Raising Strong Deneration
1. Anza akiwa mtoto - Kutokana na wataalamu, wanashauri uanze kuanzia yupo mchanga kabisa. Hata kama unaona haelewi, lakini anza kuwekeza kuanzia kipindi hicho. Ongea naye kwa upendo, punguza stress unapokuwa naye, Imba ukiwa naye. Muwekee michezo yakujifunza ya kitoto. Toys za namba, herufi tena zenye rangi tofauti tofauti ambazo atakuwa akiziona tokea mtoto. Rangi kali kwa mtoto zinasaidia kujenga ubongo wake. Ziimbe hizo namba na herufi kila unapotaka kucheza naye.
5. Mtafutie Toys, zinazoendana na umri wake awe nazo nyumbani:- Toys za watoto, zinaongeza uwezo wa kufikiri. Sio lazima zikawa gali. Au mfundishe kutengeneza kama enzi zile sisi tunakuwa lakini hatukuwa na toys za kisasa kama za wakati huu. Lakini tulikuwa na mipira, midoli, magari, etc. Yote hiyo tulitengeneza na tukawa na furaha. Zaidi wekeza katika toys zitakazomsaidia kujifunza.
16. Hakikisha mtoto wako anapata muda wa kutosha wa kulala:-
17. Msaidie mtoto wako kujiwekea malengo fulani, kisha msisitize amalize:- Haijalishi ni malengo ya namna gani. Hata kama ni kuchora picha kesho, au kutengeneza mpira, au kumaliza kusoma kitabu chake cha hadithi. Msaidie ajiwekee hayo malengo na hakikisha unamfuatilia kwa kumtia moyo amalize. Itamsaidia sana baadaye katika ukuaji wake. Hatakuwa mtu wakuanza jambo na kuacha katikati.
18. Msifie JUHUDI zake:- Kumsifia mtoto kwa kile anachofanya, au tuseme kumpongeza kwa juhudi zake anazoweka kwenye jambo kutamjengea kujiona anauwezo wa kufanya jambo fulani na akafanikiwa. Ataweza kujitegemea maishani na kuweka juhudi katika kila jambo, lakini kwa kumsifia tu kuwa una akili sana kila wakati, kunaweza kumfunga na kumfanya akawa muoga wakujaribu mambo mengi kuhofia kufeli. Ila usimsifie kupita kiasi, anaweza kubweteka. Mpe sifa zinazomstahili na kumfanya aongeze juhudi.
How To Raise Smart Kid!
Wataalamu wa mambo ya watoto na Sayansi, wanashauri muda muafaka wakuwekeza kwa mtoto wako ni pale anapokuwa mdogo ndio kipindi mwafaka cha kuwekeza kile unachotaka awe pindi atakapokuwa mkubwa, kwa kuwa ubongo wake unakuwa hauna mambo mengi na ndio anakuwa. Unaweza kuwekeza chochote kile kitakachomsaidia au kuharibu maisha yake ya badaye. Yafuatayo ni mambo yatakayo kusaidia kumkuza mtoto wako awe na akili nzuri {CHILD'S INTELLECTUAL GROWTH} na mwerevu {SMART} yaliyoshauriwa na wana Sayansi na wataalamu wa Mambo Ya Watoto.
1. Anza akiwa mtoto - Kutokana na wataalamu, wanashauri uanze kuanzia yupo mchanga kabisa. Hata kama unaona haelewi, lakini anza kuwekeza kuanzia kipindi hicho. Ongea naye kwa upendo, punguza stress unapokuwa naye, Imba ukiwa naye. Muwekee michezo yakujifunza ya kitoto. Toys za namba, herufi tena zenye rangi tofauti tofauti ambazo atakuwa akiziona tokea mtoto. Rangi kali kwa mtoto zinasaidia kujenga ubongo wake. Ziimbe hizo namba na herufi kila unapotaka kucheza naye.
2. Msomee Vitabu - Anza kumsomea vitabu hata pale unapoona ni mdogo kabisa haelewi.
Hiyo inamsaidia kuanza kujifunza lugha vizuri, na itamsaidia kumjengea tabia yakupenda kusoma , na ataweza kufanya vizuri shuleni na kufanikiwa akiwa mkubwa.
Kusoma vitabu ni moja ya kitu muhimu sana kitakachomsaidia mtoto wako kuwa Smart.

3. Pata muda wa Mazungumzo na mtoto wako - Hiyo itamuongezea uwezo kujiamini kama akiona wewe kama baba au mama unaweza ukaacha mambo yako kumsikiliza yeye, pia
itamsaidia kuongea vitu vya maana au kuongea kwa ufasaha. Pata muda wa kuongea na mtoto na umsikilize. Usipende wewe ndio uwe unaongea tu pale unapokuwa naye. Muulize habari za shuleni na mwache akusimulie na muulize maswali ili kujua uwezo wake wakupambana na changamoto akiwa peke yake, kisha mshauri.

4. Pata muda na mtoto wako, Cheza naye, Mfanye ajisikie unampenda au yeye ni wa maana - Wataalamu wamechunguza na kusema watoto ambao wanajua kuwa wanapendwa, hata kukumbatiwa na wazazi/walezi wao au wanao pata muda wakucheza na wazazi wao, wanakuwa vizuri sana. Inawajengea uwezo wa kufikiri zaidi. Tafuta michezo midogo midogo itakayokufanya uwe karibu na mtoto. Hata kama huwezi kutoka naye kwenda naye sehemu, ipo michezo mnayoweza kufanya kama familia. Mnaweza kucheza cards, za aina zozote zile. mfano{Karata}, au mpira. Chochote kile. Toa muda kwa mtoto wako pia.
- Msimulie stori zako za kazini, mambo gani umepambana nayo siku hiyo, jinsi ulivyoyatatua, mambo yako ya utoto. Itawasaidia kuwajenga na watajifunza kutoka kwako kwa urahisi na kuongeza urafiki kati yenu.
5. Mtafutie Toys, zinazoendana na umri wake awe nazo nyumbani:- Toys za watoto, zinaongeza uwezo wa kufikiri. Sio lazima zikawa gali. Au mfundishe kutengeneza kama enzi zile sisi tunakuwa lakini hatukuwa na toys za kisasa kama za wakati huu. Lakini tulikuwa na mipira, midoli, magari, etc. Yote hiyo tulitengeneza na tukawa na furaha. Zaidi wekeza katika toys zitakazomsaidia kujifunza.
6. Mfanye mtoto wako apende kusoma vitabu:- Mtoto anayependa kusoma vitabu anafaida kubwa sana . Ni kitu muhimu
sana mzazi unaweza kufanya kwa mtoto wako ili awe mwerevu na mwenye akili. Kusoma kunaongeza hamu yakutaka kujua zaidi na zaidi. Hata atakapokuwa shuleni haitamsumbua kusoma vitabu kama vya Hesabu, Sayansi, Historia, kutaka kujua zaidi na zaidi. Zipo faida kubwa sana za kujisomea. Mpeleke mtoto kwenye Maktaba, mfanye awe rafiki wa vitabu.

7. Mwache mtoto wako acheze :- Kipindi mtoto wako anapocheza ndio muda anapojifunza vitu vingi. Zaidi anapocheza na wenzake inamsaidia kujifunza kutoka kwa wenzake na kukusanya mawazo tofauti tofauti yatakayomsaidia.
8. Mfundishe mtoto wako kupenda mazoezi;- Hapo najua
nipagumu kama hata mzazi mwenyewe hapendi mazoezi. Lakini mtakumbuka mashuleni enzi hizo tulikuwa tukikimbia MCHAKAMCHAKA kila siku asubuhi, na mambo mengine mengi. Haikuwa bahati mbaya. Sio kwamba mazoezi yanasaidia tu mtoto kuwa imara, bali kuwa smart pia. Mazoezi yanaongeza msukumo wa damu na kujenga seli mpya kwenye ubongo, hata na kwa wazazi pia. Mazoezi ni muhimu kwa wote. Inasaidia kwa ukuaji wa ubongo wa mtoto.

9. Kuza ubunifu wake:- Kuwa makini na kile anachobuni mtoto wako. Kisifie, kibebee bango mpaka yeye mwenyewe ajue umefurahia kwa chochote alichobuni hata kama ni kidogo kwa
kiasi gani. Ubunifu wa chochote kile, utamsaidia kumjengea tabia ya kuwa mbunifu hata katika Sanaa, Sayansi au hata ubunifu katika kila changamoto atakazokuwa akipambana nazo. Muwekee mazingira mwanao ya kuwa mbunifu. Muwekee vyombo vya mziki, jaribu kama atapenda kuimba, muwekee nyimbo mbali mbali, muwekee makaratasi, rangi, penseli uone atafanya nini na hivyo vitu.

10. Fanya mziki uwe sehemu ya maisha ya mwanao :-
Wataalamu wameonyesha kuwa nyimba zinaweza kusaidia ku boost kumbukumbu ya mtoto wako, na wanaweza kujifunza kwa urahisi kwa kupitia nyimbo. Na inaweza kupunguza msongamano wa mawazo unaoweza kuvuruga akili za mtoto wako. Wanasema ubongo wa mtoto unakuwa kwa haraka kama atajifunza kwa kutumia nyimbo. Ndio maana chekechea wanaimba sana...lol

11. Mwache mtoto wako aone ukifanya mambo mazuri;- Watoto wote wanakuwa kwa kuiga. Mtoto wako anapokuona unasoma
kitabu, au unaimba, au unaandika, au unatengeneza kitu fulani, ataiga tu na mwishowe atakuwa kama wewe. Mshirikishe mwanao kwenye vitu unavyofanya. Sio kumfukuza wakati unafanya kitu fulani. Kama akihitaji utulivi sana, fanya naye, au mwambie niangalie kimya kimya baadaye ndipo uliza maswali.

12. Mpunguzie Mwanao kuangalia Tv:- Kuangalia sana Tv kutamfanya mtoto wako ashindwe kufanya mambo mengine yatakayomfanya ashindwe kukua. Atashindwa kuwa mbunifu, au kucheza, au hata kupata muda wakusoma vitabu. PUNGUZA TV kwa Mtoto.
13. Muwekee Mtoto Wako Games za Kompyuta Zitakazo Mjenga:-
Michezo kama ya mahesabu, muziki, herufi na mengine mengi yatamsaidia mtoto wako kujifunza na pia itamwandaa na tekinologia ya baadaye. Ni rahisi sana kwa mtoto kujifunza wakati anacheza. Hatachoka mapema na anauwezo wakujifunza mambo mengi magumu, kwa muda mfupi tena kwa urahisi.
14. Mwache mtoto wako ajifunze kuchukua hatua na kushindwa:- itamjengea tabia ya kuthubutu kila wakati. Hakuna changamoto atakayokuwa akikutana nayo itamuogopesha. Mwingize kwenye mashindano na watoto wenzake, atakaposhindwa uwe upande wa kumuonyesha kushindwa ni jambo la kawaida, usimkaripie. Mwache aendeshe baiskeli, aanguke au aumie, usimwambie hapo ndio mwisho. Utamuwekea hofu katika mambo mengi sana ukubwani, yatakayomtaka kuthubutu. Mpe nafasi yakutatua matatizo yake, ili ajifunze. Kushindwa ndio mwanzo wakujifunza.
15. Wape chakula sahihi;- Mpe mtoto wako chakula
kitakachomsaidie akue vizuri na kujenga ubongo. Kama vyakula vya protini {Mayai, Samaki, Nyama} vyote vitamsaidia kujenga afya njema kwa mtoto na uwezo mzuri wakufikiri.
Kwa kuwa ni shida kumpa mtoto wako kila wakati balance diet, jiwekee utaratibu wa kuwapa watoto wako Multvitamins kila siku. Huo ni mfano wake. Lakini zipo za aina nyingi tofauti.

Mafuta ya samaki kwa kujenga ubongo wake. Vipo vidonge vizuri tu ambavyo havina shombo. Vitasaidia ukuaji wa mtoto na kuongeza uwezo wakufikiri. Mafuta ya Samaki ni mazuri sana, hata kwa watu wazima.
16. Hakikisha mtoto wako anapata muda wa kutosha wa kulala:-
Mtoto anahitaji muda wa kutosha wakupunzika kabisa. {Kulala usingizi} ili kuruhusu ukuaji wa ubongo wake. Mtoto anayepata muda wakutosha wakupumzika, inamuongezea uwezo wakufikiri.
17. Msaidie mtoto wako kujiwekea malengo fulani, kisha msisitize amalize:- Haijalishi ni malengo ya namna gani. Hata kama ni kuchora picha kesho, au kutengeneza mpira, au kumaliza kusoma kitabu chake cha hadithi. Msaidie ajiwekee hayo malengo na hakikisha unamfuatilia kwa kumtia moyo amalize. Itamsaidia sana baadaye katika ukuaji wake. Hatakuwa mtu wakuanza jambo na kuacha katikati.
18. Msifie JUHUDI zake:- Kumsifia mtoto kwa kile anachofanya, au tuseme kumpongeza kwa juhudi zake anazoweka kwenye jambo kutamjengea kujiona anauwezo wa kufanya jambo fulani na akafanikiwa. Ataweza kujitegemea maishani na kuweka juhudi katika kila jambo, lakini kwa kumsifia tu kuwa una akili sana kila wakati, kunaweza kumfunga na kumfanya akawa muoga wakujaribu mambo mengi kuhofia kufeli. Ila usimsifie kupita kiasi, anaweza kubweteka. Mpe sifa zinazomstahili na kumfanya aongeze juhudi.
19. Mjengee mtoto wako akili ya kujua kuwa TUNAJIFUNZA kila siku:- Mwonyeshe mtoto wako hakuna kikomo cha kufahamu mambo, hata wewe mwenyewe bado unajifunza. Itajenga kuwa na akili wazi yakuendelea kuwa na shauku ya kujifunza mambo au kufundishika. Na hata atakaposhindwa jambo, hataogopa atajua bado ananafasi yakujifunza zaidi.
20. Mjengee tabia yakujitegemea:- Acha kumdekeza mtoto na kumfanya awe tegemezi. Muhusishe na shuguli za nyumbani tokea
mtoto. Endapo unataka awe kiongozi mzuri baadaye, mpe majukumu yatakayomfanya afikirie yeye mwenyewe na kuchukua hatua kama kiongozi. Acha kumzungushia wasaidizi kila mahali. Msichana wa kazi anamfanyia kila kitu, hata hajui wakati gani ananjaa na
anatakiwa kunyanyuka kwenda jikoni kuchukua chakula, au kusaidia kutengenezwa kwa chakula hicho na kupangwa mezani, kwa kuwa dada wa kazi anamfanyia kila kitu au wewe mwenyewe unafanya kila kitu kwa kumuhurumia, eti anachoka shuleni. Mwache ajue jinsi ya ku manage muda wake. Aamke, aandae kifungua kinywa, asafishe chumba chake, nguo zake ziwe sehemu sahihi kama chafu basi aweke yeye mwenyewe sehemu ya nguo chafu, hata kama hatafua basi zikishafuliwa ajifunze kujikunjia nguo zake, na bado awahi shule n.k Akiwa na tabia hiyo tokea mdogo, hatashindwa kujipanga ukubwani.

21. Mzawadie mtoto wako:- Sio vibaya kumpa ahadi mtoto wako kwa matokeo fulani unayoyatarajia kutoka kwake. Itamsaidia kujituma zaidi na zaidi ili kupata hiyo zawadi unayohisi itamsaidia mtoto wako.
22. Punguza kum {MICROMANAGE} wakati wote:- Acha kuwa nyuma ya mgongo wake na kumwambia kitu gani afanye na kumkosoa kila wakati. Mwache awe mbunifu yeye mwenyewe na wewe uwepo kuunga mkono kile anachotaka kufanya yeye sio unachotaka wewe afanye kila wakati. Itampa uwezo wakufikiri hata akiwa peke yake kwenye mitihani shuleni au maishani.
Mithali 22:6 Mfundishe mtoto namna ya kuishi vizuri, naye hatasahau njia hio hata Uzeeni.

0 comments: