Lifestyles,

Be Grateful...

Monday, September 07, 2015 naomimwakanyamale 0 Comments

KUPO KUJISAHAU KWINGI, KUTAKA ZAIDI NA ZAIDI KILA IITWAPO LEO, KITU KINACHOTUCHUKULIA MUDA WETU MWINGI, AMANI HATA FURAHA KATIKA KUSAKA HIYO ZAIDI NA KUSAHAU KABISA KUANGALIA YALE MUNGU ALIYOKWISHA TUBARIKI NAYO. CHUKULIA MFANO MDOGO TU PALE UNAPOKUWA UNAMUOMBA MUNGU NA KUTAFUTA KAZI. UKISHA PATA HIYO KAZI JIANGALIE WEWE MWENYEWE JINSI UNAVYOILALAMIKIA HIYO KAZI. UTAANZIA MSHAHARA AMBAO ULIUKUBALI MWANZONI KABLA YA KUANZA KAZI, UTALALAMIKIA MAZINGIRA YA KAZI, BOSI NAKUSAHAU KABISA SHIDA ULIYOKUWA NAYO MWANZONI WAKATI UNATAFUTA KAZI. TURUDI KWENYE FAMILIA ZETU MKE/MUME/MCHUMBA/WATOTO/NDUGU TULIO NAO JINSI TUNAVYO WAFANYIA, NI RAHISI KUTAFUTA KUTENDA MEMA NJE NA KUPENDEZESHA WA NJE NAKUSAHAU KABISA WATU WAKARIBU MUNGU ALIOTUPA. NAKUANZA KUWALALAMIKIA KILA WAKATI TENA HATA KWA WATU WA NJE BILA KUSHUKURU KWA WAO KUWEPO KWENYE MAISHA YETU.
NIVIZURI KUOMBA KWAAJILI YA BARAKA MPYA, LAKINI NI MUHIMU KUJUA, KUTAMBUA, NA KUMSHUKURU MUNGU KWA ZILE BARAKA ALIZOTUPA KWANZA.

0 comments: