Books,

UTAMBULISHO WA KITABU CHA ENDLESS LOVE,

Monday, August 31, 2015 naomimwakanyamale 0 Comments



Usipitwe na hadithi hii iliyosheheni mikasa mingi iliyojaa majonzi, mapenzi mazito  na ya kweli. Utaona jinsi penye nia wakati wote huwa pana njia, kama ukikusudia na kutokata tamaa.

 
Kwenye hadithi hii utakutana na Mercy, msichana mrembo mwenye asili ya Venezuela na Mbantu kutokea wilayani Lushoto, mkoani Tanga. Aliishi maisha ya kifahari sana nchini Marekani, lakini alijikuta akiangukia kwenye matatizo makubwa  sana duniani akilia kutafuta msaada mchana na usiku, baada ya kutupwa nchini Tanzania tena kijijini kwa baba yake, Mlalo Tanga. Baada ya kufungiwa kijijini huko kwa miaka kadhaa, Mercy alijikuta akitangatanga mchana na usiku huku akiwa mgonjwa sana na njaa ikimnyanyasa. Ghafla, dunia  ilimbadilikia na kuanza kukandamizwa huku ikimtafuna bila huruma. Maisha ya Mercy yalijawa na usaliti, misiba na kujikuta peke yake mpaka alipoangukia kwenye mikono ya  kijana wa Kinyamwezi, Ben.


Ben ndiye aliyemuokoa Mercy  kutoka kwenye ‘suluhisho’ lake la kutaka kujiua, baada ya  Mercy kukata tamaa kabisa ya maisha.

Baada ya maisha yake kupitishwa kwenye moto mkali sana, na Mercy akibaki akijiuliza kwa nini alizaliwa na kupita alikopita, ndipo alipogundua kusudi la yeye kuwepo duniani. Haikuwa rahisi kwa Mercy hata kidogo, lakini yalikuwa ni majaribu yake, na ilimpasa kusimama. 
Sasa, unaweza kusoma hata kwenye simu yako. Karibu



0 comments: