Raising Strong Deneration

JINSI YA KUTAMBUA KIPAJI CHA MTOTO NA KUKIKUZA.

Thursday, May 04, 2017 naomimwakanyamale 0 Comments

Pale mtoto anapojua anaweza kufanya kitu fulani, tena vizuri sana, na mzazi akamtia moyo katika hicho kipawa chake, kinamjegea kujiamini sana. Tena endapo ukafanikiwa kugundua kipaji cha mwanao mapema, na ukawekeza katika kipaji hicho tokea mtoto, unarahisisha maisha ya mtoto wako. 
Ndio maana utagundua wapo watoto wadogo tu, lakini ni Mamilionea. Hiyo si kwa bahati mbaya, ni kwa kuwa yupo mtu fulani, aligundua kipaji hicho na kuamua kuwekeza kwenye maisha ya mtoto huyo. Endapo ukaweka mazingira mazuri kwa mwanao, na wewe kama mzazi ukamuwekea Self Esteem, He/she will never be the same.


Wazazi mnaweza kugundua kipaji cha mtoto wenu kwa kumpa nafasi ya kufanya vitu tofauti tofauti huku mkimsaidia kwa kumpa ushirikiano. Hizi ni hatua unazoweza kuchukua:-

1. Mzazi/Mlezi ndio uwe mtu wa kwanza kumjenga mtoto na kumwambia anaweza kufanikiwa kwa chochote atakachoweka bidii
kukifanya. Toa maneno ya kumjenga mwanao. Mpe mifano ya watu waliofanikiwa kwa kuweka bidii, na mwambie hata yeye anauwezo wa kufanya chochote apendacho na akafanikiwa. Msifie vile alivyo na akili timamu, mweleze kipo kitu kikubwa sana ndani yake ambacho Mungu amemuwekea, na endapo atakitumia vizuri, atafanikiwa kama au zaidi ya fulani na fulani. Lazima ajue yeye ni watofauti. Tuache kutukana watoto, matusi yanayo haribu ujasiri wao.

2. Jihusishe na maisha ya mtoto wako. Lazima kuweka mazingira yakuzungumza na mtoto wako
mara kwa mara. Muulize siku yake ilikuaje. Kitu gani alifurahia kwa siku hiyo na kitu gani hakufurahia huku mkicheza. Ondoa sura ya kazi wakati ukizungumza naye, tulia, muonyeshe unamsikiliza. Soma naye au tafuta kitu chochote mnachoweza kufanya naye pamoja ili kufanya akuone kama rafiki. Hata kama ni mama anapika, mpe kazi ndogo hata kumenya kitu hapo jikoni huku mkizungumza.

3.Kuwa makini na kile mtoto wako anapenda kufanya. Kile anachofanya bila kusukumwa au kukumbushwa. Kisha msaidie kuongeza ujuzi au mpeleke kwa watu wanaoweza kumuendeleza. eg. Kama anatoroka nyumbani kwenda kucheza mpira, sio kuanza kumchapa. Tafuta jinsi utakavyoweza kujihusisha na huo mchezo, na kumkuza zaidi. Mwambie ungependa kwenda naye ukaone jinsi anavyocheza na wenzake. Nenda ukamshangilie mtoto wako. Hata kama ni kwenye mazingira ambayo siyo yakuvutia, nenda naye ukamtie moyo. Utaona hata uchezaji wake utabadilika, na ataongeza bidii.


4. Mpeleke mtoto/watoto wako kutembelea sehemu wanazoweza
kujifunza. Kama Maktaba, kuangalia sinema zitakazo wafanya wajifunze kitu, kwenye museums, maduka ya vitabu na wewe ukionekana upo pale kimawazo. Sio uko pale wakati macho yako yapo kwenye simu wakati wako.



5. Tafuta sehemu ambazo mtoto wako anaweza kujitolea katika jamii. Mfundishe na mtie moyo
wa kufanya kazi za kujitolea. Mfano:- Makanisa mengi yanakuwa na projects nyingi tu. i.e kutembelea wagonjwa, kuona yatima, kwenda magerezani, kusafisha
sehemu mbalimbali ikiwemo kanisani kwenyewe au kwenye mazingira, kusaidia watoto wenzake pale kanisani n.k






6. Fanya Homework na mtoto wako. Saidiana na walimu wa mtoto wako kumlea mtoto. Jua style
yake ya usomaji, weakness na strength za mwanao kwa kupitia walimu wake wanae shinda naye shuleni kwa muda mrefu tena wewe ukiwa haupo. Wafanye walimu wako wawe rafiki zako.





7. Mjengee tabia mtoto wako ya kuangalia watu waliofanikiwa. Kama ni kwenye TV mwambie aangalie jinsi mheshimiwa fulani anavyoongea kwa kujiamini, jinsi anavyojua kupanga maneno kwa
ufasaha, jinsi anavyosimama mbele za watu na kuzungumza kwa kujiamini. Kisha mpe zoezi hilo mtoto wako. Mpe hata dakika tano mwambie aandae hotuba fulani asimame mbele ya familia nzima ajaribu kuongea au kama ni mwimbaji, basi aimbe mbele yenu huku mkimtia moyo.




8. Tafuta mtu kwenye familia au jamii inayowazunguka, ambaye unajua atakuwa mfano
mzuri kwa mtoto wako, ambaye anaweza kumwongoza vyema na mtoto wako akamwangalia kama role model wake. Mkabidhi huyo mtu amfuatilie kwa karibu, kwa maombi na kuzungumza naye mara kwa mara, ili msaidiane naye kwenye malezi. 

Mfano:- Nakumbuka enzi hizo za kina mama wa ubatizo ndio walikuwa karibu sana na sisi


WATOTO NI DHAMANA MUNGU AMETUPA, IPO SIKU TUTAULIZWA. KAMA SI NA JAMII, BASI NA MUNGU. TUWEKEZE KWA WATOTO WETU.
MUNGU AWABARIKI.

0 comments: