Nilipotea! Part7 – Sehemu ya A
Mara bibi yake na Maya wakawa wanarudi wakikimbia pamoja na mlinzi. “On your fit, NOW. This is not the time to freeze, son!” Bibi yake aliongea huku akiingia kwenye gari akimtaka Net asimame pale alipokuwa amekaa. “Come on! Get in the car. We have to run. Tunda needs us.” Bibi yake akaweka msisitizo kwa Net wawahi hospitalini akimwambia afanye haraka kwakuwa Tunda anawahitaji kwa wakati huo. Net akasimama na kuingia ndani ya gari.
“Nilikuonya Barbara, na nilikwambia Vic anahitaji msaada wa haraka ambao nyinyi wazazi wake mnaonekana mmeshindwa kumpa. Sasa, kama unampenda Vic, ndani ya masaa mawili hakikisha wewe mwenyewe, unamfikisha kituo cha polisi. Baada ya hayo masaa mawili nikiambiwa hayupo kituo cha polisi, nitajua umeshindwa tena, ndipo hapo sasa itabidi mimi niingilie kati. Na nina uhakika hutataka kuniona mimi nikiingilia kati.” “Amefanya..” Mama yake Vic akataka kuuliza, lakini bibi Cote akamkatisha. “Umebakisha lisaa limoja na dakika 56. Usipoteze muda.” Bibi Cote akakata simu.
Kwa kuwa Tunda alikimbizwa hospitali ya serikali ya karibu, ilichukua kama dakika 20 kufika pale. Walishushwa mlango wa mbele na helcopter iliyokwenda kumchukua daktari wa kina Cote ndio ilikuwa inatua juu ya jengo hilo. “Huyo ni Dr. Ross. Naamini atakuwa hajachelewa.” Bibi Cote alizungumza hivyo akiwa anashuka kwa haraka akikimbilia ndani. Dereva wake alimshusha mbele kabisa kwenye mlango wa kuingilia ndani ya jengo hilo la hospitali.
Wakati wanaingia ndani ni kama uongozi wa hapo hospitalini ulikuwa ukimsubiria bibi Cote kwa kuwa habari zilishafikishwa kuwa Tunda anakimbizwa hapo akiwa hana fahamu na ni mama mjamzito wa mimba kubwa. Si kwa Tunda, ni utaratibu wa wagonjwa wote ili kuhakikisha kuwa wanapomfikisha mgonjwa mwenye hali ya mahututi, awe anasubiriwa na wahusika sahihi. Sasa ikaongezeka kuwa ni Mrs Cote na mlinzi alishapiga simu yakuomba uongozi wa hospitali kutua ndege hiyo ndogo itakayomleta daktari wa Cote. Umakinifu ukaongezeka na habari zikawa zimefika kwa uongozi wote na madaktari bingwa wa hapo kuwa Mrs Cote analetwa hapo.
Kina Cote waliingia wakakuta uongozi wa hospitali unawasubiria ndani ya mlango, wakiwa pamoja na polisi. “Mrs Cote anaendeleaje?” Hilo ndilo lilikuwa swali la kwanza kabla hajajibu salamu. Wakawatoa pale mbele ya watu wengine wakawa kama wanaingia ndani huku wakijaribu kuwapa taarifa za walipofikia na Tunda, hata kabla hawajafika mbali, akawasogelea daktari akikimbia. Alionekana anatokea chumba ambacho sio mbali sana na pale. “Lazima mtoto atolewe sasa hivi.” Bila salamu akaenda moja kwa moja kwenye pointi akimtizama bibi Cote na Net.
“Huyu ni daktari wa watoto.” Wakamtambulisha. “Hewa
kwa mtoto inaanza kushuka. Tunda ameshindwa kupokea hewa yaku...” Kabla
hajamaliza, mlango wa lifti iliyokuwa inatokea juu kabisa ya hilo jengo,
ukafunguliwa. Wote wakageuka. Akatoka Dr Ross akionekana ni kama na yeye
alikuwa na haraka sana. “Thank God!” Alisikika bibi Cote mara baada yakumuona
Dr Ross pale.
“Zungumza nao ili uelewe ni nini kinachoendelea.”
Bibi Cote alimwambia Dr Ross aliyekuwa akifuatilia afya ya Tunda na mtoto wake
kila week. Akasogea karibu akaanza kuuliza maswali ya kitaalamu huku akipewa
majibu ya kidaktari hata dakika 5 hazikuisha akawa ameelewa kila kitu.
Walizungumza kwa lugha za kidaktari wakitajiana majina magumu wao kwa wao. Akamgeukia
Net. “Lazima mtoto atolewe sasa hivi na kama nilivyokuwa nimewaambia wewe na
Tunda, mtoto wenu ameshakomaa na..” “Okay.” Net akakubali kwa haraka bila
kutaka maelezo mengi.
“Lakini lazima nimuone mke wangu kabla
hamjamfanyiwa chochote.” Net akasisitiza. “Unaweza kuwa naye kwenye hatua za
mwanzoni kwenye chumba cha upasuaji, ila wakianza kumshugulikia yeye na mtoto,
itabidi....” Mara wakasikia kelele za mashine chumba alichopo Tunda. Manesi
wengine wakazidi kukimbilia humo ndani. Baada ya kama dakika tano wakaona Tunda
anatolewa kwenye hicho chumba huku anakimbizwa na wauguzi pamoja mashine
zilizokuwa zikipiga kelele mfululizo. Walimuona muuguzi mmoja juu ya kitanda
alicholazwa Tunda, amepiga magoti juu ya Tunda akijaribu kumfanya aheme kwa
kumminya kifua chake kwa nguvu, tena mfululizo.
Kelele zilizokuwa zikipigwa ili lift ifunguliwe na
watu wapishe njia, ilizidi kuwaogopesha wote. Tunda alikuwa akikimbizwa chumba
cha upasuaji akisindikizwa na hekaheka za madaktari na manesi wengi. Alionekana
akiwa amefunga macho ametulia kabisa pale kitandani japo walikuwa wakimminya
kwa juhudi zote. Baada ya lift kufunguka, waliingia wote na kitanda cha Tunda,
Net naye kama mchale, akakimbia na kuingia ndani. Kufumba na kufumbua,
wakajikuta wamebaki Maya, bibi yao pamoja na mlinzi nyuma yao. Wauguzi wote
waliondoka hata wale waliokuwa wakizungumza nao pale walikimbilia kwenye ile
lifti pamoja na Dr. Ross. Pakatulia kimya, macho yao wote yakiwa yametua kwenye
mlango wa ile lifti iliyowabeba wote.
Wakajikuta kila mtu akiwaza lake. Kuanzia kile kilichokuwa kikiendelea pale, hali ya Tunda walivyomuona nyumbani na pale. Maya akaanza kulia taratibu. “Kama Tunda akifa, nahisi na mimi nitakufa Nana.” Bibi yake akamsogelea na kumkumbatia. “Usiogope Maya.” “No Nana. Hujui mahusiano yangu na Tunda. Ameniahidi atakuwa na mimi kila wakati. Ananisikiliza. Tunda ana muda na mimi, Nana. Ndio mtu pekee nimempata ambaye yupo karibu na mimi na kujali kwa undani. Kila mtu hajui ni kwa nini nilikuwa nikitumia madawa, lakini Tunda ametoa muda wake na kuzungumza na mimi.” Bibi Cote akashangaa sana.
Kwa kuwa mengi yalikuwa yakiendelea kwa wakati mmoja, bibi Cote akaona hilo alinyamazie kwa wakati huo. “Nisikilize sweatheart. Tunda yupo chini ya uangalizi mzuri sana. Macho na akili za kila daktari aliyekuwepo chumbani kwa Tunda vipo kwa Tunda na mtoto. Na kwa kuwa wanajua ni Cote, watahakikisha Tunda anapona na anarudi kwetu salama.” “I do love and need Tunda in my life, Nana!” Maya aliendelea kuweka msisitizo wa vile anavyompenda na kumuhitaji Tunda maishani. “We all do baby. We all do.” Akajaribu kumtuliza kwa kumuhakikishia kuwa hata wao wanampenda na kumuhitaji Tunda. Mmoja wa nesi akawasogelea na kuwashauri wakae sehemu ya kusubiria wagonjwa waliokuwepo chumba cha upasuaji. Akawaongoza njia, wakaenda kukaa.
Cote
junior cote the 5th!
B |
aada
kama ya dakika 40 hivi akawafuata yule daktari wa watoto aliyekuja mwanzoni.
Lakini safari hii alikuwa na tabasamu la faraja usoni, akawaambia waongozane
wakamuone mtoto. Kidogo ikawa faraja. “Haya sio mazingira niliyopanga ayakute
Cote. Sio hivyo kabisa!” Alilalamika bibi Cote.
“Hivi ndivyo anavyopenda Vic. Hawezi kuruhusu kitu kizuri
kitokee kwenye maisha ya watu kama yeye hajahusika na kupewa sifa. Amehakikisha
ameniharibia mimi, watu wakanipuuza, sasa hivi ameamua kummaliza na Tunda!
Pengine watu safari hii watamjua hila zake.” Maya aliongea huku
akilia. Wakielekea wanapowekwa watoto waliotoka kuzaliwa.
Bibi
yake aliumia sana alivyozungumza vile Maya. Tokea hilo tukio litokee, Maya
amekuwa akiongea mambo ya kumuumiza sana huyo bibi nakumfanya ashindwe
kuongeza. Maya amekiri Tunda ndiye mtu pekee ambaye ametoa muda wake
kumsikiliza hata kujua ni kwa nini au ilikuaje akatumia madawa ya kulevya. Tunda
ni mgeni kwao kabisa na ameweza kuwa na Maya kwa karibu kwa kiasi hicho! Si
yeye tu bibi Cote, wote waliomzunguka Maya waliishia kumtoa kwenye mikasa bila
kutafuta chanzo. Na hata aliposema ni Vic ndiye anayehusika, hakuna aliyejali.
Sasa
bomu jingine la Vic limewalipukia na wao usoni. Tena zikiwa zimebaki siku 4 tu
harusi kufungwa, week mbili ili mtoto wao azaliwe. Vyote hivyo Vic
amevibadilisha kwa muda mfupi sana, tena kwa kuwagarimu wao, garama kubwa sana.
Ya pesa na uhai.
“Anaendeleaje
Tunda?” Akauliza bibi Cote angalau kujitoa kwenye kilio cha Maya. “Bado wanamshugulikia.
Lakini amejifungua mtoto mzima kabisa. Tulifikiri angehitaji kuwekwa kwenye
mashine kwa muda mrefu, lakini anaonekana ameshakomaa kabisa. Anahitaji
uangalizi wa masaa 24 tu ili kujiridhisha kama yupo salama.” Aliongea yule
daktari wa watoto akionekana ametulia.
Aliwafikisha
kwenye hicho chumba, lakini waliambiwa wanamwangalia kwenye kioo tu, sio
kuingia ndani. “Ni kweli ni mkubwa! Ni Cote kweli
kweli!” Alisikika bibi Cote kwa sauti ya kuhamasika, wakamuona anafuta
machozi. Maya naye akaanza kulia kwa furaha baada yakumuona yule mtoto. “He is so cute and tall! Hafanani na Net wala Tunda!” Wakacheka
huku wakilia.
“Net
amemuona?” Akauliza bibi Cote. “Ndiyo, alimuona kulekule chumba cha upasuaji.
Ndiye aliyesema tuje kuwaita mumuone.” Bibi Cote akarudisha macho kwa mtoto. “Hivi sivyo nilivyotaka kukutana na Cote kwa mara ya
kwanza!” Akalalamika tena bibi Cote kwa sauti ya chini iliyoweza
kusikika. “Kwa nini hatuwezi kumshika!?” Akauliza kwa kusikitika Maya. “Umeona
pale alipowekwa na mashine pembeni yake?” Wote wakamwangalia yule daktari na
kurudisha macho kwa Cote. “Japokuwa anaonekana amekomaa kwa nje, lakini bado
tunataka kuwa na uhakika hakuna kinachobadilika angalau kwa masaa 24 na
kujiridhisha kabisa kuwa kila kitu ndani na nje kinafanya kazi sawa.” Wakatulia
kidogo wakimwangalia.
“Rudi
chumba cha upasuaji, waambie zimepita dakika 50 sasa, hakuna aliyetoka kutupa
taarifa za Tunda. Nahitaji kujua kinachoendelea.” Akamwambia yule daktari wa
watoto. Akaondoka na kuwaacha pale wamesimama wakimtizama mtoto.
Maya
alipiga picha baadhi na kumchukua video huku akiongea maneno mazuri kwa Cote,
akampiga picha na bibi yake na kumuomba aongee chochote. “Namshukuru Mungu upo salama na nimefurahi unafanana
kabisa na Cote wangu.” Maya akacheka, bibi Cote akajifuta machozi. “Mungu anajua ni kiasi gani nakupenda na nilivyokuwa
nikikusubiri nikushike kwenye mikono yangu na kupata bahati ya kukubusu tena na
tena. Wewe ni zawadi ya pekee na ya ajabu Mungu aliyotupa. Nakuombea afya njema
na ulinzi wa kimungu kwenye maisha yako yote ya hapa duniani. Ukafanikiwe
katika kila utakalochukua hatua na kulifanya. Zaidi ya Cote mwenyewe.”
Maya akaridhika. Wakajichukua video pamoja. Akazima camera ya simu na kurudisha
mkobani.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Baada
ya muda akarudi yule daktari wa watoto na daktari mwingine. “Tunda
anaendeleaje?” Akawahi kuuliza bibi Cote. “Anaendelea vizuri. Upasuaji ulienda
vizuri. Hakuna kilichoharibika.” “Ameweza kuzinduka?” Akauliza tena bibi Cote. “Mwanzoni
alipoingia mume wake. Alifungua macho lakini hakuzungumza. Walimchoma sindano
ya usingizi kwa ajili ya upasuaji, wanamalizia kumshona watamuamsha kabla
hajatolewa. Dokta Ross amesisitiza nikwambie usiwe na wasiwasi. She is gona
make it.” Wakamuona bibi Cote anapumua kwa nguvu kama aliyepata aghueni. “Asanteni
sana.” Akashukuru bibi Cote, yule daktari akaondoka.
Simu
ya Logan ikaingia. Bibi Cote akajivuta pembeni. Maya alimuona vile
anavyobadilika kila muda unavyozidi kwenda bila yakujibu chochote. Maya akajua
mambo si mazuri. “Nimesema ni lazima Carter atoke leo.
Anatumia dawa kila baada ya masaa 6. Lazima arudi nyumbani leo. Unanielewa
Logan?” Akamsikia bibi Cote
akitoa amri. “Na watoto wa Emily hawawezi kuelewa kama
mama yao leo asiporudi nyumbani. Kwa kifupi, fanya kila linalowezekana,
kufupisha mambo yote. Na unitaarifu kujua wamefikia wapi?” Akamuona bibi
yake amekata simu kisha amesimama vilevile. Maya akajua anajaribu kutulia.
Mara
wakamuona Net anakuja. Wote wakakumbatiana.“Tunda anaendeleaje?” “Wanamalizia
ili wamtoe. Kila kitu kimeenda salama. Daktari wake amejitahidi asipoteze damu
nyingi. Wameniomba nitoke, wamalizie.” “Afadhali.” Bibi yake akasikika
kuridhika. “Tumemuona Cote.” Maya akaongeza. Wakamuona Net anafuta machozi. Akasogea
pale dirishani. “Anafanana sana na Papa!”
Wakacheka.
Baada
ya Tunda kujifungua.
T |
unda
alirudishwa chumbani kwake akiwa bado na madawa ya usingizi na amechoka. Wakamuweka sawa, na kumwekea mashine za kuendelea kuangalia
mapigo ya moyo na mengineyo. Waliporidhika, manesi na madaktari wengine
wakatoka. Alibaki dokta Ross ili kuzungumza na familia. Bibi Cote, Net na Maya
wakaingia hapo chumbani. Tunda aliwaangalia bibi Cote na Maya, akashindwa hata
kumtizama Net. Akafunga macho kabisa. Wakaona machozi yakimtoka.
“Kila
kitu kilienda sawa. Anahitaji mapumziko makubwa. Mrs Cote yupo dhaifu na bado
pressure yake hairidhishi. Imerudi kuwa kama nilivyomuona mwanzoni kabisa,
wakati kulikuwa na maendeleo! Nashauri apate muda wakutosha wa mapumziko,
na sisi tutaendelea kumfuatilia. Naamini
akipata mapumziko yakutosha baada ya siku tatu, angalau tunaweza kufikiria
kumruhusu arudi nyumbani.” Bibi Cote akamshika mkono. “Nakushukuru sana. Asante
kwa kuja kwa haraka na kuweza kumsaidia Tunda. Asante sana.” Akashukuru bibi
Cote. “Chochote kwa ajili yako Ms Cote.” Akajibu yule daktari wa wakina mama.
Akazungumza
kidogo na wao wakapa muda wa kuuliza maswali, akatoka kama kuwapisha. Kimya.
Tunda hakufungua macho tena. Bibi Cote akasogea pale kitandani akamnyanyua
mkono na kuubusu kisha akabaki ameukumbatia. “Pole sana Tunda. Pole
sweetheart.” Akarudia rudia yule bibi
lakini Tunda aliendelea kutokwa na machozi. Simu ya bibi Cote ikaita. Akajua
lazima atakuwa tu ni Logan ambaye ndiye
aliyetaka kumsikia kwa wakati huo. “Nitarudi baada ya muda mfupi sana.” Akaaga
na kutoka.
“Pole
Tunda.” Aliongea Maya kwa kiswahili kabisa, lakini hata Tunda hakufungua macho.
Tunda huyu alijawa kusalitiwa na maumivu makali sana. Ya upasuaji na maneno ya
Vic yaliyomkumbusha mengi. Alibaki akitokwa na machozi bila hata kutaka
kufungua macho kabisa. Net alipomsogelea ili kumfuta machozi, akahisi harufu
yake, bila kufungua macho akajua ni yeye, taratibu tu bila fujo nyingi wala
kufungua macho akakwepesha uso upande mwingine kama anayemwambia usiniguse.
Wanandoa
hawa walikuwa na kutoelewana tokea siku iliyopita Net alipogomba sana na
kushindwa kutulia hata Tunda alipomtuliza wakiwa wanachagua chakula. Akaja
akaongeza kugongelea msumari Vic. Walisimama hapo, Net na Maya wameshageuka
wasaliti wake kabisa. Alitamani waondoke, wampishe hapo kwenye hicho chumba. Net
akaelewa kuwa hataki amguse. Lakini hakuanzia hapo. Ni tokea jana yake
waliporudi nyumbani, Tunda alikimbilia chumbani na kujifungia. Net akajua kuna
mengi aliyobeba hapo Tunda. Ila wasijue ni nini Vic aliongea.
Maya
aliona alichofanya Tunda, na bado aliendelea kulia. Asijue kama na yeye asogee
au amwache. “Utapona tu Tunda.” Akaongeza Maya kwa upole, kisha akamtizama kaka
yake. “Labda tumuache apumzike mpaka kesho.” Akamshauri kaka yake kwa sauti ya
chini. Nesi akaingia na sindano kwenye tray. Akamkuta akilia. Akamsogelea.
“Upo
sawa Tunda? Au maumivu ni makali sana?” Yule nesi alimuuliza kwa upole.
Wakamuona Tunda akitingisha kichwa kukataa huku akilia kwa uchungu sana. “Lakini
pia lazima nikupe dawa ya maumivu ili kuhakikisha maumivu hayarudi tena.”
Wakamuona anatingisha kichwa kukubali. “Naomba nisikilize Mrs Cote. Afya yako
sio nzuri. Unahitajika kupumzika kabisa. Daktari amekuandikia dawa za usingizi
kabisa. Ninazo hapa pia. Nitakuchoma ili ulale kabisa. Naomba utulie.” Wakamuona
anavuta pumzi kwa nguvu lakini machozi yakiendelea kumtoka.
Yule
nesi akamfuta machozi na kumchoma sindano kwa kupitia sindano iliyokuwa
imepitishiwa ndipu inayoingia mkononi mwake. “Nitazima taa zote kasoro ile
ndogo pembeni ili kumfanya atulie kabisa. Hata hivyo dawa niliyomuwekea,
itamfanya alale kabisa. Nashauri hata nyinyi mumpishe, na ikiwezekana hata hao
polisi hapo nje muwaombe waje wazungumze nae baada hata ya masaa 24, ili
kumfanya atulie kabisa.” “Asante.” Akashukuru Net, yule nesi akaondoka.
Net
akarudi pale na kuinama. “Nakupenda Tunda. Nakupenda sana mke wangu. Naomba
usije kulisahau hilo.” Akaongeza kilio. Akambusu kichwani. “Nitarudi tena kesho
asubuhi, pengine dawa zitakuwa zimeisha na tutaweza hata kuongea. Cote
anaendelea vizuri. Naamini kesho wataweza kumleta huku.” Tunda hakufungua
macho. Net akamfuta machozi. Safari hii hakukataa. Akabaki akimwangalia kwa
muda, wakamuona anavuta pumzi taratibu, wakajua dawa zimeshamchukua. Nesi
aliwaambia wakitoka atarudi ndipo atazima taa. Net akamfunika vizuri, akabaki
akimtizama.
“Twende
Net. Atakuwa sawa. Tumpe muda wa kupumzika.” Maya akaongea na kaka yake kwa
upole. Akamshika mkono. Net akambusu tena Tunda. Wakatoka. Walimkuta bibi yao
anazungumza na polisi huku amekuwa mwekundu haswa. Wote wakasogea. “Tafadhali
naomba mumuache kwa sasa. Mbali na upasuaji aliofanyiwa, Tunda yupo dhaifu
sana. Hata sisi tumeombwa tuondoke ili tumpishe apumzike kabisa.” “Hata hivyo
wameshampa dawa za usingizi. Amelala kabisa, hawezi kuzungumza.” Net akaongeza
kwa bibi yake.
Polisi
wakasema watarudi kesho yake, wakaondoka. “Hakuna kitu tunachoweza kukifanya
sasa hivi, turudini nyumbani. Nimeweka ulinzi hapo nje ya mlango wake, nimesema
ni wauguzi tu ndio wanaoruhusiwa kuingia hapo, na nimekataza hata wauguzi
wasiingie na simu humo ndani.” “Asante Nana.” Hivyo tu ndivyo alijibu Net
akionekana amelemewa hawezi hata kuzungumza.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Wakiwa
njiani kwa kuwa kila mtu alikuwa kimya. Net macho dirishani, bibi Cote macho
dirishani, Maya akaona atoe simu yake. Akakuta mmoja wa rafiki yake amemtumia
video na ujumbe. ‘It’s all over the social media. It went viral Maya! Ni mbaya mno. Renee
ameisambaza makusudi anasema ni ushahidi wake yeye kwa vyombo vya usalama.
Hakumtendea ubaya wowote Tunda na alimuonya Vic lakini Vic hakusikia. Ndio
maana tokea mwanzo alianza kuchukua video.’ Maya akashtuka sana.
Akawasha
ile video. Waliposikia sauti ya Vic, wote mpaka bibi yake wakamgeukia Maya. “Ni
nini tena?” Akauliza bibi Cote. Maya
akawasomea ule ujumbe. Bibi Cote akataka ile sauti iunganishwe na spika za gari
ili kuweza kusikia vizuri. Mpaka video inaisha Tunda ameanguka chini, Maya na
Net wakaelewa ni kwa nini Tunda alikuwa akilia na kushindwa hata kuwatizama
usoni.
Bibi
yake akamtizama Net akiwa amebadilika. Mwekundu mpaka anatetemeka midomo. “Haikuwa
kama anavyosema, Nana. Tafadhali naomba uniamini.” “Hapo ndipo mtakapojua
wakati wote nilipokuwa nikiwaambia juu ya Vic, na mimi sikuwa nikidanganya.
Lakini mlishindwa kuniamini. Kwa hili Net, hakuna jinsi ukajitetea na
kuaminika.” Maya akaweka msisitizo.
“Vic
amedanganya makusudi na kuongeza maneno aliyokuwa akiyasikia mtandaoni ili
kumuaminisha Tunda. Tafadhali Nana!” “Nataka unijibu swali moja tu Net. Jibu la
‘ndiyo au hapana’. Unanielewa?” Maya mpambe akasogea kabisa kama vile
waonane vizuri usoni. “Nakuahidi nitakuwa mkweli Nana.” “Nataka jibu la ndiyo
au hapana. Basi.” Akaweka msisitizo bibi Cote.
“Okay.”
Akakubali Net na yeye akionekana ameishaingiwa hofu kubwa kama anayejua swali
la bibi yake. Akajiweka sawa yule bibi.
“Vic alilala na wewe baada ya kufunga ndoa na Tunda? Ndiyo au hapana. Basi.”
Net akabaki kimya. “Net?” Net akamwangalia bibi yake. “Ndiyo au Hapana?” “Kwa
nini hutaki nijieleze Nana?” “Net! Kama kuna maelezo yeyote juu ya hili, mimi
na wewe tunajua wazi hukukusudia nijue. Na inaonekana zilifanyika juhudi za
makusudi ili mimi nisije hata kuambiwa. Nataka ibakie hivyo. Kwa manufaa ya
nani! Wewe unajua ni kwa nini ulificha. Sasa, kabla sijafanya chochote zaidi na
kujidhalilisha, au kumdhalilisha Tunda zaidi, nataka jibu kwa ufupi tu. Ndiyo
au Hapana?” Akamuona Net anatokwa na machozi huku akimwangalia.
“Son?”
Bibi yake akamwita taratibu kwa unyonge kama aliyekwishapata jibu lakini
anatamani isiwe vile alivyofikiri. “Ndiyo.” Akakiri
Net kwa machozi. Bibi yake alimwangalia kwa sekunde kadhaa. Yale macho tu, Net
alijua bibi yake ameumia sana. “Naomba usimamishe gari. Sasa hivi.” Dereva
akaegesha gari pembeni, mlinzi wake akashuka na kumfungulia mlango. Akatoka
ndani ya gari. Wakamuona ametoka akatembea kidogo, akainama huku ameshika
magoti. Mlinzi alisimama hatua chache pale alipokuwa ameinama bibi Cote.
Kwa Tunda.
H |
uku nyuma kwa Tunda, alilala mpaka
saa sita usiku, akaamka. Nesi aliingia amamkuta ametulia kimya kitandani.
Alipotaka kumpima, akakataa. “Ukaniletee mtoto wangu kwanza.” Tunda aliongea
taratibu tu akikwepesha mkono. “Mtoto yupo kwenye uangalizi mpaka kesho atakapo
ruhusiwa na daktari.” Nesi akamjibu kwa ustaarabu tu. “Basi na muda huo ndio na
wewe urudi hapa ndani. Hakikisha si wewe wala muuguzi mwingine anarudi tena
humu ndani bila mtoto wangu.” Tunda akamaliza hivyo na kufunga macho.
“Mrs Cote!”
“Naomba uzime na taa ya pale kwenye sinki.” Akamaliza Tunda bila kumwitika yule
nesi na hakufungua tena macho wala hakutaka amguse. Akamsikia yule nesi
ametoka. Baada kama ya dakika 20 akahisi taa kubwa zimewashwa. “Muone mama!
Muone!” Akasikia sauti ya mtu mzima ikiongea kitoto, Tunda akafungua macho kwa
haraka, akajua ameletewa mtoto wake.
Alikuwa mtoto wa kizungu kabisa. Wakamsogezea karibu. “Unauhakika huyu ni Cote!?” Tunda akauliza huku akilia. “Ndiye. Jitambulishe kwa mama.” Yule nesi akamwambia Cote huku akimfunika vizuri. Wakampandishia kitanda juu kidogo akawa kama amekaa kidogo ila uzito ukawa mgongoni. Nesi aliporidhika amekaa vizuri, Tunda akampokea kama asiye amini. Akasoma jina mkononi. ‘Cote Junior Cote’. Akambusu na kumkumbatia. “Naomba muda na mtoto wangu.” “Uliniambia nikikuletea mtoto utakubali nikupime. Naomba niangalie pressure kwanza.” Yule nesi wa pili aliongea na tabasamu la kubembeleza. “Asante sana. Nakushukuru.” Tunda akampa mkono.
“Naona pressure sio mbaya. Ukija kupumzika na kuamka tena, utajisikia vizuri zaidi.” “Hata sasa najisikia vizuri.” Akajibu Tunda, macho kwa mtoto wake. “Naweza kumnyonyesha?” Wakaangaliana wale wauguzi wawili pale kwenye chumba cha Tunda. “Nimesubiri kumnyonyesha huyu mtoto kabla hata hajazaliwa! Naomba msiniwekee kipingamizi.” Tunda akawasihi. “Alikuwa kwenye uangalizi mpaka wa mapafu. Naomba nimpigie simu daktari wake niulize kwanza.” “Kwani ni mgonjwa?” Tunda akauliza taratibu tu akimtizama Cote aliyekuwa amelala.
“Mpaka sasa kila kitu kinaonyesha yupo sawa kabisa. Ila naomba niulize kwanza.” Yule nesi ambaye alionyesha ni wa upande wa watoto, akamueleza vizuri tu Tunda, mpaka akaridhika. “Sawa.” Tunda akakubali. Yule nesi akatoka kwenda kuwasiliana na daktari wa watoto. Baada ya muda akarudi na kuambiwa anaweza kumnyonyesha tu. Wakamuweka sawa, Tunda akawaomba wamsaidie kumuamsha. Alifurahi sana alipofungua macho. “Anamacho yenye rangi kama ya Net!” Tunda aliongea huku akimshika vizuri baada ya nesi wake kufanikiwa kumwamsha.
Wakampisha. Japokuwa hakuwa akitoa chochote, lakini Tunda akafurahia kule kuona mtoto wake akivuta chuchu zake. Hakuwa akiamini kama ni yeye ananyonyesha. Cote alivuta hizo chuchu akaishia kulala tu, hakupata kitu. Lakini hiyo furaha aliyopata Tunda kwa kunyonyesha, hakuwa na jinsi yakueleza. Akamuweka kifuani, akamkumbatia kwa upendo, akajirudisha kulala. Nesi aliingia. Akamchukua mtoto kwa makubaliano akiamka tena, ataletewa tena mtoto. Ilikuwa usiku huo lazima Cote arudishwe alipokuwa amehifadhiwa kwa uangalizi zaidi. Bila hata dawa, Tunda akarudi kulala tena. Lakini wakampa dawa ya pressure.
Aliamshwa saa 10 ya asubuhi. Safari hii aliletewa mtoto aliyekuwa akilia njaa. Tunda alifurahi sana. “Labda akivuta akiwa na njaa yatatoka!” Akampokea huku akilia. Alipomuweka tu kifuani, akatulia na kuanza kuvuta. Tunda na wale manesi wakacheka. Akavuta kwa nguvu, akaanza kusikia chuchu zikisisimka. Akawaambia wale manesi. Wakamwambia haitachukua muda mrefu, ubongo utapata taarifa kuwa kuna chakula kinahitajika, yataanza kutoka.
Tunda
aliendelea kunyonyesha huku akimtizama huyo mtoto kwa furaha yote. Alishasahau
hekaheka za Vic na msaliti Net. Akili zikawepo hapo kwa mwanae. Baada ya kama
nusu saa wakamchukua mtoto, Tunda akasafishwa na kupewa dawa, akarudi kulala.
Tunda atoweka kwenye mazingira
ya kutatanisha.
Usiku
wa kwa kina Cote ulikuwa mzito sana. Saa 12 alfajiri, Net akawa amesharudi
kwenye chumba alichokuwa amelazwa mkewe hapo hospitalini. Hakumkuta yeye wala
kitanda. Hicho kikamfariji akijua hakuna baya lililompata usiku. Kama ingekuwa
ni kifo, basi angekuta kitanda tu na wangeshakuwa wamepigiwa simu. Akahisi
labda amechukuliwa kwa vipimo fulani. Akakaa hapo kidogo akitafakari kitu cha
kumwambia Tunda kutokana na kile alichoona Vic amemwambia. Akakaa kama dakika
tano zaidi, akaona atoke akamuulize mlinzi aliyempita hapo nje bila hata
salamu, aliyekuwa ameachwa siku iliyopita ili kumlinda Tunda .
“Amekuja
kuchukuliwa kama dakika 20 zilizopita. Amekwenda kufanyiwa MRI ili kujua kama
alivyoanguka jana kama kuna sehemu aliumia.” Mlinzi akatoa hayo maelezo kwa
Net. Net akaafikiana naye akiona inaleta maana. Akarudi ndani kwenye chumba
alichokuwa amelazwa mkewe, akakaa. Baada ya nusu saa Maya na bibi yake
wakaingia hapo. “Tunda yuko wapi?” “Mlinzi ameniambia wamekwenda kumfanyia MRI
ili kujua kama ameumia popote ndani.” “No. Nilisema Tunda asi asi... No.” Akatoka
bibi Cote kwa haraka.
“Nilikwambia
nini jana?” “Kila anapokwenda Tunda niwepo. Ila muuguzi aliyemchukua amesema ni
kipimo ambacho huko anapokwenda ni wafanyakazi tu ndio wanaruhusiwa kuingia.” “No.
No. Noooooo!” Bibi Cote akakataa kwa hasira sana. “Nahitaji kuzungumza na
kiongozi aliyekuwepo zamu jana.” Akaanza bibi Cote kwa sauti. Ile kelele yake
ikasikika na manesi waliokuwepo chumba cha pili wakatoka na mapokezi ndogo ya
hiyo gorofa aliyolazwa Tunda pia wakasogea.
“Jana
nilizungumza na uongozi wa hospitali na kumuacha huyu mlinzi kuwa amfuate Mrs
Cote popote atakapotakiwa kwenda, tena kama nimuhimu. Kwa nini Mrs Cote
anafanyiwa MRI bila mlinzi wake?” Tayari bibi Cote alikuwa akiwaka mpaka
daktari wa zamu akaja. “Ni muda gani umepita tokea apelekwe?” Yule bibi
akaunganisha swali kwa mlinzi. “Dakika 52 mpaka sasa.” Akajibu yule mlinzi.
Walipogeuka kuwangalia daktari na wale manesi, walishakimbilia chumbani kwa
Tunda. Wakafuata nyuma.
“Mrs
Cote hana kipimo cha MRI!” Akaongea dokta wa zamu akiwa anasoma kwenye tablet
yake. Wakaangaliana. “Piga simu MRI kuuliza.” Wote wakarudi mapokezi kwa
haraka. Kupigwa simu MRI, Tunda hakuwepo. Baada ya dakika 10, hospitali
ilishafurika polisi na ikawa imefungwa, hakuna kutoka wala kuingia. Anatafutwa
Tunda.
Bibi
Cote akataka apelekwe yeye mwenyewe kwenye chumba kinachohifadhiwa kamera za
hospitali yote. Akaongozana na mapolisi, Net, Maya na mlinzi wa bibi Cote nyuma
wakimfuata huyo bibi aliyekuwa akitembea kama anakimbia. Mlinzi aliyekuwa
ameachwa nje ya mlango wa Tunda naye alikuwepo. Akaeleza muda kamili Tunda
alipokuja kuchukuliwa. Muhusika wa zile kamera akarudi nyuma mpaka kwenye muda
ule aliosema mlinzi kuwa Tunda alikuja kuchukuliwa. Na kweli. Wakamuona muuguzi
akimtoa Tunda akiwa kwenye kitanda chake vilevile akionekana amelala.
Akamsukuma mpaka kwenye elevetor. Lift.
Akaonekana
ni kama anayejua anachokifanya na kuifahamu vizuri ile hospitali na zilipo
kamera zote. Hakugeukia kamera hata moja. Kwa hiyo hawakuona sura yake ila
mgongo tu. Wakahamia kwenye kamera ya ndani ya lift. Wakamuona anatoa simu
mfukoni, kama amempigia mtu simu, wanazungumza lakini ndani ya lift walikuwa
wakirikodi bila kuchukua sauti, kwa hiyo hawakusikia mazungumzo. Wasiwasi
ukaanza kuwaingia.
Tunda
hakuonekana hata kutingishika. Ni kama aliyekuwa kwenye usingizi mzito sana.
Wakamuona ameshuka naye mpaka gorofa ya tatu, akamtoa sehemu ya kuegesha
magari. Wakahamia kwenye kamera ya sehemu ya kuegeshea magari. Wakaona kijana
mmoja anatoka kwenye gari ndefu tu na yenyewe kama ya wagonjwa, ila nyuma
imefunikwa kabisa. Hamna hata madirisha. Wakasaidiana kumbeba Tunda,
wakamwingiza nyuma ya hiyo gari na yule nesi naye akapanda kulekule alipolazwa
Tunda. Yule kijana alionekana amevaa soksi usoni, akafunga mlango wa nyuma, akapanda
upande wa dereva na kuondoa gari kwa kasi.
Net
alitoka hapo anakimbia mpaka sehemu ya kuegeshea magari, akakuta kitanda kile
alichokuwa amelalia Tunda kimeegeshwa palepale pembeni, lakini Tunda hayupo. Hapo
hapo bibi Cote akatoa simu. “Samahani kwa usumbufu.
Lakini ninashida ambayo haiwezi kusubiri hata sekunde.” Akaanza bibi
Cote. Chumba kizima kikawa kimya. Akasikiliza kidogo kisha wakamsikia akijibu. “Asante. Lakini hii ni kwa masikio yako na macho yako tu,
mpaka nitakapokuruhusu uzungumze na mwingine.” Upande wa pili akajibu.
Kisha
akaendelea. “Mrs Cote amechukuliwa hapa hospitalini na
watu nisiowafahamu au bila ruhusa.” Akamgeukia yule muhusika aliyekuwa
akiwaonyesha kwenye Kamera. “Naomba
mtajie muda wa hiyo gari ilipoacha viwanja vya hospitalini na aina ya gari
yenyewe, ili anisaidie kufuatilia kwenye satellite. Sasa hivi tafadhali.
Nakuweka kwenye speaker.” Akamtajia aina
ya gari na muda. Huyo aliyepigiwa simu akauliza maswali machache sana akaomba
awarushie na wao kile anachokiona. Hilo likawa jema. “Nipo
hapa na polisi pamoja na uongozi wa
hospitali.” Akaweka angalizo bibi Cote kwa mtu aliyempigia simu ambaye
hakumtaja jina.
Baada ya sekunde chache wakachangaa wamerushiwa picha kamili na wao wakaanza kuona anachokiona yule mtu wa bibi Cote. Ile gari ilionekana imetoka pale hospitalini. Wakaifuatilia kwa kuiangalia. Ilikuwa ikienda kwa mwendo kasi. Na kwa kuwa walitoka alfajiri sana, bado nje kulikuwa na giza na hapakuwa na magari mengi. Ni kama dereva alijua ni wapi apite na nini chakufanya. Alivutwa kwa karibu, bado alikuwa amevaa soksi usoni. Na watu wa nyuma kwenye hilo gari hawakuonekana kabisa ila yeye tu dereva aliyekaa mbele.
Wakaona anapeleka gari kwenye barabara yenye magari mengi kidogo. Akaendesha mpaka barabara hiyo inapopita kwenye tunnel. Kama chini au ndani ya daraja iliyozibwa kote isipokuwa mbele na nyuma. Haikuwa tunnel ndefu lakini akapita hapo. Akavuta kamera kuona alipotokea. Hawakuona gari. “Mbona sioni tena hiyo Van/gari!?” Akauliza bibi Cote kwa wasiwasi. “Huyo dereva aliyemchukua Mrs Cote ametumia akili sana!” Akaongea yule mtu kule kwenye simu. “Sielewi!” Akaongeza bibi cote.
“Amepita chini ya daraja makusudi ili kutupoteza. Lazima kuna mtu wa tatu au wapo zaidi ya wawili ambao wanashirikiana.” Polisi mmoja wa palepale ndani ya kile chumba akaongeza. Wote wakamgeukia. “Ambaye atawasaidia kubadilisha gari. Alijua hiki kinachofanyika sasa hivi kitatokea. Mtafuatilia gari kwa satellite. Kwa kiyo ameliacha hilo gari ndani ya hiyo tunnel.” Maya akaanza kulia.
Hapo hapo ikapigwa simu ya polisi ambao wapo doria karibu na hiyo tunnel, waende kuangalia. Kisha askari wawili na wenyewe wakatoka kwa haraka wakikimbia kufuata hiyo tunnel. Baada ya dakika 5 tu, simu ikapigwa na polisi waliokuwa doria ambao walishawasili pale chini kwenye tunnel. Walitaarifu kulikuta hilo Van/gari nyeupe hapo lakini hapakuwa na mtu yeyote ndani.
Bibi Cote akafunga macho kwa muda. Wakamuona anapiga number nyingine simu. Iliita mara moja tu. “Wamemuiba mke wa Net hapa hospitalini asubuhi hii. Tafadhali nisaidie.” Akasikiliza kidogo. “Ndiyo.” Wakamsikia akijibu lakini akiwa ameishiwa nguvu kabisa. Akamkabidhi mmoja wa kiongozi wa polisi ile simu. Bila kujua anazungumza na nani, lakini akiwa amejiandaa kuwa lazima ni kiongozi mkubwa tu kwa kuwa ni bibi Cote, akaanza kwa heshima. Yule mtu alionekana kujitambulisha na kuomba taarifa kwa ufupi. Alikuwa mkuu wa CSIS. {Canadian Security Intelligence Service}.
Wote, bibi Cote, Maya, Net pamoja na mlinzi aliyekuwepo akimlinda Tunda wakatakiwa kwenda kituo cha polisi kwa mahojiano.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Lile tukio likachukua sura mpya na nzito. Mpaka Net
akawa kwenye matatizo kutokana na ile video na kile kilichozungumzwa na Vic kwa
Tunda. Walipofika tu kituo cha polisi waliambiwa Tunda anatafutwa na watu wenye
uzoefu sana. Anatafutwa kuanzia kwenye satellite mpaka kwenye lile gari
lililohusika kumtorosha Tunda, tayari wapo watu wataalamu kwenye eneo la tukio.
Wakifanya uchunguzi ndani na nje ya hilo gari kuona kama wanaweza kupata
fingerprints/alama za vidole au hata nywele itakayokuwa imeachwa humo ndani ili
ikapimwe ijulikane waliomchukua Tunda ni kina nani. Ila wakaomba ushirikianano
wao.
Kwa haraka sana bibi Cote akaitika bila shida.
Wakaingizwa kwenye chumba kikubwa sana cha mkutano chenye tv. Wakashangaa kuona
na kina Carter, Ms Emily na walinzi wote waliokuwepo jana na siku hiyo
wanaingizwa pale. Akafika mkuu wa kituo na kiongozi wa CSIS. Bibi Cote
akasimama na kusalimiana nao kwa kuwa aliwafahamu vizuri tu. Wakaongea kidogo,
kisha akaanza yule kiongozi wa CSIS.
“Ninaomba mtoe ushirikiano wenu wa asilimia 100,
ili kuweza kusaidia vyombo vya usalama kumpata kwa haraka Mrs Cote. Hakuna aliyekamatwa
wala kuhisiwa anahusika mpaka sasa. Jambo lolote lile mnaloona litasaidia hata
kidogo tu, tafadhali usiache kuwaambia polisi watakao husika kwenye kuwahoji
baada ya hapa.” Akaendelea yule mkuu wa CSI.
“Tutawawekea video ambayo ni muhimu sana kuiangalia
na kuisikiliza kwa makini ili kuweza kujibu maswali mtakayoulizwa baadaye
kutokana na video hii.” Wakakubali bila shida, lakini kila mmoja akiwa na
wasiwasi. Mara akaingia Vic na Renee, wakisindikizwa na polisi lakini hawana
pingu. Walikaa pembeni kabisa. Wakaongezeka polisi mle ndani ya kile chumba
chote na taa ikawashwa vizuri, kukawa na mwanga wa kutosha.
“Ili kuharakisha mambo na wote tuwahi kwenye
shuguli zetu, tafadhali usiongee chochote kama hujaulizwa. Na kila mmoja
atapata muda wa kuongea anachotaka, pale atakapopewa nafasi.” Akasisitiza mkuu
wa polisi. Kimya. Wakashangaa inawekwa video aliyochukua Renee ya mazungumzo ya
Vic na Tunda mpaka mwisho. Bibi Cote alibaki kimya. Maya akilia na Net ndio
hakuwa akitizamika. Mwekundu, anapenga kamasi kila wakati na macho yalikuwa
yamevimba haswa.
Ile video ikaisha. Watu wote kimya. “Utakaposikia jina lako likitajwa, tafadhali ongozana na polisi mpaka chumba cha mahojiano. Huko utapata nafasi ya kuuliza chochote, na ninarudia tena. Mpaka sasa hatuna muhalifu. Ila nyinyi mpo hapa kwa kuwa ni watu wa mwisho mliokuwa karibu na Mrs Cote, tunahitaji ushirikiano wenu.” Kimya. Wakaitwa walinzi wote waliohusika kumlinda Tunda siku iliyopita na mpaka anatoroshwa pale hospitalini. Wakahojiwa kila mmoja kwenye chumba chake huku wakichukuliwa video.
Bibi Cote.
Ikafika zamu ya bibi Cote. Akaongozana na polisi
mpaka chumba maalumu cha mahojiano. Wakajitambulisha kwake kwa majina yao wote,
bibi Cote akiwatizama tu, akaanza kuulizwa maswali. “Uliona na kusikiliza mazungumzo
ya Mrs Cote na Vic?” “Ndiyo.” Akajibu
bibi Cote kwa ufupi tu akiwa ametulia ila sio jasiri vile.
“Uliyajua mahusiano
kati ya Net na
Vic?” Bibi Cote akakunja uso kidogo. “Wakiwa
bado vijana wadogo. Ndiyo.” “Baada ya hapo?” “Net alikaa muda mrefu tu
bila kuwa na msichana yeyote. Ndipo akataka kumuoa Chloe, lakini alisema moyo
wake uko kwa Tunda. Ndipo akaachana na Chloe na kurudi nchini Tanzania
kumtafuta Tunda.” Akajibu Bibi Cote. “Wewe ulishawahi kukutanishwa na Chloe na
mkapata naye muda wa mazungumzo?” “Ndiyo.” “Ulimuonaje?” Bibi Cote akafikiria
kidogo. “Okay!” Akajibu bibi Cote huku akifikiria.
“Just Okay?” Yule anayemuhoji hakuwa ameridhika na
hilo jibu ikabidi aulize tena. “Kumbuka alitakiwa kuwa mkwe kwangu sio mke wangu au mume. Mtu sahihi kwangu alikuwa
Cote na ndiye aliyenioa. Sasa nani anaolewa na Nathaniel au anamuoa Maya ni juu
yao wao.” Bibi Cote akatumia akili za
haraka.
“Lakini si Vic?” Akamuuliza kwa kumtega. “Unamaanisha
nini?” Na yeye bibi Cote akauliza akijua anategwa. “Kwenye ile video, Vic
alimwambia Tunda wewe ndiye mtu pekee unayesimama kati yake na Net.” “Unakumbuka
kumsikia Vic akisema mimi nimesema hivyo?” Bibi Cote akauliza kwa makini
akimtizama machoni. “Hapana.” Akajibu yule anayemuhoji bibi Cote.
“Lakini anaonekana Vic anauhakika juu ya hilo.”
Akadakia mwenzake na yule anayemuhoji. “Kwa hiyo hapa mnataka nizungumzie juu
ya hisia za Vic?” Akawauliza bibi Cote akiwatizama kwa zamu. Kimya. “Kama
hakuna swali la nyongeza, naomba nikasaidie kutafutwa kwa Mrs Cote.” “Hiyo kesi
sasa hivi ipo chini ya CSIS. Sisi sasa hivi ndio tunafuatilia. Na hiki
unachokifanya sasa hivi ni hatua moja wapo yakupatikana kwa haraka Mrs Cote.”
“Kwa kuzungumzia hisia za Vic!?” Akauliza bibi Cote.
“Kwa kusaidia kujua motive au lengo. Aliyemchukua alikuwa na nia gani!” “Labda kwa ufupi tu, tuanze kwa kusema ni kwa sababu ni Cote. Pengine wanataka umaarufu au pesa. Kwa hiyo muda na wakati wowote mtu anaweza kupiga simu akitaka alipwe pesa ili wamrudishe. Mmeshalifikiria hilo?” Akaongeza bibi Cote. “Simu zenu zote zipo chini ya mitambo ya CSIS. Atakayepiga, aliyepiga, anayewasiliana tokea jana, wote mnachunguzwa. Hilo usiwe na wasiwasi nalo.” Bibi Cote akavuta pumzi na kujirudisha nyuma.
Net!
Kwa Net mambo yalimgeukia vibaya sana. Mpaka
akafika mahali akasema hatajibu tena kitu mpaka Logan awepo. Walianza taratibu
tu. “Mahusiano yako na Chloe yalikuaje?” “Mazuri tu mpaka nilipomuomba tuhamie
naye nchini Tanzania na kukataa ndipo mambo yalipoanza kubadilika.” “Kivipi?” “Chloe
alitaka nimuoe kisha nimuache pale nyumbani, halafu mimi niende popote ninapotaka.
Wakati mimi nilitaka mwanamke ambaye nitakuwa naye popote.” Akajibu Net.
“Ndipo ukamuacha?” “Ndiyo.” “Alilichukuliaje swala
la kumuacha?” Net akatulia kidogo kama anayefikiria. “Mr Cote?” “Alilia sana.
Lakini nilimwambia ninampenda mwanamke mwingine, ambaye ni Tunda.” “Oooh! Kwa
hiyo ulimwambia unamuacha sababu ya Tunda na si kwa kukataa kwake kwenda nchini
Tanzania?” Hapo Net akajua ameshajichanganya. Akatulia kidogo.
“Mr Cote?” Wakamuhoji tena. “Tunda alikuwepo kabla
ya Chloe. Lakini Tunda akanipotea ndio maana nikaamua kumuoa Chloe kabla ya
papa kufariki ili angalau ashuhudie nikiwa nimeanzisha familia kabla
hajafariki.” Akajibu Net. “Je, Chloe alijua kama unamtumia kwenye kutimiza
ndoto zako kwa babu yako?” Net akakunja uso. “Sikuwa nikimtumia mimi Chloe!”
“Ndivyo ulivyosema Mr Cote. Au tukuonyeshe ulichozungumza muda mfupi uliopita?”
“Najua ni nini niliongea.” Akajibu kwa jeuri Net.
“Je, Chloe alijua kuwa unamuacha kwa ajili ya
Tunda?” Net akatulia. “Mr Cote?” Net akanyanyua uso kuwatizama. “Chloe alijua
kama unamuacha kwa sababu ya Tunda?” “Huu muda tunaopoteza hapa, si tungeutumia
kumtafuta mke wangu?” Akagomba Net. “Hivi hapa ndio tunamtafuta Mrs Cote. Maana
aliyemchukua anaonekana anajua wazi ni nini anafanya. Kwa kuwafahamu nyinyi vizuri
sana na Mrs Cote, pengine kwa kupitia nyinyi wenyewe. Sasa kwa kujibu maswali
hapa, ndipo tutajua ni wapi pakumpata Mrs Cote. Sijui kama umeelewa?” Kimya.
“Narudia swali. Je, Chloe alijua kama unamuacha kwa
ajili ya Tunda?” “Ndiyo.” Akajibu Net akiwa ameshabadilika kabisa. “Kwa hiyo
ulimtamkia wazi kuwa unamuacha kwa ajili ya Tunda.” “Ndiyo.” Net akajibu huku
ameinama kama ambaye anazidi kuumizwa. “Mpo kwenye mahusiano na Vic kwa muda
gani?” Yule muuliza maswali wa kwanza akauliza. “Sipo kwenye mahusiano na Vic,
mimi ni mume wa Tunda.” Wote wakamwangalia na kalamu mkononi akiwa amekaa mbele
yao.
“Labda tuweke msisitizo. Tunahitaji ukweli.” “Na
mimi najibu ukweli. Sipo kwenye mahusiano na Vic.” “Tunao ushahidi aliotupa
jana Vic, ukionyesha mkinywa chumbani kwako na mkifanya mapenzi.” Net
akatingisha kichwa kwa kuumia sana.
“Ilikuwa hivi.” Net akaanza. “Nilijua mke wangu
angetoka jela na tungerudi naye kuishi huku. Katika kutengeneza chumba changu,
au watu waliokuwa wakitengeneza chumba changu ili kuchukua sura yangu na mke
wangu tu, niliwaambia watoe picha zote ambazo walikuwepo watu wengine na Vic
alikuwa mmoja wao.” Akaendelea Net.
“Niliwapigia simu Troy na Lean. Wakaja nyumbani
nikawakabidhi kumbukumbu za picha zetu tulizokuwa tumepiga sisi wanne, yaani na
Vic akiwemo. Nikawaambia itabidi nimtafute na Vic nimkabidhi. Waliondoka na
baadhi ya picha, tukikubaliana zinazobaki nije kumkabidhi Vic.” Net akaendelea.
“Nilitoka kazini. Ilikuwa mida ya jioni tu. Nikampigia simu Vic kumuomba apite
kesho yake pale nyumbani achukue zile picha. Vic akaniambia yupo karibu na
pale, anaweza kufika jioni hiyo. Sikuona tatizo.”
“Lakini haikuwa hivyo. Haikuchukua muda mfupi kama
alivyosema Vic kuwa yupo karibu na pale. Alifika nyumbani kama baada ya masaa
mawili. Alinikuta nimekaa mimi na mdogo wangu Maya. Tulikuwa tumemaliza kula,
tunakunywa tu. Maya akaniaga, akaelekea chumbani kwake kwenda kulala. Maana
ilishakuwa muda wa kwenda kulala. Ms Emily alishaondoka kwenda nyumbani kwake.
Mara nyingi Ms Emily huondoka muda unaofanana na Gino, ambaye ni mpishi wetu.
Carter ambaye miaka yote huwa anaishi hapo, na yeye muda wake wa kazi
ukishaisha, anahamia upande ulipo sehemu anayoishi. Ndani ya nyumba hiyo hiyo.”
“Vic akaagiza kinywaji. Carter alipoleta, akaaga
moja kwa moja kuwa anakwenda kulala. Akatuacha mimi na Vic. Kwa kuwa na mimi
nilitaka kulala ili niwahi kazini siku inayofuata, nikamwambia Vic anisubiri,
niende chumbani nikamletee picha zake. Akauliza kwa nini natoa picha zake
kwenye chumba changu? Nikamwelezea kuwa mke wangu anatoka jela. Tunaanza upya.
Nikamwambia ninaanza kumbukumbu mpya na mke wangu. Sitaki kuje kuwe na maswali
au picha zao sehemu nitakayokuwa ninalala na mke wangu.”
“Kama Vic alivyo. Akalalamika huku akiniuliza
maswali mengi juu yangu na Tunda, nikajaribu kumjibu, mwishoe kwa hasira,
nikamwambia mimi siwajibiki kwake kwa lolote. Nikaondoka nikaenda chumbani
kumchukulia vitu vyake. Ile nimeingia tu chumbani, Vic naye akanifuata na ile
juisi yangu niliyokuwa nikinywa. Akaniomba msamaha na kuniambia ni kweli
alitakiwa kuheshimu swala la kuoa kwangu. Na mambo mengine mengi. Alikuwa
ameshanikabidhi kinywaji changu tokea alipoingia. Kwa hiyo wakati anaongea,
mimi nikaendelea kunywa.” “Ilikuwa ni kinywaji gani?” Akauliza anayemuhoji.
“Juisi tu. Haina kileo. Ni matunda tu. Huwa
anatengeneza mpishi wetu pale nyumbani. Na utaipata hapo nyumbani kwetu tu.”
“Okay, endelea.” Akamtaka Net aendelee. “Vic ni mzungumzaji. Ni wale watu wenye
uwezo mkubwa wakuelezea jambo hata dogo na kulipa kisa kikubwa tu. Wakati
akiendelea kuzungumza, nikajisikia kama kizunguzungu. Nikamwambia. Akaniambia
labda ni uchovu tu, nijaribu kukaa.” Wakamuona Net akitingisha kichwa kwa
masikitiko.
“Nilikuja kustuka asubuhi. Nipo kitandani kwangu na
Vic na wote tupo uchi! Nilipaniki mpaka na yeye akaogopa maana nilifungua macho
nikamkuta pembeni yangu akinitizama. Nilipiga kelele na kuruka kitandani.
Kwanza nilikuwa nimechelewa kazini. Na si kawaida yangu yakupitiliza muda.
Kuangalia saa ilikuwa siku ya kazi na ni saa nne asubuhi. Ile kelele ikamfanya
Carter aje agonge chumbani kwangu.”
“Nikamuuliza ni kwa nini hakuniamsha au hata kuja
kuangalia kwa nini nimelala muda wote huo siku ya kazi! Akasema aligonga pale
chumbani, lakini Vic akamwambia nimeomba muda wa kupumzika! Ndio ikabidi Carter
aondoke bila kuzungumza na mimi mpaka hapo nilipomwita tena. Palepale mbele ya
Carter nikamuuliza Vic, ni kwa nini aliongea vile. Akasema usiku nilimwambia
kuwa nimechoka sana. Kwa hiyo akafikiri nahitaji muda wakupumzika kwa kuwa
nimekuwa na mambo mengi. Carter akaondoka.”
“Nikamuuliza na yeye kwa nini yupo pale? Akasema
aliniona asiniache kwenye ile hali.” “Hali gani?” Akauliza mmoja wa afisa
aliyekuwa akimuhoji Net maswali. “Na mimi nikamuuliza hivyo hivyo. Akajibu hali
niliyokuwa nayo ya uchovu na upweke. Akaanza kuongea mambo mengi. Mimi
nikamwambia achukue zile picha na aondoke asiwahi kurudi kuja kulala tena pale.
Nikamwambia mimi nimeoa na sitakuwa tayari kumsaliti mke wangu. Nikamsisitiza
kuwa nampenda mke wangu.”
“Vic aliondoka. Sikumsikia tena mpaka siku
aliporudi tena chumbani kwangu na mke wangu, akamkuta mke wangu amelala.
Nilimgombesha sana Vic na kumuonya asiwahi tena kurudia kuja kuingia chumbani
kwetu na nikamwambia asirudi tena pale nyumbani mpaka atakapo karibishwa kwa
kuwa mambo yamebadilika, mimi ni mume wa Tunda na pale ni nyumbani kwa mke
wangu pia. Akaondoka akilia huku akinikumbusha tulipotoka na mambo mengine.
Lakini mimi nikamwambia hiyo ni zamani nikiwa sijaoa.”
“Juzi nipo kwenye kuonja keki ya harusi yangu na
mke wangu, ndipo tukapata taarifa yupo nyumbani kwetu. Ikabidi kukimbia kwenda
kujua amefuata nini?” “Video inaonyesha alimwambia Mrs Cote kuwa anamazungumzo
na yeye. Kwa amani tu. Kwa nini unafikiri Carter aliingiwa na wasiwasi na
kumtafuta bibi yako kwa haraka?” Afisa mwingine akarusha swali kwa Net.
“Carter anamfahamu Vic. Huwa hana jema na hakubali
kushindwa. Anajua wazi kitendo cha Vic kutofika pale nyumbani mpaka akaribishwe
na hakuwa amekaribishwa kwa muda mrefu, Carter alikiri kwangu jana kuwa alijua
Vic atakwenda kumkorofisha mke wangu tu, ambaye hakuwa akijisikia vizuri. Ndio
maana alimtaarifu Nana kwa haraka.” “Kwa nini sio wewe? Hudhani ni kwa kuwa
anajua upo kwenye mahusiano na wote wawili kwa hiyo unaweza kutotilia uzito!
Ukapuuza umuhimu wa kuingilia kati?” “Hata Carter anajua sipo kwenye mahusiano
na Vic, na anajua nampenda mke wangu!” Net akajibu kwa kushangaa.
“Sasa kwa nini hakukutafuta wewe mwenye mke,
amtafute bibi yako?” Yule afisa akasisitiza swali lake. “Narudia tena. Carter
anamfahamu Vic tokea yupo mdogo. Jambo la haraka linalohitajika kufikia akili
ya Vic na akatulia na kumsikiliza mtu, nilazima Nana ahusishwe. Ni mtu ambaye
anaweza kumfanya Vic akatulia bila hata Nana hajafungua mdomo. Ule uwepo wake
tu, unatosha kwa Vic.” “Unafikiri ni kwa nini?” “Siwezi kuzungumzia hisia za Vic
jamani! Naomba nikamtafute mke wangu.” Net akasimama.
“Kabla hujaondoka. Tunaomba uangalie hizi picha na
video.” Wakamgeuzia laptop. Akajiona yeye na Vic wakifanya mapenzi chumbani
kwake. Net akakaa akiwa ameishiwa nguvu. “Mimi sijui Vic amefanya nini, lakini
mimi sikumbuki hata kufanya mapenzi na Vic miaka ya karibuni. Ni zamani sana
kufanya mapenzi na Vic, hata kabla ya Chloe. Na sitajibu swali jingine lolote
mpaka awepo mwanasheria wangu.”
“Mimi nafikiri hivi Mr Cote.” Akadakia mmoja wa
wale maafisa wawili waliokuwa wakimuhoji maswali, kabla Net hajanyanyuka tena.
Alikuwa ni afisa mwanamke. Alionekana yupo makini sana. “Unafikiri nini?”
Akauliza Net akiwa amekunja uso. “Nafikiri hivi. Baada ya kupata mtoto
aliyekufanya umchukue Tunda kutoka Afrika. Huoni umuhimu wake tena. Na kwa kuwa
umebahatika kupata mtoto tayari tena akiwa salama, umeamua kumtowesha kabisa
Tunda. Sio kwa talaka ili asije kuchukua mali zako.” Net akashangaa sana.
“Unawezaje kusema hivyo!?” Net akashangaa sana. “Kwa
yote uliyozungumza hapa, ukijaribu kukana mahusiano yako na Vic, mpaka
tukakuonyesha ushahishi wako ukifanya naye mapenzi. Tena miezi michache tu
iliyopita. Tena bila kushurutishwa! Ukionekana unafurahia kabisa unachokifanya
na Vic kwa hisia zote! Wazi inathibitisha alichozungumza Vic ni kweli. Kuwa,
kilichokufanya umchukue Tunda ni mtoto tu. Kwamba, ulikwenda kuachana naye
baada ya haya mapenzi mazito hapa.” Akamuonyeshea ile video yake na Vic kwa
kidole akigusa ile laptop, Net akafunga ile laptop kwa nguvu.
“Sasa mimi nakuhakikishia Mr Cote. Nitakukamata tu.
Nitatafuta ushahidi wangu wote juu ya hila yako na hao uliowatuma kumtorosha
Tunda, na nitakufunga. Hata kama mtatumia akili ya namna gani kumficha Tunda.
Mimi nitawakamata!” Yule afisa ambaye alikuwa mwanamke akasimama kwa hasira na
kwa kujiamini mbele ya Net. “Na usikae mbali wala usisafiri mpaka uchunguzi
utakapo kamilika. Umenielewa?” Akamgeukia Net. Walikuwa watatu tu kwenye hicho
chumba cha mahojiano. Wao maafisa wawili. Wakike na kiume, pamoja na huyo Net
waliyemchemsha kupita kiasi.
“Mr Cote! Huruhusiwi kutoka nje ya nchi mpaka
uchunguzi utakapo kamilika. Na ujue utakuwa ukifuatiliwa. Usifanye watu ni
wajinga. Mtu mmoja tu Tunda, hawezi akawa anafatwa katikati ya ulinzi mkali
kiasi hicho. Halafu achemshwe mpaka aanguke na kupoteza fahamu na ulinzi ukiwa
upo hapohapo wanamtizama tu Vic kama sio wote wanajua mahusiano yako na Vic!” Akaendelea yule dada huku akiwa amesimama.
“Halafu eti leo amelazwa hospitalini, anatoroshwa
kirahisi kabisa katikati ya ulinzi mkali kiasi hicho! Halafu eti mtu
anayemtorosha anajua wapi zipo kamera, na jinsi yakuzikwepa asionekanike! Wapi
apite na nini chakufanya kirahisi tu! Akamudu kuondoka na mgonjwa asiye na
fahamu, na kitanda kizima, asiulizwe wala kuzuiwa na yeyote yule, mbele ya
mlinzi aliyepewa maagizo asiruhusu Tunda atolewe pale! Kama hana baraka za mtu
wa ndani ni nini?” Bila kuongeza neno Net akasimama na kumpita yule afisa pale,
akatoka kabisa pale ndani ya kile chumba kimyakimya.
Kwa Maya.
Maya alichukuliwa na yeye mpaka kwenye
chumba cha mahojiano. Akakutana na maafisa wawili vijana. Walijitambulisha kwa
majina yao kamili lakini akili za Maya haikuwa kwenye kumfahamu yeyote kwa
wakati ule, akabaki akiwatizama na macho mekundu kwa kulia. “Mahusiano
yako na Vic yakoje?” Afisa mmoja akaanza
kwa hilo swali na kumshangaza sana Maya. Akabaki ametoa macho kama anayemuuliza
“WHAT!”
“Miss
Cote?” Akamwita kama kumstua. “Mlisema kujibu maswali hapa si lazima, si
ndiyo?” Akauliza Maya. “Ndiyo.” Akachukua pochi yake akasimama. “Nilisikia
ukisema Tunda ni dada ambaye hukuwahi kufikiria kama unaweza kuja kuwa naye.
Unampenda, anakupenda na kukujali. Si ndiyo?” Afisa mwingine akamuwahi. Maya
akageuka alishafika mlangoni. “Kama unataka arudi, lazima utusaidie. Na kwa
kadiri tunavyochelewa ndivyo itakavyokuwa ngumu kumpata.” Akaongeza yule afisa.
Taratibu tu.
“Sasa
kama unalijua hilo, kwa nini bado umekaa hapo ukitaka kuzungumzia habari za mtu
kama Vic!?” Maya akauliza. “Kwa nini si
Vic?” Akamuuliza kwa haraka. Maya akageuka vizuri. “Ukiangalia kwenye mitandao
yenu ya kipolisi, jina Maya Cote ni baya sana. Lakini
ni sababu ya Vic. Hakuna aliyetaka kuniuliza na kunisikiliza isipokuwa Tunda,
juzi.” Maya akaanza kutokwa na machozi. “Kama
Vic ndiye aliyemchukua Tunda, nawahakikishia kabisa, hamtampata Tunda kwa
kumuhoji mtu yeyote hata yeye mwenyewe Vic. Kwa kuwa ni mzuri sana katika uovu
wake.” Maya akarudi na kukaa na kujifuta machozi.
“Aliniingiza
mimi kwenye madawa ya kulevya. Akahakikisha sitoki. Na nilipotoka, akahakikisha
ananirudisha. Vic anatumia madawa ambayo akikulevya au akiwapa watu wake
wakuleweshe, kesho yake yale madawa yanapoisha mwilini, hukumbuki ulichofanya.
Ukiwa kwenye hiyo hali, atahakikisha anakupiga picha wakati unafanyiwa uchafu
na kukuchukua video kama ushahidi wake kuwa ulifanya kwa hiari.” Maya
akaendelea.
“Hakuna
aliyeniamini mimi, wala kuchukua muda wake kuchunguza vyanzo vyote vya uchafu
wote juu yangu mnaouona mtandaoni, isipokuwa Tunda ambaye wamemuiba. Sasa
nafikiri sasa hivi Net ataamini na kuonja kule Vic alikokuwa akinipitisha
mimi.” “Kwa nini unasema hivyo?” Akamuuliza tena.
“Nakujibu
swali hili tu, halafu nakwenda kumtafuta Tunda. Mimi mwenyewe bila hata msaada
wa Cote.” “Kwa nini?” Akamuuliza tena. “Nimekwambia nitakujibu ‘kwa nini’ ya
kwanza tu.” Bado alikuwa akiongea na kumwangalia yule afisa aliyefanikiwa
kumrudisha wakati anataka kutoka.
“Okay.”
Akajibu kumuonyesha ameridhia. “Siku anayosema Vic kuwa aliitwa kuja kulala
pale na Net, mimi nilikuwepo na Net tukizungumza. Akaniambia Vic atafika hapo
kuchukua nafikiri picha zake za zamani au vitu ambavyo vilibaki kwa Net kwa
muda mrefu. Nisikilize kwa makini.” Maya akajiweka sawa. “Mimi huwa siwezi hata
kumtizama Vic kwa sekunde nyingi. Amejawa ushetani usoni kwake, na
ameshanitenda bila watu kunisaidia na kuniamini. Amenichafua, na kuniharibia
sana.”
“Anyways.
Alipoingia tu Vic, sikutaka hata kuhisi uwepo wake. Mimi niliwaacha sebuleni,
nikaenda kulala. Kesho yake asubuhi wakati mimi nakwenda kazini, nikashangaa
kukuta magari yote ya Net na Vic yapo nje!” Maya akatulia kidogo. “Katika watu
waadilifu wa kazi na washika muda ambao nimeshawahi kukutana nao, Net ni mmoja
wao mbali na Papa pamoja na Nana. Net hajawahi na hajui kuchelewa kukoje. Mbali
na mali nyingi alizorithishwa sasa hivi, Net alirithi huu usemi tokea anakua.
Unasema hivi, ‘Early is on time. On time is Late.
Late is unacceptable.’ Hayo ndio
maisha ya Net.” Maya akaendelea.
“Nasisitiza
kuwa, Net hajui kuchelewa ndio inakuaje. Na ukitaka kumkasirisha Net, usijali
muda. Kila mtu anayefanya kazi na Net, anajua hilo na kuliheshimu. Basi. Mimi
nikashtuka sana na kuogopa ni nini kimempata Net nakushindwa kuwepo kazini, na
imekuaje mtu aliyekuwa akimlilia mkewe masaa machache kabla ya Vic kuja
nyumbani, leo alale na Vic mpaka asubuhi!”
“Maana
Nana alikuwa yupo safarini. Akampigia simu Net kumuulizia maswala ya Tunda huko
jela. Net akaanza kulia kwa Nana kuwa hajasikia chochote. Na alimtuma tena mwanasheria mwezi huo ambao
yeye hakwenda, lakini Tunda alikataa kutoka. Baada ya kuzungumza wote na Nana,
baada ya kama nusu saa ndio Vic anakuja kuchukua mizigo yake, eti Net aje alale
naye mpaka asubuhi! Wewe inakuingia akilini?” Maya akauliza. Safari hii
akawatizama wote kwa zamu.
“Labda
alikuwa amezidiwa na Vic akamkumbushia Net mapenzi.” Yule afisa mwengine
akajibu. “Net haongozwi na hisia. Wakati wote, Net amekuwa akimtanguliza Mungu.
Alikaa muda mrefu tu bila kufanya mapenzi. Tena kwa kujua kutoka hata kwa Chloe
aliyekuwa mchumba wake aliyetaka kumuoa. Chloe alikuwa akilalamikia marafiki
zake, ndio ikasambaa na kutufikia kuwa Net ameshindwa kufanya naye mapenzi
amemwambia mpaka ndoa. Muiteni Chloe mumuulize kama Net ni mtu wa kukimbilia
kitandani na wasichana.”
“Labda
kwa Vic!” “Ndivyo hata na yeye Vic atakavyowaaminisha na kuwapa ushahidi.
Lakini mimi sijali kile utakachoamini. Ila nataka kukwambia hivi, siku ile
asubuhi ilibidi nirudi kumuuliza Carter kulikoni. Carter akasema alikwenda
kugonga chumbani kwa Net, akatoka Vic akiwa amevaa shati la Net na kumwambia
aondoke awapishe, Net amechoka. Nikamwambia Carter kuna kitu hakipo sawa, Net
sio mchokaji katikati ya kazi na kushindwa kuwepo kazini kwa wakati. Mimi nikaondoka.”
“Kwenye
saa tano hivi, asubuhi, Net akaja ofisini kwangu na kuanza kuniapia kuwa hakuna
kitu kilichotokea kati yake na Vic
anaomba nimuamini. Alionyesha kupaniki sana. Akasema hata kama angekuwa dhaifu
kiasi gani, asingethubutu kulala na Vic pale mbele yangu huku nikijua ameoa.
Angelala naye popote lakini sio pale na hajui ni nini kilitokea na kupitiwa na
usingizi mzito kiasi hicho mpaka kesho yake.” Maya akaendelea.
“Mimi
nimetumiwa hiyo video na Gina. Vic
akizungumza na Tunda. Nimejua mambo yafuatayo. Na nitamwambia Tunda
nitakapompata. Na nitampata Tunda na nitamwambia ukweli.” Maya akaongea kwa
uhakika. “Siwezi nikamruhusu Vic amtoe Tunda kwenye maisha yangu. Hata kidogo!
Amechukua kila kitu kwangu, lakini si Tunda.” “Ni mambo gani umejua?”
Akamuuliza kwa haraka maana Maya alishaonyesha kukasirika zaidi.
“Kwanza,
Vic haruhusu mtu yeyote kuwa na Net.” “Mbona alimwacha Chloe akawa na Net?”
“Nani amekwambia alimwacha? Ni mshenzi Vic asiyeweza kujisaidia. Ni vile Chloe
hakujua ni vipi Vic anavyomtenga na Net. Na alitumia akili za ujanja, akamfanya
mpaka Net ajithibitishie kuwa Chloe si mke wake. Na kwa taarifa yako tu, Vic anahusika kwa asilimia 100 kwa Chloe
kuachwa na Net.” “Ki vipi?” Akauliza
yule afisa aliyemrudisha.
“Sitakujibu
hilo sasa hivi, mpaka unisaidie kumpata Tunda. Nisaidie kumpata Tunda, ndio
nitajibu maswali yako yote na
nitakueleza ubaya wote wa Vic na vile hata wazazi wake wanavyomsaidia na ndio
maana hamuwezi kumkamata Vic kwa hizi njia zenu. Ila kama nilivyokwambia. Nia
ya Vic ni kumtoa Tunda pale ndani kwenye ile nyumba ya ndoto zake. Vic tokea
anakuwa alikuwa akiota kuja kuishi mle ndani kama mke wa Net. Ndio maana tokea
mwanzo kabisa kwenye mazungumzo yake yote kwa Tunda chakwanza kabisa,
alihakikisha anamgombanisha na watu wote wa mle ndani ya ile nyumba. Mpaka
wafanyakazi waliomuonyesha Tunda upendo, amewachafua kwa Tunda.”
“Pili,
amemfanya Tunda ajione yeye hana uwezo wa kuwa mke wa Net, na Net hampendi ila
anampenda mtoto aliyebeba. Akamwaminisha hata cheo alichopewa Tunda,
hakistahili kwa sababu ya historia mbaya
ya nyuma ya Tunda. Ambayo haipo hata nusu na historia yakutisha ya Vic. Na
akamuaminisha ni kwa kuwa hana elimu wakati Tunda anauwezo mkubwa wa kutenda na
kufikiria kuliko mpumbavu Vic. Na nitakwambia kwa nini wakati naondoka.”
“Tafadhali!”
Yule afisa aliyefanikiwa kumtuliza akajiweka sawa. “Nikikwambia kitu,
unaniahidi kunisaidia kumtafuta Tunda?” Maya akamuuliza akitaka uhakika. “Hata
hapa nilipo namtafuta.” Akamjibu yule afisa. “Hapana. Usinifanye mimi mtoto
mdogo. Mnachofanya hapa ni kupoteza muda na kumtafuta mtu wa kumtupia lawama
ili mfunge kesi. Mimi nataka uwe na mimi
kufuatilia kila nitakapokuwa nikipata fununu ya mtu aliyemteka Tunda.” “Wewe
utajuaje?” Maya akakunja uso.
“Wewe
hujasikia kuwa mimi nilikuwa nikila madawa yakulevya na kufanywa mapenzi mpaka
club!?” Maya alimtupia swali la moja kwa moja na kumbambaisha sana yule afisa. “Najua
unajua. Kwa hiyo nitaanza na walevi wenzangu.” “Nilijua umeacha!?” “Kumbe
unanifuatilia!?” Maya akamuuliza kwa kumsuta. Alikuwa kijana mzuri sana.
Alionekana anajua kazi yake, na mzoefu. Na afisa mwenzake pia akamgeukia kama
anayemsuta. Akaonekana kuishiwa hoja.
“Kwa
hiyo unaahidi kunisaidia au niondoke?” Maya akamuuliza tena. “Kila kitu
kitafanyiwa utaratibu wa..” Maya akanyanyuka kwa hasira. “Mbona unaondoka?” Na
yeye akasimama. “Mimi na wewe wote tunajua unaongea tu.” “Hapana.” “Ni mara
ngapi mimi nimekamatwa nikiwa nimelewa na madawa ya kulevya na niliyekuwa naye
pia akiwa amelewa. Mlishawahi kujiuliza nyinyi kama watu wa usalama kwa raia,
nani anakuwa anatupiga picha na nani anauzia vijana wadogo kama sisi hayo
madawa?” Maya akauliza kwa uchungu sana.
Wale
maafisa wote wawili, aliyekaa na aliyesimama, wakabaki wameduaa. “Exactly!”
Maya akataka kutoka. “Subiri kwanza Miss Cote.” “Unanipotezea muda. Na kama
ulivyosema. Tunavyozidi kuchelewa hapa ndivyo itakavyo kuwa ngumu kuja kumpata
Tunda. Na mimi sipo tayari kumpoteza Tunda.” “Nitakusaidia Miss Cote.” “Hapo
tunaweza kuzungumza.” Maya akarudi
kukaa. Na yeye akakaa.
“Nakusikiliza.”
“Ulisema jina lako ni nani tena?” Maya akauliza. “Roy.” Akadakia afisa
aliyekuwa akiwasikiliza. “Hapana. Sio wewe. Ni wewe. Jina lako. Moja tu, la
kwanza. Usinitajie majina mengi mpaka la baba yako. Moja tu ili baadaye usianze
kunizungusha na taratibu zenu za kiusalama mlizofundishwa shuleni.
Utanichelewesha.” Maya aliongea kama asiyetaka kupotezewa muda zaidi. “Malcom!”
Akajitambulisha yule afisa aliyefanikiwa kumtuliza. “Okay.” Maya akasikika
ameridhika.
“Kama Vic ndiye anayehusika kumteka Tunda,
hamtampata kwa kumuhoji yeyote kati yetu. Kwa kuwa mpaka sasa Vic anamajibu
yote sahihi, tena kisheria, kama anayeulizwa mahakamani, kuhusu kila mmoja wetu
hapa mpaka walinzi wanaolipwa na Cote. Tena atakuwa alikuwa nayo hayo majibu
tokea hajafanya kitu hata kimoja. Namaanisha tokea hata hajamfuata Tunda
nyumbani.” Akaanza Maya.
“Ila
kwa kuwa nimpumbavu, mjinga wa mwisho kabisa. Na mimi namjua tokea
tunamgombania Net, ipo sehemu atakosea tu. Na hapo ndipo tutamkamata. Hana
akili ya kufanya jambo kubwa kwa muda mrefu! Hawezi.” “Unazungumza kama ambaye
umeshakuwa naye kwenye tukio fulani!” Malcom akaongeza kijanja, sio swali. “Sana
tu. Nisikilize kwa makini.” Maya akajiweka sawa. Malcom na Roy wakajiweka
vizuri, kalamu mkononi.
“Kijana
wa mwisho aliyenitafutia Vic ili anirudishe kwenye madawa ya kulevya ili
nisichukue cheo cha Nana, alianza naye kwangu vizuri tu. Anaitwa Andy.” Maya
akaanza. “Lakini kadiri nilipotaka kumfahamu Andy, nikagundua ni wa Vic kwa
kuwa hakuwa amemuandaa vyakutosha. Bila Vic kufikiria, kwa kila swali
nililokuwa nikumuuliza Andy, Vic akaishia kumpa majibu ya maisha anayoishi baba
yake yeye ambayo ni ya hali ya juu sana hayaendani na yeye Andy hata kidogo.”
“Andy
akaanza kunitajia biashara anazofanya ambazo ndizo anafanya baba yake Vic. Saa,
nguo, pafyumu, viatu na vitu vingi tu vya thamani alivyokuwa akimpa Andy, aje
navyo kwangu, yule kijana mwenyewe alikuwa akijishangaa jinsi alivyovaa vitu
vya thamani.” Roy akacheka kidogo, Malcom alitoa tabasamu tu.
“Wakati
amevaa mwenyewe?” Malcom akauliza. “Ehe! Yaani hapo ndipo nilipojiridhisha kuwa
Vic ni mjinga. Anampa majina ya biashara ambazo anatakiwa anidanganye kuwa
anafanya, ukimuuliza juu ya hizo biashara, hata yeye mwenyewe Andy alikuwa
hazijui hizo biashara!” “Lakini ulihisi tu hukuwa na uhakika kama ni Vic?” “Nitakuja
kupata uthibitisho kamili juu ya hilo, na wewe utakuwa shahidi. Nipe muda tu.
Lakini japokuwa Andy alikuja kama tapeli kwangu, nikaishi naye vizuri sana,
mpaka akashindwa kunitenda vibaya. Nilikuja kumsikia akimwambia Vic kwenye simu
kuwa, hataweza kunitendea mimi ubaya, kwa kuwa mimi ni mtu mzuri na sionekani
kama naweza kuja kumdhuru.” “Ulijuaje kama anazungumza na Vic?” Malcom
akauliza.
“Ndio
nimekwambia nitakupa uthibitisho. Kwa kuwa sasa hivi amenichokoza vibaya sana,
nitahakikisha anawekwa mwangani.” Akabaki akimtizama. “Najua sasa hivi chochote
nitakachoongea na wewe utanipuuza kwa kuwa watu wananichukulia mimi kama mlevi
tu.” Maya akaongea kwa unyonge na kulalamika, akainama kama anayefikiria.
Wakamuona anajifuta machozi.
“Mimi
sitakuchukulia kama mlevi. Nitaheshimu kila kitu utakachoniambia na ninakuahidi
nitafanyia uchunguzi.” Maya akamwangalia na kujifuta tena machozi. “Kweli?”
Akamuuliza kwa upole. “Kweli. Nakuahidi hivyo.” Malcom akamthibitishia
kwa utulivu tu. Maya akamtizama, wakabaki wakiangaliana kama wanaosomana, Maya
akainama kidogo kama aliyeridhika na kile alichoona machoni kwa Malcom.
Roy
akakohoa kidogo. “Hiki kilichompata Net. Akaamka akiwa hajui kilichotokea usiku
uliopita, ndicho kilitupata siku moja, mwanzoni kabisa mimi na Andy.”
Akaendelea Maya baada ya Roy kuwashtua kwa kukohoa. “Ile nyumba aliyokuwa
akiishi Andy, nilijua wazi amekodiwa na mtu. Hiyo ni habari ya siku nyingine.”
“Siku
hiyo tulitoka kwenye movie jioni tu. Tukarudi nyumbani kwa Andy, mimi mwenyewe
nikaenda kuchukua juisi iliyokuwa kwenye friji. Tulinunua mimi na Andy.
Tukaiweka kwenye friji. Tuliagiza pizza. Ndio tukawa tukila na hiyo juisi.”
“Hamkuwa mkinywa pombe?” Akauliza Malcom. “Kumbuka nilikuwa nimetoka rehab.
Sikuwa nikinywa kileo chochote kile. Andy alikuja kunipenda sana. Na
nilishamsimulia maisha machafu niliyoishi nyuma. Akaniahidi kunilinda.” Maya
akainama kama anayefikiria.
“Kwa
hiyo hatukuwa tukinywa kabisa.” Maya akaaamua kuendelea tu aache kufikiria. “Lakini
tulipokula ile pizza na kuinywa ile juisi siku ile, tukashangaa kuamka asubuhi
tukiwa kitandani kama tuliofanya mapenzi usiku. Tuliamka tukiwa uchi kabisa! Tukaulizana
na Andy, wote kumbukumbu ziliishia tukiwa tunakula. Kwenda pale sebuleni
tulipokuwa tukila, ni pasafi kabisa hata boksi la piza limetupwa! Mimi na Andy
tukashangaa. Tukaishia kutaniana labda tulifanya hayo yote tukiwa usingizini.”
“Basi,
lakini mimi nikahisi ni ile juisi tu. Nilimwambia Andy nataka kuonja au kuinywa
tena ile juisi ili tujiridhishe kuwa ilikuwa sio ile juisi, lakini ukweli
nilikuwa na hamu yakulewa tu. Nafikiri kule kunywa kwa mara ya kwanza na
kunilevya, kulitibua kiu.” “Ulikunywa?” Akauliza Malcom taratibu tu. “Ndiyo.”
Maya alijibu akiwa ameinama. Kwa unyonge na aibu. “Nakumbuka Andy alinikatalia
kabisa na kuniambia anakwenda kuimwaga. Mwanzoni Andy alihakikisha sirudii
ulevi. Alinilinda kwa kila namna ili nisiingie kwenye matatizo tena. Ukweli
mwanzoni alijitahidi.” Maya alimtetea kidogo, akaona aendelee tu maana wale
maafisa wote walibaki kimya wakimtizama.
“Anyways.
Haijalishi tena. Turudi kwa kile nilichokuwa nikiwaambia juu ya ile juisi.
Wakati anakwenda kuifuata jikoni kwenye friji ili aimwage, simu yake ikaita.
Nakumbuka ni kama akakasirika baada yakuangalia simu yake, akatoka kwenda
kuzungumza nje, na mimi nikaikimbilia ile juisi na kwenda kuinywa. Nililewa
tena.” Maya akaongea kwa upole.
“Hudhani
kwamba ndilo lilikuwa lengo la Andy?”
Akauliza Malcom. “Kwa ile juisi na mwanzoni, hapana. Alinikataza kabisa
na alikuwa akienda kuimwaga ndipo hiyo simu ikaingia. Lakini sema Andy anakuja
hapa.” Maya akajiweka sawa. “Baada ya ile siku ni kama akaacha au kama
aliyeshindwa tena kunizuia kwenye ulevi. Lakini nilipokuja kuamka kesho yake
akaumia sana na kunilaumu kwa nini sikumsikiliza wakati alinionya nisinywe tena
ile juisi? Akaongea kwa kuumia sana. Niliondoka pale kwa kuwa alikuwa
amekasirika na mimi sikuwa nimerudi nyumbani hiyo ilikuwa siku ya 4.”
“Akanipigia
simu baada ya kama siku mbili nilipoondoka, akaniomba msamaha wa kukasirika na
kuniambia amenitayarishia kitu kizuri zaidi. Nilipokwenda nikakuta amenunua
wine kitu ambacho alijua wazi sitakiwi kunywa, ila akanipa akaniambia tufurahie
tu, hataruhusu nilewe sana. Ila hakuonekana na furaha kabisa. Kwa kuwa mimi
nilikuwa na kiu, nikanywa sana. Sikumbuki kumuona yeye hata kumaliza glasi ya
kwanza aliyokuwa amejimiminia. Ila mimi nakumbuka kunywa tena na tena. Safari
hii nakumbuka mpaka nikamaliza chupa yote. Siku hiyo nakumbuka kilichonilevya
ilikuwa ni ile wine. Na nilifanya makusudi, yaani nilitaka kulewa.”
“Ilipoanza
tu pombe, yakaja na madawa. Lakini chakushangaza, hata mwezi haukuisha,
zikaanza kutumwa picha zangu nikiwa nimelala chumbani, au sebuleni kwa Andy
tukiwa tunafanya mapenzi. Kilichonishangaza ni mpaka picha za siku ile ya
kwanza kabisa yulipokunywa juisi na Piza! Sasa jiulize, ni nani aliyekuwa
anatupiga hizo picha na kutuchukua video vizuri tu. Sio kwa kuegeshwa kamera.
Hapana. Picha na video nzuri kabisa. Zikionyesha kila upande, kama hapakuwa na
mtu wa tatu ambaye aliyekuwa na funguo,..” “Na uhuru wa kuingia ndani kwa
Andy.” Akamalizia Malcom.
“Hapo
umeelewa.” “Labda rafiki wa Andy!” Akaongeza Roy. “Andy hakuwa na rafiki.
Alisema alihamia kwenye huu mji akiwa mgeni na mimi ndiye mtu pekee niliyekuwa
nikifahamiana naye. Sikuwahi hata kumuona akisalimiana na mtu.” Roy akakunja
uso. “Najua huamini. Na wewe sio wa kwanza. Hata Net naona sasa hivi ndio
ataelewa kile nilichokuwa nikiwaambia na kunipuuza. Na ipo siku nitathibitisha kuwa
ni Vic na ndipo Mungu atamuhukumu kwa sheria.” Mara mlango ukafunguliwa.
“Miss
Cote, asante kwa ushirikiano wako. Tutakapokuwa na swali la nyongeza
tutakutafuta, ila kwa sasa unaweza kwenda tu.” Aliingia na kuongea baba mmoja
mtu mzima kabisa. Ndipo Maya akageuka pembeni akaona dirisha kubwa la kioo.
Akajua wapo watu wengine waliokuwa wakiwasikiliza.
Maya
akarudisha macho kwa Malcom. Akamuona amebadilika kabisa usoni, akarudisha sura
ya kazi. Ile sura ya kumbembeleza wakati anamuhoji maswali ikapotea. Maya
akajua alikuwa vile ili tu kumtumia kumtoa maswali. Hakumaanisha chochote.
Akainama kama aliyeumia sana. “Ilikuwa kidogo tu nikuamini!” Akamwambia Malcom
kwa macho na sauti yakukatishwa tamaa. Maya akachukua pochi yake akatoka bila
kuongeza neno jingine. Akawaacha pale wale maafisa wawili. Malcom na Roy pamoja
na yule aliyeingia pale kama kiongozi wao.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Familia
hiyo ya Cote ilionja uchungu ambao hata hawakuwahi kudhania maishani. Tunda
aliibwa. Badala ya watu kuwahurumia, wakageuka kuwa wao ndio watuhumiwa.
Mitandaoni kukajaa tuhuma zakupita kiasi. Kila mtu ndani ya hiyo familia akituhumiwa
kivyake.
Anaibiwaje
mgonjwa katikati ya ulinzi mkali kiasi hicho kama sio njama za mtu kutoka
ndani! Ni nani mwenye uwezo huo kama sio amesaidiwa na mtu kutoka ndani! Vic
yupo sahihi. Kila mtu akawa upande wa Vic. Mtoto ambaye alikuwa akisubiriwa kwa
hamu zote, na matayarisho kama kitoto chakifamle, kila mtu akibashiri ujio wa
Cote, habari ikawa imegeuka. Yeye hayupo tena kwenye picha. Ila picha za baba
yake akifanya ngono mtandaoni na hawara.
Ilikuwa
hali ya kusikitisha iliyojaa wasiwasi kwa familia hiyo ambayo nyumba yao ilijaa
watu wa usalama, ndani na nje. Hapakuwa na utulivu, redio call za polisi ndizo
kelele zake zilisikika humo ndani kila wakati.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Tunda yuko wapi? Nani anahusika? Usikose muendelezo.
0 comments: