Nilipotea! Part7 – Sehemu ya B
Msako Unaendelea.
Mpaka giza linaanza kuingia, hapakuwa na fununu yeyote
ya nani aliyemteka nyara Tunda na wala wapi alipopelekwa mzazi huyo mwenye
kidonda kibichi kabisa cha uzazi. Watu wa usalama wenye sare na wasio na sare
walimwagwa kila mahali akitafutwa Tunda Cote. Redio kwa television zilitangaza
utekwaji nyara kwa Tunda, kina Cote wakiomba msaada kwa yeyote hata mwenye
fununu tu, ajitokeze na ahadi ya pesa nyingi sana kama zawadi kwa atakayetoa
habari za kweli.
Polisi walisubiria sebuleni kwa kina Cote simu ya
mtekaji aombe pesa. Lakini mpaka ilipofika saa moja usiku, wakaamini haukuwa
utekaji wa pesa. Itakuwa wivu au kisasi. Wengine walisema kama sio wao kina
Cote wanahusika, basi muhusika anatafuta tu umaarufu wa kuweza kumteka Cote
katikati ya ulinzi mkali.
Lakini watu wengi walimsema vibaya sana Net na
mahusiano ya wizi aliyokuwa akiyaendeleza na Vic. Wakamshtumu kwa maneno mabaya
sana kwa kusababisha ubaya kwa Tunda. Kuanzia anafuatwa na kutukanwa na Vic
mbele ya ulinzi wao. Tena ndani ya nyumba yao. Na baadaye kudanganya ameibiwa
akiwa na mlinzi ambaye hata hakujeruhiwa! Ni kama walikabidhiana tu. Shutuma
kwa familia hiyo ziliendelea mpaka bibi Cote akaagiza hiyo nyumba izimwe kila
tv na redio ili kumfanya aweze kufikiria.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Net
alishashugulikia mpaka Viza yao kama juma moja lililopita. Tiketi zilishakatwa
kwa watu hao watano. Baba yake Tunda, mama Penny, Mchungaji mwenyewe, Penny cha
maneno na Pendo. Gino alishaambiwa siku hiyo kungekuwa na wageni. Hata menu ya
siku hiyo Gino alishaiandaa. Vyakula vya kitanzania kidogo na vigeni kwa wageni
wao pia.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Kwani hata kina Cote wenyewe walikuwa wakichunguzwa na kufuatiliwa kwa kila kitu wanachokifanya. Bado vyombo vya usalama walisema hawana mtu au watu wanaowashuku. Kwa hiyo mpaka hapo, kila mmoja anapaswa kufuatiliwa kwa karibu na wakaombwa kutoa ushirikiano. Mbali na hao maafisa matatu hapo sebuleni waliokuwa na bibi Cote na Net, wengine walikuwa wakizunguka hiyo nyumba nje na ndani, kila sehemu mpaka vyumbani waliombwa waache milango wazi. Mtu asifunge mlango endapo anataka kuwa chumbani. Siku hiyo hakuna aliyefanya kazi.
Bibi Cote hakumsemesha wala kumtizama machoni Net. Net akajua amekasirika kwa alilotenda. Akaamua kumuacha kwanza mpaka hasira zitulie na ile hekaheka ya polisi kuingia na kutoka pale nyumbani kwao ipungue. Maana simu na redio call zilikuwa zikipigwa mfululizo na afisa hao walikuwa wakipita huku na kule. Mara jikoni, wakati mwingine vyumbani. Yeyote anayenyanyuka kuelekea popote, alifuatwa. Hapakuwa na utulivu hata kidogo.
Mtoto wa Net na Tunda, Cote, alishaletwa nyumbani tokea mchana wake, kwa ombi maalumu la bibi Cote. Akiangalia usalama wake. Cote alirudishwa nyumbani kwa makubaliano daktari kwenda tena kumuangalia hapo siku inayofuata. Japo mpaka anaruhusiwa hakuonekana na tatizo lolote, lakini aliruhusiwa na nesi maalumu wa watoto. Na Maya naye akawepo hapo kusaidia.
“Ni nini?” Mmoja wa polisi akamuuliza Net akijua amesoma kitu juu ya Tunda kwenye simu yake. Bibi yake alimtizama tu na kugeuka pembeni. “Niliwaalika familia ya Tunda. Kesho ndio walikuwa wanaondoka nchini kwao kuja huku kwa harusi. Itabidi.., Itabidi..” Net akaanza kufikiria. “Sitaweza kufikiria kama mama Penny atakuja na kukuta hii hali.” Net akasimama kabisa akiwaza. Kila alipomfikiria mama Penny! Aje akute Tunda ametekwa nyara! “Hapana.” Net akapinga kabisa.
“Utabiri wake
utakuwa umetimia.” Akaumia sana moyoni Net. Wakamuona amesogea mpaka
dirishani, simu mkononi anawaza. “Mungu wangu nisaidie nimpate Tunda. Kama
kuna muujiza ninao uhitaji mwaka huu au maishani, naomba hili liwe la pekee.”
Net akaomba kwa uchungu, asijue anafanyaje. Hakuruhusiwa kwenda mbali na hapo.
Na aliambiwa anafuatiliwa kwa karibu sana na polisi. Net alishakuwa mtuhumiwa
wa kwanza. Mengi yalikuwa yakiendelea kwa Net kwa wakati huo. Mambo yalimgeukia
kila mahali.
Carter amemficha kama Vic alilala nyumbani kwake! Wamemsababishia aibu na kuonekana ni mama anayeshindwa kutawala nyumba yake. Halikuwa jambo dogo hata kidogo. Kwake imemuharibia sana. Kuwa yapo mambo yanaendelea nyumbani kwake, yeye hafahamu. Ni uzembe wa namna gani huo! Kwa hakika walimfunga mdomo huyo bibi. Alibaki ametulia kwenye kiti chake kimya.
Akijitahidi sana ni kusimama kwenda msalani au kwenda chumba alicholazwa mtoto na kumwangalia. Basi. Anarudi hapo hapo kukaa. Net aliumia sana, lakini hakujua jinsi yakujitetea. Ni bora angemwambia akajua chakufanya mapema hata kabla hajamkaribisha Tunda mbele ya umati mkubwa kiasi kile. Pongezi nyingi alishapokea kutoka kwa watu wakubwa wa nchi mbali mbali. Wakimpongeza kwa kupata mkwe, Tunda, ambaye atampokea madara. Leo anashutuma za kuzuia penzi la kweli la mjukuu wake huyo aliyemnadi kwa nguvu sana! Vic amemshutumu vibaya sana na akatoa uthibitisho wa penzi zito alilofanya na huyo Net.
Inamaana yeye
bibi Cote anatetea haki za wanawake wengine huku akikandamiza wengine! Inamaana
ipo hila ndani ya kile alichokuwa akikifanya na kukipigania miaka yote.
Vic aliwapiga pabaya sana. Na safari hii na wao wakaonja maumivu ya Vic. Walimpuuza Maya miaka yote akiwaambia juu ya Vic, wakamuona yeye ni teja tu, sasa na wao wamefedheheshwa vibaya sana.
Bibi huyo naye alichafuliwa vilivyo huko mitandaoni. Na yeye walimlaumu kusababisha kutekwa kwa Tunda. Wengine walisema kama asingekuwa yeye kumzuia Net kuwa na mwanamke anayempenda, yaani Vic, ambaye inamlazimu kumuingiza chumbani kwake kwa siri bibi huyo akiwa hayupo, inamaana mabaya mengi yasingetokea. Alisemwa vibaya sana na wakamkashifu vilivyo.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Usiku uliopita bibi Cote alipompigia simu mama yake Vic na kumwambia anampa masaa mawili, kabla masaa mawili hayajaisha kweli Vic na wazazi wake walishajisalimisha kituo cha polisi pamoja na mwanasheria wa familia ya kina Vic. Vic akajitetea vizuri tu. Aliwaambia polisi yeye alikwenda kuzungumza na Tunda kwa amani kabisa. Hakujificha. Hata walinzi wa Cote na Carter walikuwepo wakati akiingia nyumbani kwa Cote. Vic alisema yeye hakumgusa, wala kumtukana Tunda. Tunda alianguka yeye mwenyewe, mbele yake wakiwa wamekaa kiti cha mbali kabisa.
Mwanasheria wa familia hiyo ya kina Vic, akawaambia mpaka hapo Vic sio mtuhumiwa. Yupo tayari kujibu chochote watakachomuuliza. Waliondoka usiku huo huo kurudi nyumbani bila shitaka lolote. Kwani Vic aliwathibitishia maafisa hao wa usalama kuwa, mahusinao yake na Net sio kificho kwa yeyote pale kwa kina Cote. Kila mtu analifahamu hilo. Hakwenda pale kwa kina Cote kama mgeni ila mpenzi wa Net na ndio maana hakuzuiliwa.
Kulithibitisha hilo ndipo Vic akawaonyesha ule ushahidi wa ile video yake yeye na Net wakifanya mapenzi baada ya Net kuoa, akiwaambia Net alioa kimakosa huko nchini Tanzania, ndoa yao haitambuliki kwa sheria ya kimataifa. Na kweli. Wale maafisa walipoangalia ile video kwa haraka, wawili hao kwenye video, hawakuonekana kama si wapenzi au kwamba Net ameshurutishwa. Alionekana akitoa ushirikiano mzuri tu kwa kile wanachokifanya.
Na Vic hakuishia hapo. Akatumia ile video aliyochukua Renee kama ushahidi wake mwingine. Vic akabadilisha. Akawaambia alikwenda pale kwa kina Cote na Renee kama shahidi wake na yeye ndiye aliyemtuma Renee achukue ile video kama ushahidi kuwa hakuna baya atakalotenda kwa Tunda, ila alikwenda kumwambia ukweli. Hapakuwa na sababu ya kumshikilia Vic. Kwa shutuma ipi? Vic akaachiwa huru kabisa.
Hata bibi Cote hakumfuatilia tena Vic, kwani alijua ni kama kuzuia mvua isiloweshe aridhi. Kumbe Vic huwa anaitwa kwa siri nyumbani kwake! Akaona anyamaze kabisa. Hata Logan alipompigia simu kumwambia kuwa Vic ameruhusiwa, hakujibu hilo. Alisisitiza wafanyakazi wake pia watolewe. Zaidi Carter na Ms Emily. Wakati huo anazungumza na Logan na kutoa amri hiyo, bado Tunda hakuwa ametekwa nyara. Alipotekwa nyara na polisi kwenda nyumbani kwa kina Vic, walimkuta Vic nyumbani kwao ametulia kimya. Walimtaka kituoni, bila kubisha, akapiga simu kwa mwanasheria wao akamweleza kila kitu, akamwambia watakutana kituo cha polisi. Aende nao tu hao polisi.
Vic akasindikizwa tena kituoni na wazazi wake wote wawili. Na baadaye mwanasheria wao akaongezeka hapo kituoni kuongeza nguvu kwa Vic kisheria. Mpaka hapo Vic kama mpenzi wa Net, hakukutwa na hatia.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Net akaamua asipige simu kwa mama Penny wala kwa baba yake Tunda, ila akawatumia ujumbe mfupi tu.
Tarehe ya harusi imesogezwa mbele. Hapatakuwa na harusi tena jumamosi
hii mpaka tutakapo wataarifu tena. Simu ya Tunda imesumbua, msione kimya.
Lakini kila kitu kipo sawa, msiwe na wasiwasi. Nitawataarifu tena siku ya
nyinyi kuja. Asante.
Nathaniel Cote.
Kwa hiyo
mazingira tulivu na ya kuwafaa mama Penny na familia yake yalishaandaliwa ili
kuwafanya watulie pale nchini kumlea Cote na mama yake. Inamaana hata kazi
yakupamba huko nchini hakuwa amechukua kwa kuwa alijua hatakuwepo nchini kwa muda
mrefu. Tunda alishamuhakikishia kuwa watamlipa kwa kipindi hicho atakachokuwa
akimsaidia uzazi. Asiwe na wasiwasi kabisa juu ya pesa.
Akawafungia kabisa simu zao zisiingie kwenye simu yake na Tunda. Na hakuishia hapo. Akaandikia ubalozi wa Canada usiku huohuo kuwa anafunga kwa muda ukaribisho wa kina mama Penny aliowatumia na kuwaombea Viza, mpaka atakapowataarifu tena. Kwa maana nyingine ni kama Net alikuwa akiwafungia pia kuwa kama kina mama Penny wataamua kusafiri hivyo hivyo, wasiruhusiwe kuingia hapo nchini kwa Viza hiyo ya kuwa wanakwenda kwa kina Cote. Inamaana waanze upya, kivyao kuomba visa nyingine ya kuingia nchini hapo. Hapo Net akajiambia hata kama wataanza kuomba Visa nyingine, mpaka waipate, atakuwa ameshampata Tunda. Akatulia.
Kwa Tunda.
T |
unda alitolewa hospitalini akiwa amechomwa sindano ya usingizi akiwa
bado usingizini palepale hospitalini. Alitolewa pale hospitalini wala asijue
alipo na anapopelekwa. Akahamishwa
kutoka kwenye gari moja kupelekwa gari ingine, hana taarifa na chochote. Walimpeleka kwenye nyumba ilikuwa mbali kabisa na hapo
mjini. Ipo peke yake porini, wakaenda kumuweka chini kabisa kwenye hiyo nyumba.
Basement ambayo haikuwa haina hata dirisha.
Usiku Tunda akafungua macho kwa shida akiwa na usingizi mzito. Akamuona mwanamke wa kizungu aliyevaa nguo za kinesi akimsafisha kidonda. “Mtoto wangu yuko wapi? Naomba niletee kabla sijarudi kulala.” Hakujibiwa. Yule nesi ambaye hata hakuona sura yake vizuri kwa usingizi, akamuongezea dawa ya usingizi. Hapo hapo Tunda akarudi kulala.
Maya na Harakati za kumsaka Tunda.
M |
aya alikuwa akilia na kufikiria mfululizo. Akapata wazo. Akaamua kutoka
pale. Ilikuwa bado muda wa yule nesi wa mtoto kuisha na kuondoka pale,
akamuomba asiondoke mpaka atakaporudi. Yule dada akakubali kubaki pale akimlea
Cote kwani Maya alimwambia atamlipa zaidi kama atachelewa kurudi. Yule nesi
akafurahia hilo, akakubali kubaki huku akiomba Mungu Maya achelewe huko
anakokwenda ili yeye abaki na huyo mtoto muda mrefu atengeneze pesa zaidi.
Hakutaka wale maafisa wamfuate. Maya aliyezoea
kutoroka kwenye hilo jumba, hakupata shida kuwachomoka hao maafisa wote na
hakumuaga mtu. Akaondoka kimya kimya. Alipofanikiwa kutoka tu hapo kwenye
viwanja vya Cote, Maya akampigia simu Gina. Aliyekuwa amemtumia ile video. Simu
yake ikaita muda mrefu sana bila kupokelewa.
Gina ni rafiki wa karibu sana wa Maya. Na ni mmoja
wa marafiki waliomfundisha Maya kutumia madawa ya kulevya. Na wakaendelea
kutumia naye madawa, Maya akiwa ndiye mnunuzi kwani Gina na yeye alitoka kwenye
familia ya kawaida tu. Lakini pia Gina yupo karibu na rafiki mmoja wapo wa Vic.
Ava.
Ava na Renee walikuwa marafiki lakini ni kama
wafanyakazi wa Vic. Wanafanya chochote wanachoambiwa na Vic, na huwa wanatembea
naye popote pale kama watumwa wake. Siku alipomfuata Tunda, Vic alikuwa na
Renee, ambaye alimrikodi Vic akizungumza na Tunda. Maya akajua kwa kupitia Ava,
Gina ataweza kumsaidia kumpata Renee ambaye atakuwa na habari zote kutoka kwa
Vic mwenyewe kwani alikuwa naye tokea mwanzo wanamfuata Tunda.
Maya alipoona Gina hapokei, akaamua kumpigia simu
Renee mwenyewe aliyechukua hiyo video. Yeye Renee naye ni binti wa hapo hapo
Norfolk. Lakini hakutoka kwenye familia ya kitajiri kama wao. Amekuwa katikati
ya Vic na Maya. Anajua visa vyao watoto hao wa matajiri. Hakuna aliyeweza
kuwaingilia Vic na Maya. Kina Renee wakawa watizamaji tu.
Aliposhindwa kumpata Renee, akaamua kumpigia tena
simu Gina. Ikaita tena na tena mwishoe Gina akapokea. “Nina
shida sana yakuzungumza na Renee, tafadhali naomba uzungumze na Ava, amwite
Renee nyumbani kwao mimi niende kwa kina Ava nikazungumze na Renee.” “Hilo
unajua wazi halitawezekana Maya. Hasa kipindi hiki. Unawajua Ava na Renee. Ni
kama wamekula kiapo kwa Vic.” Gina akamkatisha tamaa Maya, akaanza
kulia.
“Lazima nimpate Renee leo, Gina.
Lasivyo nahisi nitachanganyikiwa. Hapokei simu zangu. Tafadhali nisaidie Gina.
Uko wapi?” Maya akamuuliza huku akifuta
machozi. “Nipo Club.” “Unaweza kutoka? Tafadhali Gina.
Mimi huko ndani siwezi kuingia, zaidi leo.” Gina akakubali kuonana na
Maya usiku huo. Maya akaongeza mwendo mpaka club. Akaegesha gari sehemu yakujificha
kidogo, akamtumia ujumbe Gina kuwa amefika, akatoka.
Alionekana amekunywa, lakini hajalewa sana.
Mchangamfu tu. “Nimetoka kuzungumza na Ava sasa hivi baada ya kuagana na wewe.
Nikamuuliza kama anajua Renee alipo, anasema hata yeye hapokei simu zake. Jana
alikwenda nyumbani kwa Renee akakuta kumefungwa kabisa. Anahisi pengine
anajificha au ametoroka kabisa baada ya siku ile ya tukio lakuanguka Tunda.
Hadhani kama yupo Norfolk.” Gina akamwambia Maya.
“Atakuwa amekwenda kujificha wapi?” Maya akaendelea
kumuuliza Gina. “Sasa niachie mimi hiyo kazi. Mpaka kesho, nitakuletea jibu
zuri. Acha nikazunguke ndani niulize taratibu. Usiwe na wasiwasi.” “Tafadhali
Gina, ukisikia chochote hata kama ni usiku vipi, nitafute. Nitahakikisha pesa
yote aliyoitangaza Nana kama zawadi, unaipata wewe.” Hapo akamtia morari Gina
akarudi ndani club kwa haraka ili kupeleleza zaidi.
Maya akabaki pale kwenye gari akilia. Akawa
amegonga mwamba. Hajui tena chakufanya ili kumpata Tunda. Alibaki akilia huku
ameinamia usukani. Akasikia kioo cha gari yake kikigongwa. Akanyanyua uso huku
amejawa machozi. “Malcom!” Maya akashangaa
na kushusha kioo. Malcom ni yule afisa wa CSIS aliyekuwa akimuhoji Maya maswali
na Maya akaondoka akiwa amevunjika moyo.
“Unanifuatilia nyuma!?” Maya akamuuliza kwa kumshangaa. “Ndiyo.” Malcom
akamjibu bila kumficha. Maya akashangaa sana. Maya akidhani anatoroka nyumbani
kwao kwenye ulinzi ule kali na kujipongeza amefanikiwa kuwatoka afisa usalama
hao, kumbe walimwacha tu na kumfanikisha atoroke ili kumfuatilia nyuma kujua ni
wapi anakwenda. Gari yake yenyewe aliyonayo hapo ilishategeshwa vinasa sauti
kujua na kusikiliza kila mtu atakayezungumza naye. Kwa hiyo hata mazungunzo
yake na Gina walisikizwa mwanzo mpaka mwisho. Walimtegemea kwa asilimia 80 kuwa
atatoroka ndio maana yeye gari yake ilitegeshwa mapema sana bila yeye mwenyewe
kujua.
Maya akabaki ameduaa haamini. “Mtu wa karibu yako
ametekwa nyara, Maya. Mpaka sasa hatujapata hata mtu mmoja ambaye anahisiwa.
Itakuaje waje wakurudie na wewe?” “Angalau nitakuwa
na Tunda. Haya maisha hayana maana bila Tunda.” Maya akaendelea kulia. “Tulia
kwanza tuzungumze Maya. Naweza kuingia ndani ya gari yako?” Maya akatoa loki za
mlango. Malcom akaingia upande wa pili.
“Nisikilize Maya, jitahidi kutulia ili uweze
kufikiria. Nimezungu na wewe kwa muda mfupi sana, nimeona uwezo wako mkubwa
sana wakufikiria. Sasa kwa akili hizo, zinaweza kutusaidia kumpata Tunda.” Maya
akajaribu kutulia.
“Unajua Andy alipo?” Lilikuwa swali lililomshtua
sana Maya. “Kwa nini!?” “Unakumbuka
uliniambia nini juu ya Vic?” Maya akatulia. “Sisemi kama ndiye aliyemteka nyara
Mrs Cote, lakini sio vibaya kuanzia kwake.” Maya akajiweka sawa kutaka
kumsikiliza zaidi. “Kwani nyinyi mlivyomuhoji Vic amesema nini?” Maya akauliza.
“Siwezi kukwambia kwa undani ila ni kama vile ulivyosema. Vic anajibu la kila
swali. Na yupo makini mpaka binafsi ananitia wasiwasi! Ni kama alikuwa akijua
ni nini ataulizwa na polisi. Akaandaa mpaka ushahidi wa video na picha wa wapi
alikuwa na nini alikuwa akifanya!”
“Nilikwambia Mal, Vic hamtamuweza kwa hoja.
Anaandaliwa na mwanasheria wao. Na usifikiri ni hivi hivi tu! Vic alishakuwa au
ana mahusiano na yule mwanasheria wao. Hawezi akaruhusu Vic akamatwe.” Malcom
akashangaa kidogo. “Kwani yule mwanasheria si anamke na watoto?” “Kumbe!
Ilikuwa karibu mkewe amwache sababu ya Vic. Sema yule mwanasheria huwa analipwa
pesa nyingi sana na baba yake Vic, hawezi kuacha kazi kwao. Ikabidi mkewe
atulie tu. Kwa hiyo Vic anajua ni nini aseme na atengeneze ili asikamatwe.” “By
the way nimependa ulivyoniita Mal.” Malcom akachomekea hilo.
“Bwana Mal! Focus ili tumpate Tunda.” “Huoni
umecheka kidogo? Tulia tupange vizuri.” Maya akatulia kidogo kama anayefikiria
kitu. “Nikuulize swali Malcom?” “Uliza tu.” “Unaniahidi hutanidanganya?” “Hata
kidogo.” Maya akamwangalia kama anayetaka uhakika. “Huniamini?”
“Nimeshadanganywa sana mpaka sijui yupi atasema ukweli na yupi ataanza na
ukweli na kuishia na uongo!” Maya akaongea kwa kukata tamaa.
“Nakuahidi sitakudanganya kwa chochote, hata kama
nitajua kitakuumiza, nitakwambia tu. Na kama ni mambo ya ofisini ambayo siwezi
kuzungumza na wewe, pia nitakwambia ukweli. Kwa hiyo usitie mashaka kwangu.
Uliza tu.” Maya akamtizama machoni kama anayemsoma. Akaridhika. “Unataka kujua
nini?” Malcom akamuuliza taratibu tu.
“Upo hapa kama afisa wa CSIS au kama Malcon
uliyeniahidi nikwambie halafu utanisaidia?” “Vyote.” Malcom akajibu. Maya
akamtizama, akanyamaza. “Sasa mimi nimehangaika mpaka nimejua alipo Andy.”
Malcon akavunja ukimya kwa habari iliyomshtua Maya. Akamgeukia vizuri na
mshangao usoni. Akabaki kama bubu mbele ya Malcom.
“Nafikiri tuanze na Andy” Akaendelea Malcom. “Wewe
anza naye, mimi huyo mtu sitaki kabisa kumuona.” “Kwa nini?” Maya akanyamaza na
kugeukia pembeni. “Bado hisia za mapenzi zinakusumbua?” Malcom akamuuliza
taratibu tu. “Nooo! Hata kidogo!” Maya akakataa kabisa. Malcom akabaki
akimtizama. “Ni vile ali..” “Kuumiza?” Akamalizia Malcom kwa swali. Maya
akanyamaza na kugeukia tena pembeni.
“Kama unamtaka Tunda, nilazima kumtafuta Andy ili
tujue anamfahamu vipi Vic. Anauwezo wa kufanya nini? Yeye alikuwa akimlipaje?
Maana kwenye akauti ya Vic, hayaonekaniki malipo yoyote ya ajabu yakututia
wasiwasi. Sasa tutafute kujua kama kweli anatumia watu kufanya maovu yake, na
je huwa anawalipa vipi?” Maya akashangaa sana. “Yaani mmeshamchunguza kwa
umbali huo!?” “Bibi yako ameomba msaada wa mtu mkubwa sana CSIS. Na unajua vile
bibi yako anavyofahamika na kile anachokifanya. Amesimama kupigania haki za
wengi. Kwa mara ya kwanza kwenye maisha yake yote na harakati zake zote, leo
ndio analia shida. Amepata mwitikio mkubwa sana.”
“Hiyo kesi inafuatiliwa kuliko nitakavyokueleza
hapa. Macho na masikio ya watu wengi wakubwa ndani na nje ya nchi yapo kwenye
hii kesi. Kesi ya Mrs Cote imechukua sura ya kitaifa. Kushindwa kupatikanika
kwa Mrs Cote ni kudhalilisha usalama mzima wa nchi. Kwa hiyo ni lazima kufanya
uchunguzi wa kina. Hakuna kulala, mpaka Mrs Cote arudishwe nyumbani.” Maya
akabaki akifikiria.
“Fanya kwa ajili ya Tunda.” “Sasa hivi giza
limeshaingia. Inabidi kurudi nyumbani kukaa na mtoto. Kwanza ni umbali gani
mpaka huko anakoishi Andy?” Akauliza na kuguna Maya kwa kusikitika. “Nini?” Malcom
akamuuliza. “Hata sijui kama jina hilo ni lake kweli!” Maya akaongea kwa
mashaka. “Anaitwa Jake Cole.” Maya akatoa macho. “Malcom!” “Sijala Maya. Tokea
tunaachana mpaka sasa hata sijapumzika! Kama ungeweza kunisaidia leo nikakutana
na Andy au Jake, ingerahisisha sana.” “Mbona inakuwa ni kama wewe ndio
unashida? Ni kama unataka nikusaidie kazi yako tena!” Maya akaongea kwa
kulalamika.
“Nimekwambia tokea mwanzo Maya. Nipo hapa kwa kofia
mbili. Kwa kile nilichokuahidi kwamba ukijibu maswali yangu nitakusaidia, na pia
nikifanikiwa mimi, ujue na wewe utafanikiwa. Kama kweli Vic yupo nyuma ya
utekwaji, utampata Mrs Cote. Kama yupo nyuma ya hayo madawa, tutajua ukweli
wote. Utathibitisha kwenye kesi zako na lililompata kaka yako. Na kama hayupo,
basi utajiridhisha, na mimi nitakamilisha kazi.” Maya akaona ni win win
situation. Akakubali.
“Basi ngoja nimpigie simu nesi ambaye yupo na mtoto
ili nimuombe kama anaweza kuendelea kukaa na mtoto.” “Wakati ukizungumza naye,
mimi nitakusubiri kwenye gari yangu.” Maya akashangaa kidogo. “Hatuendeshi gari
hii?” “Hapana. Naomba mimi nikuendeshe.” Wakabaki wakiangaliana. “Please!”
Akaweka msisitizo Malcom. “Acha gari yako hapa, nitakurudisha hapahapa.”
“Sawa.” Maya akakubali.
Malcom akatoka kwenye gari ya Maya na kurudi garini
kwake. Maya akazungumza na yule nesi, akaonekana hana tatizo kabisa lakubaki na
huyo mtoto. Hata angeweza kulala. Hilo likamfurahisha Maya. Akafunga gari yake
na kuhamia kwenye gari ya kawaida tu ya Malcom. Akaingia na kufunga mkanda.
Akatulia. “Uliniuliza ni safari ya muda gani.” “Ni mbali sana?” “Kiasi. Masaa
mawili.” Maya akashangaa. “Sasa unajuaje kama tutamkuta nyumbani?” “Kuna gari
ya usalama ipo nje ya nyumba yake, wanasema yupo.” Maya akawa hajaelewa.
“Mal! Naomba niambie ukweli. Ni nini kimewashinda
nyinyi watu wa usalama kumuhoji Andy mpaka mimi!?” “Ndio maana nasema wewe una
akili sana Maya.” Malcom akamsifia na kuendelea. “Kila dakika inayokwenda
tukiwa hatujui Mrs Cote alipo, ni mbaya zaidi. Tungeweza kumchukua Jake au Andy
kwa nguvu tu na kwenda kumuhoji. Lakini inaweza kuchukua muda mrefu sana kuweza
kupata ukweli wote kutoka kwake na sisi muda huo hatuna. Na mbaya zaidi, kwa sasa
Andy au Jake, hana chakupoteza. Kiasi chakumtisha nacho ili kuzungumza kwa
haraka.” Bado akawa amemchanganya Maya.
“Unamaanisha nini?” “Mara nyingi ili kuweza kutoa
siri kwa mtu, tena kwa haraka huwa tunatumia kumtisha ndugu au mambo mabaya
aliyofanya zamani. Kwenye rekodi za Jake, hana kosa baya. Na maisha yake ya
nyuma hayana doa.” “Ndugu?” Akauliza Maya. “Ndio nataka kukueleza. Jake ni mtoto
wa pekee kwa mama yake. Ni kama mama yake alizaa na mume wa mtu, yule mwanaume
akamtelekeza. Akalelewa na mama tu, bila ndugu yeyote.” Maya akajiweka vizuri
kumjua Andy mpenzi aliyemchanganya zamani.
“Mama yake alipoanza kuugua. Akapoteza kazi. Jake
ndio akawa akimuhudumia nakushindwa kusoma au tuseme kufanya kazi. Maisha
yakawa magumu na wakapoteza insuarance pia. Mama yake akashindwa kupata
matibabu. Haya tumeambiwa mchana wa leo na mwanamke aliyekuwa akifanya kazi na
mama yake kwenye supermakert. Sasa sisi tukiunganisha tunafikiri hivi, Vic
alikutana na Jake kipindi hicho cha shida yake akihangaika kumtunza mama yake
bila kazi. Akapenda ule uzuri wake, ndipo akampa hiyo kazi ya kuwa na wewe,
iliyokuwa ikimsaidia kumtunza mama yake.” Maya akashangaa sana.
“Maana huyo mwanamke anasema mara kwa mara alikuwa
akienda kuwatembelea Jake na mama yake. Walikuwa kwenye shida sana. Na mara
nyingine yeye alikuwa akiwasaidia chakula. Lakini mambo yakabadilika gafla.
Yule mama akatafutiwa na Jake nesi wakumuuguza, yeye akasema amepata kazi mbali
na pale. Na akaanzishiwa matibabu ya hali ya juu.” “Mungu
wangu Mal!?” Maya akaanza kulia. “Sasa ugumu unakuja hapa, yule mama
alifariki. Ni kama walichelewa matibabu kitu kilichomuumiza sana Jake. Sisi
tukienda kwa Jake, hatuwezi kumtoa ukweli kirahisi. Ila kwa kuwa wewe umeishi
naye, unajua udhaifu wake na ulisema alikupenda, anaweza kufunguka kwako kwa
haraka na ikatusaidia kukomboa wakati.” Maya akapotelea mawazoni.
“Nikuulize kitu Maya?” Maya akamgeukia. “Unafikiri
utaweza?” Maya akavuta pumzi kwa nguvu. “Kwa kuwa na wewe unanitumia kufikia
lengo lako kama wengine tu, niambie kile unachotaka kusikia kutoka kwa Andy au
Jake. Nitamfanya aseme.” Maya aliongea kwa unyonge huku ameinama. “Sikutumii
Maya!” “Wewe niambie ni nini unataka nikafanye kwa Andy. Nimalize tuachane kwa
amani.” “Tafadhali usinifikiri kwa ubaya.” Maya akacheka kwa kuguna.
“Malcom! Haya ni maisha yangu. Na
nimeshazoea. Kila anayenisogelea ni kwa sababu anataka kujinufaisha na mimi.
Huwa wanakuja kwa njia au sababu tofauti tofauti ila mwisho wao kama si pesa,
basi mwili wangu. Sasa kwa kuwa nimeshapanda ndani ya gari yako. Na viongozi
wako wamekutumia wewe kijana mwenye sifa kama za Andy tu, wakijua ukitumia
wajihi wako nitafanya kile utakacho, acha tumalize hili, ili tuachane kwa amani na haraka.” Maya aliongea kwa kuumia sana na kujifuta machozi.
Akajiegemeza pembeni karibu ya dirisha, akanyamaza. Na Malcom naye akanyamaza
na kuendelea kuendesha.
Gina kwa Maya.
Simu yake ikaanza kuita. Akaitoa kwenye pochi.
Alikuwa Gina akaipokea kwa haraka sana akijua anacho cha muhimu chakumwambia na
kwa kuwa alimwahidi pesa, akajua atahangaika tu ili kujinufaisha na yeye. “Umempata Renee?” “Nasikia ametokea polisi usiku huu
kujisalimisha na kuuliza kama anatafutwa. Ameulizwa maswali machache,
akaruhusiwa kwa kuwa ni kama maelezo yake yamefanana kabisa na Vic. Hawana
hatia. Ila nasikia ameambiwa asikae mbali kama kuna swali ataitwa.” Maya
akavuta pumzi kwa nguvu akatulia.
“Maya?” Gina akaita. “Najua hiyo ni kazi ya Vic tu.
Itakuwa ameenda kutafutwa Renee na wazazi wake Vic ili aende akazungumze
alichoambiwa na kufundishwa na mwanasheria wa wakina Vic.” Maya akawaza
kwa sauti. Gina kimya. “Nashukuru Gina.” “Sasa
utafanyaje?” “Acha nifikirie. Mpaka baada ya masaa mawili, nitakuwa nimeshapata
jibu.” “Haya, kila la kheri. Ila kuwa mwangalifu.” “Gina!” Maya akamwita
kabla hajakata simu.
“Nipo bado.” “Nikuulize swali unaniahidi
hutanidanganya?” Akamsikia
Gina akicheka kilevi kama kawaida yake. “Swali gani?”
“Nilipokuwa nikilewa, watu wakinifanyia mambo mabaya, unajua ni nani aliyekuwa
akinichukua video na kunipiga picha hata nilipokuwa vyumbani, kwenye gari au
vyooni?” Kimya.
“Gina?” Kimya. “Katika hili ujue nitapata tu ukweli
Gina. Iwe kutoka kwako au kwa Andy ambaye namfuata sasa hivi. Ila ujue
nitajua.” Kimya, lakini alisikia kelele nyuma ya simu ya Gina. Inamaana
alikuwa akisikiliza ila akawa kama amekufa ganzi. “Gina?”
Maya akaita na kutizama simu yake. Hapo hapo Gina akakata. Malcom
akamtizama na kurudisha macho barabarani. Akampigia Gina simu ikawa haipo
hewani kabisa.
Maya Kwa Aliyekuwa
akimuuzia Dawa.
Malcom akaona anapiga tena simu nyingine. “Umelewa?” Akamsikia Maya akimuuliza mtu wa upande wa
pili wa simu. “Kwanza pole kwa matatizo.” “Nina swali
dogo tu. Ukinijibu hilo, utakuwa umenisaidia sana.” “Nini?” “Ile cocaine
tuliyokuwa tukitumia club, ulikuwa ukinunua wapi?” “Unajua hilo siwezi kukujibu
Maya.” “Kwa nini?” “Nikuhatarisha maisha yangu!” “Sawa. Nisaidie swali
jingine.” Maya akaendelea. “Cocaine uliyokuwa
ukiniuzia mimi ni sawa na uliyokuwa ukiwauzia wengine?” “Yako ilikuwa grade A,
wengine ilikuwa ni unga tu wakawaida.” “Unamaanisha nini?” Akauliza Maya
huku akimwangalia Malcom.
“Mimi sijui Maya. Ndivyo nilivyokuwa
nikipewa huko nilikokuwa nikinunua. Walikuwa wakinipa yako tofauti na wengine.
Walisema hiyo inakustahili wewe mwenye pesa, wengine niliambiwa wanapewa unga
tu wakawaida sio unga wenyewe sababu ya pesa yao.” Malcon na Maya wakaangaliana.
“Nani alikuwa akikwambia hivyo?” “Maya!”
“Nataka kujua na ninakuahidi sitakutaja.” “Nihurumie Maya. Wewe ni wangu,
lakini ukumbuke ndio nimetoka tu jela. Na nimetoka kwa kuponea tu! Niliyekuwa
nikimuuzia hayo madawa kwenu, ndiye amenitoa. Siwezi kumtaja.” “Basi
nashukuru.” Maya akakata simu.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
“Au ulitaka nikudanganye ili kukufurahisha?” Maya
akamwangalia na kunyamaza. “Maya?” “Nitazungumza na Andy, Malcom. Usiwe na
wasiwasi. Mimi ni mtu wakusimamia maneno yangu.” “Hata mimi ninasimamia maneno
yangu, na si tapeli. Sikutumii. Nakuhakikishia Maya, hata sasa hivi ukikataa
kwenda kwa Andy, ukaona nakutumia vibaya. Sitakulaumu. Nitakurudisha na
nitakuacha kwa amani kabisa.”
“Hapana. Twende tu. Sina ninachokwepa kwa sasa. Ni
mimi Maya. Hakuna geni litanitokea kutoka kwa yeyote likawa la ajabu na
waliyonifanyia wengine. Na kama nilitumiwa kwa mabaya, naweza kutumiwa na kwa
mazuri. Twende tu, tumalize hili.” Malcom akamwangalia. “Lakini bado ahadi
yangu ipo palepale.” Maya akamwangalia na kunyamaza. “Nitakusaidia mpaka kujua
ukweli. Na nitahangaika mpaka kumpata Mrs Cote.” Maya akanyamaza bila kujibu
kama aliyemuhesabu kuwa ni walewale tu, huna tofauti.
Malcom akaendesha mpaka kituo cha mafuta,
akasimama. “Maya?” Akamwita, Maya akamwangalia. “Nimekuahidi sitakudanganya
hata kama ukweli utakuuma. Nitakwambia ukweli ulivyo. Nataka kujua, tunakwenda
kwa Jake ukiwa na mtazamo kuwa nakutumia?” Maya akanyamaza nakuanza kulia. “Niambie
tu ukweli. Kama ndivyo hivyo unavyofikiri, nakurudisha sasa hivi. Mimi
nitatafuta jinsi ya kupata ukweli kutoka kwa Jake na nitakuwa sawa tu. Lakini
sitaki kuendelea kukuumiza. Mimi sio Andy au Jake, na ninakuahidi sitakuwa
hivyo.” Malcom akabembeleza. Maya akajifuta machozi.
“Samahani kama umejisikia ni kama nakutumia tu.” “It’s okay Malcom.” “Hapana. Sio sawa. Nataka uwe
huru kufanya kile unachojisikia moyoni. Na bado nakuahidi nitahangaika kivyangu
ili kukusaidia na wewe. Na nitafanya kila niwezalo kumpata Mrs Cote.” “Kwani wewe ndio umepewa hilo jukumu?” Maya
akauliza huku akijifuta machozi. “Ili kurahisisha kazi na wakati, tumegawana.
Kwa hiyo mimi sio kiongozi na sipo peke yangu. Katika hili nafikiri
wamenichagua kwa kuwa wameniona nikijana mwenzako.” “Kwa hiyo kumbe nilipatia?”
Akamuuliza Malcom.
“Ndio maana natamani kukusikia mawazo yako Maya.
Unaakili nzuri ya kufikiria. Usinikasirikie bwana!” “Watu wamekuwa wakinitumia
sana Malcom.” “Nafahamu sana tu. Ila mimi nakuahidi sitakutumia vibaya, tena
bila wewe kujua.” Maya akatulia kama aliyeridhika. “Ni sawa?” Malcom akauliza
kwa upendo. Maya akatingisha kichwa kukubali, na tabasamu lililosindikizwa na
machozi. Ungependa kumtizama mtoto huyo mwenye asili ya kitanzania na uzungu.
Alijaliwa usichana wa kitoto, akitulia, hachoshi kumwangalia. Tunda alipenda
kumwangalia wakati wote na kucheka.
Malcom akarudisha tabasamu na kuondoa gari kuelekea
kwa Jake/Andy. Mpenzi wa zamani wa Maya. Angalau wakaanza kucheka, Malcom
akamfundisha jinsi ya kumwingia Andy na kuhakikisha anajibu maswali yote. “Jitahidi
kuweka au kuficha hisia zako mbali.” Maya akafikiria kidogo. “Nikwambie kitu
Mal?” “Nakusikiliza.” “Unaponiambia niweke hisia zangu mbali kwa Andy, nataka
nikwambie ukweli juu ya Andy.” Maya akaanza.
“Katika wanaume wote ambao umewahi kusikia nimekuwa
nao na kuniona nao mitandaoni, hakuna aliyeonyesha mapenzi ya kweli kwangu kama
Andy.” Maya akamuelezea mahusiano yake yeye na Andy kuanzia mwanzo mpaka
mwisho. “Hudhani ni kwa kuwa kwanza alikuwa kazini. Alikuwa na shida sana na
pesa. Ikabidi afanye kazi yake kwa bidiii. Na ndipo inakuja kitu cha pili.
Alipatia kazi yake kwa kuwa alianza na wewe akiwa anakujua vizuri?” Malcom
akamuuliza.
“Upo sahihi kabisa. Lakini Andy alikuja kunipenda
kwa dhati, mpaka mimi mwenyewe nilijua napendwa! Mimi nikidanganywa huwa najua.
Unafikiri ni kwa nini Gina amenizimia simu?” “Kwa kuwa anajua akikudanganya
utajua?” Maya akacheka. “Unaakili Malcom!” “Kama wewe.” Wakacheka. “Mwanzo wa
Andy na mwisho wake ulikuwa wa tofauti kabisa. Tuliachana na Andy nikiwa
nampenda.” “Najua wewe ulitolewa jela na mwanasheria wenu, Logan. Ulijua ni
nani alimtoa Andy?” Maya akashangaa sana.
“Kwa hiyo wewe Malcom unanifahamu kwa asilimia
ngapi?” “90.” Akajibu Malcom bila kusita. Maya akacheka kidogo kama
anayefikiria. “Ngoja nikwambie ukweli Malcom. Nilipofungwa jela kabla yakutaka
familia yangu wajue, nilipata muda mrefu bila madawa, kwa hiyo sikuwa nikilewa,
nikaweza kufikiria. Nikajiuliza kuanzia mwanzo mpaka pale tulipokuwa tumeishia
na Andy, nikajua kuwa ile ni kazi ya Vic tu.” Maya akatulia kidogo. Kisha akaendelea.
“Niliumia sana Malcom. Nilimchukia vibaya sana Andy. Kwa kuwa tokea tunaanzana
sikujificha kwake. Nilimwambia ukweli nia yangu yakutaka kubadilika na kuacha
maisha mabaya niliyoishi nyuma. Nilimwambia nimeacha marafiki wote, natulia na
yeye tu. Ni kweli Andy alionyesha kunipokea kwa mikono miwili, kumbe ili
alipwe! Iliniuma sana.”
Maya akaendelea. “Nilijitetea. Na logan akanitetea.
Kuwa tulipokuwa club mimi na Andy kuna mtu alituwekea madawa. Mimi nikashinda
kesi. Sasa sikutaka hata kumtafuta au kujua aliishia wapi. Kwanza nilikwenda
rehab. Nilipokonywa simu na kufungiwa mawasiliano yote. Nilikuwa nikitoka rehab
nakwenda mahakamani. Halafu ndio kipindi hicho tulikuwa tumefiwa na Papa. Papa
yangu mimi alikuwa kama baba yangu. Kwa hiyo nilikuwa na wakati mgumu, ya
kwangu tu yalikuwa yamenilemea. Sikuwa na nguvu yakumfuatilia tena Andy, kwanza
sikutaka hata anisogelee tena.” “Pole Maya.” Maya akanyamaza.
“Kwa hiyo sasa hivi nani ndio amebahatika?” Malcom
akamchokoza baada yakumuona amekosa raha. Maya akamwangalia na kunyamaza. “Maya?”
“Mambo yamebadilika Malcom. Kwangu mimi mwenyewe na watu wanao nizunguka.”
“Kivipi?” Maya akafikiria. “Kabla sijaangukia kwa Andy, ni kweli nilikusudia
kubadili maisha yangu. Nilitamani kutulia. Ndio nikaharibu tena. Na hiyo
haikuwa mara ya kwanza. Nafikiri na wewe unajua.” Malcon akatabasamu ishara ya
kuwa anajua.
“Sasa kwa kuharibu kote huko. Kutangaza nitatulia,
na bado nikaendelea kuharibu tena na tena. Unafikiri mwanaume gani wa maana.
Aliyetulia. Mwenye akili zake. Sio tapeli kama kina Andy na wengine niliokuwa
nao, atakubali kuwa na mtu kama mimi!?” Maya akauliza na kuendelea. “Sina sifa
nzuri popote na siaminiki, Malcom. Kwa kujibu swali lako. Nimebaki mimi peke yangu na ndio Mungu akanipa Tunda.”
Maya akaanza kulia.
“Tunda ananipenda sana Malcom.
Isingekuwa upendo wa Tunda kwangu, usiku huu nisingekuwa njiani nikihangaika.
Natafuta nini! Ni vile sitaki kumpoteza.” “Usilie
nikwambie kitu.” Maya akajifuta machozi. “Cha kwanza, nina imani kuwa tutampata
Mrs Cote. Cha pili, mwanaume anayekupenda kwa dhati, atakupokea hivyohivyo
ulivyo na historia yako ilivyo. Na akakupenda na kukulinda.” Maya akamwangalia.
“Huanimi kwa kuwa hajaja Mr. Right. Akija,
utakumbuka haya maneno yangu. Atakupenda mpaka utafurahia na kusahau hao
matapeli wote waliokuwa wakikupendea pesa, na kuona fahari kuonekanika
mitandaoni na wewe.” Maya akanyamaza. “Kaa mkao wakumpokea. Atakuja tu.” “Wewe
umeoa Malcom?” “Nilioa, tukapata mtoto mmoja wa kiume, lakini tuliachana na mke
wangu.” Maya akakunja uso na kumwangalia Malcom vizuri.
“Unaonekana wewe ni mdogo sana Malcom! Umeoa lini
na kuacha lini? Au uliingia kwenye ndoa kujaribisha, ulipoona mambo magumu
ukakimbia?” Malcom alimtizama kwa tabasamu ambalo Maya akajua sio la furaha,
akarudisha macho barabarani. Hakujibu. Maya akamuona amepotelea mawazoni.
Akajua kuna linalomsibu. Na yeye akanyamaza.
Kwa mara nyingine
tena Maya kwa Andy.
M |
alcom alimfikisha mpaka nje kabisa ya nyumba ya
Jake. “Unataka niingie mwenyewe!?” Maya akauliza kwa kushangaa kidogo. “Nafikiri
itakuwa vizuri akuone peke yako kwanza. Mimi nipo hapa nje. Ukinihitaji
nitakuja.” Maya akafikiria kidogo. “Naomba tu tuongozane.” “Maya!” “Namfahamu
Andy. Hatakuwa na neno. Twende.” “Hawezi kuwa huru kuzungumza na wewe kama mimi
nitakuwepo.” “Sasa wewe utasikiaje mazungumzo yetu?” Malcon akatulia kidogo.
“Malcom?” “Tutakuwa tukisikiliza kila kitu.” Maya
akaingiwa hofu. “Inamaana na viongozi wako?” “Ndiyo.” Maya akabaki akimtizama. “Usiogope.”
Malcom akajaribu kumtuliza. “Inamaana hata haya mazungumzo hapa ndani ya gari
walikuwa wakiyasikiliza!?” “Hapana. Nyumbani kwake ndio kumetegesha tokea
mchana. Alitoka, wakapata nafasi ya kuingia. Wametegesha kamera na spika.” Maya
akazidi kuogopa.
“Mtamfunga tena?” “Inategemea.” “Sitaki mumfunge.
Waambie viongozi wako kama watamfunga mimi sitakwenda kuzungumza naye.” “Siwezi
kufanya hivyo Maya.” “Basi nirudishe kwenye gari yangu.” Maya akagoma na
kumshangaza Malcom. “Kweli Malcom. Japokuwa amenitenda vibaya, mimi siwezi
kumlipa kwa kumkamatisha kwenu. Nirudishe kwenye gari yangu. Sitazungumza na
Andy.” “Kwa hiyo unataka aje atumiwe kuja kumwangamiza binti mwingine kama
alivyofanya kwako wewe?” Hapo Maya akafikiria.
“Na kama kweli Vic yupo nyuma ya hilo au kweli
anatumia madawa kutenda watu vibaya, huoni utakuwa umemtoa mwangani? Utasafisha
jina lako na la kaka yako ambaye sasa hivi anakashfa mbaya tu mtandaoni na pia,
utaweka kikomo kwa binti wengine wasifanyiwe kama wewe na kaka yako. Halafu
huwezi jua anaweza kusaidia vipi kupatikanika kwa Mrs Cote. Chochote kutoka kwa
yeyote, tunahitaji ili kuweza kumpata Mrs Cote akiwa salama.” Hicho kikamuingia
Maya.
“Unafahamu kifaransa?” Maya akamuuliza. “Nafahamu.”
Maya akakunja uso. “Sikutegemea jibu la ndiyo!” “Kumbuka kazi ninayofanya Maya.
Inanilazimu kujua lugha pia. Kwa nini umeniuliza?” “Nataka ukinisikia nikizungumza
neno la kifaransa, ujue nazungumza na wewe. Kwa hiyo naomba kuwa makini ili
nisidhurike. Hatujui Andy yule niliyekuwa naye kama ndiye huyu Jake wa sasa na
hatujui ameapishwa vipi na Vic.” “Hilo ni wazo zuri sana.” Malcom akamsifia
kama kawaida yake.
“Unaona ile gari pale?” Maya akachungulia nje. Ilikuwa
mbali kidogo na ilipokuwepo nyumba ya Andy. “Basi ile ni gari ya CSIS. Imejaa
mitambo ya sauti na video nzuri tu. Na kuna watu wazuri tu wa usalama ndani ya
ile gari na hili eneo lote, hata wale wanaopita pale na wale waliokaa pale kama
wahuni tu. Ni watu wa usalama.” Maya akashangaa sana. Akamwangalia Andy, “Inamaana
nilikuwa nikisubiriwa mimi!?” Akauliza Maya. “Ndiyo.” Malcom akajibu
nakuendelea.
“Kwa ufupi nataka kukuhakikishia kuwa, hili eneo
limezungukwa na maafisa wa CSIS. Na kwa kuwa wewe ni Cote, akili na macho ya
wakubwa wote wa CSIS yapo hapa tulipo sasa hivi, na ndani ya hiyo nyumba alipo
Jake ili kuhakikisha hakuna linaloharibika hata kidogo. Usiogope. Tutaona na
kusikia kila kitu. Ukijisikia tu upo hatarini, niite.” Akamuona anashuka bila hata kuaga. Malcon akaondoa
gari pale karibu na nyumba ya Andy.
Maya & Andy.
M |
aya akasogea mpaka mlangoni. Akavuta pumzi mara kadhaa. Wakamuona anasugua viganja. Akavuta
tena pumzi. Akafunga macho kwa muda ndipo akaweza kugonga mlango. Jake
akafungua. Alishtuka mpaka Maya akamuona usoni. Wakabaki wakitizamana kwa muda.
“Maya!” “Umenisahau?” Maya akamuuliza. “Sikutegemea kukuona hapa hasa baada ya
yote yanayoendelea kwenye familia yenu!” Maya akabadilika na kuweka sura ya
huzuni. “Unakumbuka wakati ule nilipokuwa nipo kwenye matatizo nilikuwa
nikikukimbilia wewe Andy?” Maya akaanza kwa sura ya majonzi.
“Ingia ndani. Ingia.” Akamshika mkono na kumvutia
ndani. Akafunga mlango. Maya hakutaka hata amguse. “Tunda hakuwa wifi yangu tu
Andy, alikuwa rafiki wa pekee ambaye sijawahi kumpata.” “Pole sana Maya.
Nilikusikia kwenye tv, siku ya kumkaribisha nchini. Pole sana.” “Sijui
nitafanyaje Andy! Polisi wameshindwa kumpata. Wamejaribu
kufuatilia gari iliyomtorosha, watekaji wake wanaonekana wanaakili sana.
Wamepotelea chini ya daraja.” Maya akaanza kulia.
“Njoo nikwambie kitu. Usilie.” “Nini?” Maya akauliza. “Nimekumiss Maya. Njoo
angalau tukae hapa nikushike tu. Nitakwambia kitu.” “Kwa hiyo huwezi kuniambia
mpaka unishike?” “Maya! Wewe huna hamu na mimi?” “Wewe ulikuwa wapi siku zote
hizo usinitafute mpaka mimi nikufuate?” Maya akamuuliza.
“Hayo ni masharti niliyokuwa nimepewa na
mwanasheria wenu. Logan?” “Logan! Alikwambia nini!?” Maya akauliza kwa
kushangaa sana. “Atanitetea mimi na wewe kama nitamuahidi kama sitarudi tena
kwenye maisha yako. Na akaniahidi nikirudi tu, atahakikisha anatafuta ushahidi
wakutosha kuwa mimi ndiye nahusika kwenye kukulevya na kukufanyia mabaya.”
“Sasa ulikuwa na wasiwasi gani wakati mimi na wewe wote tulikuwa tukilevya.”
Jake akanyamaza.
Maya akamsogelea. “Usiniambie kama wewe ndiye
uliyekuwa ukinilevya Andy!” “Nooo. Sio mimi kabisa Maya. Kumbuka mimi ndiye
niliyekuwa nikikukataza usinywe hata pombe.” “Sasa kwa nini siku ile tuliamka
tukiwa hatujitambui tulifikaje kitandani wakati tulikula tu Piza na juisi?
Ukanidanganya kuwa na wewe hujui ni nini kilitokea. Halafu tukaja kukuta video
na picha za siku ile mitandaoni? Ulinidanganya, kumbe ulinilevya Andy!”
“No no nooo Maya. Sio mimi na Mungu wangu ni
shahidi. Sio mimi. Mimi nilikukataza na unakumbuka nilikasirika mpaka
nikakugombesha ni kwa nini ulikuja kuinywa tena ile juisi wakati nilikukataza?”
“Kwa nini ulinikataza kama hukujua kama inakileo? Na kama wewe hukuweka, nani
aliweka?” Andy kimya. “Unajua nini Andy, umenidanganya vyakutosha. Hukuwahi
kunipenda na wewe umekuwa ukinitumia kama wengine. Naondoka.” “Hapana Maya.
Naomba usiondoke.” Andy akakimbilia mlangoni.
“Nina mengi ya kukwambia ila akili haijatulia. Nipo
kama nimechanganyikiwa.” “Ndio utulie uniambie ukweli.” “Siwezi kutulia mpaka
unitulize Maya. Wewe unajua kunituliza.” Maya akashangaa sana. “Umechanganyikiwa
Andy! Wewe ni mwenda wazimu. Yaani kwa tuhuma zote hizi ambazo umeshindwa
kujieleza hata moja! Bado unaniomba penzi!?” “Nina hali mbaya na wewe ndio
utaweza kuniweka sawa.” Akamsogelea.
“Nisikilize Maya. Ukiniweka sawa, nakuhakikishia
nitaweza kukusaidia hata kumpata Mrs Cote.” Maya akashangaa na kuanza
kutetemeka. Ila akajaribu kutulia. “Huwezi kunifanyia hivyo Andy. Umeniumiza
sana. Angalau tuweke mambo sawa, ndipo turudi kwenye mapenzi. Huwezi kunitaka
kimapenzi wakati umenivuruga.” “Sio mimi. Hata mimi nimevurugwa Maya. Walikutoa
kwangu nikiwa nakuhitaji. Hata mimi nimevurugwa.” “Nani?” Maya akamuuliza.
“Maya! Nisaidie tafadhali. Huwezi jua ni kiasi gani
nakuhitaji. Siwezi kukubaka, lakini ujue unao uwezo mkubwa sana wakunifanya
nitulie ili nifanye kazi. Tokea niliposikia Mrs Cote ametoroshwa, nilijua
naweza kumsaka kutumia ile komputa pale. Iangalie ipo wazi, lakini nashindwa
kufanya kazi.” “Kwa nini?” Maya akauliza kwa kumshangaa sana. “Kusikia jina
lako tena kwenye mitandao, nikakuona ukilia, ukiomba msaada. Nikakimbilia
kompyuta nikijua naweza kukusaidia kumpata Tunda, ili usilie. Lakini pia
kukaniharibu akili kabisa. Nikakumbuka wakati ule tukiliwazana kila mmoja wetu
akiwa kwenye matatizo. Nikaingiwa tena na hamu ya ajabu. Siwezi kufanya
chochote.” Maya alimshangaa akabaki ametoa macho.
“Wewe niache nikuguse kule nitakapo, ndipo nitaweza
kufanya kazi. Unakumbuka vile nilivyokuwa nikitulia wakati nipo na wewe?” Maya
akabaki anamtizama. “Mapenzi niliyokuwa nikifanya na wewe, yalikuwa
yakinituliza sana. Vic amekuwa akinilipa niwe namfanyia mapenzi kama yale
tuliyokuwa tukifanya na wewe, lakini bado sijawahi kuridhika kama nilivyokuwa
nikifanya na wewe. Niruhusu nikuguse akili itulie nitakwambia kila kitu.”
Machozi yalianza kumtoka Maya.
Akajua ni kweli Vic anahusika. Akakumbuka Malcom
alimwambia ajitahidi kutawala hisia zake. “Usilie Maya.” “Yaani ulikuwa na mimi pamoja na Vic?” “Nooo. Sio
wakati ule ule. Nilipotoka jela ndipo Vic akanifuata tena. Akaniomba nifanye
mapenzi na yeye hata kwa malipo kama nilivyokuwa nikifanya na wewe.” “Vic aliona wapi sisi tukifanya mapenzi?” Jake
akajishika kichwani kwa mikono yote miwili, akageuka na kuondoka pale. Ikabidi Maya
ajitulize ili aweze kumtuliza na yeye azungumze.
“Andy?” Maya akamsogelea na kumvuta taratibu. “Niambie
ni wapi Vic alituona tukiwa tukifanya mapenzi. Lasivyo naondoka na sitafanya
mapenzi na wewe tena.” “Naomba usiondoke Maya. Kama kukusikia na kukuona kwenye
tv kumenichanganya hivi, je kukuona na kukugusa kabisa! Naweza kujiua kama
ukiondoka na kuniacha hivi.” Maya akashangaa sana. “Wewe ni mgonjwa wa akili na
upo kwenye matibabu?” “Zamani!” Maya alishtuka akatamani kukaa chini.
“Andy! Kwa nini hukuniambia kama unaugonjwa wa akili?”
“Kwa kuwa nilipona kabisa. Na nilipokupata wewe ndio ikawa zaidi. Nisaidie
Maya.” Maya akajua anaongea na kichaa hapo. Na kimeshatibuka. Akajua hatima ya
Tunda ipo juu yake. “Nahisi hali yangu imerudia Maya. Nilitaka kumtafuta Mrs
Cote lakini nimeshindwa. Mimi ni mjuzi sana wa kompyuta. Tena bila kusoma. Nina
kipaji hicho tokea mtoto sema mama alishindwa kuniendeleza sababu ya uwezo.”
“Hicho walichofanya hao waliomteka nyara, ni kitu
cha kijinga sana. Nilikigundua mchana. Lakini nikashindwa kabisa kufikiria. Nisaidie Maya.” Akashangaa anaanza kulia. “Nikupeleke
hospitalini?” Maya akamuuliza huku akianza kumuogopa. “Hapana.
Fanya mapenzi na mimi kama wakati ule. Ninauhakika akili itatulia. Nitaweza
kufikiria na kufanya kazi vizuri tu. Nitaweza kufuatilia lile gari la pili
lililombeba Mrs Cote. Lakini sasa hivi siwezi tena. Nisaidie Maya. Mrs Cote
yupo matatizoni na ni lazima nimsaidie.” Akawa kama amechanganyikiwa
kabisa. Analia utafikiri yeye ndio Net akitaka kumsaidia Tunda.
Akapiga magoti mbele ya Maya akilia huku amemshika
Maya magoti. “Ninauwezo mkubwa sana Maya.
Nitakuonyesha. Nina uwezo wa kuingia kwenye mitandao ya usalama wote wa hii
nchi. Hata CSIS, nikafanya ninachotaka na nikatoka bila hata mtaalamu wao
kuhisi kama niliingia. Namaanisha bila kukamatwa.” Maya akashtuka sana.
Akajua wamemsikia. “Usilie. Tulia kwanza. Simama.” Akamuwahi ili asiendelee
kuongea. Akasimama na kujifuta machozi.
“Utaniambia na maswala ya Vic?” “Nina uhakika
nitakumbuka kila kitu. Na nitakusaidia kukwambia ni wapi alikuwa akipata madawa
ya kukufanya ulewe na kesho yake usikumbuke kitu ulichofanya siku iliyopita.”
Maya akashangaa zaidi. “Na nitakusindikiza mpaka kwa aliyekuwa akimuuzia.
Alishawahi kunituma kwake nikachukue dawa kwa ajili yako. Unakumbuka ile video
nyingine walirusha, walituchukua tukiwa hotelini? Nilikupeleka siku ya birthday
yangu? Tukalala huko kama siku mbili hivi? Sijui kama unakumbuka?” Maya kabaki
kimya.
“Unasahauje Maya? Ile video mpaka ukashangaa
walitupataje vizuri kwa kiasi kile halafu ukashangaa walijuaje tulipo wakati
tulikuwa nje ya mji, na hukuwa umemuaga mtu yeyote! Bado hukumbuki tu kama
mimi!?” “Nakumbuka Andy!” Maya akaongea kwa uchungu sana. “Basi ujue ile hoteli
alitutafutia Vic na ile video ilitoka vizuri vile ni kwa sababu safari ile Vic
alitafuta wachukua video wataalamu. Aliandaa kila kitu siku moja hata kabla ya
sisi kufika kule. Ndio maana ikabidi anitume mimi kwenda kwa huyo mtu wake
kununua hizo dawa kulekule Norfolk kwenye mji wenu. Ni dawa maalumu anazotumia
kwako.”
“Na kwa kuwa siku ile alitaka video
ndefu na nzuri, alitafuta wataalamu kabisa wa kutuchukua video. Chumba kilikuwa
na wataalamu watupu siku ile. Wakifanya kazi ya kuchukua ile video yetu tu. Vic
alisimamia yeye mwenyewe, alisema hataki kitu kiharibike. Sema nimewasahau
majina yao. Ukinisaidia, nitawakumbuka wote. Nashangaa mimi huwa sina tabia
yakusahau vitu! Kwa nini sasa hivi sikumbuki vizuri?” Akajishika kichwa na
kuanza kulia.
“Fix me, Maya! Wewe huwa unajua
kunifanya nitulie. Lazima nirudishe kumbukumbu. Siwezi kusahau vitu nilivyokuwa
nikivijua. Please Maya!” Maya akaanza
kutokwa tena na machozi. Alijisikia uchungu sana. Inamaana inabidi kufanya
mapenzi na huyo kichaa ili kumpata Tunda na kusafisha jina lake na kaka yake! “Naomba hii usichukue video tafadhali. Itabidi tu kufanya
kama anavyotaka ili aweza kusaidia. Na kama niliweza kutumika kwa ujinga, kwa
hili sina budi kufanya. Ila usichukue video tafadhali.” Maya aliongea
kwa kifaransa akimfikishia ujumbe Malcom. Lakini akashangaa Andy ameelewa yeye.
“Mimi siye niliyekuwa nikichukua Video kwa ajili ya
kukutumia Maya. Ni Vic. Vic ndiye aliyefanya kwa ujinga. Mimi nafanya kwa
mapenzi ya kweli kwa kuwa nakupenda.” Andy akajibu kwa kingereza vizuri
tu kama vile Maya alikuwa akimuongelesha yeye. Maya akashtuka sana akajua
amekamatwa au hajaelewa.
“Inamaana unaelewa lugha ya kifaransa?” Ikabidi
amuulize. “Yeah. Kwani sikukwambia? Nilizaliwa Ufaransa. Mama yangu alikwenda
kule kusoma, akapewa mimba na mume wa mtu. Wakakubaliana wafanye siri.
Nilipofikisha miaka 10, siri ikajulikana. Mke wa yule baba akataka kunidhuru
mimi ili nisichukue mali zao. Ikabidi mama atoroke. Lakini hiyo sio lazima. Fix
me, Maya.” Maya alikuwa akimshangaa Andy, akashindwa kuelewa alikuwaje naye
kwenye mahusiano mpaka kumfikiria ndoa akiwa hamjui kwa kiasi hicho!
“Kwa hiyo ulikuwa ukitumia jina hilohilo Andy?”
“Nooo. Andy sio jina langu. Hilo amenipa Vic. Jina langu ni Jake. Na tukiwa
tunafanya mapenzi sasa hivi, niite Jake sio Andy. Andy ni jina la Vic.” Machozi
yakaanza kumtoka tena Maya. Andy
hakwepeki, anataka penzi. “Naomba usilie mbele yangu Maya. Utazidi
kunichanganya na kunifanya nizidi kuchanganyikiwa nakushindwa kumpata Mrs Cote.
Unajua kila dakika inayozidi kupotea ndivyo anavyozidi kuwa matatizoni?” Jake
akazidi kusisitiza bila mapenzi, hawezi kusaidia.
“Unakumbuka ulikuwa ukipenda
kunifanyia nini?” Maya
akamuuliza kwa uchungu sana. Akamuona Andy anacheka cheka. “Naruhusiwa kuanza?”
Akauliza Jake kwa heshima sana akiwa mbele ya Maya. “Lakini unaniahidi
utanisaidia Andy?” “Hapana. Niite Jake. Jake ndio jina langu.” “Sawa Jake.
Unauhakika baada ya hapa utanisaidia.” “Nimekuhakikishia Maya. Ninauhakika
baada ya mapenzi na wewe nitakumbuka kabisa.”
“Unajua Vic alikuwa akinilipa nikamfanyie mapenzi kama
niliyokuwa nikifanya na wewe, lakini yeye alikuwa akifurahia mimi sikuwa
nikifurahia?” “Uliniambia Jake.” “Unafikiri ni kwa nini?” “Wewe niambie.”
Akamuona anatabasamu huku aking’ata meno. “Kwa sababu Vic sio Maya, na hatakaa akawa
Maya. Upo na ladha ya tofauti.” Jake akaanza kumsifia kwa undani kabisa. Jinsi
alivyokuwa akifanya naye mapenzi. Maya hakuwa akijua kama watu wa usalama
wanawasikiliza au walishafunga kila kitu baada ya kuongea na Malcom kwa
kifaransa.
“Unataka tukafanyie wapi?” Maya akaona amkatishe.
Maana alikuwa akiongea mambo mazito mno. Akaangalia pale walipo. Ni kweli
paliendana na Jake mwenyewe wala siye Andy aliyekuwa amekutanishwa na Vic.
Ilikuwa nyumba ya kawaida sana hata thamani yake ilikuwa ya kawaida mno. “Unakumbuka
tulikuwa tukianzia popote? Nikiwa na wewe Maya, sihitaji kitanda kuridhika. Au
wewe unahitaji kitanda?” Akawa ameanza kumvua nguo Maya.
“Nafikiri chumbani ni pazuri zaidi. Halafu
tukimaliza, tutakuja kufanya kazi hapa.” “Asante kwa kunisaidia Maya. Unajua
ukinisaidia mimi, nitaweza kumsaidia Mrs Cote. Unajua na yeye anafanyiwa kama
alichofanyiwa mama yangu akiwa nchini Ufaransa?” Akaanza Jake huku akiendelea
kumtoa Maya nguo. Maya alitulia tu huku akitetemeka na machozi. Alijua historia
yake inajirudia. Kufanywa mapenzi mbele ya kamera. Ila safari hii mbele ya
macho ya usalama wa taifa.
“Walimteka nyara mama. Wakampa masharti aondoke
nchini kwao. Asirudi tena na wala asije kusema kama mimi ni mtoto wa yule baba
lasivyo wataniua mimi. Mama alipokubali ndipo wakamuachia. Ndipo tukatoroka
kuja huku kama kujificha. Mrs Cote hana tofauti na mama yangu. Lazima
nimsaidie.” Gafla yeye ndio akaonekana anauchungu na Tunda kuliko yeyote.
Akawa amemaliza kumtoa nguo Maya. “Oooh
Maya! Maya wangu. Vic hawezi kujifananisha na wewe hata kidogo!” Akambeba hapo
Maya, mpaka chumbani alipotaka Maya. Alimsikia akigugumia kama aliyepata nafuu.
Alifanya mapenzi na Maya akiwa ametulia wala sio kichaa. Alihangaika na huo
mwili wa Maya, kama aliyekuwa akijitibu kiukweli. Kila alipomaliza, aliendelea
huku akimwambia Maya, hiyo ni mara ya mwisho. Jake alifanya mapenzi na Maya
huku akimshukuru na kumsifia, mpaka akaridhika yeye.
“Mbona unalia Maya!?” “Kwa
sababu ya furaha Jake. Nilikuwa na hamu na wewe.” Jake akambusu. “Umeridhika
sasa?” Akamuuliza kwa upendo. “Nitakuomba tumalizie
tena baadaye. Sasa hivi tumtafute kwanza Mrs Cote.” “Upo sahihi Maya.
Wasije kumuua.” Maya akajitahidi sana kutulia ili kuweza kutimiza lengo, sadaka
yote aliyotoa isiwe bure, kwani machozi yalikuwa yakiendelea kumtoka kama mvua.
“Unafikiri Vic anahusika katika
kumteka Tunda?” “Sijui Maya.
Lakini Vic anaweza kufanya chochote. Twende kwenye kompyuta.” Na kweli Jake
akawa ametulia mpaka akamshangaza Maya. Hapo akaamini ni kweli ni kichaa. Maya
akatoka hapo chumbani kwenda kutafuta nguo zake kule zilipokuwa zimeachwa.
Akaziokota huku akilia sana. Mikono imeshilia
matiti yake. Alipotaka tu kuvaa Jake akatoka. “Naomba usivae Maya. Si umesema
tutarudia?” “Nasikia baridi Jake. Acha nivae.”
“Oooh pole. Basi nikusaidie kuvaa.” “Naomba nitumie
choo kwanza. Nitarudi baada ya muda mfupi.” Akamsindikiza mpaka chooni.
Akaingia humo ndani na kuanza kulia sana. Alilia Maya, mpaka akahisi Jake
atamsikia. Akaogopa asije akaharibu tena. Akaosha uso tena na tena ndipo
akatoka.
Alitoka na kumkuta Jake ameshavaa na ametulia mbele
ya kompyuta akionekana amezama kwenye kile anachokifanya. Akamwambia Maya na
yeye avute kiti akae pembeni yake amuonyeshe jinsi ya kumtafuta Tunda.
Vic mbele ya Maya & Jake.
W |
akati ndio Maya
anatulia tu ili aone anachokifanya Jake kwenye kompyuta, wakashangaa mlango wa
nyuma unafunguliwa kwa nguvu. Alikuwa Vic. Amevaa nguo nyeusi juu mpaka chini
na kofia. Nywele zake za Blond amezificha ndani ya kofia kabisa kama asiyetaka
mtu amtambue. Akawatolea bastola yenye kiwambo cha sauti. Maya akashtuka sana. “Unafanya
nini hapa Vic?” “Hilo swali muulize Jake, au wewe bado unamfahamu kwa jina
nililompa mimi la Andy?” Vic akamuuliza Maya kwa kumkejeli.
“Niangalie mimi Vic. Naomba usimdhuru Maya.” Jake
akataka kusimama. “Hatua moja mbele, nakupiga bastola Jake. Sikutanii. Rudi
kukaa.” “Basi hiyo bastola nielekezee mimi sio Maya.” Jake akamsihi. “Kwa nini?
Hilo umeligundua lini? Mbona ulikubali pesa yangu na kumfanyia kila
nilichokutuma? Leo ni kipi kimegeuka?” Vic aliongea kwa ujasiri akionekana
amekasirika sana. “Kwa nini ulinifanyia hivyo Vic?” Maya akauliza huku
akitetemeka. “Wewe ni mshenzi Maya. Ulianza vita na mimi ukifikiri utashinda!
Mimi nina pesa na watu. Marafiki zako wote uliodhani ni marafiki zako, ndio
wabaya kuliko mimi.” “Wewe ni muongo Vic.” Maya akabisha. “Sasa unafikiri
nimejuaje kama upo hapa kama sio rafiki yako kuniambia?” “Gina!” Maya
akashangaa sana.
“Wewe ni mjinga Maya. Miaka yote hiyo ndio leo
unaniuliza! Sasa hapa leo sio wewe wala Jake mtakaotoka wazima. Hili jambo ni
lazima nilimalize leo. Umenisababishia mateso mengi. Wewe ndio umesababisha Net
azae na mwanamke mwingine.” “Wewe ni mgonjwa wa akili Vic. Ni kipi
kinachokufanya ufikiri kuwa wewe ni mke wa Net!?” “Hata mama yenu ananikubali
kuwa mimi ndiye mke sahihi wa Net. Sio Malaya Tunda.” Moyo wa Maya ukapasuka.
“Ndivyo anavyokudanganya mama? Na kwa taarifa yako
tu, mama anamtumia yeyote yule kumuangamiza Tunda. Wewe si wa kwanza na wala
hutakuwa wa mwisho.” Akamrushia Maya urembo alioukuta pembeni ya meza. Jake
akadaka kwa haraka kabla haujamfikia Maya.
“Ameniambia mimi ni wa tofauti. Net ni mtoto wake
anamfahamu. Hakuna mwanamke atakaye mfaa Net kama sio mimi. Unafikiri ni kwa
nini nilikwenda kulala na Net?” “Ulimlevya na ndio ukalala naye.” Maya
akamkanusha. “Ni kwa sababu hata yeye alikuwa na hisia na mimi ndio maana
japokuwa alikuwa amelewa lakini aliweza kufanya mapenzi na mimi. Na kwa taarifa
yako, ilikuwa zaidi ya lisaa.” Maya akaona atampoteza na asipate kotekote.
Kwake na Jake.
“Wewe na mama wote ni wendawazimu. Haitakaa
ikatokea Net akawa na wewe Vic. Usikubali mama akakupotezea muda.” “Sasa kwa
ile video niliyosambaza mimi na ile ya Renee, mama yako amesema ile hakuna mtu
anaweza kumuamini tena kama kuna mapenzi kwa Tunda ila Net ananipenda mimi.
Wewe ninakuaa hapahapa, na Tunda hatakaa akaonekanika hata kama mkihangaika mpaka
kuleta FBI wa Marekani.” Maya akatumia akili ya haraka.
“Popote ulipomficha Tunda, tutampata.” “Nani
amekwambia mimi nimemficha Tunda? Sina huo muda. Mimi nipo hapa kwa ajili yako
Maya. Umesababisha machungu mengi sana wewe. Hivi unajua umenisababisha kuua
usiku huu?” Maya akaanza kutetemeka. “Nani amekwambia uanze kuchimbua mambo
yaliyokuwa yamezikwa? Nani amekwambia uanze kutafuta watu ambao hakuna hata mtu
aliyejua kama wapo?” “Kama nani? Mimi sijamtafuta mtu yeyote zaidi ya Tunda.”
Maya akajikaza na kujitetea.
“Acha uongo Maya. Unazidi kuniudhi.” Akataka
kumsogelea ili ampige, Jake akamzuia. “Hukutoka kumpigia simu Gina sasa hivi na
kuuliza ni nani aliyekuwa akikuchukua video?” Vic akauliza kwa ukali. Maya
kimya. “Hujapiga simu kwa mtu aliyekuwa akikuuzia unga wewe?” Maya akazidi
kuingiwa hofu asijue nani ameshauwa kwa kupiga kwake simu. “Nisikilize Vic.
Hapa bado hujaua mtu yeyote yule. Unaweza kuondoka hapa na mtu asijue hata kama
ulikuwepo hapa. Na mimi na Jake hatutasema.” Jake akatingisha kichwa
kukubaliana na alichosema Maya.
“Unafikiri mimi ni mjinga! Kwa yote uliyojua hapa.
Na ujinga huo anaotaka kukwambia Jake sasa hivi, ni kipi kitakachokufanya
usinipeleke polisi wewe usiyenipenda kwa kiasi hicho?” “Jake hajaniambia
chochote.” “Mimi si mjinga. Tokea muda nilipopigiwa simu kuwa unakuja kwa Jake,
mpaka sasa hivi, mlikuwa mkifanya nini kama sio Jake kukiri kuwa mimi ndiye
niliyemwajiri akurudishe kwenye ulevi?” Vic mwenyewe akakiri na bastola
mkononi.
“Nakuhakikishia hajaniambia kitu. Mimi nilimfuata
kwa ajili ya mapenzi. Nilikuwa nina hamu naye.” Maya alikosa chakujitetea,
akaishia kujifunga zaidi. “Kwa hiyo mmefanya mapenzi!?” Vic alishtuka sana,
akauliza kwa sauti ya juu sana mpaka Maya akazidi kutetemeka. “Tulia kwanza
Vic.” “Umenisaliti Jake. Mimi ndiye mwanamke ulitakiwa kulala naye, sio huyo.”
Akaenda kumgonga Jake na bastola kichwani mpaka akampasua.
“Acha Vic. Unamuumiza.” Akampiga teke Maya. Maya
akaanguka. “Naomba msiingie kwanza.” Akaongea Maya kwa kifaransa akimfikishia
ujumbe Malcom. Maana alijua kwa ile fujo, polisi lazima waingie. Hofu ilikuwa
imemuingia Maya, akajua yupo hapo na wagonjwa wawili wa akili, lakini ilikuwa
lazima ampate Tunda kwa garama yeyote ile. Alishatoa mwili wake kwa kufanyiwa
mapenzi kwa muda mrefu tu. Maya akagoma kuyafanya yaishe bila kufanikisha hata
kimoja juu ya Tunda.
Kwa kesi yake na kaka yake ni kama ilishakamilika.
Wakapata ushahidi wakutosha na Vic alishakiri kila kitu na akasema ameua.
Akajua Vic hatakuwa tena tatizo maishani. Ameshajikamatisha kwenye vyombo vya
usalama. Swali likabaki kama sio yeye aliyemchukua Tunda, nani amemchukua
Tunda. Maya akakusudia mtoe huo kweli Vic. Kufa na kupona mpaka kieleweke.
Bado Jake
alikuwa akivuja damu kichwani. “Usimguse Jake. Tafadhali Vic. Mimi sikujua kama
ni mwanaume wako ndio maana leo nilimfuata kimapenzi. Nakuahidi...” “Mmefanya mapenzi kwa muda gani? Sitaki unidanganye
Jake?” Vic na yeye akaanza kulia kama aliyesalitiwa haswa. Maya akazidi
kushangaa.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Mambo yanazidi kupamba moto, Ritha amerudi pichani. Amefanikiwa kutengeneza jeshi jingine dhidi ya Tunda. Safari hii huko ugenini amekwenda umbali gani? Kama Vic amekiri hajamchukua Tunda, nani anaye Tunda? Nani ameshauwawa usiku huo?
Endelea kufuatilia...
0 comments: