, akili zikawa kwa hao watoto
wake wawili tu na miradi yake.
Tunda
na mumewe wakawa na maisha yao tofauti ndani ya nyumba hiyo iliyokuwa imejaa
kelele za Manda na wanae, akihangaishana na wasichana wake wa kazi na miradi.
Yale maisha Tunda akawa ameshayazoea kabisa. Baba Tom hataki Tunda apewe kazi
kabisa, ili atulie na shule, kumbe mapenzi.Ukitaka ugomvi na baba Tom, ni
amkute Tunda anakazi humo ndani. Tunda akawa ni wa kula, kulala na kujifunza
jinsi ya kumfurahisha baba Tom, basi. Akawa hodari kweli kweli kwenye mapenzi
kuliko shuleni.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Tunda kwa mama mzazi, mikononi kwa baba wa kambo akiwa ameshakuwa
mzoefu na faraja yake asiyoweza kuishi bila hiyo. Nini kitaendelea kati ya
mchezo huo unaochezwa kwa makini sana na baba Tom? Tunda alishatamani hata
wafumaniwe, lakini kabla ya kutenda, alizipanga karata zake vizuri sana. Manda
hajawahi hata kuhisi, na Tunda ameshakuwa mzoefu haswa.
Huwa wanasema, ‘Za
mwizi ni arubaini’.
v Je, ni nani atakamwatwa na mfupa?
v Nani atakuwa muhanga wa mchezo wa baba Tom?
v Ni yeye mwenyewe baba Tom, au
ni Tunda, au ni Manda?
v Ni nani ataathirika zaidi?
Endelea kufuatilia….
http://mtazamohalisi.com/
0 comments: