Nilipotea! - SEHEMU YA 8.
Maisha ya Tunda Mtaani.
T |
unda akiwa pembeni ya kituo hicho cha Mwenge, kwenye moja
ya sehemu wanayouza
chakula, akisubiria chakula chake kiletwe, akiwa amejiinamia,
akasikia wale wahudumu wakisemezana kama
walio paniki na kuingiwa na hofu. “Wewe
ndio alisema upeleke.” “Hakutaja jina bwana! Alisema mmoja wenu alete.” “Sasa
mmoja wenu ni nani kama sio wewe ambaye unashika pesa za mama
hapa!” Mwenzie akauliza kwa kumshangaa.
“Sasa wewe si ndiye uliyepokea simu!?”
“Kwa hiyo!?” Tunda akawasikia wakiendelea kubishana.
“Sasa anakuja mzee mwenyewe! Nyinyi
endeleeni kubishana hivyo hivyo!” Msichana aliyekuwa akigawa vinywaji na kusafisha meza, alisikika kuingilia
mazungumzo ya hao vijana wawili. “Ni
nini kigumu huwa hamuelewi nyinyi!” Ilisikika
sauti upande wa kuingilia. Ikizungumza kwa ukali kidogo. Tunda akanyanyua
kichwa na kumtizama huyo anayegomba na kuogopwa. Maana kulizuka ukimya kwa wale wahudumu wote. Tunda akajua ndiye huyo Mzee. Alisogea mpaka karibu
kabisa na pale alipokaa Tunda, akavuta kiti pembeni yake akakaa.
Hakuwa Mzee kama walivyomsema. Ila alikuwa mtu mzima. Kijana
mkamilifu tu. Alionekana ni kama anasogelea miaka ya 50, lakini bado hajafika huko. Akajua huo uzee ni wa
pesa. Mmoja wa wale wahuhudumu akamsogelea. “Samahani sana. Nilikuwa nimletee mama. Lakini tumekuwa na wateja
wengi sana. Nisingeweza kumuachia Udi na Sande peke yao. Nilitaka wateja wapungue,
ndio nilete.” Tunda akamgeukia kwa kujiiba yule baba aliyekuwa anaombwa
msamaha na kupewa maelezo kwa heshima zote, akaonekana kuelewa kidogo. Yule
kijana akaendelea kujieleza. Katika
mazungumzo yao Tunda akajua mkewe ndio mmiliki wa ile biashara pale,
yeye amepita tu kuchukua pesa baada ya wale wafanyakazi
wa pale, kushindwa kumpelekea pesa mkewe kwenye biashara yake nyingine.
Tunda akaendelea
kusikiliza kwa makini. Akavutiwa na muonekano wa yule baba. Alionekana
anajielewa. Jua kali vile, lakini bado
alionekana msafi, halafu kwa umri ule kuwa amevaa safi
vile mchana huo, akajua ameacha gari tu mahali na pesa ipo. Akavutiwa
kumsikiliza zaidi. Akili zake zikahamia hapo kwenye mazungumzo yake na huyo muhudumu wa hapo. Akasikia na yeye anatafuta mtu
mwingine atakayeweza kufanya kazi kwenye baa yake ya Sinza. Wazo lilimjia Tunda,
aombe kazi. “Lakini akinipa
kazi, nitaishi wapi? Sina hata pakulala usiku wa leo!” Tunda akajiuliza
mawazoni mwake.
Wazo la pili la harakaharaka likamjia,
la kumtongoza yule baba. Aliona anakabidhiwa
pesa nyingi tu. “Sasa kama hiyo pesa yote ni ya mkewe, yeye
atakuwa akiingiza kiasi gani!” Tunda akawaza na kuzidi kuvutiwa na
kuafikiana na wazo la kumtongoza na si kuomba kazi. Akajifanya kama
hakuwa amesikia chochote. Akamgeukia
mara baada ya yule muhudumu kuondoka. “Mbona hunywi kitu chochote?” Tunda akamuuliza kwa sauti ya kujali. Yule baba
akamgeukia Tunda kama asiye na ukakika kuwa
anamsemesha yeye. Akakutana na macho matulivu ya Tunda yakimtizama
kumuashiria anazungumza naye.
“Jua ni
kali sana. Kunywa hata maji, mimi nitakulipia.” Tunda
akaendelea kuzungumza naye kwa sauti
tulivu ya ukarimu. Akaanza kumvutia. Akatulia kidogo kama aliyepigwa na butwaa na
yale macho ya Tunda. Tunda akajua
tayari. Akamtolea tabasamu kama kumshtua. Yule baba
akagutuka kidogo. “Asante binti. Nimetingwa na mambo mengi, nashindwa
hata kujifikiria! Nashika hiki, hiki kinaachia. Ukifanikisha hapa, pale
panaachia! Unajikuta unahitajika kila mahali!” Akalalamika. “Pole sana. Lakini afya yako ni muhimu.” Yule baba
ikabidi kumtizama Tunda kwa makini.
Kwa haraka ili kumpumbaza zaidi akaunganisha.
“Kunywa kwanza maji, halafu ndio uniambie
kinacho kupeleka kasi hivyo!” Tunda aliendelea kuzungumza kwa sauti tulivu yakujali na kumuwekea
yale macho yake mama yake aliyokuwa akiyaita ya paka na yamezubaa. Akamuona yule baba anasogeza kiti upande wake,
halafu kama aliyejishtukia akakirudisha palepale kilipokuwa amekaa mwanzoni. Tunda akatabasamu na kuinama.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Hiyo ndio
ikawa sifa yake na kitu kinachomtambulisha hapo shuleni kwao. Ukisikia jina la Tunda tu likitajwa hapo shuleni kwao, basi
sifa ya macho inafuata. Hilo likamshangaza sana Tunda aliyekuwa akijua anamacho
mabaya sana. Likamjengea ujasiri. Ndipo sasa
akaanza kujifunza kuyalia pozi na kutengeneza sauti yake kuwa ya chini na taratibu. Na kwa kuwa hakuwa akisikilizwa
nyumbani na wala hachangii chochote darasani, haikuchukua muda kuifanya sauti yake kuwa atakavyo Tunda.
Na alikuwa akiamua kuyatumia macho hayo
na sauti yake ya utulivu, kukulainisha, ilihitajika mwanaume kwelikweli kutoka. Ni moja ya vitu vilivyokuwa
vikimchanganya hata baba Tom. Hakuacha
kusifia na macho yake. Basi Tunda alianza kutumia kwa makusudi kama silaha yakuchanganya vijana japo hakuwahi
kuwakubali kwa kumuhofia baba
Tom. Basi kabla hajasimama na mtu kutizama kaumbile kake,
Tunda alianza kwa kutumia macho yake na
sauti.
Mwalimu
aliyekuwa akimfundisha tuition ya Kifaransa ndio alikuwa akimuona jinsi
anavyopagawa. Alipogundua kuwa Tunda ni mkimya.
Wanaweza kuanza kusoma mwanzo mpaka mwisho na hajachangia chochote,
akatengeneza mazingira ya kumfundisha
peke yake. Akazungumza na baba yake, ili kumsaidia
zaidi. Akamwambia baba Tom kuwa Tunda ni wale wanafunzi wanao hitaji
msaada wa karibu, ni ngumu kujifunza na watu wengi. Na kwa kuwa baba Tom
alijua Tunda anapenda Kifaransa, ili kumfurahisha Tunda, akakubali tution ya yeye peke yake na huyo mwalimu tu. Hakuishia
hapo. Walipopata hiyo nafasi yakujikuta wawili tu, akaanza kutengeneza
mazingira yakumzoea zaidi Tunda.
Wakati
mwingine alianzisha mazungumzo nje kabisa na
kile anachomfundisha. Tena katikati ya kumfundisha, ili tu azungumze na kumtizama. Tunda aliligundua
hilo, na alishavutiwa naye kwani alikuwa kijana zaidi ya baba Tom, mzuri, mcheshi, lakini asingethubutu
kumkubali kwa kumuogopa baba Tom, japo
alishakaribia kutaka kumbusu Tunda. Alishamsogelea mpaka kabisa midomoni,
Tunda akasimama kwa haraka akiwa na yeye ameshashawishika kabisa. Alimuomba msamaha Tunda na kumsihi asimwambie baba yake ambaye
walikuwa wakifahamiana. Tunda akamwambia
asijali, hata yeye angependa kuwa naye, lakini mazingira hayakuwa
yakiruhusu.
Akiwa
kidato hicho hicho cha pili wakajenga
urafiki wakaribu sana. Wakisifiana kwa hili au lile, lakini yeye zaidi alisifia
macho na sauti ya Tunda na kuishia wakicheka
mambo ya kawaida na kumtaka Tunda awe anaongea chochote. Ndipo Tunda alipojenga
ujasiri wakutengeneza sentensi za Kifaransa. Japo kwa kukosea, lakini akawa
anafurahia na kumrekebisha. Ndio chanzo cha Tunda kufahamu lugha hiyo kwa kiasi.
Ni hiyo tution pekee na ya kingereza ambayo hakuruhusu baba Tom aingilie.
Hakuwa akikosa hata mara moja ili tu
akakutane na huyo mwalimu aliyekuwa
kijana, akimsifia sana macho na
sauti yake.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
“Kula basi kidogo.” “Acha nichukue basi hata soda,
tuondoke zetu.” Tunda akajua tayari ameshamkamata. “Na mimi nasubiria chakula
changu.” “Basi utanikuta nikikusubiria upande wa kushoto wa hili banda. Akamuelekeza aina ya gari yake na wapi amkute. “Sawa.”
Wakakubaliana. Akachukua soda yake,
akawaaga wale wahudumu wa mkewe, akaondoka.
Kweli,
Tunda akafungiwa chakula chake, akalipia na kuondoka kwa haraka kumfuata yule baba. Kama aliyekuwa anahofia
Tunda atamkimbia, alimkuta akimsubiria pembeni
tu hata hakufika kwenye gari. Tunda akacheka moyoni. Wakaongozana
mpaka kwenye gari yake.
Walipofika kwenye gari akamuona anababaika
hajui aanzie wapi kuomba penzi. Gafla akapoteza dira, hajui pakuanzia. Akabaki akichekacheka na kuumauma maneno hata gari
likamshinda kuwasha. Tunda akaamua kumsaidia. “Uliniahidi utaniambia kinachokuchanganya
na kukufanya ushindwe kujifikiria wakati
wewe bado damu inachemka kabisa.” Tunda akadai kwa kubembeleza. Akacheka kufurahia
kusikia damu inachemka. “Naruhusiwa kukutengeneza
vizuri?” Tunda akauliza tena kabla ya kujibiwa swali la
kwanza, tena kwa upendo huku akimtizama.
“Wapi?” Akauliza kwa wasiwasi huku akijiangalia wapi hajakaa
sawa. Alikuwa amevaa tisheti ya rangi ya bluu. Akajitazama hakuona tatizo. Akajitizama
tena na tena hakuona tatizo. Tunda
alipomuona anazidi kubabaika, akarusha
swali la tatu kabla hata hajajibiwa la kwanza na la pili. “Kwani kuna mipaka?” “Hapana, ruksa kabisa. Hamna
mipaka.” Gafla yeye akasikika mdogo mbele ya Tunda.
Tunda akatabasamu huku akimtizama. “Nitengeneze tu.” Akamsisitizia
Tunda akibembeleza.
Tunda akanyoosha mkono wake moja kwa moja kwenye zipu ya
suruali yake. Akaanza kumchanganya mpaka akaamua wakatafute chumba
kwenye nyumba ya kulala wageni. Tunda alifurahia
sana moyoni. Akaondoa gari pale alipokuwa ameegesha
nyuma kabisa ya kituo hicho cha Mwenge,
karibu kidogo na hosteli za wanachuo njia ya kwenda Sinza. Tunda akaanza
kula. “Tunakwenda wapi sasa?” Tunda
akauliza kwa utulivu. “Sehemu ambayo
hatutasumbuliwa.” Tunda akacheka taratibu, na kumuwekea chips yai kidogo mdomoni. “Wewe ni mkarimu!” Akamsifia Tunda, Tunda akacheka tu. “Lakini usinipe
tena. Wewe kula tu. Mimi nilishakula.” “Unauhakika?” “Kabisa.” “Sawa.” “Nashukuru
lakini.” Akamgeukia na tabasamu usoni.
Tunda
akaendelea kula huku yeye akiendesha. Alimpeleka kwenye kijihoteli kizuri, kilikuwa
kimejificha mitaa ya Mikocheni B. Mwanzoni
Tunda alidhania ni nyumba ya mtu. Kwani ilikuwa katikati na makazi ya
watu. Lakini ilizungukwa na majumba ya uhakika
yenye mageti yao marefu. Hakuona hata mtu
akizurula hapo mtaani. Yule baba akaingiza gari yake mpaka ndani kabisa.
Akashuka yeye, wakati Tunda akimsubiria ndani ya gari. “Huyu atakuwa
mwizi mzoefu!” Tunda akawaza akiwa peke yake pale kwenye gari.
Baada ya muda akarudi. “Nimeshapata chumba.
Twende.” Tunda akakusanya ile mifuko aliyokuwa
amewekewa chakula, akashuka. Akafunga gari yake kwa rimoti ya mkononi,
akaongoza njia, Tunda akimfuata nyuma. Kwa
kuwa alishakula, walipoingia tu
chumbani
akameza dawa ya maumivu kwa ajili ya lile bega lililokuwa likimpa maumivu
kiasi. Kisha akaingia kazini. Kwa muda mfupi
aliokuwepo naye pale kitandani, akijituma kwa juhudi zote kumpa ya
ukweli, akihakikisha anamchanganya vyakutosha ili kumfanya asitamani kuondoka pale na atamani kurudi tena.
“Nitakuona lini tena?” Akamuuliza
kama anayemuomba siku ile isiwe mwisho. “Umenichanganya mpaka nimesahau kukuuliza jina!” Tunda akatoa tabasamu la
ushindi. “Naitwa Ani.” “Nitakuonaje Ani?” “Wameniibia simu. Tena ni
jana tu wakati nazunguka mitaani na madalali nikitafuta chumba!” Tunda
akajilalamisha. “Lazima tutafute simu nyingine. Lakini tukiachana hapa,
nitakuonaje tena?” Huduma aliyotoka kupewa hapo akazidi kumtamani Tunda na
kuona anamuhitaji zaidi.
Tunda akajua ameshamkamata. “Wewe
tu.” Tunda akajibu huku akijisogeza tena. “Mimi nataka nikuone tena Ani. Tafadhali sana.” “Ningekuwa na simu, na sehemu
yakueleweka yakuishi, ingekuwa rahisi kupanga mipango yakueleweka.
Lakini hata sijui kama nitafukuzwa pale au
la! Yule Mzee ananisumbua! Sina raha. Halafu nahisi ni tamaa tu. Anao
wake wawili, na bado ananitaka na mimi!
Ananilazimisha niwe mke mdogo.” “Haiwezekani!” “Kweli. Halafu naogopa, wakati mwingine anaweza
kuja mpaka pale kwenye nyumba yake akijua wapangaji wengine hawapo. Akinibaka!” Tunda akajilalamisha
huku akimchezea yule baba taratibu.
“Aisee hapo ni pakukimbia kabisa.” “Ndio
nilikuwa nafikiria labda nirudi tu kwa bibi kijijini.” “Hapana.” Yule baba
akashtuka sana. “Sasa niambie nafanyaje hapa
mjini? Hata simu tu ya mawasiliano sina!” Tunda akakaa akiwa uchi kabisa. “Mbona simu
sio tatizo kabisa! Naweza kwenda kukuchukulia
hata sasa hivi! Na kwakuwa hapa panaonekana ni patulivu, unaweza ukapumzika tu hapa kwa siku chache mpaka tutakapopata
chumba kizuri utakachopenda. Huwezi jua ni kwa nini tumekutana leo! Tafadhali usiondoke kwa haraka. Tutafikiria pamoja
chakufanya.” Kweli? Maana usije ondoka hapa ndio ukawa umeniacha mimi moja kwa moja!”
“Sithubutu. Mimi nakuhofia wewe. Usije nikimbia Ani, utakuwa umenionjesha tu
halafu..” Tunda akamkalia tena yule baba
akiwa amejilaza pale kwenye kitanda ameegemea mto, akamuona anababaika
tena. Akashindwa hata kutoa neno linaloeleweka.
Tunda
alikuwa akimcheka sana moyoni jinsi alivyokuwa anaweweseka, alihisi lazima ni mshamba au hakuwahi kukutana na wakumpagawisha kwa
kiasi kile. “Ila hapa amewezaje kupata chumba kwa urahisi hivi au tu amepajuaje!?
Maana hapa jinsi
Palivyojificha!
Huwezi kukamatwa wizi labda mtu awe anakufuatilia.” Tunda aliendelea kuwaza wakati akimzungusha
kwa mara nyingine tena pale kitandani kwa hili
na lile muda huo wa mchana, jua kali nje na ilikuwa siku
ya kazi. Tunda aliporidhika kuwa amemuweka sawa
na lazima atarudi tu, ndipo alipomuachia. Alimuachia pesa nyingi sana, huku
akimbembeleza asimtoroke.
“Tafadhali
nikukute Ani.” “Sasa niende wapi
na wakati nimekwambia hali
ya ninapoishi!? Nasubiri tufikirie kwa pamoja kitu chakufanya. Wawili ni
wawili tu.” “Hapo umenena. Na mimi huko ninapokwenda,
nitaanza kukuulizia sehemu. Lakini nataka iwe sehemu tulivu ili tusiwe
tunasumbuliwa.” “Na sasa sio unitafutie sehemu za mbali, halafu unaniacha nyumbani peke yangu, unashindwa kuja kunitembelea!”
Hilo likazidi
kumchanganya yule baba. “Yaani nitamiliki
mimi mwenyewe!” Akauma meno
huku akimtizama Tunda asiamini kama ndio hana mpango wakumuwekea mipaka! Kwamba
na yeye anataka kuwa naye! Akazidi kuona amebahatika siku hiyo kumpata Tunda.
“Siwezi
kukuacha peke yako Ani.” Tunda akacheka kwa deko. “Twende ukaoge ndio utoke. Usitoke hivyo.” “Yaani unanisindikiza!?” Hakuamini. “Sasa nani
anakusugua huko bafuni. Nataka nikuoshe vizuri, sio ufike mbele za watu unanuka.” Akazidi kumchanganya. Tunda akatoka hapo akielekea bafuni, bila hata shuka. Akamsikia anaruka pale kitandani anamfuata
kwa haraka. Baada ya fujo zakutosha za Tunda za huko bafuni nako, Tunda akamfukuza.
“Ulisema
unatakiwa kwenye baa yako ya Sinza. Nenda kazini,
mimi utanikuta nakusubiria.” Akachekacheka
kama mjinga mbele ya Tunda.” “Naamini nikirudi tutapata muda mzuri zaidi.” “Uwahi sasa! Sitaki kukuingiza
kwenye matatizo huko nyumbani.” Hilo nalo akalifurahia kuwa anajali na kuheshimu maisha yake. Wakatoka hapo bafuni, akaanza kumfuta maji mgongoji
huku wamekaa kitandani. “Ningekuwa na mafuta yangu hapa, ningekupaka. Lakini sina.” “Basi itakuongezea
pesa zaidi ukanunue. Lakini yangu usinunue
yenye harufu kali.” Tunda
akacheka na kumbusu mgongoni. “Siwezi bebi. Sitaki kukuingiza matatizoni.”
Gafla anaitwa bebi! Hilo nalo akapenda.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Alimuacha
Tunda pale chumbani yeye akatoka kwa
kufukuzwa na Tunda. Alishataka kuahirisha, abaki naye, Tunda akamkatalia.
Alibaki pale kwenye kile chumba kizuri, kisafi,
akifurahia kutengeneza pesa ya haraka haraka
kwa kiasi kile. Maana yule baba alijitutumua na kumuachia pesa karibia yote aliyopewa
pale kwenye ile biashara ya mkewe, Mwenge. Tunda alizihesabu zile pesa
huku akicheka. “Na simu amesema
ataniletea!” Tunda akawaza huku akizirusha zile pesa juu. Zikasambaa chumba chote na pale
kitandani. Akaendelea kucheka huku akigaragara
na zile pesa pale kitandani. “Nimelala masikini, nikiteswa na kipigo juu, nimeamka tajiri kilaini!” Tunda hakuamini.
Akaamua
ile ndio iwe biashara yake. Na akakusudia yule baba ndio atakuwa mteja wake wa kwanza. Angalau amtumie hapo
mwanzo, wakati akijipanga zaidi. “Nitambana
huyu, mpaka asijielewe. Atamwaga pesa hapa bila kujijua.” Tunda
aliendelea kumpigia mahesabu. Na kwa kuwa alionekana
nimtoaji, akajua mambo yake yamekuwa sawa.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Dada aliyemkuta
pale saluni alikuwa mcheshi sana. Tunda akaomba amtengeneze vizuri na
kumwitia mtu wakumtengeneza kucha akiwa anamuhudumia. Bila kuchelewa kijana wa kucha akaingia hapo. Baada ya
kuoshwa vizuri nywele zake ambazo hazikuwa na dawa, wakati anatengenezwa
kichwani, yule kijana wa kucha akaanza kumuosha
miguu. Kazi mbili kwa wakati mmoja zikaanza. Urembo wa nywele na kucha. Alimshonea
wiving fupi. Akaikata kwa mtindo uliompendeza sana Tunda. Nakufanya uso wake wa
mchongoko kuonekana vyema zaidi. Usingeweza kumtambua Tunda huyu na yule aliyekuwa amelazwa hospitalini
masaa machache yaliyopita au yule aliyekuwa mtumwa nyumbani kwa shangazi yake.
Kijana wa kucha naye akawa amemtengeneza vizuri kucha za miguuni, akambandika kucha nzuri kwenye vidole vya mikononi. Tunda alitoka hapo akiwa wa tofauti sana. Akaingia sasa madukani, akiwa nadhifu. Akajinunulia mafuta mazuri,{Lotion} yakunukia, kisha akamnunulia na yule baba mafuta ya maji ya kawaida tu. Akahakikisha pia yanafaa kwa masaji. Akajinunulia chupi nzuri za kisichana, nguo chache za kulalia, nzuri na za kuvutia. Akaingia kwenye maduka ya nguo. Akajinunulia vigauni kadhaa. Kisha Akamnunulia mke wa yule baba chocolate nzuri zenye muundo wa kopa. Akacheka kwanza yeye mwenyewe. Akatoka hapo akajinunulia vitu vidogo vidogo vya kujitengeneza. Aliporidhika na vitu alivyohitaji, akachukua tena taksii akarudi pale kwenye ile nyumba ya kulala wageni, na kujitupa kitandani mpaka usiku wa saa mbili aliposikia tena mlango unagongwa.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Tunda
alikuwa amepumzika vya kutosha kuifanya kazi
yake vizuri. Akasimama kufungua mlango. Akabaki ameduaa akimshangaa Tunda. “Nimepotea
mlango nini!?” Tunda akacheka na kurudi
ndani na yeye akafuata nyuma na mifuko,
Tunda alijua mmoja wapo unachakula maana harufu ya kuku wa kuchoma
ilienea chumba kizima. “Nimekuletea na chakula.”
“Asante na karibu ukae.” Akakaa akionekana wazi bado anamshangaa Tunda.
Tunda akacheka taratibu akimtizama. “Mbona umebadilika gafla hivyo!?” “Nimependeza
au nimetisha?” Tunda akamuuliza na tabasamu usoni, akijua wazi amependeza.
“Umependeza
sana. Unazidi kunichanganya Ani!” Kabla hajatoa alicholeta Tunda akamuwahi yeye. “Nilikuwa najua utawahi ili tupate muda hata wa
masaji! Ona mafuta haya nimekununulia.
Mazuri na hayana harufu.” Tunda akayatoa kwenye moja ya mfuko, akamnukisha
huku anamkalia na kupitisha kucha zake taratibu mapajani mwake. “Ndio
inakuaje?” “Ningekufanyia, lakini masharti yake unatakiwa upumzike
baada ya masaji. Sasa nikianza sasa
hivi, utachelewa nyumbani.” “Hamna
neno.” “Hapana bebi. Sitaki uwe unachelewa nyumbani kwa mkeo. Kwanza
nimemnunulia zawadi.” Yule baba akahisi
hajaelewa. Tunda akasimama, akarudi na mfuko mkononi.
“Unamaanisha ni zawadi ya mama Amini?” “Kumbe
mtoto wako mkubwa anaitwa Amini?” Tunda akauliza huku anarudi
kumkalia. “Ndiyo.” “Kwa hiyo na wewe nikuite baba Amini?” “Hapana.” Akakataa
kwa haraka. “Wewe endelea kuniita hivyo hivyo.” Tunda akamcheka
moyoni. Akajua amefurahia kuitwa Bebi. “Ni
nini umemnunulia?” Tunda
akatoa. “Kijizawadi chake yeye. Sio tena ukifika unampa mbele ya kina Amini, halafu waishie kumuomba!” Akacheka. “Sijawahi kumnunulia...” Akasita.
“Ndio unaanza sasa.” “Akiniuliza yameanza
lini?” “Wewe mwambie katika pitapita zako ukaona hizi chocolate, unataka ale mkiwa peke yenu,
chumbani kwenu.” Akacheka kama anayemtafakari
mkewe.
“Nini sasa?”
“Sijui, lakini ngoja nikamjaribu.” “Hakuna mtu anakataa zawadi na kila kitu
kina mwanzo.” Akabaki akicheka kwa wasiwasi kama anayesita. “Vipi?” “Sijawahi. Lakini acha nikajaribu. Nashukuru sana kwa kunifikiria. Kweli una
moyo mzuri.” “Basi ndio uwahi. Sio ufike huko umkute amekasirika kwa
kuchelewa, ushindwe hata kumkabidhi zawadi yake.” “Anajua kama nipo kwenye baa zetu. Huwa nachelewa kurudi nyumbani.
Anaelewa.” “Na mchana huwa unafanya nini?” Tunda akamuuliza taratibu. “Nina baa nyingine kule
Ilala pia. Ile ipo busy kuanzia asubuhi wanauza kifungua kinywa, chakula cha mchana na usiku ndio zaidi.
Na pia napatengeneza vizuri kuwe
na night club. Mziki pia. Sasa kwa kuwa ni katikati ya makazi ya watu wengine, huo ukumbi wa mziki, nautengeneza upya
kwa kuweka sound proof. Ili sauti zisitoke nje. Sasa lazima niwepo
kusimamia.”
“Pole.Utakuwa unachoka!” “Nimeshazoea.” “Basi kesho katikati ya kazi uje nikufanyie masaji. Itakusaidia mwili kujisikia vizuri, na sisi tupate muda wetu.” “Nashukuru kunifikiria Ani. Kwa hiyo sasa hivi niondoke?” “Naomba nikuage. Sitakuchelewesha.” Akajifanya yeye ndio anamuomba penzi, tena kwa kumbembeleza kumbe anatamani aondoke, apumzike. “Nitashukuru Ani. Na kesho nitajitahidi kuhangaikia sehemu yetu nzuri. Nimeshaanza kuzungumza na watu. Naamini tutafanikiwa tu.” Bila kujibu au kuonyesha ni habari njema sana, akamparamia baba wa watu. Akambadilishia mara mbili tatu akamuacha hajielewi hapo kitandani akihema, yeye akaenda bafuni.
Wakati
anarudi, amejifunga taulo safi la hapohapo hotelini jeupe, refu, akamwambia asogeze hiyo mifuko aliyokuwa amekuja
nayo. Alikuwa amemnunulia simu, Samsung
Galaxy mpyaaa iliyokuwa ndio imetoka. Tunda mwenyewe akashangaa kwa muda huo mfupi
aliwezaje kupata simu nzuri vile. Alitegemea simu ya kawaida
sana. Akaipokea, asiamini. “Nitaenda kulipia
chumba mimi mwenyewe. Ili wasikusumbue.” “Nakushukuru bebi. Uzidi kubarikiwa
na uongezewe.” “Na wewe pia Ani. Nimependa moyo wako.” Tunda
akacheka taratibu huku akiangalia ile simu yake. Akamvuta mkono wake wakulia, nakuubusu.
“Asante.”
Tunda akashukuru tena na sauti yake ya chini
na macho yake ya upole. “Karibu. Ukiwa na shida yeyote. Namaanisha
yeyote ile, tafadhali usisite kuniambia Ani. Kukimbilia kwa bibi iwe wazo la mwisho kabisa. Jua nipo kwa
ajili yako.” Hata masaa 24 hayakuwa
yameisha, baba anajitia kitanzi kwa binti ambaye hata jina amedanganywa!
Walizungumza kidogo, akaaga akiwa amekumbuka
zawadi ya mkewe. Akaishika mkononi. Tunda akacheka. “Nitakuona kesho Ani, asante kwa zawadi.” “Karibu na uwe na usiku mwema. Naamini kesho na mimi
utanipa muda mrefu kidogo. Tukae hata masaa mawili!” Tunda akajilalamisha kwa deko.
“Kabisa. Kesho nitakuwa hapa. Naamini nitakuja na habari njema.” “Hata kama hutafanikiwa mambo ya sehemu yangu ya kuishi, usisite kuja kuniona tafadhali.” “Lazima nitarudi Ani, usiwe na wasiwasi. Tunda akampa busu la shavuni. “Haya nenda, usije kuchelewa zaidi nyumbani.” “Sawa. Lakini siwezi kukuacha hivi hivi.” Akawa amesahau kabisa kama alimuachia pesa mchana. Akatoa tena waleti. “Si uliniachia mchana!” Akajifanya kama hataki. “Pesa yenyewe umenunulia mpaka zawadi! Sitaki upate shida.” Tunda akapokea na cheko. Mzee akatoka na kumuacha Tunda kwenye chumba kizuri, akipulizwa na kipupwe, AC, na pesa mkononi.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Tunda alibaki mle chumbani akicheka peke
yake. “Kumbe ndio rahisi
hivi! Hii ndiyo ajira yangu. Nitaenda kuongeza kondomu tu.” Tunda aliendelea
kucheka akijipongeza. Akawasha simu aliyokuwa ameletewa,
huku bado haamini macho yake. Kutoka hospitalini na kufikia kwenye maisha
ambayo hakutegemea! Kula ugali kwa maziwa mgando/mtindi kwa takribani miaka
miwili mfululizo akiwa kwa shangazi yake. Akahamia chakula cha hospitalini! Usiku
huo kuku wa kuchoma anamsubiria yeye hapo chumbani! Kwake aliona ni muujiza.
“Tena
uzuri wa ajira hii, hawahitaji kujua nimesomea nini, wala hamna maswali magumu. Nikuongeza ujuzi
kitandani ili wakionja tu wachanganyikiwe na kumwaga mipesa yao kama huyu.” Tunda
aliendelea kujisemea huku akicheka peke yake kama aliyeokota dhahabu. Aliendelea
kujiwekea mikakati mingi huku akiangalia mapesa aliyoyapata kwa siku
moja. “Kwa elimu niliyo nayo, hakuna mwajiri anayeweza kunilipa pesa
kama hii. Huu utundu wa kitandani nilionao ndio ajira yangu tosha.” Tunda aliendelea kuwaza.
Lakini katikati ya mipango yake akawa kama amegutushwa na
wazo. “Nikiruhusu huyu baba Imani
sijui Amini, anitafutie nyumba, atataka kuhamia hapo na kunimiliki mimi kama
mkewe. Na akishanifanya mimi mke wake, hawezi kuendelea kunihonga pesa yote
hii. Atanizoea. Sitaki mazoea kama ya baba Tom. Sitaki kuja kuumizwa.” Hasira zikampanda Tunda na kumbadili moyo kabisa.
“Kwanza akishanizoea, hatakubali kondomu.
Atajidai mimi mkewe, ataishia kunipa mimba, halafu aje aniache nikiteseka.” Tunda akazidi kuwaza huku
akiumia. “Lakini hata kizazi chenyewe kipo!” Hapo
akakumbushwa jinsi alivyotolewa mimba kikatili. Akawaza hili na lile, akaanza kufikiria tena jinsi ya kuishi na baba Amini
kwa akili ili aendelee kunufaika na pesa yake ila si kwa kujifunga kwake kabisa
kama nyumba ndogo au mkewe. “Hakuna kuzoea mwanaume. Hakuna
mabusu ya mdomoni. Mwiko.” Tunda
akaendelea kuwaza usiku huo na kujiwekea
mikakati ya kudumu ya maisha.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Aliamka asubuhi
akiwa ameshapanga maneno ya ukweli na uhakika
kumuaminisha baba Amini akija pale. Akatoka hapo mida ya saa tatu kurudi kituo
cha daladala za Mwenge. Akaanza kuulizia wapi atapata madalali.
Akazunguka huku na kule, akaelekezwa kwa
vijana kadhaa, akawapigia simu. Lengo la Tunda ni kupata sehemu
ya kawaida, lakini tulivu na
inayofikika mchana na usiku. Hakutaka sehemu ya vichochoroni ambako
ikimlazimu kurudi nyumbani usiku, awe
na hofu ya usalama wake.
Kama
kawaida ya madalali. Wakaanza kumtembeza. Alizunguka mpaka akachoka. Simu za baba Amani akimuuliza
alipo kila baada ya dakika kadhaa zikaanza. “Haya ndiyo ambayo sitayaruhusu. Sitaki
kumilikiwa kama alivyonimiliki baba Tom. Leo mwisho.” Tunda aliwaza, mwishowe akaamua kurudi hotelini alikokuwa akisubiriwa.
Alishakuwa
amekasirika. Aliachana na dalali kwa makubaliano
watafutane tena kesho yake. “Chukua hata taksii, fanya haraka urudi.” Hayo ndio
yalikuwa maagizo ya mwisho yaliyomkera zaidi Tunda. Alikuwa amekasirika
karibu kupasuka. Alifungua mlango bila hodi. “Mimi
sio mke wako. Acha kuniamrisha kama mtoto mdogo.” Aliingia na kuanza kugomba. “Huwezi kuniita unapojisikia wewe. Hunijui
na sikujui. Acha kujipa amri juu
yangu. Au kwa kuwa umenipa hii simu?” Tunda akairusha kitandani. “Au kwa kuwa pia nimekushirikisha shida zangu zote mpaka sehemu ninapoishi,
ndio unajichukulia mamlaka ya kunitawala
wakati..” “Tulia kwanza Ani. Tulia kwanza.” “Hapana. Huwezi kunifanyia hivyo. Usinichunge
mimi kama mtoto mdogo.” Tunda akazidi kugomba.
“Unajua
nilipokuwa lakini?” “Samahani. Nahisi nilipaniki. Nikajua umenikimbia.”
Akajishusha.
“Nina kimbia vipi wakati vitu vyangu umevikuta humu ndani na tumeachana kwa makubaliano ya kutafuta sehemu ya kuishi?”
“Mimi sikujua kama na wewe unahangaikia, Ani! Nilitaka wewe upumzike. Mimi ndio
nihangaikie.” “Hapana. Nimebadili mawazo. Unaonekana wewe utanisumbua sana. Sitaki.” Tunda akaanza kukusanya vitu vyake kama anayetaka
kuondoka.
“Nikupaniki Ani! Naomba yaishe bwana.” Akaanza kumfuata
nyuma akimbembeleza. “Nilikuja na habari
njema, sasa nilipokukosa hapa nikajua umenikimbia.” “Kwa hiyo huniamini?” “Tumekutana jana tu Ani! Tafadhali
nipe nafasi nyingine. Na mimi najifunza.” “Mbona
sasa huombi msamaha?” Tunda akamuuliza
kwa ukali kidogo. Akaanza kucheka. “Njoo
kwanza hapa. Nimekuja na msamaha mkubwa.” Tunda
akabaki amesimama akimwangalia.
“Njoo
basi Ani! Acha hasira.” “Omba kwanza msamaha, lasivyo naondoka.” “Hata magoti napiga.” Tunda akashangaa kweli anapiga magoti. “Nisamehe Ani wangu.” “Acha kuwa kama mtoto anayelilia nyonyo bwana! Mpaka
madalali walikuwa wakinishangaa, wakahisi nimeacha mtoto mchanga nyumbani!” “Nilipaniki. Nilikuwa
nimejiandaa kuja kukukuta hapa. Jana ulinipa wakati
mzuri sana. Halafu...” Tunda alibaki akimtizama kwa kumsuta mpaka
akashindwa kumalizia alichotaka kusema, akacheka. “Njoo basi Ani, mama. Hasira haziishi!” Akarudi kukaa.
“Wewe
niambie habari njema zenyewe kwanza. Maana
kama ni sehemu ya kuishi, sitaki tena. Najitafutia kwangu, tutakuwa tukikutana
unapokuwa tayari. Sitaki usumbufu.” “Umekasirika
Ani. Acha hasira, njoo. Njoo nikwambie kitu kizuri. Njoo mama.” Tunda akasogea. “Njoo ukae hapa basi! Akimuonyeshea miguuni kwake. “Ongea
kwanza. Mimi nanuka jasho, mpaka nikaoge. Umenikimbiza kimbiza!” “Mimi sijali kama unanuka jasho. Njoo.” Tunda akaenda kumkalia. “Nina
habari njema zaidi ya sehemu ya kuishi. Unaona lile begi pale?” Tunda
akageuka. Akaangalia. “Kuna nini
mle ndani?” “Pesa tupu.” Tunda akamwangalia kama asiyemuelewa.
“Umekuja na baraka Tunda! Unaonekana unanyota kali sana. Na kuna mtu alishanitabiria kuwa kuna kitu kizuri kinanijia kwenye maisha yangu. Akaniambia kikija hicho kitu, mambo yangu yataanza kufunguka.” Tunda akapandisha nyusi moja juu kama anayemshangaa. Na kukunja mikono kifuani. “Sasa hapa kitu kizuri ni mimi au hizo pesa!?” “Ni wewe Ani. Yaani nyota yako na yangu imeendana.” Tunda akabaki amekunja uso.
“Kwanza mimi naitwa Sadiki.” “Mtoto wako anaitwa
Amini! Majina ya wapi hayo!?” Sadiki
akacheka. “Najifungua kwako Ani, ili ujue sisi tumekusudiwa kuwa pamoja.” “Sitaki
kuolewa mke wa pili mimi?” Tunda akasimama. “Kwanza sitaki kuolewa kabisa.” “Nakwambia ni zaidi ya hapo Ani.” Na yeye
akasimama. Sadiki alionekana amechangamka
kweli kweli. “Mbona
umehamasika hivyo! Kama unafikiri begi la pesa ndio litanihadaisha
na kunifungia ndani kama mkeo, jua HAPANA.” Tunda akaendelea kumuwekea
ngumu.
“Nakwambia
utakuwa zaidi ya mke.” Tunda
akakunja uso. “Tatizo hutaki kutulia Ani! Maisha yetu hayatakuwa kama zamani. Na
wewe hivyohivyo. Yaliyotabiriwa yametimia
baada ya kukutana na wewe. Tulia, acha hasira, nikupe habari nzima la hilo begi
na maendeleo yetu kuanzia hapa. Najua na wewe utafurahi tu.”
Akamsogelea
tena.
“Kwanza nusu ya zile pesa pale zitakuwa zetu. Mimi na wewe. Utakuwa huru kufanya kile unachotaka, sitakuuliza swali juu ya matatumizi wala huhitaji kunipa mahesabu yake.” Tunda akaanza kulainika. “Na nusu yake?” Tunda akamuuliza. “Mama Amini anajua juu ya hizo pesa. Lazima azione. Halafu mimi na wewe tutaanza kuingiza mapesa.” Sadiki akawa anaeleza kwa kuhamasika haswa. Tunda haelewi. “Watu si wanalia pesa ngumu kuiweka mfukoni?” Sadiki akauliza kwa kicheko. “Basi sisi tutashamiri. Tutaingiza mamilioni ya pesa tukiwa hapa hapa Tanzania. Lakini tukiwa mimi na wewe. Kama utakubali lakini!” Bado Tunda alikuwa amesimama, hajaelewa.
Sadiki akasogelea ule mkoba. Akatoa pesa baadhi akaziweka mezani. “Hizi ni zako na zangu tu. Kwa matumizi yako tu. Huna haja ya kuhangaika tena.” Tunda akabaki kimya. "Nakusikiliza Ani. Niambie kile unachotaka sasa hivi, nifanye. Utulie.Nishakuomba msamaha mpaka wa magoti! Niambie nini unataka Ani. Ili tuanze kuneemeka kwenye jangwa.” Sadiki aliendelea kuongea kwa kuhamasika. Tunda akabaki ameduaa kwenye pesa alizomilikishwa gafla!
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Kufunga na kufungua Tunda anamilikishwa mapesa. Sadiki anampa ahadi kubwa ya
Neema katikati ya wenye shida na
shidani. Tena si ahadi tu, amemkabidhi kabisa
pesa isiyo na maswali. Amemwambia yeye atakuwa zaidi ya mke!
Ø
Ni nini anamaanisha?
Ø
Ni nini hicho cha tofauti watafanya pamoja na Sadiki ambaye
anaonekana ameshafanikiwa kimaisha. Ana mke
ambaye naye ni mfanyabiashara mzuri tu, na tayari wana biashara
zinazoonekana kufanya vizuri tu! Tunda anaingiaje
kwenye picha akiwa na huo mtaji alioambiwa ni wa NYOTA nzuri tu?
Ø
Yepi atafanya na Sadiki?
Ø
Je, ni kweli ni Neema?
Tunda ameingia mtaani. Atapita
kwingi, atafanya mengi ili kuweza kuyamudumu maisha.
Endelea
kufuatilia sehemu ya 9.
0 comments: