Lifestyles
LIKIZO ACTIVITIES.
IDEAS YA VITU VYAKUFANYA WATOTO
WAWAPO LIKIZO.
Kipindi hichi cha likizo ni muhimu kwa mtoto kupumzisha akili baada ya masomo ya mwaka mzima, lakini mzazi pia anaweza kutumia muda huo vizuri kuwekeza vitu vya msingi kwenye maisha ya mtoto wake. Yapo mambo mengi sana watoto wanaweza kufanya wawapo likizo tena yasiyo hitaji pesa nyingi. Kama:-
- Weka mahusiano mazuri, tena ya karibu kati ya mtoto wako na Mungu:- Hapa inatakikana juhudi za makusudi kutoka kwa wazazi. Hakuna umri sahihi wakumsogeza mtoto karibu na Mungu. Kuanzia umri anapoanza kuweza kutambua watu na vitu, lazima mtoto amfahamu Mungu wake, hilo ndilo la KWANZA na MUHIMU. Mfundishe kusoma vitabu vya Mungu vyenye hadithi za kweli za Mungu. Itamsaidia kufungua ufahamu wake. Utaona utofauti wa tabia yake awapo nyumbani na shuleni matokeo yake lazima yatabadilika tu. Mimi ni shahidi katika hilo. Ipo nguvu ya mtoto kufahamu neno la Mungu na kuwa na hofu na Mungu kuliko hofu ya wewe mzazi. Mwache yeye mwenyewe asome mambo ya Mungu, amfahamu Mungu na kama ni mdogo, pata muda wakumsimulia mambo ya Mungu.
- Tembeleni Maktaba/Library.
- Tembeleeni Sehemu za Kihistoria
- Nunua Cards:- Hapo unaweza kununua KADI za namna tofauti tofauti kutokana na kile unachotaka wajifunze. Kadi zinaweza kuwafanya wakajua kitu fulani kwa njia rahisi na haraka huku wakifurahia. Mfano:- Ukitaka wajifunze majina ya wafuasi wa Yesu, au Nchi zote ulimwenguni na Miji yao Mikuu, au Ukitaka wajifunze aina ya WANYAMA kwa lugha fulani, basi unawanunulia KADI za namna hiyo WACHEZEE NA WAKATI MWINGINE PATA MUDA WAKUCHEZA nao. KINGINE kizuri ambacho huwa natumia kwenye familia yangu ni KARATA. Ni mchezo tunapendelea sana kucheza nyumbani kwetu kama familia. Mara nyingi tunacheza WOTE Inafurahisha na kuwaweka pamoja, lakini zaidi inamjengea mtoto uwezo wa kufikiri kwa haraka na kufanya maamuzi AKIWA YEYE PEKE YAKE. Pia inamsaidia kupambana na changamoto na kumsukuma kufanya juhudi ili kuwa mshindi. Jaribisha hiyo.
- Wape dakika 20 kila siku kusoma kitabu:- Kitabu chochote atakachochagua yeye.
- Punguza muda wakuangalia tv kwa siku ili wajifunze kazi za nyumbani na waweze kufikiria na kuweza kufanya kitu kingine.
- Wanunulie Karatasi, Rangi, Penseli na Mkasi wa umri wao. Wape muda wakuwa wabunifu na hivyo vitu wakati na wewe ukiendelea na kazi zako pembeni yao.
- Watengenezee mazingira ya kukutana na wenzao na kucheza pamoja.
- Fanya Talent Show ya familia. Wape siku ambayo watajiandaa na kuwaambia siku hiyo nyinyi kama wazazi, mtakaa chini mkiwaangalia kila mmoja akionyesha kipaji chake.
- Panga siku ya kwenda kutembelea ndugu, jamaa na marafiki huku ukiwashirikisha kwenye ununuzi wa zawadi.
- Waingize kwenye shuguli za kujitolea/Volunteer, iwe kwa jamii kusafisha mazingira, kuwaona wagonjwa, kutembelea yatima, kusaidia wasiojiweza, kusafisha kanisani na mengine mengi.
- Vacation ya familia tu. Hapa kama upo uwezo, ni vizuri angalau mara moja kwa mwaka, nyinyi tu kama familia mkatoka kwenda sehemu kutembea, wazazi wakiwa wameacha kazi zao na kupata muda na watoto wao tu. Inaweza isichukue muda mrefu, hata siku mbili tu, mkawa mbali na nyumbani ni muhimu sana.
- Fanyeni mashindano yeyote yale kama familia, au familia mbili. Mfano kushindana kucheza mpira wa miguu. Hapo haijalishi jinsia.
- Karibisha familia yenye watoto kama wako kwa chakula nyumbani kwako na washirikishe watoto kuandaa mlo huo.
- Weka mazingira ya kupata angalau mlo mmoja na watoto wako, kila siku angalau ili uwasikilize kujua siku yao na wao iliendaje.
- Panga siku ambayo utamkaribisha rafiki yako atakayeweza kuzungumza nao akiwafundisha kitu chochote kitakachowajenga. Ni vizuri wakisikia pia kwa mtu mwingine mbali na nyinyi wazazi.
- Pangeni siku angalau moja kwa juma mtakayo kaa chini nyinyi wote kama familia muangalie filamu
- Fanyeni Camp hata sebleni kwenu, mkiigiza mpo Camp labda msituni, mtoni popote pale.
- Kuza vipaji vyao. Kama ni mwimbaji, au mpiga kinanda, mcheza mpira, chochote ambacho umegundua mwanao anapenda kufanya bila kusukumwa, huo ndio muda mzuri wakumtafutia mtu au shule ya kukuza kipaji chake
- Wanunulie puzzles wacheze na wakati mwingine Shiriki.
- Watengeneze kadi wao wenyewe kuwapelekea ndugu, jamaa na rafiki.
- Wacheze Legos.
- Wasomee kitabu kizuri cha hadithi, wafanye wakae chini wakusikilize
- Wajifunze kutengeneza tiara/ kites na kuchezea nje
- Wapeleke Park wakacheze
- Wanunulie Kamba ya kuchezea, waruke Kamba. “Jump Rope” Ni mchezo mzuri sana kwa watoto.
- Mkaangalie Movie. KWENYE MOVIE THEATER.
- Wapeleke kwenye Ice cream
- Swimming
- Washirikishe kwenye usafi wa nyumba;- Wasafishe milango, madirisha, ukuta, kumwagia maua, zaidi vyumba vyao.
- Wasaidie wapike wao wenyewe angalau kitu kimoja...mfano cookies, bake cake
- Tembeeni jioni baada ya chakula, kama familia {Evening Walk}. Waruhusu waongee na kucheka huku mkizunguka tu kwa miguu.
- Watoe mara moja moja kuwapeleka watoto wako kwenye Migahawa mizuri kwa chakula. Angalau na wao waonje ladha ya kula kwa kisu na uma😋😋😋.
NA MENGINE MENGIII UNAWEZA KUONGEZA HAPO CHINI.
KARIBU.

0 comments: