NILIPOTEA! PART 6 - SEHEMU YA ‘E’.
“No nono no no noo Tunda. Tafadhali naomba utulie. Na ujue haitakaa itokee nakuacha wewe au nakusaliti. Kwa sababu nakupenda wewe. Mara ya kwanza tu kukuona, moyo wangu ulifungamanishwa na wewe. Nikakupenda. Nilihamia Tanzania kwa ajili yako Tunda. Naomba uniamini. Hata Papa na Nana wanajua hiyo sio sababu pekee iliyonifanya nimuache Vic. Nilijua hakuna maisha kati yetu. Kwa kufurahia tu utotoni ilikuwa sawa. Lakini nilimuacha hata kabla sijakuona wewe. Mungu ni shahidi. Alivyonisaliti, nilimwambia nimemsamehe lakini hatutakaa tukarudi kuwa wapenzi ila marafiki.” “Na urafiki pia sitaki!” Net akaanza kucheka.
“Usicheke
bwana Net! Tabia gani hiyo ya wanawake zako wananiingilia mpaka chumbani?”
“Hilo ni kosa kubwa sana. Nimemuonya asiwahi kurudia tena. Na ameelewa na
kuomba msamaha. Haitakaa ikatokea tena. Wewe ndio mke wangu mimi.” Tunda
akasimama. “Mbona unaondoka sasa?” “Naomba niache Net. Ulificha habari zake,
leo ndio unataka kuendelea kunikera kwa kuendelea kumzungumzia hapa chumbani
kwetu!” “Acha kukasirika Tunda. Hapakuwa na habari yeyote ya kukwambia mpenzi
wangu. Huoni nilikwambia habari za Chloe sio yeye? Kwa kuwa sio muhimu.” Tunda
akamwangalia kidogo, akaondoka.
“Acha
kunifanyia hivyo bwana Tunda!” Net akasimama akawa anamfuata nyuma wakielekea
kwenye upande wa closet ya Tunda. “Mwenzio nilikuwa kazini lakini nakuwaza
wewe.” “Usinidanganye Net.” “Kweli mpenzi wangu. Ujue nilikuwa nawaza nini?”
“Nini?” Tunda akauliza huku akiendelea kwenda.
“Nilikuwa
najiambia nitarudi kwa mke wangu, anipe pole ya kazi ya week nzima. Anibake,
nikaoge ndio twende kwenye tafrija.” Ilibidi Tunda acheke tu. “Ulivyokazania
kubakwa! Toka siku ile usemi ni huo tu!” “Usinikasirikie bwana Tunda. Mimi na
wewe kitu kimoja.” “Waonye hao unaowaita marafiki zako wasiwe wanaingia huku
ndani.” “Kwanza ameniambia umemfukuza. Ndivyo Vic anavyotakiwa. Mtu ambaye
hamuogopi. Kama hivyo atakuheshimu sana. Lasivyo angekusumbua sana Vic. Mimi
namjua jinsi alivyo mkorofi. Umefanya vizuri.” Tunda hakujibu akaingia kwenye
closet upande wake Net akamfuata.
“Nimekusifia
vyote hivyo Tunda hata kunijibu!” “Kwanza ujue bado nina hasira. Niache.” “Si
ndio nikutulize ili ukitoka hapa uwe umetulia? Sio watu wanatambulishwa mke wa
Net, unakuwa umenuna kama umelazimishwa bwana, wakati unanipenda!” Net
akamsogelea mgongoni akambusu shingoni huku akimtoa taulo. Akiwa vile vile
nyuma yake akawa anampapasa juu mpaka chini huku akimnyonya kuzunguka shingo.
Alipomuona ametulia, akamlaza mkewe palepale kwenye kapeti. Akaanza kumchezea
mpaka akamridhisha mara ya kwanza, akamgeuza, akapata bao moja na yeye.
Wakatulia
pale kwenye kapeti wakiwa wamelala. Net akamgeukia. “Nakupenda Tunda. Wala
haupo hapa kwa bahati mbaya. Sema umekuwa ni kama puzzle ambayo sasa ime fit
kwenye mapengo mengi tu. Umekuwa ni jibu ya maombi ya bibi. Na rafiki wa Maya.”
Tunda akaanza kucheka. “Maya anaakili za kitoto nyinyi!” Net akatingisha kichwa
kama anayemsikitikia mdogo wake.
“Kwani
ulishawahi kumpiga? Mbona anakuogopa sana?” “Ujinga alioufanya zamani ndio
unamsuta. Sijawahi hata kumpiga mimi.” Tunda akacheka kama anayemtafakari. “Hivi unajua wakitoka na Nana kazini
kanakimbilia hapa kitandani. Katalala hapa na habari nyingiii. Akisikia
unasalimiana tu na Carter, kanaruka kukimbilia kwa Nana.” “Najua pia kama huwa
anaogea huku kama sipo.” Tunda akacheka sana.
“Umejuaje
wakati ameniomba nisiwahi kukwambia!?” “Najua. Lakini naona nimuache tu.
Amepoteza marafiki wote. Sasa hivi yuko peke yake ndio maana anashawishika
kurudi kuwatafuta, wakati hawamshauri vizuri. Anapenda sana kuongea. Sasa
akimuona Nana yupo busy na mimi kama unavyonijua. Nina mambo mengi kila wakati,
anaishia shopping na kushawishika kwenda club. Kwa wewe kuwa naye hapa
nakumsikiliza ujinga wake huku ukimshauri, umefanyika msaada kwa wote. Haya,
kwangu ndio kabisa.” Akambusu Tumboni.
“Umekuwa
mke ambaye hata sikukutarajia Tunda. Tumefika tu hapa, nikaanza kukuacha
nyumbani mimi nikahamisha akili kazini kuziba mapengo ya siku nilizokuwa
Tanzania. Natoka asubuhi mpaka jioni sana. Lakini hujawahi kulalamika hata siku
moja zaidi ya kunitia moyo!” Tunda akacheka kidogo.
“Nashukuru
kwa hilo. Lakini ujue mambo yatabadilika. Zipo siku za jumamosi tutakuwepo wote
nyumbani na nitakuwa najitahidi kuchukua likizo tusaidiane mtoto. Sitakuachia
mwenyewe.” “Nashukuru kunifikiria. Lakini nataka ujue kabisa Net, tena bila
unafiki. Niafadhali masaa machache ninayoyapata na wewe, kuliko mengi na wanaume
wengine.” Net alifurahi sana. “Hilo limenifurahisha mno. Asante.” Wakaanza
kupeana mabusu mengine, mchezo ukaendelea palepale sakafuni mpaka akamaliza
roundi ya pili. Ndipo wakaenda kuoga na kutoka.
Tafrija ya kumkaribisha Tunda kwenye jamii.
Net
alikuwa amemshika kiunoni wakati wanatoka. Wakamkuta Nana ni kama anawasubiria.
“Are you okay?” Akamuuliza Tunda kwa wasiwasi kidogo. “She is not Nana! What do
you think?” Hawakujua Maya alipotokea, akaingilia kwa kujibu yeye swali
aliloulizwa Tunda, wote wakamgeukia yeye. Tunda akacheka. Kalikuwa kamependeza
sana. “Si ni kweli Tunda, eeh?”
Kakachochea wakati akiwasogelea, Tunda akacheka tena. “Mimi nipo sawa
Nana. Ila njaa inauma tu!” “Naona wageni wamefika, wapo wanatusubiri sisi.
Twende ukawasalimie ndio tule.” “Na mimi nitapata muda wakuongea?” Maya
akauliza. “Hapana Maya. Wewe utafanya fujo wakati Nana anataka amani.” Net
akajibu badala ya bibi yao.
“Nini
kinakupelekea kufikiria nitafanya fujo!?” Maya akajidai kumuuliza kaka yake
kama anaye shangaa sana na kuona anasingiziwa. Wote wakamgeukia kama kumsuta.
Akaanza kucheka yeye mwenyewe. “Watu wanabadilika jamani!” “Kama umebadilika
anza kwa kufuta video uliyomchukua Vic.” Maya akacheka sana. “Hivi unajua
nilikuwa nataka tu alie? Wala sijamchukua video. Siku hizi nimekua. Sina mambo
ya kitoto.” Akapita katikati yao kuelekea ukumbini.
Nana,
Net na Tunda wakamfuata huku wakicheka. “You look stunning, Maya!” kaka yake
akamsifia kuwa amependeza sana. “So as Tunda, your wife.” Akajibu kwa kujivuna
Maya. Wakacheka. Walipofika mlangoni kama aliyejua chakufanya, akampisha bibi
yake apite. Akaanza kuingia bibi Cote pale ukumbini. Watu waliokuwa wamekaa
sehemu iliyotayarishwa kwa tafrija, wakasimama na kuanza kupiga makofi wakati
bibi Cote anaelekea sehemu maalumu ya kuzungumzia.
Ni
kama waliokuwa wanapeana nafasi ya kuingia hapo ukumbini. Si kwa kufuatana
sana, lakini pia si kwa kuachana sana. Akafuata Maya, akaja Net na mkewe akiwa
amemshika mkewe kwa mkono mmoja nyuma ya kiuno. Makofi yaliongezeka na picha
zikaendelea kupigwa kwa wingi zaidi. Wote waliingia wakipunga mkono kwa wageni
wao na tabasamu usoni.
Bado
baadhi ya watu walikuwa nyuma ya ukumbi huo wamesimama wakiendelea na cocktail.
Familia hiyo iliposimama pale mbele sehemu maalumu ya kuzungumza. Ukumbi mzima
ukatulia kimya na kugeukia mbele kabisa kwenye jukwaa hilo fupi tu ambalo
lilitengenezwa vizuri sana na Tunda mwenyewe alikuwepo.
Tunda
aliweza kuona watu wamaana watupu humo ndani. Wazee kwa vijana walionekana na
heshima zao. Akamsikia bibi Cote akitamka jina la Mayor, akisalimiana naye kwa
sauti ya chini kidogo iliyoweza kusikika na kumpungia yeye mkono, kipekee.
Akashangaa kuwa mpaka Mayor wa hapo ameweza kuhudhuria! Tunda akabaki
akishangaa pale nyuma ya bibi Cote, na Net akiwa kama anampapasa nyuma ya
mgongo, kumtuliza.
“Are
you okay?” Net aliinama sikioni kwake akamuuliza kwa kunong’ona. Tunda akavuta
pumzi kwa nguvu, akatingisha kichwa kwa wasiwasi. Net akacheka kidogo kama
kumtuliza, akambusu kwenye kipanda uso kisha akamnong’oneza tena. “Usiogope.”
“Okay.” Tunda akajibu na kujaribu kutulia.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Ukumbi
mzima ulikuwa umetulia wakati bibi Cote alipoanza kuzungumza. Ni picha tu ndizo
zilizokuwa zikipigwa hapo na video kuchukuliwa. Mapigo ya moyo ya Tunda
yalikuwa yakienda kasi na kujaribu kukumbuka aliyofundishwa na Maya na bibi
Cote wala sio Net. Net yeye alitaka asihangaike kwa lolote. Atulie tu. Ila bibi
Cote alimuandaa vizuri ili asiende kushtukizwa pale mbele ya watu. Alimuandaa
kwa maswali. Alimwambia kwa sababu ni mke wa Net, na ameolewa kwenye huo ukoo,
watu wengi wangetamani kumfahamu na hata wengine kutaka kumuabisha tu kwa
maswali ya kufedhehesha.
Alimwambia
hatastaajabu kusikia maisha yake ya Tanzania yakitajwa pale. Watu wakimuuliza
maswali ya maisha yake aliyoishi. Akamfariji na kumwambia, asionyeshe kushtuka
wala kufedheheka. Ayajibu kwa tahadhari. Anayetaka kumtia aibu kwa swali la
aibu, alijibu kwa kulifanyia na yeye dhihaka. Kwa hiyo Tunda alikuwa amesimama pale akiwa
anajua kinachomkabili mbeleni, kwani aliambiwa na yeye atapata nafasi ya
kusalimia na kuwakaribisha tena pale nyumbani kwao, yeye kama mama Cote.
Bibi
Cote alimtaka aonyeshe sio mgeni na wala hana hofu. Aonyeshe amezoea na ni kama
mwenye amri na ile sehemu. Alianza na Vic. Haikuwa bahati mbaya. Ni shule ya
bibi Cote. Hata alipoambiwa na Maya vile alivyomjibu Vic, bibi Cote alifurahia
sana. Akajikuta akisema, “That’s my girl!” Akashangilia kwa ushindi
kuona Tunda ameweza kufanya kile alichomfundisha.
Hatuba kutoka kwa Bibi Cote
kwa wageni wao.
Mara
baada ya kutulia, bibi Cote alianza kwa
stori fupi iliyowafanya wageni wote wacheke
sana. Alianza hivi, “Kulikuwa na babu kizee chenye umri wa miaka karibia
90. Kilikwenda kwa daktari wake si kwa kuwa alikuwa mgonjwa, ila kutizama tu
afya yake. Daktari akamuuliza, ‘vipi unaendeleaje?’
Yule kizee akajibu kwa kujivuna sana akionekana mwenye furaha na majigambo. ‘Nina mke wa miaka 18, na sasa hivi ni mjamzito. Unafikiri
nitakuwa ninaendeleaje!?’”
Bibi
Cote akaendelea. “Yule daktari akamwambia, ‘Nina habari
moja nataka kukwambia.’ Kizee kikajiweka sawa kusikiliza. ‘Kulikuwa na muwindaji mmoja. Siku moja wakati anakwenda
kuwinda, badala yakuchukua risasi, akabeba mwamvuli. Alipofika porini, akatokewa
na simba. Akafungua mwamvuli wake kwa haraka sana, akajifunika. Chakushangaza,
akaona yule simba ameanguka mbele yake akiwa ameshakufa. Unafikiri nini?’
Daktari akamuuliza yule Kizee.”
“Yule
kizee kwa jazba kabisa, akamjibu, ‘Mjinga kabisa. Si atakuwa
yule simba ameuwawa na mtu mwingine aliyekuwa na risasi! Mwamvuli hauwezi ukaua
simba!’ Yule daktari akasema, ‘Na mimi
nilifikiri hivyo hivyo tokea mara ya kwanza ukinisimulia habari yako.’ Bibi Cote akamalizia kichekesho chake. Wageni
wote pale ndani wakaanza kucheka sana, ndipo bibi Cote alipoendelea na salamu
kwa wageni wake bila hata kutoa ufafanuzi wa kile kichekesho, lakini
walionekana wengi kuelewa.
Kuna
ambao aliwatambua kwa kuwataja kabisa majina na vyeo vyao. Kama huyo Mayor. Kisha
wanapunga mkono kila wakitajwa na bibi huyo na watu kupiga makofi. Sio makofi
ya fujo, kwa ustarabu tu. Kisha akawashukuru wageni wote kwa kufika kwao, ndipo
akaeleza lengo kubwa la kuwaita pale.
“Najua
kilikuwa ni kitendawili kwa watu wengi sana. Si wa nje tu, hata sisi watu wa
familia. Cote alifariki akiwa na shauku ya kuiona siku ya leo. Ambapo tutapata
jibu la fumbo kubwa la nani mke wa Net.” Watu wakapiga makofi. Picha zikazidi
kupigwa. “Sasa sisi tuliokuwepo hapa, Mungu ametupa neema kubwa yakushuhudia
kitendawili hiki kikijibiwa. Leo kwa heshima kubwa sana mbele za Mungu na
kwenu, napenda kuchukua nafasi hii kuwatambulisha kwenu Mama Cote, mke wa
Nathaniel, mwenyewe.” Watu wakapiga sana makofi, Tunda akapunga mkono tu na
tabasamu zuri usoni. Asiamini kama ile heshima kubwa vile anapewa yeye!
“Wamepitia
mengi sana mpaka kuwaona wawili hawa wamesimama hapa mbele yenu. Tena wakiwa
wameshakuwa na jukumu la uzazi.” Watu wakapiga tena makofi kidogo tu,
wakatulia, bibi Cote akaendelea. “Nina
uhakika ni kule tu ambako Mungu alimpitisha Tunda, ndio maana leo ameweza
kusimama hapa pembeni ya Net.” Bibi Cote akaongeza na kuendelea.
“Net
alipohamia kuishi nchini Tanzania akisema anakwenda kutafuta ‘true Love’, kwa kuwa nilikuwa na historia ya baadhi
ya watu wa kule na niliwafahamu, binafsi niliingiwa na hofu. Najua moyo wa Net,
nikajua mwisho wake atakuja kuumizwa tu. Anayo mengi yakusimulia, lakini
nakumbuka hofu yangu. Nikazungumza na Cote akiwa bado hajazidiwa sana.
Akaniambia anamwamini Net. Anaamini vile alivyomkuza na kile alichomjengea
ndani yake. Akaniambia nisiwe na wasiwasi, atakuwa sawa tu.” Watu wakapiga
makofi.
“Ni
miaka zaidi ya 4 sasa hivi imepita, kabla ya kifo cha babu yake, Net akarudi na
jina Tunda tu. Lakini ikawa ni Tunda! Tunda! Na hapakuwa na habari zake zaidi.
Alitafutwa Tunda, maana alimuona tu, akampenda, ila hakuwa amemwambia au
wamepata muda wa kuzungumza. Net alishindwa kabisa kutulia. Nikapatwa na
wasiwasi juu ya huyo Tunda ambaye kwanza hatukuwa tukimfahamu.” Bibi Cote
akaendelea.
“Nikiwa
namwamini Cote, na vile ninavyomfahamu Net, Tunda nilimuona mara ya kwanza
akiwa anachumbiwa na Net, kanisani. Kwamba nilitoa baraka zangu kwa Tunda
ambaye sikuwa nikimfahamu kabisa ila kukubali maamuzi ya Net. Na kile alichoniambia
Cote kuwa, yule atakayeletwa na Net, ndiye anayestahili kuwa mama Cote.” Watu
wakapiga makofi ya kushangilia.
“Na
kweli, nilimkubali Tunda kwa kile alichokisema Net, kabla na baada ya
kumchumbia. Nilipata habari nyingi sana za Tunda. Binafsi nilitishika, lakini
vile alivyokuwa Net, jinsi alivyomtizama Tunda na kumshika, ikaniongezea shauku
ya kutaka kumfahamu huyo Tunda ambaye Net anamuona tofauti na wengine!” Watu
wakacheka kidogo.
“Net
aliniandalia kikao na Tunda, nikapata naye muda mfupi sana ambao naamini kwa
vile mnavyonifahamu mimi.” Tunda akashangaa ukumbi mzima unacheka. “Come on
people! Cut me a slake!” Bibi Cote akalalamika na wageni wakazidi kucheka. Na
yeye akacheka na kuinama huku akicheka zaidi. “Anyway, wengi mnanijua huwa
siwezi kufumbia macho ujinga. Kitu kama ni cheusi, nitasema ni cheusi sio
kimefifia rangi.” Watu wakazidi kucheka. “Huyo ndio mimi. Hata mimi wakati
mwingine natamani ingekuwa tofauti lakini imeshindikana kabisa.” Watu wakazidi
kucheka.
“Anyways!”
Akataka watulie ili aendelee. “Nilipozungumza tu na Tunda, kwa kumuhoji swali
dogo tu, nikasema halleluja!” Bibi Cote akapiga makofi ya shangwe pale
pale mbele ya watu. “Nikasema Mungu amekubali kunipumzisha.” Watu wakapiga
makofi ya shangwe zaidi. “Tunda amekuwa puzzle iliyofit kwa kila mtu kwenye
familia yetu.” Maya akaanza kupiga makofi na kushangilia, mpaka Tunda akacheka.
“Kweli.” Akadakia Maya pale pale akiwa hana hata kipaza sauti. Bibi yake
akacheka huku akimtizama.
Akampisha
kidogo, Maya akasogelea kipaza sauti. “Nimepata dada, rafiki wakunishauri bila
wivu. By the way, ananisikiliza bila kuchoka sio kama Net.” Maya akamalizia
hivyo na kujivuta pembeni kama kumpisha bibi yake, nakufanya watu wote wacheke.
Net akatingisha kichwa huku anacheka taratibu. Tunda akaendelea kucheka. “Yaani
Maya! Umeshindwa kabisa kunyamaza?” Tunda akamvuta kidogo. “Si uliwasikia
walininyima kuongea?” Pale mbele wote wakacheka. Bibi Cote, Net, Tunda na Maya
mwenyewe.
Wakacheka
kidogo wakatulia. Bibi Cote akaendelea. “Amekuwa rafiki wa karibu wa Gino,
Emily na Carter.” Tunda akashangaa Carter, Emily na Gino wanapiga makofi mwisho
kabisa kwenye kona. Hata hakuwa amewaona. Akacheka Tunda huku akiwatizama.
Wageni wengine wakaongeza kupiga makofi.
“Anawajali
na kuwaheshimu kama watu wa muhimu sana kwake. Na hayo nayasikia kutoka kwao
wenyewe. Ms Emily alikuwa akisema, wanajisikia vizuri akiwa nao. Amejawa
heshima kwao, na anawapenda. Tofauti ambavyo walitarajia kutoka kwa mke wa Net!”
Watu wakapiga makofi.
“Kwangu
Tunda amekuwa ni mtoto wa kike ambaye nilikuwa nikimtafuta kwa muda mrefu sana.
Ameshindwa kabisa kuniita Ms Cote kama wengine. Ananiita Nana, kitu ambacho
sikumwambia Tunda mwenyewe, ila kinanifurahisha sana.” Akamgeukia Tunda,
wakacheka. Net akambusu mkewe. “Nafikiri imechukua muda mfupi sana kunizoea na
kunipenda, pamoja na kunijali. Ananisikiliza, na anafurahia kuwa na mimi. Hilo
sio la kufundishwa, au kujitahidi, unaweza kuliona usoni mwake.” Watu wakapiga
makofi.
“Akinisikia
tu nimetoka kazini. Maana siku hizi huwa nawahi kutoka kazini kabla ya mume
wake. Popote nilipo, atanifuata kutaka kujua kama nipo sawa. Siku yangu
ilikuwaje! Ilimradi awe tu karibu na mimi. Amevunja ule ukuta wa ukwe,
amejifanya mtoto kwangu. Najisikia vizuri.” Watu wakapiga tena makofi. “Ni
miezi miwili imefika tokea awepo hapa. Mumewe amekuwa na kazi nyingi mpaka
akanitia wasiwasi, ikabidi kuzungumza na Net. Net akaniambia nisiwe na
wasiwasi, Tunda mwenyewe anamuhurumia kwa majukumu yake, anaelewa na anamtia
moyo kwa anachokifanya.” Watu wakapiga makofi zaidi.
“Najua Net anayo mengi zaidi, lakini kwa machache haya, namshukuru sana Mungu kutuletea Tunda kwenye maisha yetu. Nyumba imekuwa na amani na utulivu kama yeye mwenyewe Tunda alivyo. Mtulivu sana. Naomba tutengeneze mazingira yakumfanya Tunda ajisikie nyumani. Na aweze kuishi hapa vizuri na sisi. Kwa sababu ndiye mama Cote, na wala hatapokelewa mama Cote mwingine.” Maya akaanza kushangilia yeye mwenyewe, ikabidi tu na wageni waalikwa wacheke na kupiga makofi.
Maya Naye atoa yake kwa
Ufupi.
Bibi
yake akamkaribisha Net. Net akasogea huku akicheka na kumtizama Maya. “Unataka
kuongea nini Maya?” Net akamuuliza huku akicheka. Maya akasogea kwa haraka
kwenye kipaza sauti bila yakumjibu kaka yake kama asiyetaka abadili mawazo. Net
akampisha huku wakicheka. “Mimi nataka kusema nampenda sana Tunda. She is
sweet, nice, loving, calm na anapenda wengine pia wapate na wafanikiwe.
Kikubwa..” Watu walishaanza kupiga makofi.
“Kingine
kikubwa.” Maya akataka watulie amalize kwa haraka kabla kaka yake hajachukua
kipaza sauti. “Napenda, japo sijamwambia yeye mwenyewe Tunda. Ila napenda jinsi
anavyo mjali na kumuhudumia Net. Utapenda kumuona vile anavyomuhudumia Net,
anapotoka kazini!” Watu wakapiga makofi.
“Net
anakuwa wakwanza kwenda kazini na mara zote huwa tunamwacha ofisini. Tunda atahakikisha
asubuhi anakuwa na mumewe mezani. Na usiku akisikia tu mume wake amerudi, hata
kama tupo sehemu na Nana, ananyanyuka kwenda kumpokea. Atazungumza naye kidogo. Atampa hata juisi.
Sio kwa kumwita Ms. Emily ndio afanye! No. Anakwenda yeye mwenyewe kuchukua,
anamletea. Ndipo Net anaendelea na kitu kingine na vitu vidogo vidogo vya Net, na
chakula cha usiku pia, anaandaa meza yeye mwenyewe, sio wafanyakazi.” Watu
wakapiga makofi.
“Kwangu
au kwetu ni ngeni. Hatukutegemea kuona hivyo kwa mke wa Net. Tulijua tutaletewa
Diva. Lakini Tunda amekuwa tofauti! Hataki kutumikiwa. Na ukimfanyia kitu
chochote hata kidogo tu, hata kina Ms Emily wanasema. Hatakuonyesha kama unastahili
kumtumikia. Amejawa shukurani sana.” Wakapiga tena makofi.
“Anampenda
Net kama yeye Net, sio kama Nathaniel Cote.” Wakapiga tena makofi. “Binafsi kwa muda mfupi nimeishi naye hapa,
amenibadilisha sana jinsi ninavyoishi na kujihudumia. Nimependa jinsi
anavyofanya mambo yake. Na mimi namwiga bila kumwambia.” Watu wakapiga makofi
nakucheka. Tunda akacheka. “Yaani Maya!”
Tunda akasikika taratibu. “Kingine, amehusika kwenye kunirudisha shule.
Alizungumza na mimi kipindi hicho hata kabla Net hajamchumbia, mpaka nikaona
umuhimu wa kujikana kwa miaka mitatu ili kuweza kupata shahada hii ya masoko.”
Watu wakapiga makofi.
“Na
amenitia moyo na shauku yakujifunza lugha zaidi kama Net. Kwa ajili yake nimeanza
kujifunza kifaransa. Nina zaidi ya mwezi sasa. Najifunza na anakubali
kunisikiliza ninapojifunza kuongea.” Net akatingisha kichwa. “I love her so much. Amekuwa dada ambaye na
mimi kama Nana alivyosema, nilimtamani kwa muda mrefu. Lakini
Net ametuletea. Asante Net.” Akamkumbatia kaka yake na kumbusu. Akaenda
kumbusu na Tunda. “Na mimi nakupenda Maya.” Maya akacheka kwa deko. “Najua sana kama unanipenda.” Akajibu kwa kujivuna
kidogo huku akisogea pembeni namkufanya mpaka bibi yao acheke.
Hatuba ya Nathaniel Cote
Net akarudi kwenye kipaza sauti. “Nana
amezungumza mengi na muhimu sana. Ni kweli haikuwa rahisi kusimama hapa na
Tunda kama inavyoonekana. Tumepitia mengi magumu sana. Nimshukuru Mungu kwa
kutupigania kwa kibinafsi mimi na Tunda.” Watu wakapiga makofi.
“Shukurani
za kipekee kwa my loving, my sweetheart, Nana.” Net akarudi nyuma kidogo
akambusu bibi yake na kumkumbatia kwa muda. Wakamuona anafuta machozi. Akarudi
na kutulia kidogo. Wakamuona akiendelea kufuta machozi. Tunda akasogea pale
alipokuwa amesimama akamshika mkono kama kumtuliza. Net akamwangalia, Tunda
akampa tabasamu. “Thanks.” Akashukuru na kuendelea.
“Kwa
mzazi mwingine yeyote, ninauhakika. Kuletewa mtu kama Tunda kwenye ukoo,
ingesumbua sana. Kungekuwa na maswali mengi. Pengine kunipinga kama wengi wa
watu walivyonichafua mitandaoni juu ya uwamuzi wa mimi kuwa na Tunda.” Kimya. “Lakini
nilipomfuata Nana, na kumwambia nimefikia maamuzi ya kumuoa Tunda, Nana
aliahirisha mkutano uliokuwa ufanyike Germany, akamtuma mwakilishi wake,
akaandaa safari kurudi na mimi nchini Tanzania, kuchumbia.” Watu wakapiga
makofi.
“Nana
alikwenda Tanzania, akitumia ndege yake, ulinzi ambao wote tunajua uligharimu
sana, ili tu kuwa na mimi kwa mwanamke ambaye alishamchunguza, akaambiwa habari
zake, bila swali lolote ila kunikabidhi pete yake ya thamani sana aliyokuwa amevalishwa
na Papa. Akitaka nikamvalishe Tunda.” Watu wakapiga makofi yakushangilia, bibi
Cote alikuwa akitingisha kichwa kukubali.
“Hakuishia
hapo. Hata kipindi nilipokuwa huku, na mke wangu alipokuwa amefungwa. Japokuwa
watu walimkashifu Nana kwa wazi kabisa. Kumwandika vibaya sana magazetini na
mitandaoni kuwa anaua ukoo wa Cote, bado Nana alisimama na sisi. Akinitia moyo
kuwa ni majaribu yetu mimi na Tunda, Mungu atatusaidia tu. Na kweli, alisimama
na sisi bila kukata tamaa wala kunung’unika.” Tunda hakuwa akijua, akajikuta
anamwangalia yule bibi na machozi yakimtoka. Hakujua kama walimchafua hivyo kwa
ajili yake.
“Kutoka
ndani ya moyo wangu, namshukuru sana Nana kwa kuniamini. Amesimama na mimi
pamoja na Tunda, kuhakikisha, leo naweza kulala kitanda kimoja na mke wangu!
Haikuwa rahisi hata kidogo. Asante nana.” Watu wakashangilia. Tunda naye
akamshukuru bibi Cote.
“Pia
napenda kumshukuru sana Maya kwa upendo wake kwa mke wangu. Ni kweli anampenda
mke wangu bila unafiki. Na ninauhakika yeye ndio amefanya maisha ya Tunda pia
kuwa rahisi sana hapa ndani. Asante Maya.” Akamsogelea na kumkumbatia,
akambusu. “You are welcome.” Akajibu Maya.
“Kwa
Gino, Ms. Emily ambaye kwetu ni kama Nana au mama, na kwa Carter. Asanteni sana
kwa upendo wenu kwa mke wangu. Gino asante kwa chakula kizuri kwa Tunda.” Gino
akapunga mkono, watu wakapiga makofi. “Thanks Man!” Akaongeza Net na kuendelea.
“Ms. Emily, asante kwa kutengeneza
mazingira rafiki kwa mke wangu. By the way she likes you.” Ms. Emily akacheka
wakati akipunga mkono. “Kwa Carter! Ambaye nimekuwa akiniona. Amekuwa kama Papa
wa pili kwangu. Asante kwa kumwangalia mke wangu na kuhakikisha yupo salama na furaha
wakati wote.” Tunda akacheka na Carter akawakonyeza.
“Wakati
namuomba Tunda aje kuishi na mimi huku, hakuwa akimjua Nathaniel Cote ambaye
nyinyi mnamfahamu. Alikubali kuja huku akiwa anatamani tuishi naye Tanzania.
Lakini aliniambia hivi, ‘natamani tuishi Tanzania Net. Ndio na mimi kwa mara
ya kwanza nafanikiwa kimaisha. Nimeweza kutengeneza pesa kwa jasho langu na
familia yangu inanitegemea. Lakini najua, sitakuwa na amani kuishi mbali na
wewe’.” Watu wakashangilia kwa kupiga makofi kwa muda mrefu kidogo.
“Wakati
huo Tunda anazungumza na Net, wa kitanzania. Ninayeishi maisha ya kawaida
kabisa. Nilikataa watu wasimwambie Tunda ukweli wa Nathaniel huyu aliyesimama hapa
mbele yenu. Ila mimi kama mimi. Tunda alinichagua mimi kama Net, kitu
nilichokuwa nikikitamani sana.” Watu wakapiga makofi tena. “Tulipokuwa
tukijiandaa kuja huku, akiwa bado ananifahamu kama Net niliyetaka amfahamu kwa
wakati ule, aliniomba kuwa, ni afadhali akose kila kitu, lakini asiwahi
kunikosa mimi kama Net.” Watu walishangilia sana.
“Haikuwa
kama hivyo. Nilifika huku na majukumu mengi mno. Nikaanza kujisuta moyoni,
nakujiuliza nitafanyaje sasa na huyu mke aliyeniomba asinikose?” Watu wakacheka
kidogo. “Ni rahisi kutoa udhuru siku ya kwanza na ya pili au hata juma la
kwanza. Lakini sio mwezi mzima! Kutoka asubuhi kurudi wakati mwingine usiku!
Jumatatu mpaka jumamosi ambapo bado hakuwa na nguvu.”
“Nikaanza
kujisuta mwenyewe moyonu. Lakini Tunda ndio amegeuka kuwa faraja na kunitia
moyo katika ninalofanya. Ametulia nyumbani akinisubiria kwa maandalizi ya
kuniandalia yeye mwenyewe chakula mezani, kama alivyosema Maya.” Watu wakapiga
tena makofi. “Tena akiwa amejawa moyo wakunihurumia na majukumu mazito! Amechukua
majukumu ya Gino ya usiku yakunisubiria mimi ili aniandalie chakula. Na asubuhi
kama napata kifungua kinywa, lazima ataamka awe na mimi mezani. Atakula kitu
kidogo tu, angalau kuwa na mimi pale mezani.” Watu wakapiga tena makofi.
“Ameniambia
kitu ambacho kimeninyanyua na kunifanya nisijutie kumsubiri. Kwa hakika, mimi
mwenyewe najua Tunda ni mke ambaye Mungu amenipa zawadi ambayo najua kwa wengi
hawawezi kukubaliana na mimi. Ni Tunda pekee ndiye anayeweza kuvaa viatu vya
mke wa Net.” Wakapiga makofi sana.
“Sio
kwa miezi miwili aliyoishi hapa ndani tu. Ni kwa miaka yote niliyomfahamu
Tunda. Nafikiri wakati Mungu alipokuwa akimtengeneza Tunda, alikuwa
akinifikiria mimi.” Tunda akainama. “Kitu gani kingine alikwambia?” Mayor
alitupia swali nakuamsha kicheko kwa wote. Net alikuwa ameinama kumbusu Tunda
kichwani akacheka.
“Wakati
namuomba msamaha kwa kutokuwepo hapa nyumbani na yeye kwa muda mrefu, tena sio
akiwa amelala tu. Akizunguka kufanya hili na lile akisaidia mambo ya hapa
ndani. Nikaanza kuweka ahadi zakubadilika. Nakumbuka tulikuwa tumejilaza kwenye
closet yake.” Tunda akamfinya. Net akaruka. Watu wakazidi kucheka.
“Ooooh
Net!” Mmoja akashangaa ile kubwa ya kukejeli. Mwingine akadakia “Man!
Tulikufundisha nini juu ya kuingia kwenye vyumba vya kuvaa wasichana?” Rafiki
zake ndio waliamsha kicheko zaidi pale ukumbini. Tunda aliweza kuwatambua kuwa
ni wale waliofika Tanzania kushuhudia akimchumbia. Watu wakazidi kucheka. Net
alicheka mpaka akageuka nyuma. “Aibu zako.” Tunda akamnong’oneza.
“Anyways.”
Net akageuka akitaka kuendelea. Watu wakatulia huku wakicheka taratibu. “Tunda
alisema ni heri muda mfupi anaopata na mimi, kuliko muda mrefu ambao angepata
na mtu mwingine.” Watu walishangilia sana wakipiga makofi mpaka Tunda mwenyewe
akashangaa. Hakutegemea kumsikia Net anaongelea hilo hapo.
“Kingine,
aliniambia Tunda.” Watu wakatulia na kurudi kukaa. Tunda mwenyewe akapatwa hamu
ya kujua. Akamtizama mumewe. “Kimebaki akilini mwangu na kunitia moyo. Aliniambia
hivi, nitamnukuu.” Akamgeukia Tunda, wakacheka.
“Aliniambia
hivi, tena akiwa ametulia kama kawaida yake nikiwa nimechelewa kutoka kazini.
Najisuta. Akijaribu kunituliza. Akasema, ‘Sijui maisha yatatupeleka wapi,
lakini nimekusudia kufanya kila niwezalo ili kusimama, kukusaidia na kukuunga
mkono katika kila hatua ya maisha yetu, ili kuwa mwanaume ambaye hata babu yako
alikukusudia uwe.’ Huyo ndiye Tunda, niliyekwenda mbali kumtafuta awe mke
wangu.” Watu walizidi kupiga makofi mpaka wakasimama. Na Net naye akawapa
nafasi yakutosha kupiga makofi. Maana hata safari hii bibi yake alipiga sana
makofi.
“Namuomba
Mungu atusaidie. Kwa kuwa sisi bado ni vijana. Tunaanzisha familia huku tukiwa
tuna majukumu mengi! Basi mzidi kutuombea, ili Mungu atujalie kuwa watu aliotukusudia
kwenye jamii yetu.” Hapo napo watu wakapiga makofi.
“Sitawasahau
Troy na Lean kwa kuacha shuguli zenu zote kuja Tanzania kunisindikiza kwenye
kumchumbia Tunda. Kwangu inamaana kubwa sana. Mlisimama na mimi tokea tupo watoto
mpaka Tanzania! Asanteni sana.” Watu wakawapigia makofi Lean na Troy, marafiki
hao watatu, waliotambulika kwa muda mrefu sana.
“Lakini
bado hatujamaliza safari.” Net akaongeza na kumgeukia bibi yake. Akasogea
pembeni kama anayempisha pale kwenye kipaza sauti. Bibi Cote akasogea na
tabasamu kama mwenye habari njema. “Baada
ya jumamosi ijayo. Ile nyingine, kabla ya Tunda kujajifungua, tutakuwa na
harusi ya kanisani ya Tunda na Net.” Bibi Cote akatangaza, watu wakashangilia
sana.
“Kabla ya kuzaliwa kwa ‘Cote Junior Cote, the fifth’.”
Bibi Cote akaongeza na kuamsha shangwe zaidi. Watu wakazidi kushangilia kwa
kupiga makofi kiustarabu huku miluzi ya kina Troy pia ikisikika. “It’s a
boy!” Rasmi, haikuwa bahati mbaya, bibi
Cote akawa ametangaza jinsia na jina la mtoto anayetarajiwa. Picha zilizidi
kupigwa kwa Tunda. Net akambusu mkewe, na kumpapasa tumbo kidogo. Bibi Cote
akarudi nyuma na kumpisha tena Net.
Akarudi
kwenye kipaza sauti. “Yes. It’s a boy! Mtoto wetu wa kwanza wa kiume Mungu
aliyetuzawadia. Sasa kabla hajaja na kumganga mke wangu, na kuchukua nafasi
yangu, nataka nikamlipe fungate aliyokuwa akinidai.” Watu walizidi kushangilia.
“Tunajua unachoenda kufanya Net.” Rafiki zake walipayuka na kuamsha vicheko,
Net aliinama akicheka huku akitingisha kichwa. Watu wakazidi kucheka.
“Kwa
hiyo Troy na Lean, kazi haijaisha.” Akawatuliza Net kwa kuendelea kuongea. “Nitahitaji
msimame na mimi mpaka mkinifikisha mbele za Mungu, siku hiyo ya harusi yetu ya
pili, ndio mtabakiwa na kazi ya kusimama na mimi kuhakikisha nakuwa mume mzuri
kwa Tunda, kama mlivyonisaidia na kusimama na mimi wakati wote.” “Tupo pamoja
Net.” Troy na Lean wakajibu na watu wakapiga tena makofi.
“Asanteni sana.” Net
akawashukuru rafiki zake. Akamgeukia mkewe. “Karibu Tunda, hawa ndio watu wa Norfolks.
Marafiki, majirani na wanajumuia. Jisikie upo nyumbani.” Wakampigia makofi
wakati Net anatoka kwenye kipaza sauti na kumpisha Tunda.
Tunda Mbele ya wakuu!
Tunda
alisogea kwenye kipaza sauti, Maya akaanza kushangilia. Watu wakaanza kucheka
na kupiga makofi. “Maya!” Tunda akaongea kama anamsikitikia. “By the way,
analala na kuoga chumbani kwetu akijua Net hayupo.” Tunda aliongea hivyo
nakufanya watu wacheke sana. “Mimi nilijua ni siri yetu! Come on now!” Maya alilalamika
kwa sauti ya chini iliyosikika na kufanya watu wazidi kucheka. “Huwezi
kutosheka na Tunda. Sio kosa langu. Muulizeni Net.” Maya akaongeza nakufanya
watu wazidi kucheka, angalau hofu ikapungua kwa Tunda.
Palipotulia,
Tunda akataka kuanza, Net akarudi pale mbele kama aliyesahau kitu na kutaka
kuzungumza. Tunda akampisha. “Samahanini kidogo. Kwa leo sitaruhusu maswali kwa
Tunda. Naomba tumpe muda. Naamini mengine yatajijibu kutokana na tutakavyoishi.
Naomba leo iwe kumkaribisha tu. Asanteni sana.” Japokuwa hakuzungumza na bibi
yake, lakini hata bibi yake alipiga makofi kuashiria ameafikiana na hilo, kisha
akampisha Tunda.
“Nawashukuruni
wote kwa kufika hapa. Kwangu sichukulii kitu cha kawaida. Mngeweza kutoa udhuru
tu, kwa kwa hii ni kwa ajili yangu mimi ambaye ni mgeni kabisa kwenu. Lakini
kuwaona hapa, imeninyenyekeza na kuona upendo wenu kwetu. Asanteni sana.”
Wakapiga makofi sana. “We love you Tunda!” Troy akapayuka katikati ya kundi,
Net akacheka na wengine. “Asante Troy.” Tunda akashukuru akimtambua moja kwa
moja kama kumuonyesha anamkumbuka huku akicheka.
“Mimi
sitaongea mengi sana juu yangu, ila shukurani juu ya yale Mungu amenitendea
kwenye maisha yangu. Hakuna hata moja ambalo mnaliona na kulisikia kutoka kwa
wote waliozungumza ambalo nilidhani ninastahili.” Tunda akatulia. “Nilipokuwa
jela, sikutaka kukutana kabisa na Net. Alikuwa akija mara kwa mara akitaka
kuniona. Lakini nilishindwa kabisa kumuona.” “Why?” Mmoja ambaye alionekana
kama mwandishi wa habari, akauliza akitaka kujua ni kwa nini!
“Nilisema
hakuna maswali.” Net akakataa kwa ukali kidogo. Tunda akamgeukia. “It’s okay
babe.” Tunda akamwambia kwa upole tu. “Una uhakika?” Net akataka uhakika,
asijue mkewe amefundwa vizuri sana na bibi yake pamoja na Maya. Hapo alipokuwa Tunda japo ilikuwa mara yake ya
kwanza tokea kuzaliwa kuzungumza mbele ya umati mkubwa vile, tena uliojaa watu
wa maana watupu! Wazungu wa Canada, lakini alikuwa anajua vipi azungumze na asimamaje
pale mbele za watu.
Tunda
akatingisha kichwa kumkubalia mumewe na tabasamu la kumuonyesha yupo sawa kabisa.
Net akaridhia kuwa ajibu hilo swali. Tunda akarudi kwenye kipaza sauti. Akaanza
taratibu tu. “Cha kwanza nilikuwa nimekusudia kulipa gharama ya maamuzi mabaya
niliyokuwa nimechukua kabla yakumpa Yesu maisha yangu. Hiyo nilikusudia kwa
maneno na vitendo. Hata nilipokuwa mahakamani, mshitaki wangu alipojaribu
kutengeneza kisa vizuri, niliomba kumsaidia. Niliona anaongea ambacho na yeye
anasikia kama wengi wenu. Nilikiri kosa langu na kukubali adhabu yangu.” Watu
wakapiga makofi kidogo, Tunda akawakata ili aendelee kuzungumza.
“Nilipokuwa
jela, nilijigundua ni mjamzito. Nikaanza kuugua sana. Sikutaka Net anione
nikiwa kwenye ile hali. Net alimtaka huyu mtoto hata kabla mimba yake
haijatungwa. Nakumbuka siku ananiambia tumtafute huyu mtoto, Net alinimbia kwa kumtaja jina
lake kamili ‘Cote Junior Cote’. Mpaka akaniogopesha!” Watu wakacheka.
“Seriously,
who does that!?” Tunda akauliza na kufanya watu wacheke zaidi. “Mimi najua huwa
watu wanatafuta mtoto. Mimba ikishatungwa na pengine kujulikana jinsia, ndipo
wazazi wanampa jina. Lakini sivyo alivyofanya Net. Alijua anamtaka nani.
Akamuomba Cote kwa Mungu.” Tunda akacheka kidogo. “Natamani ningerikodi yale
maombi ya Net usiku ule wakati akimuomba Cote kwa Mungu. Yaani aliomba kama
vile alikuwa akimuona Cote yupo sehemu, ndipo akamsihi Mungu amlete kwetu,
akimwambia Mungu sisi tupo tayari kumpokea Cote. Yaani kwa kumtaja kwa jina,
kuwa ndiye anayemtaka aje kwanza. Hakika nilifungua macho wakati anaomba
nikamtiza.” Watu wakazidi kucheka.
“Na
baada ya hayo maombi, hakutaka kufungua mlango wa mashaka hata kwangu mimi
mwenyewe. Akabakia na mazungumzo ya jinsi tutakavyompokea na kumlea Cote, kama
kaka ya wengine Mungu atakao tubariki baada ya Cote, tena akisema kama mimi
nitataka wengine.” Watu wakapiga makofi huku wakicheka.
“Sasa
nilijua kama akijua nipo jela na mtoto wake, wote. Yaani mimi na yeye Net,
tungeshindwa kufanya kazi. Nilijua angechanganyikiwa asijue chakufanya na
angenikatisha tamaa yakuweza kutumikia adhabu yangu.” Watu wakapiga makofi. “Hata
alipotuma wakili wakuja kunitetea, pia nilikataa kumuona. Niliamini nimetubu
kutoka moyoni, na Mungu alinisamehe dhambi zangu zote. Lakini siwezi kukwepa
kulipa gharama ya makosa yangu. Nilijua lazima mimi mwenyewe nikubali kulipa.”
Watu walishangilia sana mpaka wakasimama tena. Tunda akainama.
Walipotulia
akaendelea. “Kingine, nilikuwa nikimpa muda Net ili afikirie zaidi ni nini
anataka na kama kweli anajua mtu anayetaka kujihusisha naye. Nilijua ananijua
sio kwa kusimuliwa au kusikia mitandaoni. Yeye ndiye mtu pekee anayenifahamu
vizuri. Net ananijua kuliko mtu yeyote hapa duniani. Zaidi hata ya mama yangu
mzazi. Lakini nilitaka apate muda wakufikiria bila kusongwa. Kumfikiria Tunda kama
Tunda ambaye yupo kifungoni. Tena kwa kosa la fedheha! Nilitaka kumpa muda
wakutosha bila kumshawishi kwa kuona nimebeba mtoto wake. Sikutaka anichague
sababu nimebeba mtoto wake au kwa sababu nitakuwa mama wa mtoto wake! Hapana.”
Watu walishangilia sana, wakasimama tena kama kuonyesha heshima kwa kile alicho
zungumza.
Tunda
akaendelea baada ya kutulia. “Tulikutana wote, mimi na Net, tunatafuta mapenzi
ya kweli. Yeye akitaka mtu ampende kama yeye bila kujua historia yake ya
maisha. Na mimi nilitaka mtu atakayenipenda kama mimi Tunda, akiwa anaijua
historia yangu ya nyuma. Lakini bado anichague mimi kama Tunda.” Watu napo hapo
wakapiga makofi.
“Kwa
miezi 6. Kila mwezi Net alikuwa akija jela akitaka kuniona bila mafanikio.
Hakuchoka wala kukata tamaa mpaka nilipotoka.
Nilimkuta Net akinisubiri nje ya gereza.” Tunda akaina na kujifuta
machozi. Watu wakapiga makofi. Net akamsogelea. Akampapasa mgongoni na kumbusu
akatulia.
“Napo
hapo pia sio kwamba nilimkimbilia! Hapana. Nilikimbilia hotelini kwenda
kupumzika. Nilitoka nikiwa mgonjwa sana. Sikuwa na nguvu na yeyote na chochote.
Nilikwenda hospitalini. Nikarudi hotelini kujiuguza. Sikuwa nikijua kama bado
Net ananisubiri. Akiwa hajui nilipo, wala hatuna mawasiliano, Net alinisubiri
mpaka tulipokutana tena.” Tunda akatulia kidogo kama anayefikiria kitu.
Kisha
akaendelea. “Alichonishangaza mpaka leo. Kwa historia niliyokuwa nayo, halafu
nikafungwa jela kwa kosa hilohilo, eti natoka jela nikiwa mjamzito. Nikampotea
kwa majuma mawili nimejifungia asipopajua, bado Net
aliamini mtoto ni wake bila hata mimi mwenyewe kumwambia kama ni mimba yake!” Hapo Tunda
akalia kidogo. Watu wakapiga makofi tena kwa muda mrefu kidogo kama kumpa
nafasi atulie.
“Mazingira
aliyonikuta kwa mara nyingine tena baada ya kumpotea nilipotoka jela, ilikuwa ni
eneo nililokwenda kufanya kazi. Baada yakupona, nikaamua kurudi kutafuta kazi
ili kuweza kumtunza mtoto. Sikujua kama Net atampokea mtoto au kama tutaendelea
na mahusiano. Kwanza hata sikujua kama bado yupo nchini Tanzania ananitafuta
mimi! Niliamka asubuhi sana kwenda kazini, kumbe yule aliyekuwa amenipa kazi
alimtaarifu Net kuwa nimemuomba kazi na nitakuwa kazini muda huo.”
“Net
alipofika tu, akaomba amsalimie mtoto. Nikiwa kwenye mshangao, akapiga magoti
na kumsalimia mtoto. Akajitambulisha kwa mtoto kama yeye ndio baba yake na
akamwambia mtoto kuwa anasikitika hawakuwa pamoja kwa muda wote huo, ila akamuahidi
atafanya kila awezalo ili waweze kuwa wakipata muda wa pamoja!” Watu
wakashangilia sana.
“Ile
imani aliyokuwa nayo kwangu na kwa Mungu akiamini Mungu anaweza kumbadilisha
mtu! Na jinsi anavyonipenda Net! Na kunithamini! Kwanza jinsi anavyonitizama
tu, najua ananipenda.” Watu wakapiga makofi.
“Umeshawahi
kwenda kwenye mgahawa mzuri sana! Ukiwa na njaa. Ukaagiza chakula ulichodhani unakihitaji
na kitakuridhisha nafsi yako! Ukala, lakini bado ukahisi kuna kitu
hakijakamilika? Sijui kama imeshawahi kuwatokea nyinyi?” Tunda akauliza na kuendelea.
“Halafu ukiwa kwenye ile hali ya kutoridhika, anakuja muhudumu aliyekuwa
akikuhudumia. Unamueleza kile unachopitia kwa wakati ule baada ya kula kile
chakula alichokuletea pengine na kinywaji. Unaweka msisitizo kwake kuwa, japo
alileta kitu sahihi, na pengine akakuhudumia vizuri tu, lakini kuna kitu hakija
kamilika!” Tunda aliongea kwa hisia zote. Kila mtu alitulia kumsikiliza.
“Pengine
muhudumu anaweza kukupa pendekezo lakumalizia na desert. Labda ya cake. Unaomba
kuona menu za hizo cake. Unaangalia mwanzo mpaka mwisho. Unachagua velvet cake.
Ukidhani itakidhi ile haja yako unayoisikia kwa wakati ule. Inaletwa.” Akatulia
kidogo. Ukumbi mzima ulikuwa umetulia kabisa kumsikiliza huyo Tunda ambaye
amevikwa heshima ambayo hakutarajia.
“Unapokula
ile keki na kuifurahia. Sio kwamba uliiagiza kwa kutaja majina yote ya
ingredients zilizochanganywa mpaka ikatokea ile keki! Mtakubaliana na mimi
hapana. Nina uhakika hutamwambia muhudumu niletee sukari, iliyochanganywa na
maziwa, mayai, vanila, butter na kadhalika.” Watu wakacheka sana.
“Hapana.
Utaomba tu velvet cake. Ila mpishi aliyetengeneza ile keki, tokea mwanzo alijua
achanganye nini mpaka kitokee kitu kizuri kitakachomfurahisha mlaji
kitakachoitwa velvet cake. Ndivyo ilivyokuwa kwa Net, wakati Mungu ananikabidhi
mume.” Watu wakashangilia sana.
Tunda
akaendelea. “Amekuja na kila kitu ambacho Mungu anajua nahitaji. Wapo waliosema
nimempendea pesa.” Watu wakacheka. “Najua ni wengi walisema, wanasema na
kufikiri hivyo. Lakini Mungu alijua nahitaji pesa ndio maana akanipa Net.
Sitaomba msamaha wala kujitetea kwa hilo.” Watu walicheka sana na kupiga
makofi.
“Sitaona
haya wala sitajivunga kuwa sijafurahia kukutana na Net huyu ambaye sikujua kama
yuko hivi. Nilimwambia Nana, bila kumdanganya. Sijui kama anakumbuka?” Tunda
akamgeukia. Nana akasogea. “Ngoja nimsaidie.” Watu wakacheka. Bibi Cote
akaanza. “Aliniambia hivi, mara ya kwanza nazungumza naye, wakati nikiwakilisha
malalamishi ya wengi, kuwa anampendea Net pesa. Nilimwambia anitajie pesa
yoyote anayotaka nitamlipa, ili tu amuache Net kama anampendea Net pesa. Tunda
akaniambia mengi lakini akiwa ametulia. Nitafupisha.”
“Aliniambia,
‘Nimeteseka sana na maisha kufika hapa nilipo. Sitakudanganya kukwambia eti
nipo tayari kuolewa na mwanaume masikini. Hapana. Isipokuwa Net.’” Watu
wakashangilia sana. “Subirini kidogo. Aliendelea akasema ni kwa Net tu, ndiye
yupo tayari kumuweka ndani na kumlisha hata kumtunza kama hana pesa. Lakini sio
mwanaume mwingine yeyote yule. Na aliniambia wazi ni kwa ule umbali ambao Net
amefika naye.” Watu walipiga makofi kwa kushangilia mpaka wakasimama tena huku
wakicheka.
Tunda
naye alikuwa akicheka vile bibi Cote alivyokuwa akimnukuu kwa kumwigiza mpaka sauti.
“Nana!” Tunda akaendelea kucheka huku akimtizama bibi Cote, asiamini vile
alivyompatia sauti yake. Mpaka Net alikuwa akicheka huku wakimtizama bibi Cote,
hata yeye asiamini kama ni yeye! Akamaliza kumwigiza Tunda, akaondoka pale
mbele, Tunda akarudi huku akicheka. “Siamini Nana!” Bibi Cote na yeye akaanza
kucheka.
“Anyway,
sasa kuja kuona Net yule ndiye huyu! Kwa kweli ninafuraha na wala sitajivunga au
kujitetea kwa hilo.” Watu wakaanza kucheka tena. “Nampenda mume wangu. Nimeamua
kusimama na yeye kwa kila hatua ya maisha yetu. Jua litoke, mvua inyeshe,
nitakuwa na Net kama Net wangu niliyekabidhiwa na Mungu wangu kwa upendo mkubwa
sana.” Hapo watu wengi walishangilia sana.
Bibi
Cote mwenyewe hakutegemea. Akamsogelea na kumbusu. “Thank you, baby girl.” Bibi
Cote akambusu tena. Na Net mwenyewe ikamgusa sana. “Asante Tunda. Nakushukuru.”
Net akajikuta akiongea kwa kiswahi pale pale mbele ya watu. Akamkumbatia. “Nakupenda Net.” “Na mimi nakupenda.”
Wakaanza kupeana mabusu palepale, watu wakishangilia.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Kwa
Tunda kutoa ahadi nzito vile mbele ya umati kwa familia hiyo iliyokuwa
ikiwindwa na wao wakihofia kupata mkwe ambaye ataingia pale kwa ajili ya
kujinufaisha tu! Aolewe na kuomba talaka ili apewe nusu ya mali iliyotafutwa
kwa jasho sana na kina Cote. Ilimgusa sana kila mtu kwenye familia hiyo.
Kuona Tunda ametangaza
mpaka kifo! Tena huyo bibi alimuonya Tunda kwa kumsisitizia kuwa, asije akazungumza
jambo lolote siku hiyo mbele ya watu kwa kuwa hata baada yamiaka 20 anaweza
kuja kukutana na maneno yake. Alimwambia hiyo tafrija itarushwa hewani live. Alimwambia macho ya wengi ulimwenguni, wenye
vyeo vyao na mashabiki tu, watakuwa wakifuatilia hiyo tafrija kuanzia mwanzo
mpaka mwisho.
Aliweka
msisitizo kwa Tunda kuwa ni tafrija ambayo itakuwepo kwenye vyombo vya habari
vingi sana ndani na nje ya nchini. Zaidi alimtahadharisha kwa kumwambia kila
litakalozungumzwa hapo, litajadiliwa kwa muda mrefu sana mitandaoni, magazetini
na hata maredioni. Kwa hiyo akamwambia kila neno hapo ni kumbu kumbu ambayo
itatunzwa hata kuja kuonyeshwa mkwe wa huyo mtoto aliyembeba hapo tumboni. Kwa
hiyo asiropoke, wala kuongea neno ambalo hamaanishi.
Kwa
kitendo cha kutamka hapo hadharani, bibi Cote alijua ni ahadi ya ukweli. Si kwa
mumewe tu. Hata kwake na kwa familia nzima. Kuwa yupo pale na wao, na hana
mpango wa kuondoka. Iliwagusa sana.
**************************
“Mwisho
kabisa.” Watu wakatulia na kuendelea kumsikiliza. “Nilipokuwa nakuja huku, baba
yangu alikuwa na wasiwasi sana na wenyeji wangu. Kama watanipokea kwa jinsi
nilivyo. Lakini nimejikuta nimepata familia ambayo hata sikuwahi kuwa nayo.
Sijawahi kuishi kwenye familia kama hii.” Wakapiga makofi wakijua kitakacho fuata
ni sifa kwa familia hiyo maana ulikuwa usiku wakuongea mazuri tu. “Na
ninaposema familia ni kila mmoja niliyemkuta ndani ya hii nyumba. Wamegusa
maisha yangu kipekee sana. Naomba nianze kwa kumshukuru Gino, ambaye amefanya
maisha yangu kuwa rahisi kwa kunisaidia kula ninachopenda kama nyumbani. Asante
Gino.” Wakapiga makofi.
“By
the way, sijawahi kuona mpishi anayeweza kupika vizuri, tena chakula cha asili.
Kwa kutajiwa tu. Tena akaweza kukitoa mpaka ladha ya asili, iliyo sahihi kama
Gino! Hongera sana Gino. You are the best.” Gino akapunga mkono. Watu wote
mpaka familia ya Cote, wakaongeza kumpigia makofi.
Kwa
Gino ilikuwa kitu kikubwa sana. Inamaana usiku huo jina lake na sifa zake
zilivuma na kusikika na wengi sana. Wenye nacho na wasio nacho wanaofuatilia
hilo tukio na watakaoendelea kufuatilia hilo tukio. Akafurahia sana.
“Ms.
Emily!” Tunda akaendelea. “Amekuwa rafiki wa karibu. Ananifundisha mengi ya
hapa ndani na kuniandaa kuja kuwa mama mzuri na mke bora kwa mwanaume kama Net ambaye
amekua akimuona tokea mdogo mpaka sasa. Anaupendo mkubwa sana kwangu. Asante
Ms. Emily.” Wakapiga makofi. Ms Emily akapunga mkono.
“Babu
Carter.” Carter akacheka. “By the way babu is swahili word for grandpa. Kwa
hiyo nimempa Carter jina la babu.” Wakapiga makofi. “Asante kwa kila kitu.
Kunipokea na kuhakikisha nipo sawa kila wakati. Namaanisha kila wakati. Hata
nikizidisha muda wa kulala, kwake ataingiwa na wasiwasi. Nisipokula vizuri au
kwa wakati wake yeye, kwake hatalifurahia. Anataka kuniona nina furaha na nipo
salama wakati wote.” Watu wakacheka. “Thanks
Carter.” Net naye akaongeza.
“Nana!
Akamgeukia. Wewe nikushukuru kwa kunipokea jinsi nilivyo na kuniweka karibu
yako na kuniamini na kila kitu.” Wakapiga sana makofi. “Umekuwa kama Net kwangu.
Kutoa ndani yangu yale ambayo hata sikujua kama yapo! Unanijali sana na
umeniweka karibu yako kama mtoto wako kabisa! Asante sana.” “Karibu Tunda.”
Akajibu bibi Cote wakati watu wakipiga makofi.
“Maya!”
Tunda mwenyewe akaanza kucheka. Wengine nao wakacheka mpaka Maya. “Namuhesabu
kama mdogo ambaye alizaliwa akafichwa ndio tumekutana. Alinipenda siku ya
kwanza tu aliponiona nikiwa hata sijaanza mahusiano na Net. Mpaka leo,
amekuwa..” Tunda akacheka tena. “Huwa Net akiondoka tu, nahesabu dakika ambazo
ataingia chumbani kwetu. Hana asubuhi wala usiku, uchangamfu wake upo vilevile.
Ananifuata mpaka chooni!” Watu wakacheka.
“Ni
mtu ambaye unatamani atoke kazini arudi nyumbani au asubuhi asiende kazini bila
kukupitia kukuaga.” “See Net! Tunda mwenyewe ndiye anayetaka nije chumbani
kwenu kila wakati!” Wakacheka. “Anyways, najihesabu kubarikiwa kuwa na wewe
Maya. Nakupenda sana na ninakuombea kila siku ili hiyo furaha idumu siku zote.
Asanteni sana. Na karibuni.” Watu wakapiga makofi na kusimama wakati Tunda
anatoka kwenye kipaza sauti.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Bibi
Cote akasogea pale mbele kwenye kipaza sauti. “My My My!” Akasema bibi Cote kama anayestaajabu, watu
wakazidi kupiga makofi bado wakiwa wamesimama. “Seriously! Si mmemsikia
wenyewe? Natamani ningekuwa hata nimewekeza hata wazo ili leo nijisifie, lakini
!” Watu wakaanza kucheka.
“Anyways,
huyo ndio mke wa Nathaniel Cote. Na sisi tuliletewa kama hivyo nyinyi.
Tukamkubali na kumpa nafasi. Namaanisha wote waliokubali kumpa nafasi kwenye
hii nyumba, sasa hivi tunamfurahia. She is special!” Wakapiga makofi.
Ukanyoshwa
mkono kutoka katikati ya wageni wao. “Najua swali lako.” Akasema hivyo bibi
Cote na kuamsha kicheko. Mwenye pesa akiongea chochote, kila mtu anacheka. “Jibu
ni NDIYO. Kile mlichokisikia nikikitamka nchini Tanzania, ni kweli. Nahisi,
narudia tena, nafikiri, hata kama Net asingemleta Tunda kama mkewe, na
nikakutana na Tunda, bado naamini ndiye angekuwa mtu badala yangu.” Watu
walishangilia sana.
Tunda
akaona watu wakimchukua video na picha zaidi. “Zipo sababu au sifa nyingi sana
nilizokuwa nikizitafuta kwa mtu atakayefanya majukumu yangu, Tunda anazo hizo
sifa kwa asilimia 90, japo yeye mwenyewe hakuwa akijua kama yeye ni mtu
sahihi.” Watu wakapiga sana makofi na kusimama tena.
“Nitakuja
kueleza hilo wakati mwingine, kama Mungu akitupa uzima. Lakini leo nitazungumza
kwa kifupi tu kukuthibitishia kuwa sikukosea kwa Tunda.” Watu wakarudi kukaa
ili kusikiliza. “Alikuja akiwa dhaifu. Daktari akashauri apumzike kabisa na
kumtenga na watu ili kuepusha maamumbukizi yeyote kwake nakumfanya aumwe.
Daktari alisema hakuna mwanya hata mdogo wa Tunda kuumwa chochote kile. Hata
mafua! Lazima wote tumlinde.” Akaendelea.
“Aliendelea
na matibabu mpaka daktari akaridhika kuwa anaweza kutoka sasa, ndipo nikampeleka
kule kwenye kituo. Alipokwenda mara ya kwanza, akataka turudi naye tena. Nikamrudisha
tena bila yakumuuliza ni kwa nini ametaka nimrudishe. Huwa tunamuacha hapa wakati tunakwenda kazini.
Siku hiyo nikiwa kazini, nikapata taarifa kuwa yupo yeye mwenyewe kwenye kile
kituo, bila hata mimi kuniambia. Nikapata hamu yakujua ni kwa nini yupo pale!
Kipi kilimrudisha mara ya pili na hiyo ya tatu akiwa peke yake! Nikaamua
kumuacha kabisa, ila nikawaambia apewe ushirikiano kwa chochote kile.” Ukumbi
wote kimya.
“Kuna
mama na binti zake walikuwa wageni kabisa pale kituoni. Binti mkubwa alishindwa
kabisa kutulia pale na alikuwa akimsumbua sana mama yake na wafanyakazi wa pale.
Kumbe Tunda aliwaona mara ya kwanza kabisa nilipompeleka. Mimi hata sikujua
kama kile kitu kilimgusa Tunda. Maana tulifika pale kiongozi wao akawa
anatuelezea kwa kutulalamikia juu ya huyo binti kwenye familia hiyo ngeni. Tukazungumza
na kuondoka bila Tunda kuongea chochote.”
“Kumbe
Tunda akaamua kumfuatilia yule binti. Akaanza na yule binti taratibu tu. Kimya
kimya. Mpaka akaweza kufikia moyo wa yule binti. Nimeambiwa amebadilika kabisa.
Alianza kwa kuomba msamaha wafanyakazi wote wa pale kituoni. Ametulia na
ameanza kusaidiwa na wataalamu wa afya.” Watu wote wakasimama na kupiga makofi.
“Huwa
naamini sana hisia zangu.” Yule bibi akajisifia. Watu wakacheka. “Let me have
it!” Akaongeza nakufanya watu wazidi kucheka. “Sikumtuma Tunda. Nilichofanya
siku ya kwanza nikumtambulisha kwa wafanyakazi niliowakuta pale siku ile, na
ile kuwaambia wampe ushirikiano ambao hata hakuhitaji, basi. Lakini Tunda alirudi
yeye mwenyewe. Akiwa amepanga yeye mwenyewe na Carter kumtafutia usafiri wa
kumpeleka pale, basi. Alirudi kule bila kutaka mitandao ijue kama wengi wetu.” Watu
wakacheka sana.
“Wala
hakujitangaza popote. Akarudi nyumbani na maisha yake yakaendelea kimya kimya
kama yeye mwenyewe alivyo mtulivu. Hata mimi hakuniambia.” Watu wakapiga
makofi. “Na mimi wakati wote tangu nilipoanza hii taasisi nilikuwa nikiomba
Mungu anipe watu wa jinsi hii.” Wakapiga tena makofi. Net alikuwa amemuwekea
mkewe mkono na kumbusu mara kwa mara. Tunda mwenyewe alishangaa.
“Kwa
hiyo Ndiyo. Na ninazidi kumshukuru Mungu kwa kuniongoza kwa mtu sahihi.
Kadiri ninavyoutazama jinsi moyo wake ulivyo na wale watu aliowakuta pale. Na
kwa kadiri Mungu atakaponijalia uwezo, nitahamisha yote yaliyoyomo hapa na hapa.”
Akajishika kichwa na moyoni. “Nitahamishia kwake na kumsihi Mungu aendelee
kumsaidia. Na nyinyi naomba mumpe nafasi na tumsaidie. Na nina hisi, Tunda
atakuwa nakuja kufanya bora zaidi yangu.” Haya yeye mwenyewe bibi Cote alicheka
alipomalizia hivyo, watu wakapiga makofi na kusimama tena. “Asante Nana.” Net
akashukuru. Bibi yake akamgeukia na kucheka kidogo.
“Bado
Tunda anajukumu la umama, mke, tena mke wa Nathaniel Cote! Atahitaji kila
msaada ambao tunaweza kumpa. Na kwa kuwa nimeona jinsi walivyoweza kusimama
hawa wawili. Maya na Tunda. Na vile Tunda anavyomshika vizuri Maya, naamini
kila kitu kitakuwa sawa, tena Net na mimi mwenyewe tukiwa nyuma yao!
Ninauhakika hakuna kitakachoharibika.” Hilo nalo likawa tangazo jipya na la
kushtua kila mtu.
Maya!
Kila mtu akashangaa. Kamera zikamgeukia Maya. Akaanza kupigwa picha kwa upya na
kuchukuliwa video Maya akiwa ameduaa. Hakutegemea. “Asante
Nana. Asante sana.” Akajikuta akilia kwa mshtuko palepale mbele ya watu
wote waliokuwa wamemgeukia yeye. Ilimgusa sana Maya, mpaka akasahau jinsi
alivyokuwa amependeza na vipodozi alivyoviweka usoni kwa ustadi. Alishindwa
hata kujificha. Akabaki ameduaa machozi yakichirizika na kuharibu vipodozi
vyake usoni ambavyo navyo vilikuwa vikichirizika. Kuanzia wanja mpaka
foundation. Tunda akamsogelea. Akamshika
na Net akamkumbatia. Ile ilikuwa inamaana kubwa sana kwa Maya. Kwamba bibi yake
ametangaza kumsamehe na kuridhika na mabadiliko yake.
Ni
bibi Cote. Kioo cha jamii. Asiyekurupuka wala kufanya kosa katika mipango yake.
Ametangaza ramsi kuwa taasisi yake anaiacha chini ya Tunda na yeye Maya kama
msaidizi wake! Hakuna aliyetegemea. Maya! Binti aliyeharibu na kuchafua vilivyo
kwenye hiyo jamii! Leo bibi Cote anamkabidhi majukumu mazito vile! Alifurahi
sana Maya na wala bibi yake hakuwa amemwambia. Inamaana watu waliokuwa
wakimcheka, wameaibika. Zaidi Vic. Amerudisha heshima kwenye jamii!
“Tunda
aliniambia kabla hatujaingia hapa, njaa inauma.” Bibi Cote akabadili ile hali
pale, angalau watu wakacheka. “Najua Gino na timu yake wametuandalia vyakutosha.
Karibuni tuendelee kula na kunywa huku tukishukuru Mungu kwa yale anayotubariki
zaidi ya tulivyoomba. Karibuni na Mungu awabariki.” Akawa amemaliza huyo bibi.
Alikuwa amependeza sana na muda wote huo alikuwa kwenye kiatu cha juu.
Ndipo
wakashuka sasa kusalimia watu kwa kuwashika mkono. Tunda akamshika mkono Maya,
wakatoka pale ukumbini kwa kupitia mlango wa mbele. Akaenda naye chumbani kwake
ili atulie, na kujitengeneza upya.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Walirudi
Maya akiwa ametulia kabisa na cheko juu. Net alipomuona tu mkewe mlangoni
akiingia na Maya, akawaaga aliokuwa akizungumza nao, akamfuata. “Twende
nikakutambulishe kwa karibu kwa Mayor.” “Njaa inauma Net!” “Hatutachukua muda
mrefu. Watu wachache tu, kisha tunaenda kula. Nitahakikisha unakula wewe wa
kwanza.” Wakaendelea kunong’ona huku wakirudi kwenye kundi la watu. Picha
zikaendelea kupigwa na kuchukuliwa video katika kila kitu anachofanya Net, na
mkewe.
Alikwenda
kumtambulisha kwa Mayor wa huo mji wao. Akawatania kidogo na kumkaribisha Tunda
rasmi akimsifu mumewe aliyemfahamu kwa muda mrefu sana kwamba anamfahamu Net
tokea mtoto mdogo sana. Wakataniana kidogo kisomi ndipo wakaendelea kusalimia
wengine huku akiwa karibu na Tunda. Kila aliposogea, alisogea naye akiwa
amemshika kiunoni kwa nyuma.
Kila
alipotambulishwa na yeye akafanya kama alivyofundishwa na Maya jinsi
yakusalimia. Jinsi ya kushika mikono, na jinsi ya kutabasamu. Ujasiri
uliongezeka vile alivyokuwa amejazwa sifa usiku huo na vile alivyokuwa amependeza
kuanzia juu mpaka chini. Bibi Cote alimtolea mkufu wake, akamkabidhi kama
zawadi. Maya alimwambia ule mkufu ni wa alumasi na nigharama sana.
Alitembea
na kusogea kama Maya alivyokuwa amemfundisha, mpaka Net akashangaa. Yeye Net
alitaka Tunda awe vile alivyo. Hakuhangaika hata kumuelekeza chochote. Lakini
Maya alikuwa na kazi yakumuelekeza na kumpa muongozo wa nini chakufanya hata
jinsi ya kuzungumza mbele ya ule umati. Asimamaje, atizamaje umati wote na jinsi
ya kutabasamu, ilikuwa kazi ya Maya na bibi Cote kidogo kwa pembeni
akimsikiliza Maya anavyomfundisha Tunda.
Ila
Bibi Cote yeye alimsisitiza kuwa asiogope, kwa kuwa hakuna kitakachobadilika.
Yeye ni mama Cote tu. Aidha wapende, wasimpende, hakuna kitakachobadilika.
Akamuongezea ujasiri na kumtaadharisha juu ya atakachozungumza hapo kuwa makini
nacho. Hiyo tafrija ikaenda vizuri tu. Watu wakala na kunywa mpaka kusaza. Wakaondoka.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Wakabaki
wao wenyewe watu wa familia wakitathimini mambo yalivyokwenda. Tunda akapata
nafasi yakumshukuru bibi Cote kipekee kwa heshima aliyompa. Na jinsi
alivyomwamini. “Sikujua kuwa walikwambia habari za Lorin!” Tunda akashangaa. “Kwanza
ujue hakuna jambo linafanyika bila mimi kuambiwa.” Tunda akakumbuka hilo,
wakacheka. “Halafu yule binti alisumbua sana pale kwenye ile taasisi. Kuna
waliotaka tumfukuze yule mama na watoto wake sababu ya yule binti. Wengine
wakashauri nimtoe yule binti pale. Lakini nikawakatalia. Hivi nilikuwa nasubiri
nimalize mambo fulani, niende nikazungumze naye mimi mwenyewe nimwambie nampa
nafasi ya mwisho, lasivyo nitampeleka jela ya watoto kama kiongozi wa pale
alivyoshauri.”
“Sasa
kuja kuambiwa Lorin ameomba msamaha na ameomba aanze kufuata taratibu ya kwanza
kabisa. Kuanzia afya yake mpaka kurudi shule! Nikashangaa sana. Ndipo
wakaniambia walikuona ukizungumza naye. Ukamfuata pale zaidi ya mara mbili
akawa ametulia kabisa na hatoroki tena pale.” “Ulizungumza naye nini?” Maya
akauliza. Tunda akacheka kidogo akawa kama anafikiria.
“Sijui
nini kilimgusa zaidi! Ila nafikiri ni Mungu tu. Maana nilianza kumuwekea
mazingira yakuniamini. Nikazungumza naye taratibu kama vile Net alivyofanya
kwangu. Kuweka mazingira rafiki kwanza.” Tunda akaendelea taratibu tu. “Mwanzoni
alikuwa mbishi na anahasira sana. Nafikiri sababu ya hayo mazingira aliyopitia
na mama yake pamoja na wadogo zake. Taratibu nikamuwekea mazingira ya
kuniamini. Nikamsimulia na mimi kule nilikopita mpaka nikampata Net. Akiwa tu
msaada wala si mpenzi. Nikamwambia kama nisingekubali msaada wa Net, ningebakia
vilevile.”
“Nikamwambia
hapo anajiadhibu kwa makosa ya baba yake. Nikamwambia hastahili kubeba hasira
kwa mabaya aliyofanya baba yake na mengineyo. Tukazungumza sana mpaka nikamuona
analia na kufunguka. Ndio maana nilikuwa nikirudi mara kwa mara ili tu
kuzungumza naye. Alishakosana na watu wa pale karibu wote. Pakawa na ukuta kati
yao.” “Aliwasumbua sana. Tena kwa kuwatusi vibaya sana.” Akaongeza bibi Cote.
“Aliniambia
mwenyewe. Na nikamwambia ili aweze kusaidiwa pale, nilazima aanze kwa kuwaomba
wote msamaha. Ndipo watamwangalia kwa jicho jingine. Ajishushe, achukue msaada
wake, atoke na yeye akawe msaada kwa wengine.” “Nimesikia amechangamka!
Anamsaidia hata mama yake kuogesha wadogo zake.” Wakacheka.
Net
akambusu. “Unakumbuka nilikwambia utakuwa msaada kwa wengi?” Tunda akacheka
huku akitingisha kichwa. “Naona umeanza mwenyewe bila kusubiri nikusaidie.”
Tunda akacheka. “Najua una mambo mengi Net. Na kwa kuwa Nana na Maya wapo, na Nana
ameniambia muda na wakati wowote nikiwa na swali asipokuwepo naweza kumpigia.”
“Kabisa Tunda. Ukikwama popote. Hata kufanya chochote, ukakwamishwa kwa
chochote. Nipigie.” Akavuta kumbukumbu kidogo.
“Lakini
kwa jinsi ilivyoenda leo, sidhani kama kuna utakapokwenda usipewe huduma ambayo
wangenipa mimi.” “Kweli Nana!?” “Kabisa. Nana akiongea jambo ndio mwisho na
wote wanajua.” Maya akaingilia. Wakamuona anaanza kucheka. “Yess!” Wakamsikia akishangilia
kwa furaha. Wakajua amekumbuka kitu chakumfurahisha. Wote wakacheka. “Sasa hivi
nakuwa mtu mzima. Sifanyi tena mambo ya kitoto.” Akaanza kujiwekea mikakati
yake. Wote wakacheka.
“Naacha
kupost vitu vya kijinga huko mitandaoni. Nakuwa kama Tunda. Mtulivu!” wakacheka
sana kama hawamsadiki. “Si mtaniona! Sibishani tena na Vic. Matendo tu. Kwanza
nishajua nipo juu yake sana. Halafu sasa hivi mimi ninamajukumu mazito sio kama
yeye kujipendezesha na kuzunguka kwenye magari ya kifahari kutoa mipango tu
bila utelekezaji!” “Hapo utakuwa kweli
umebadilika. Na watajua tu.” Waliendelea kuzungumza hapo wakijipanga. Mpaka
muda wa kwenda kulala, wakatawanyika.
Maandalizi ya Harusi ya Pili ya kanisani Tunda
& Net.
Tunda
ndiye aliyeachiwa jukumu zima la mambo ya harusi. Achague kile anachokitaka
yeye. Kuanzia rangi, mapambo, chakula, keki, kila kitu kisha amwachie Stacy,
ambaye ni mtu maalumu anayeshugulikia hiyo harusi. Ndipo yeye sasa Stacy
amalizie kila kitu baada ya Tunda kuchagua anachokitaka. Kuhakikisha kila kitu
kinafika ukumbini kwa wakati.
Net
alimwambia kwa mila na desturi za huko nchini kwao, upande wa bibi harusi ndio
wanagharamia harusi nzima. Yaani wazazi wa bibi harusi. Na bibi harusi ndiye
anayechagua kila kitu cha harusini. Upande wa bwana harusi wanakuwa kama
waalikwa tu. Kwa hiyo akamwambia anampa heshima yakufanya anachotaka kwenye
hiyo harusi. Achague atakacho yeye.
Makampuni
ya maana yalikuwa yakipishana hapo kwa Cote, kumuonyesha Tunda vitu mbali mbali
ili kupata hiyo kazi yakufanikisha harusi yao ambayo walijua ni kuuza kazi zao
kwa asilimia kubwa sana. Harusi ya Nathaniel Cote! Kila mtu alitaka apewe yeye
kazi.
Stacy alikuwa na kazi
ya kuchagua katika kila idara, makampuni matatu mazuri. Anawekeana nao miahadi
kutokana na muda wa Tunda, kisha wanakwenda kujinadi sasa kwa Tunda.
Tunda
alikuwa na kazi ya kuangalia kwa makini ili asije chagua kitu akaharibu shuguli
nzima ya matajiri hao. Makampuni yalituma wataalamu wao mbali mbali kwenda
kumshawishi Tunda ili wachaguliwe wao. Upande wa chakula, alimtaka Gino na Maya
wamsindikize kwenda kuonja aina hiyo ya chakula. Yeye Net alisema chochote
atakachochagua Tunda hatakuwa na shida.
Stacy
alimletea Tunda caterers kama wanne ambao alimwambia Tunda, hao ndio wanasifika
kwa chakula kizuri na maandalizi yao ni ya ustadi. Tunda alimuomba kwanza menu
yao. Kujua huwa wanatoa vyakula vya namna gani kwanza, hata kabla hajakutana
nao. Alimtaka yeye Stacy ndio alete menu ili kupunguza kuonana na watu wengi.
Stacy alipoleta menu, akamuomba muda wa kuzipitia akiwa na Gino kwanza ili
kuelewa kila chakula na Gino amshauri.
Walishauriana
kujaribu chakula cha caterers wakubwa wawili ambao Tunda alivutiwa na menu zao.
Wakapanga muda wa kwenda kuonja baadhi ya vyakula na juisi ili kuweza kufanya
maamuzi sahihi. Kwa upande wa kuonja hivyo vyakula, walitakiwa wahudhurie watu
watano. Kwa kuwa bibi Cote alionekana katikati ya week anakuwa na ratiba
inayobana, basi Tunda akamuomba Maya aungane nao ili kuchagua ladha sahihi ya
chakula ambacho anadhani wageni waliozoea kuwaalika, wangefurahia. Maya
alikubali, akasema atatokea kazini kuungana nao. Kwa hiyo watakutana eneo
husika.
Katikati ya Yote,
Kabla ya Harusi.
Katikati
ya hekaheka hiyo ya kukamilisha maandalizi ya harusi kwa wakati, ili iwe nzuri
na baada ya hapo na Net naye akatulie kwenye fungate. Busy kazini kuweka mambo
sawa, kabla ya siku ya harusi yao ili baada ya harusi apate muda mtulivu na
mkewe. Na mkewe naye busy akitaka asiharibu kitu.
Bibi
Cote naye kuna ambao mbali na kuwatumia kadi za mwaliko, ilibidi kuzungumza nao
kwa simu. Na kutafutwa sehemu maalumu za kushukia wageni hao mamilionea,
wanaotoka nje na ndani ya nchi ya Canada kushuhudia Nathaniel Cote akioa.
Vyombo
vya habari vilitangaza. Magazeti yaliandika. Mashabiki wao ndio walijaa
mitandaoni wakihesabu siku. Kila mtu alitaka kuhudhuria harusi hiyo, lakini
mwaliko ulikuwa kwa wachache, ila vipo vyombo vya habari vilitangaza kurusha
harusi hiyo ‘Live’, baada ya kuomba na kupewa ruhusa
na familia hiyo ya Cote. Ikaanza kazi ya kushindana mitandaoni watu wakikisia gharama
nzima ya hiyo harusi. Wengine walipingiana dau hadharani. Wakaja gauni
atakalovaa mke wa Net. Yaani Tunda.
Watu
walishindana mtandaoni wakibashiri gharama ya gauni tu atakalovaa siku hiyo
Tunda. Nani atabahatika kutengeneza gauni hilo au ni designer gani atabahatika
nguo yake kuvaliwa na Tunda siku ya harusi yake! Hilo nalo likawa jambo.
Mjadala uliopewa muda na mashabiki wengi tu. Hapo bado walikuwa wakiendelea
kumthaminisha Tunda kwa vile alivyotokea siku ya kutambulishwa kwake. Bado mijadala
ilikuwa ikiendelea mtandaoni. Watu wakichambua neno moja hadi jingine kutoka
kwa kila mtu aliyezungumza siku ile. Kuanzia bibi Cote, Net, Tunda hadi Maya.
Kila mtu alisema lake. Wenye wivu walizidi kuumia kwa sifa zilizokuwa
zimemwagwa kwa Tunda na kuponda hadharani kutokana na ile hotuba.
Penzi
la kweli lililotangazwa na kuonyeshwa pale hadharani. Wakaanza kujadili hata jinsi
Net na Tunda walivyosimama na kushikana mikono. Yale mabusu! Kila mtu akasema
lake. Na kweli ulikuwa mjadala ambao ulijaa kwenye mitandao na magazetini. Ya
udaki yaliandika kwa undani. Yale magazeti ya maana, yaliwapongeza nakuongea
mazuri. Wakiwatakia kila la kheri kwenye maisha yao. Kukajaa hekaheka kila
upande. Shamra shamra wengine wakisubiria siku ya harusi kwa hamu, na wengine
wakiona ni kama walidhalilishwa hadharani.
Kwa Upande wa Vic!
Vic
alishajitangazia kuwa yeye ndio angekuwa mke wa Net na mchukua kiti cha bibi Cote. Leo Tunda aliyemfukuza
nyumbani kwake kwa dharau kiasi hicho ndiye anajaa magazetini akisifiwa vile! Tunda
anaonekana akipewa mabusu hadharani na mwanaume ambaye bado anamuhesabu ni
wake! “Net ananistahili mimi. Net ni wangu!”
Vic alilia mbele ya wazazi wake. “Tunda amebeba
mtoto wa Net na si mimi!” Kila alipokumbuka nakusikia juu ya Tunda na
Net, Vic alizidi kulia.
Maya
ndio anachukua nafasi aliyoisubiri kwa hamu tokea miaka na miaka! Ikawa tofauti
kwa Vic, wazazi wake na wapambe wake waliona yeye Vic ndiye anayestahili kuliko
Maya au Tunda. “Mlevi yule ndio anachukua cheo
changu! Alikuwa akifanywa mapenzi mpaka kwenye gari, hadharani, kwenye vyoo vya
clubs, leo yule bibi ndio anampa nafasi yangu! It’s not fare mom.” Vic
alizidi kulia na kusononeka moyoni.
Mbaya
zaidi ni kama akatolewa kabisa kwenye picha. Hakutajwa hata kwa upande wa marafiki
wa Net. Net hakumtaja kati ya marafiki zake. Alimtaja Troy na Lean tu! Vic
amekua pamoja na Net. Amelala chumbani kwa Net tokea yupo binti mdogo tu. Net ndiye aliyekuwa mwanaume wake wa kwanza
kufanya naye mapenzi. Na wakawa kwenye mahusiano ya muda mrefu sana. Leo Tunda
anamwambia hajawahi hata kumsikia, na Net naye anashindwa hata kumtaja mbele za
watu! Hilo likamuuma sana. Ulikuwa ni udhalilishwaji ambao, ilikuwa bora afe,
kuliko kuona hiyo harusi ikifungwa.
Na
kumdhihirishia hilo, aliambiwa asifike tena pale nyumbani isipokuwa kwa mwaliko
maalumu. Akashangaa maandalizi yanaendelea, hakuna hata anayemtafuta hata kwa
swali! Inamaana hayupo hata katika kundi la wasimamizi wa harusi! Ni Troy tu na
Lean! Vic akaumia sana.
Kwa Upande wa Ritha/ Mama
Mzaa Chema.
Ritha
naye huko alipokuwepo habari zilimfikia bila chenga. Japokuwa alikuwa mji
mwingine, lakini hapohapo nchini Canada, alipata kile kinachomtokea Tunda huko
mjini Norfolk. Tunda alijaa kila kona akipambwa na bibi Cote. Hata watoto wake
wakuwazaa hawakuropoka hata kwa bahati mbaya kutaja jina lake kwenye tafrija
nzima! Yaani ni kama hajawahi kuwepo kwenye maisha yao! Nana akawa kama mama wa
wanae. Halafu Tunda ndiye anasifiwa na
kupewa kiti!
“Kwanza
hajasoma kama mimi!” Hilo nalo
likamuuma sana Ritha. “Wakati mimi nahangaika kuzaa, na kulea, yeye alikuwa anafanya
umalaya tu!” Ritha akazidi kuumia nakusahau Tunda ni kama mtoto wa kumzaa
kwa umri alionao. Mdogo hata kwa Net. Lakini hilo la umalaya hata yeye Tunda
alikiri hadharani na kujisifia kuwa amelipa deni. “Anakula jasho langu!
Amechukua familia yangu! Watoto wangu wanashindwa kunikumbuka, anachukua nafasi
yangu!” Ritha akazidi kuumia. Akajidharau kuona ameanza jambo na kuishia
katikati! Anashindwa na Tunda! “Haiwezekani!” Akasema Ritha kwa kuumia
sana.
Mawazo
yakamrudisha kwenye sifa alizomwagiwa na wote. Maya, bibi Cote na Net. Kitu
kikapanda ndani yake. Hasira zikawaka. “Yaani malaya huyu amenipokonya kila
kitu mpaka uhuru wangu!” Ritha akaangalia alipo. Kutoka kwenye jumba la
kifahari, ameishia kwenye Condo! Gorofa alilopangisha kijisehemu na wengine
wakiishi kwenye jengo hilohilo, juu yake na chini! “Haiwezekani!” Akakumbuka
heshima kubwa aliyokuwa amejipatia nchini Tanzania na Kampuni ya Cote
aliyomiliki kabla ya kuja kwa Tunda kwenye maisha yake. Vyote ni kama
vilipotea. Akaishia kuuza kila kitu na kukimbia nchi! Na hayo yote alihesabu ni
sababu ya Tunda.
Ni
kweli Ritha hakuwa na shida na pesa. Alikuwa na ajira nzuri tu, lakini mpweke.
Hakuna ule utukufu aliokuwa nao wakati anaishi nchini Tanzania kabla Tunda
hajaingia kwenye picha. Au kabla hajaamua kuanza vita na Tunda. Akili na mawazo
ya Ritha vikagoma kabisa kuona Tunda anafikishwa kanisani na yeye ndio kubaki
mama Cote anayetambulika kila mahali. “Mimi ndio mama Cote. Kila mtu alilijua
hilo na lazima ibakie hivyo.” Kwa hasira sana, akatamka Ritha na kuanza
kuweka mikakati ya jinsi ya kumaliza alichoanza. Akajiona atakuwa mtu wa ajabu
sana, kuanza jambo na kutomaliza. Mwanamke mwenye akili ambaye hata Bibi Cote mwenyewe
anamkubali, akaanza kujipanga upya kurudi vitani.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Watu wawili wanguvu,
Vic&Ritha, na mipango yao ambayo haijawahi kushindikana wameamua kusimama
kinyume na Tunda. Wote hawakubali kushindwa, na hawajawahi kushindwa. Vic alimmudu
vizuri sana na Maya. Ritha alifanya makubwa yanawauma mpaka hapo walipo.
Sasa Je, nini kitamtokea
Tunda katikati ya maandalizi mazito yakifahari ya harusi yake na Net?
Ritha alimtoa kwenye fungate
akiwa na pingu akishindwa kufanikiwa kusimamisha harusi sababu ya uwepo wa bibi
Cote nchini Tz,
Je, safari hii Tunda atafanikiwa
kufika kanisani?
au
Majeshi yataungana kukusanya
nguvu dhidi ya Cote waliomwahidi Tunda ulinzi?
Endelea kufuatilia visa na
mikasa ya kusisimua.
0 comments: