Lifestyles,

UNAWAZA NINI?

Wednesday, September 02, 2015 naomimwakanyamale 0 Comments





Kila kitu kinachoonekana kuvutia kwa macho, kimeanzia kwenye wazo, iwe ni Mungu ndiye mwanzilishi au mtu aliyekubali kutulia, kusikiliza sauti ya ndani ambayo hutokana na jinsi Mungu alivyotuumbia tabia kama yake ya kufikiri vitu sahihi na kuchukua hatua. Ipo hatari kubwa sana kwa watu wenye kupenda kukimbilia kwa HARAKA kuongea mawazo yao bila wao wenyewe kutafakari wazo hilo na kumrudia Mungu kwanza kuhakikisha jambo au wazo hilo linatokana na Mungu.

Madhara ya kukimbilia kumwambia mwanadamu wazo lako kwanza, kabla ya wewe mwenyewe hujaelewa na kufanyia uchunguzi WAZO lako,  ni makubwa sana endapo hukupata mtu sahihi. Anaweza kukushauri kwa kukuangalia kwa muonekano wako wa nje, au Maisha unayoishi sasa au uliyoishi zamani au atakuambia kutokana na jinsi anavyoelewa yeye na jinsi alivyojaribu yeye na kushindwa. Utaishia kudharau mawazo yako wakati wote ukifikiri huna jambo muhimu linaloweza kutoka ndani mwako na kubaki Kuishi kwa kiwango cha chini sana ukikubali Maisha yako kuongozwa na fikira za watu wengine.

~Kubali kuwa mwazaji tena zoeza fikra sahihi {+ positive} wakati wote.
~Epukana na wazo la pili linalokujia au mtu/Watu wanaosema HAIWEZEKANI.
~Kumbuka KILA KITU KINAWEZEKANA chini ya jua. Jipe muda, fanya utafiti kwa watu WALIOFANIKIWA
~Chukua hatua. Kumbuka hakuna wakati utakao kujia unaosema ni sasa, kila wakati unachangamoto zake ni wewe kuwa juu ya hizo changamoto.

0 comments: