Lifestyles,

utambulisho wa blog ya Mtazamo halisi

Monday, August 31, 2015 naomimwakanyamale 0 Comments


               UTAMBULISHO WA BLOG HII





~HABARI ZENU! KWANZA KABISA NAOMBA NICHUKUE NAFASI HII KUKUSHUKURU KWAKUTOA MUDA WAKO NA KUANGALIA VIDEO HII. MUNGU AKUBARIKI SANA. NAITWA NAOMI, NIPO KWENYE NDOA YA MIAKA 10 SASA, NA TUMEBARIKIWA  NA MUNGU WATOTO 3.


~KUTOKANA NA MASWALI NA MAMBO MENGI YANAYOENDELEA KATIKA JAMII ZETU KATIKA SECTOR MBALIMBALI  IKIWEMO UPANDE WA NDOA, UCHUMI, SIASA, AFYA, ELIMU NA MENGINE MENGI, NDIYO YALIYONIPELEKEA KUANZISHA BLOG HII  YA MTAZAMO HALISI AMBAYO NAAMINI TUTAYAPATA MAJIBU KWA PAMOJA.

~KAMA UTAKUBALIANA NA MIMI UTAGUNDUA TU MWANZILISHI WA KILA KITU HAPA DUNIANI NI MUNGU. NA VYOTE ALIVIANZISHA KWA MAKUSUDI MAZURI TU KWAAJILI YETU SISI WANADAMU. LAKINI KWAKUSHINDWA KUJUA MATUMIZI YAKE HALISI, UTAGUNDUA KARIBU KILA SECTOR NILIYOKWISHA TANGULIA KUTAJA HAPO AWALI, KUNATATIZO AU MATATIZO MAKUBWA SANA. MFANO MDOGO TU NI KATIKA SECTOR YA NDOA JINSI ILIVYOINGILIWA HIVI LEO NA SWALA LA USHOGA. TUNAWEZA DHANI NI KITU CHA GHAFLA LAKINI HAPANA, HILI NI ANGUKO LA MUDA MREFU SANA NA LINAANZIA KWENYE NDOA TAKATIFU MUNGU ALIYOKUSUDIA KWETU. NAHII INATOKANA NA WENGI WETU KUINGIA KWENYE SECTOR HIZI BILA KUJUA MATUMIZI YAKE.

~ NAOMBA UFIKIRI PAMOJA NAMI JAPO KIDOGO TU JINSI WATENGENEZAJI WA BIDHAA KARIBU ZOTE HAPA DUNIANI WANAVYO WEKA MAELEKEZO YA MATUMIZI ZA BIDHAA WANAZOTENGENEZA IWE KWENYE BIDHAA YENYEWE AU KWENYE KIJITABU AU KIKARATASI MAALUMU CHENYE MAELEKEZO YA JINSI YAKUTUMIA BIDHAA HIYO. KWA LUGHA YA KIGENI INAITWA "MANUAL". LENGO LAO KUBWA SI KUJIONGEZEA GARAMA YA UTENGENEZAJI WA BIDHAA HIYO! HATA KIDOGO, WANAKUSUDIA KUMNUFAISHA MTEJA WAO ILI AWEZE KUTUMIA VIZURI BIDHAA HIYO BILA KUIHARIBU AU ASIJE AKATUMIA KWA KIWANGO CHA CHINI KILICHOKUSUDIWA.

~KADHALIKA MUNGU NAYE ALIPOTUTENGENEZEA HII DUNIA NA MIFUMO YOOOTE ILIYOMO NDANI YAKE ALIWEKA "MANUAL", INSTRUCTION/MAELEKEZO YA JINSI YA KUTUMIA KILA KIMOJA WAPO.

~BLOG HII ITATUSAIDIA KUPITA KATIKA KILA SECTOR MOJA BAADA YA NYINGINE KWA KUTUMIA WATU WENYE UZOEFU NAZO WATUJULISHE NI KITU GANI WAO WAMEFANYA NA KUFIKIA MAFANIKIO. TUTAKUWA NA MAHOJIANO NAO KWA NJIA YA VIDEO, KUTAKUWA NA MADA ZINAENDELEA HUMU NDANI AMBAZO ZITAKUPA NAFASI YA WEWE KUTOA MCHANGO WAKO KWA MADA HUSIKA YA SIKU HIYO, ZAIDI KUTAKUWA NA HADITHI ZITAKAZO KUWA ZIKIWEKWA, MBALI NA KUKUBURUDISHA, ZITAKUELIMISHA.


~USIACHE KUTEMBELEA BLOG HII KWA VITU VIPYA KILA SIKU.
NIKUSHUKURU TENA KWA KUTEMBELEA "MTAZAMO HALISI" NA NINA KUKUKARIBISHA TENA.

0 comments: