Nilipotea! Part 7 – Sehemu ya C
Kwa Ritha.
N |
i kweli yale mazungumzo yalikuwa yakisikilizwa na
kufuatiliwa na wakubwa wa CSIS. Pale pale Vic alipotaja jina Ritha kuwa
anahusika kuweka njama za Vic awe na Net, tayari maafisa wawili waliokuwepo
kwenye mji aliokuwepo Ritha, walitumwa kwenda nyumbani kwa Ritha. Kama kawaida
ya Ritha. Hakufanya kosa. Walimkuta usiku huo wa saa tatu sebuleni kwake,
anafuatilia tukio lakutekwa nyara Tunda kwenye vyombo vya habari.
Afisa wale wakagonga kama kawaida tu. Ritha
akafungua. “Niwasaidie nini?” Ritha akawauliza na tabasamu la kejeli usoni. “Tunamaswali
tunataka kukuuliza.” “Karibuni.” Akawakaribisha mpaka ndani. “Niwapatie
kinywaji gani?” “Hapana asante.” Wote wakajibu na kukaa. Ritha akawatizama kwa
macho makavu kama anayewaambia anawasikiliza.
“Mrs Cote amepotea.” “Kwa hiyo?” Ritha akauliza kwa
haraka. “Tunataka kujua alipo.” “Kama usalama wa taifa wameshindwa kujua alipo
tokea asubuhi. Tena wao wakiwa na vifaa vyote maalumu. Mnafikirije Mimi raia wa
kawaida nitajua alipo!?” Ritha akawashangaa kwa kuwabeza.
“Victoria Cloutier amesema wewe unahusika na
kutekwa kwa Mrs Cote.” Wakamtega kujua kama wanafahamiana na Vic. “Huyo ni nani
na kwa nini mpaka sasa hivi sipo chini ya ulinzi!?” Akili ya Ritha ikachemka
kwa haraka sana. Akajua anategwa. Akajitoa mapema sana. Akawauliza bila hata
kuonyesha hofu wala hata kuonyesha kama alishwahi hata kuzungumza na Vic.
“Mnakuja nyumbani kwangu kwa maneno ya uongo tena
mnayatoa kwa mtu ambaye hata simfahamu! Mnataka na mimi niwashitaki?” “Inamaana
wewe humfahamu kabisa Miss Victoria Cloutier?” Mwingine akauliza. “Ilitakiwa
nimfahamu!?” Ritha akauliza akionyesha kuwashangaa sana. “Tunaruhusiwa
kuzunguka humu ndani?” “Mkija na warranty nitawaruhusu kuzunguka. Sasa kwa kuwa
hamna warranty na mmekuja na tuhuma za ajabu, nawaomba muondoke sasa hivi kabla
na mimi sijaita polisi hapa kwa msaada.” Ritha akasimama na kuwafungulia
mlango. Ikabidi wale watu wa usalama waondoke tu.
Wakawapigia simu kina Malcom na kuwaambia
kilichotokea kati yao na Ritha. Hata wao walijua hawezi kukiri chochote. Ila
walimfanyia ujanja tu. Pale aliposimama kwenda kuwafungulia mlango na kuwaacha
pale sebuleni, mmoja alibandika kitu kidogo ambacho wangeweza kumsikia wakiwa
nje, kama atawasiliana na yeyote ndani. Wale
maafisa wawili wakaambiwa wasiende mbali na hapo kwa Ritha ili kama atapiga
simu kuwasiliana na yeyote yule wamsikie na kama atatoka, basi wamfuatilie
kujua anapokwenda. Tumaini likabaki kwa wale watatu mle ndani. Vic, Jake na
Maya.
Malcom kwa Maya.
H |
ofu ikawa imeshamwingia Malcom tokea Vic alipoingia
kupitia mlango wa nyuma na Maya kusema anayo bastola. Kwa mlango wa nyuma
hawakuwa na kamera. Waliweka chumbani na pale sebuleni tu ambapo waliweza kuona
mpaka sehemu iliyokuwa na meza ya kompyuta. Ni kweli Malcom alitumwa na
viongozi wake kwa Maya. Lakini ni kwa kuwa walimuona amekuwa dhaifu kwa Maya na
Maya naye akaonyesha kama amelainishwa na Malcom zaidi ya Roy. Ni kweli
walikuwa nje ya kioo wakifuatilia mahojiano yao na Maya.
Watu hao wa usalama wanaoweza kujua ukweli kwa
kusikia sauti na kusoma sura, wakagundua Malcom na Maya wamejenga kingine. Ndio
maana wakamtuma Malcom na kumtaka lazima yeye ndio akamwingie Maya ili
kufupisha na kurahisisha mambo kwa Jake. Njia nzima mpaka pale wanafika kwa
Jake, Malcom na Maya walijenga hisia nyingine mbali na kazi, bila kuambiana. Na
Malcom hakuwa ameanzia hapo kwenye mahojiano na Maya, siku hiyo ya asubuhi.
Hapana. Alipomwambia anamfahamu kwa asilimia 90, ni kweli alikuwa akimfahamu
Maya kwa undani zaidi ya hata Maya alivyoweza kumuelewa. Alikuwa ni binti
anayemfuatilia kwa muda mrefu tu tokea Malcom na Roy wapo chuoni na Roy alilijua
hilo.
Kitendo cha Jake kumtaka kimapenzi Maya usiku huo , Malcom hakuafiki kabisa. Akiwa na
viongozi wake ndani ya lile gari wakisikiliza, Malcom akawaambia yeye anaenda
kuwazuia wasifanye mapenzi. Viongozi wake wakamwambia haimuhusu. Na Maya sio
mtoto mdogo. Asipotaka kufanya mapenzi na Jake, ataomba msaada. Akitaka,
atafanya tu.
Malcom akabisha. Akawaambia yeye ndio amemlazimisha
Maya kwenda kuzungumza na Jake, kwa hiyo lazima akamtoe matatizoni. Wao
wakamwambia mpaka hapo hawajaona kama Maya yupo matatizoni, awaache wapenzi hao
wawili. Tena wakamwambia kama atashindwa kuwepo pale, aondoke.
Ikabidi Malcom awe mvumilivu. Japokuwa Maya aliomba
wazime video, pia wakakataa. Wakamwambia Malcom kwa hakika Jake anatatizo la
akili. Wakizima video halafu huku nyuma akamrudi Maya, binti wa Cote!
Watawajibishwa vibaya sana. Na wote wakamgeukia Malcom, na kumwambia hawapo
tayari kuingia matatizoni. Yeye kama hawezi kuangalia wapenzi hao wakikumbushia
enzi. Tena walimwambia kwa kumkejeli, aondoke.
Kiongozi wake akamwambia lazima kuweka hisia mbali.
“Macho na masikio yote ya viongozi wa nchi yapo kwetu. Leo unataka hisia zako
kwa Ms Cote zitufukuzishe kazi?” “Sina hisia zozote kwa Maya.” “Miss Cote.”
Bosi wao akamsahihisha kumtaka awe kikazi. “Ndiyo ni Miss Cote.” “Kama hisia
hazikusumbui, basi tulia tufanye kazi.” Ikabidi Malcom atulie. Roy rafiki yake
kipenzi Malcom ambaye walianzana naye urafiki tokea wapo kwenye chuo cha
mafunzo ya usalama wa taifa, alikuwepo hapo akisikiliza hayo mazungumzo ya Malcom
na bosi wao.
Malcom na Roy walimaliza chuo pamoja na kupangiwa
kazi sehemu moja. Kwa hiyo walikuwa marafiki wa muda mrefu na wasioweza
kutenganishwa. Kazini walipangiwa kazi sawa na hata kama nikutumwa, basi
walitumwa pamoja. Na nje ya ofisi pia ni hivyo hivyo wakawa kama kumbikumbi.
Ukitaka kujua Malcom alipo, muulize Roy, na Roy hivyohivyo. Walitokea kuelewana
sana. Familia ya Roy ikawa ni kama familia ya Malcom tu.
“Haitachukua muda mrefu Malcom. Najua
wote tumechoka. Mambo yakienda vizuri, leo kila mtu ataenda kulala nyumbani
kwake.” Roy akajaribu kumtuliza rafiki yake kwa sauti ya chini kidogo, lakini
akijua wazi tatizo sio uchovu ni wivu. Haikuwa hivyo kama walivyofikiri.
Mapenzi yalipoanza, Jake alikuwa akifanya mapenzi kwa hisia zote na Maya, tena
bila haraka akionyesha akifurahia anachokifanya. Aliita jina la Maya kwa kila
alichokifanya huku akifanya mapenzi hayo kwa kufurahia sana tu.
Jake alipomaliza safari ya kwanza na kumtaka Maya
kwa ya pili, hapo Malcom uzalendo ukamshinda. Wengine walikuwa wakiangalia,
yeye alikuwa ameinamia simu yake huku akisikia miguno ya mapenzi na vile Jake
anavyomwita Maya. Wakamuona Malcom anatoka ndani ya ile gari na kutupa
headphone za kusikilizia sauti katikati ya mchezo wa pili. Jake alisikika kwa
kukera sana kwa wenye wivu.
Jake na Maya walimaliza, na wao wakawa wameangalia
kila hatua huku maafisa hao wakifurahia nakushabikia kama watoto wadogo.
Alipoingia Vic, Roy akatoka kwa haraka kwenda kumtafuta Malcom. Akamkuta
amesimama nje kabisa ya lile gari. “Vic amewafuata.” Malcom akashtuka sana.
Akakimbilia ndani. “Naingia.” “Nimekwambia hutaingia ndani Malcom, mpaka Maya
mwenyewe akuite au tuone hatari.” Bosi wake akaweka msisitizo.
“Na ukiharibu au kuingilia hili tumaini la mwisho
la kumpata Mrs Cote, nitahakikisha unalala chumba kimoja huko jela na yule
aliyehusika kumteka Mrs Cote. Nitahakikisha na kuripoti na hutakaa kutoka
jela.” Bosi wao akamtisha Malcom. Ikabidi Malcom atulie.
Vic, Jake & Maya.
“Vic, naomba
utulie. Mimi naondoka nakuachia Jake wako.” “Hajawahi kuwa wangu. Na wala
simtaki. Nimelala na wewe leo nimegundua najipunja tu.” Vic akampiga risasi ya
mguuni. Maya akapiga yowe na kumwita Malcom kwa sauti. “Malcom!” Sababu
ya kelele ya Jake aliyekuwa amepigwa risasi ya mguu, hawakuelewa nini Maya
anaongea, lakini Maya aliendelea kupiga kelele.
Malcom alipoona kwenye video Maya anapiga kelele
kama aliyeingiwa hofu, akakimbia bila kuomba ruhusa tena. Akasukuma mlango wa
mbele nyumbani hapo kwa Jake, akajikuta
amesimama mbele yao. Kwa haraka sana Vic naye akamvuta Maya na kumuwekea risasi
kichwani. “Ukisogea hata hatua moja, nampasua kicha, Maya.” Vic alikuwa
akitetemeka kama aliyepagawa kabisa. “Nisaidie
Malcom. Vic ataniua.” Maya alikuwa akilia sana, Jake sakafuni anavuja damu kichwani na mguuni huku
na yeye akilia kama mtoto.
“Nisikilize Vic. Bado huna kosa la mauaji hapa.
Usitafute kosa la mauji ukaishia jela hata nafasi uliyonayo ya kuwa na Net
ukaipoteza.” Malcom akaongea taratibu. “Net
ameniambia anampenda mke wake sio mimi. Sina kitu cha kupoteza tena. Na yote
hayo amesababisha huyu Maya.” Akamgonga Maya kichwani kwa nguvu na
kitako cha bastola, Maya akazidi kulia kwa hofu na yeye Vic pia alikuwa akilia.
“Niangalie mimi Vic. Niangalie.” “Usinifanye mimi mjinga Malcom. Najua wewe ni polisi.”
“Mimi sio polisi. Niangalie na uniambie unafikiri Net atakuwa na nani sasa hivi
wakati mke wake ametekwa?” Malcom akajaribu kumtuliza. “Kama huamini, Net yupo
njiani, anakuja. Utamsikia yeye mwenyewe. Ndipo utaamini kuwa anakupenda na
kukuhitaji wewe. Kwani uliona hata amekuuliza lile swala la kusambaza video
yenu ya mapenzi?” Malcom akaendelea kumuliza taratibu akimchota akili.
“Hapana. Kwa kuwa Net amenikasirikia.
Net amenikasirikia mimi.” Vic akazidi
kulia kwa sauti. “Hapana Vic. Hapana. Niangalie mimi acha kulia. Unakumbuka
ulivyosema kuwa Net anakupenda wewe hawezi kuwa na mwanamke mwingine?” Vic
akatulia kama anafikiria. “Nataka kumsikia Net
mwenyewe akiniambia sio wewe Malcom.” “Basi naomba utulie. Net anakuja
kukwambia yeye mwenyewe. Na ili Net akute mazingira mazuri, nashauri mtoe huyu
anayevuja damu hapo. Mtoe nje kabisa, akukute kwenye mazingira mazuri na safi.”
Malcom akaendelea kumshauri akiwa ametulia kabisa.
Akamwambia Maya kwa kifaransa kuwa atulie asiwe na
wasiwasi. “Unaongea nini wewe? Unanichanganya!”
Vic akawa hajaelewa. “Hapana. Usichanganyikiwe. Niangalie mimi. Tulia, jiandae
kumpokea Net. Sawa?” Vic akajikuna kichwa na ule mkono uliokuwa umeshika
bastola, kama anayejaribu kufikiria lakini anashindwa. Bado mkono mwingine
alikuwa amemshikilia Maya kwa nguvu zote kama asimponyoke. Akatoa ile kofia na
kuitupa chini.
“Sasa unataka nifanye nini na huyu?
Si heri nimuue tu ili asije akasema kwa polisi?” Vic akauliza juu ya Jake kwa Malcom ambaye alikuwa haonyeshi kama ni
mtu wa usalama. Alikuwa amevaa nguo za raia. Ila safi na akapendeza. “Kama
nilivyokwambia Vic, bado unanafasi kubwa sana ya kuwa mke wa Net. Utakapomua
huyo, utakuwa na kesi ya mauaji. Watakufunga kifungo cha maisha au kukunyonga.
Utakuwa umepoteza kabisa bahati ya kuwa na mwanaume unaye mpenda. Acha mimi
nitoke naye hapa, ili kukupa muda wakutulia mpaka Net atakapokuja.” “Lakini siwezi kumruhusu Maya.” Vic akajibu huku
akifuta machozi.
“Sawa. Mtoe huyo Jake anayevuja damu ili asije
kukufia hapo na kukuletea matatizo. Na huyo Maya, nashauri uchukue tape, mfunge
mikono na miguu, umuweke chumbani. Mfungie ili Net akukute peke yako ukiwa
umetulia.” Hilo akaliafiki Vic kwa haraka. “Kwa hiyo naweza kumtoa Jake sasa
hivi?” “Fanya haraka ili nisafishe kabisa hizi damu. Sitaki Net apakute hapa
pachafu.” “Wazo zuri.” Malcom alikwenda kumbeba Jake pale sakafuni na kumtoa
nje. Tayari kulishajaa magari ya wagonjwa, ambulance na polisi pale kwenye hilo
eneo, kila mtu roho mkononi. Mtoto wa Cote yupo ndani ameshikiwa bastola! Kila
mtu hofu. Wanamwambia nini bibi Cote! Amepoteza mkwe na mjukuu! Afisa wa
usalama wakazidi kumiminika hapo. Jake akapokelewa na watu wa huduma ya kwanza
kwa haraka.
Kwa kina Cote.
B |
ado bibi Cote na Net walikuwa sebuleni na maafisa
wa CSIS wakisubiria simu yeyote kutoka kwa mtekaji au mtu mwenye fununu. Simu
ya kutoka kwa director wa CSIS ikaita. Bibi Cote akapokea kwa haraka. “Kwanza nataka usipaniki, Emily. Nisikilize kwa makini na
utekeleze kwa haraka. Mr Cote yuko wapi?” Bibi Cote akageuka kumwangalia
Net. “Yupo hapa. Ni nini kinaendelea?” “Weka kwenye
spika. Wote mnisikilize kwa ufupi, nitajibu maswali yenu baadaye.” Bibi
Cote au Emily kama alivyomtambua kwa jina la kwanza, akatulia. Net akasogea.
“Hapa tunapozungumza, ipo dalili
yakumpata Mrs Cote kwa kupitia Maya.” Bibi Cote na
Net wakaangaliana. Kwa masaa hayo matatu, hata hawakujua Maya alipo. Walijua
yupo na mtoto ndani. Yule kiongozi akawaeleza kwa kifupi kinachoendelea. Na
kumtaka Net aondoke na helcopter ya CSIS ambayo ipo umbali wa dakika tano
kufika hapo nyumbani kumchukua yeye ili kwenda kuzungumza na Vic, amtulize kwa
kumwambia kile anachojua Vic anataka kusikia, ili amuokoe mdogo wake.
“Hukufanya vizuri Mike!” Bibi Cote akamlaumu yule director kwa ngazi ya
chini sana yakufahamiana wao kama marafiki wakawaida tu, si kama kiongozi
mkubwa sana wa ngazi ya juu hapo nchini. “Kwanza ni
Maya mwenyewe ndiye aliyekuwa akimtafuta Mrs Cote. Amekutwa na mmoja wa afisa
wangu akiwa analia nje ya club akiwa anatafuta habari kutoka kwa marafiki wa
Vic. Tulichofanya sisi ni kuongeza nguvu na kumlinda. Kwa jinsi alivyokuwa,
jibu la kumkataza isingekuwa sahihi ila kumuongoza kwenye njia njema.” Hakumpa
ukweli kamili ili kufupisha habari.
“Hapa tunapozungumza, Jake au Andy...”
“Yule aliyekuwa mchumba wa Maya!?” Bibi Cote
akamkatisha kwa kuuliza swali. “Ndiyo. Kwa ufupi tu ni
Jake sio Andy kama mnavyomfahamu. Na alitumwa na Vic kwenye maisha ya Maya ili
kumuangamiza. Wote wawili wamekiri na tunao ushahidi.” Kiongozi huyo
aliendelea, asijue zile habari ni kama kumpiga kofi la usoni bibi huyo.
“Na hapa tunapozungumza, Jake ametoa
ushirikiano mzuri sana kwa Maya, amesema anayo njia yakufuatilia gari
lililomchukua Mrs Cote. Ila amepigwa risasi na Vic, ndio wapo kwenye kumsaidia
tuone kama anaweza kusaidia.” Mara
wakasikia mlio wa helcopter nje. “Naona helcopter imefika.
Na mimi nakwenda Mike.” “Kwa nini usisubiri, Emily? Itakuwa rahisi kumlinda
Maya na Nathiel. Acha akili za maafisa wote ziwe sehemu moja, kumuokoa Maya na
Net atakapoingia ndani kwa Vic mwenye risasi. Yule binti ni kichaa kabisa. Unatakiwa
umakini wa hali ya juu sana sasa hivi kwake. Ukienda kule itabidi wagawane
wengine wakulinde na wewe, Emily. Naomba usubiri.” Mike na yeye akamsihi
kama rafiki kabisa kwa kumtaja jina lake la kwanza, bibi Cote.
“She is my baby, Mike. Yupo kwenye hiyo hali sababu ya mimi kuzembea kwenye maisha yake. Mimi ndiye nimemfikisha Maya hapo. Ningemtilia maanani tokea mwanzoni kabisa, pengine ningeweza kumdhibiti Vic. Siwezi kumuacha Maya sasa hivi. Nakwenda.” Bibi Cote akakataa ushauri. Lakini walishamjua ni mtu asiyejua jibu la hapana. “Lakini lazima uelewe kuwa hutaruhusiwa kuingia ndani. Ili Vic asimdhuru Maya, lazima Net awepo peke yake na aonekane ametulia na amwaminishe chochote anachojua Vic anataka kusikia kwa wakati huu.” “Tengeneza mazingira ya mimi kuwepo huko Mike.” Bibi Cote akakata simu. Afisa mmoja aliingia akikimbia. Bila mengi, Net na bibi Cote wakatoka na wao wakikimbia.
Maya amekwenda umbali mkubwa sana ili kumpata Tunda. Na amekusudia kumpata kwa gharama
yeyote ile, arudi kwenye maisha yake.
v
Je, watafanikiwa
kumpata kwa wakati na akiwa bado hai hawajamdhuru?
v
Je, kujitoa
kwa Maya kutalipa?
v
Baada
ya kutulizwa na Maya kwa penzi la muda mrefu tu, kupigwa risasi na Vic, Je,
kichaa huyo Jake ambaye ndio kama tumaini la mwisho, kweli ataweza kuwa msaada au ndio sadaka ya Maya imepotea Bure?
Ritha ameongezwa kwenye picha lakini ameweza kuwazidi akili kwa kukwepa maswali ya mtego waliodhani wangemkamata nayo. kama kawaida yake kutumia akili za haraka kwenye kila jambo. Amekataa kabisa kuwa hausiki kwenye kumteka
Tunda na amefukuza afisa usalama.
v
Je,
anamjua muhusika ALIYEMTEKA TUNDA?
v
Je, Net
atafanikiwa kumtuliza Vic na kumuokoa dada yake?
v
Nani
ameuawa na Vic?
Usikose muendelezo
0 comments: