Story
iyo week ya kuendea harusi ya Malii ilikuwa nzuri
sana. Geb alikuwa ametulia. . Hakukumbushia kufukuzwa mtu yeyote yule kazi.
Chakula kikawa kinaliwa vizuri.
Japokuwa alikuwa akichelewa sana kurudi nyumbani, lakini alihakikisha anakula kabla ya kulala. Nanaa alimsikia akimwambia mama yake kuwa anatumia siku hizo chache za juma, jumatatu mpaka jumatano kuweka mambo ya kazini sawa kabla hajasafiri, kwa hiyo atakuwa anachelewa kurudi. Wakaelewa kuchelewa kwake.
“Usicheke bwana mama!” “Subiri sasa. Alipoona Danny haelewi, si akaamua kumwambia wazi wazi. Akamfuata Danny chumbani kwao. Asubuhi alipoona Grace katoka tu, yeye akaingia na khanga moja chumbani kwao. Akajua Grace kaenda kazini, Danny kabaki peke yake huko chumbani. Akamtongoza Danny pale pale, akavua ile khanga ndani yupo uchi, akapanda kitandani. Acha Danny aanze kupiga kelele kama mtoto mdogo. Akamvutia chooni kwao, akamfungia. Yeye akaendelea kupiga kelele. Tukakimbilia chumbani kwao tukajua kuna hatari. Kufika huko chumbani, eti Danny amepanda kitandani amesimama kabisa juu ya kitanda anapiga kelele.” “Mama!” Nanaa akabaki anashangaa.
“Kwani yalikuwa madogo! Alituacha mimi na Geb tumechanganyikiwa. Tunamuuliza kwani kulikoni? Anasema anataka James aitwe haraka sana. Geb akampigia simu James akamwambia afanye haraka aje pale nyumbani.” Mama G alikuwa akisimulia huku anacheka. “Hatujakaa sawa Grace naye akarudi. Kumbe hakwenda mbali, alienda kutafuta kitafunio. Hivi anavyokwambia Danny walikuwa wasichana wawili na hakuna chakula, ujue hatanii. Mnarudi kutoka kazini, mnaishia kula chakula cha kununua, au ndio tuingie jikoni tuanze kupika. Kikija kuiva ni saa 4 usiku wote tumechoka. Tunataka kulala tu.” “Mbona Grace huwa anapika vizuri tu?” Nanaa akauliza kwa kushangaa.
“Wewe hujachunguza vizuri. Danny hataki awepo nyumbani eti mkewe yupo jikoni masaa kwa masaa! Heri akanunue chips yai, au aje na nyama choma au rosti, mle kuliko mkewe ashinde jikoni wakati yeye yupo. Hathubutu. Au yale mambo ya mkewe amuache kitandani asubuhi kama wanawake wengine. Aamke, amuache kitandani ili amwandalie kifungua kinywa, hataki. Anataka alale na mkewe, waamke, waoge pamoja, ndio waende naye jikoni. Apike kidogo tu, atoke wakae wote. Na kitafunio cha haraka anachopikaga Grace ambacho anajua hakichukui muda mrefu huko jikoni ni chapati za maji tu. Sasa na zenyewe huwa zinachosha. Akipika kitu kigumu, ujue Danny yupo kazini. Basi apike haraka, akirudi amkute amekaa kama vile. Sio eti hajamuona mkewe siku nzima wakiwa kazini, halafu aje hapa mkewe yupo busy jikoni, hapo hamuwezi kuelewana hata kidogo na Danny.” Nanaa akacheka.
“Basi, turudi kwenye stori yangu. Grace anamuuliza mumewe umeona nyoka? Anasema hapana. Nakwambia Danny anapiga kelele kwelikweli anamtaka James aje pale haraka. Wote tukaingiwa na wasiwasi tukasema labda kapatwa na kichaa. Bahati nzuri ilikuwa siku ya sikukuu, watu hawaendi kazini, hakuna foleni. Kwa hiyo James akaja kwa haraka akamkuta bado yupo juu ya kitanda. James anamuuliza vipi? Akaanza kumuuliza James kama anakumbuka vile alivyohangaika kumpata Grace. Sasa James anamwambia anakumbuka, kwani vipi? Danny kakazana, eti James atuelezee shida alizopitia mpaka akakubaliwa na Grace. Basi James akasimulia kwa kifupi wakati huo bado kasimama juu ya kitanda kabisa, hataki kukaa. Watu wote tumetoa macho tunamwangalia. Grace amemletea maji ili anywe, hataki. James akamaliza kusimulia huku anamkatisha kila mara anamkumbusha hiki au kile. Anamwambia anasahau. Basi James akawa anarudia kueleza mpaka akamaliza. Wote tumesimama tunataka kujua mwisho wa yote ni nini kinaendelea? Maana habari za Danny na Grace kila mtu anajua.” Mama G akacheka tena.
“Sasa kwa nini alitaka kaka asimulie tena?” Nanaa akahoji. “Sikiliza sasa. Baada ya kuridhika, akamwambia afungue mlango wa bafuni. James si akamkuta dada yake yupo uchi huko bafuni. Akafunga mlango haraka kwa mshtuko. Sisi hatuelewi. Tunamuuliza James, kwani kuna nini huko bafuni? James kakaa kitandani ameinamisha kichwa kama mgonjwa. Grace akamuuliza tena Danny. Safari hii kwa ukali. Si ndio akaanza kusimulia kisa kizima kuwa Viola amemfuata hapo chumbani anamtaka kimapenzi.” Nanaa akakumbuka vile Viola na Vai walivyorudishwa nyumbani kwa haraka wakati Nanaa alivyokataliwa kuja nao huku jijini kipindi amemaliza kidato cha 6.
“Danny akaanza, ‘Huyu mtoto anakichaa kibaya sana. Grace mwenyewe wala sijamfaidi. Yaani yale matusi yakunikataa wakati namtongoza wala bado hayajaisha moyoni, eti na yeye anataka kunitoa humu ndani! Unataka kuniponza wewe?’ Yaani badala ya kusikitika, tukajikuta wote tunacheka mbavu hatuna. Vile anavyosimulia na anavyotetemeka, utafikiri amepigwa shoti ya umeme. Grace akamuuliza sasa kwa nini anaongelea juu ya kitanda? Anasema alikuwa anaweka msisitizo, ili James aje haraka, amchukue mdogo wake pale ndani, asimletee balaa.” “Maskini kaka yangu.” Nanaa akamuhurumia James.
“Nakwambia James alitia huruma. Akawa mwekundu kama nyanya. Ungemuhurumia. Alikuwa hawezi kumtizama mtu machoni. Alijisikia vibaya sana. Ungekuwepo, ungemuhurumia zaidi. Aliomba msamaha kwa Grace, mpaka akapiga magoti. Sasa Danny naye badala amfariji mwenzie James, amekazana kumshtumu eti yeye ndio amemtuma mdogo wake. Basi James yupo amepiga magoti anatubu huku anajitetea na Danny naye anaendelea kumlaumu tu. Mpaka Grace alipomgombeza Danny ndio akanyamaza. Sasa jioni yake ndio tulicheka mpaka machozi.” Nanaa akajifunika uso wake na mto.
“Aibu gani hii! Sasa wewe mama ulipomuona mwanzoni akiwa anahangaika na Geb, kwa nini hukumkataza?” “Mimi! Akaa. Nanyamaza kimya, ili kila mtu yakija kumshinda baadaye asije nilaumu. Najiangalizia kimyaa kama sipo.” “Sasa na kwa Danny? Kwa nini hukumwambia mkewe?” “Niambiwe mchonganishi, navunja ndoa za watu!? Tena na Grace mwenyewe aliniuliza hivyo hivyo. Nikamwambia kama yeye anajidai yupo busy haoni na anashindwa kumchunga mumewe, atajijua mwenyewe. Viapo alitoa yeye mwenyewe kanisani. Halafu aje ashindwe kuvitekeleza, atake watu wote tumchunge mumewe! Aku. Apunguze shuguli, amlinde mumewe.” Nanaa alikuwa anacheka nakujisahau kama watu wengine wanawasikiliza.
Waliendelea kucheka mpaka Grace naye akaingia. “Jamani mnacheka nini? Niambieni na mimi.” “Acha umbea wewe Grace. Nenda kalale na mumeo.” Mama yao alimjibu. “Si mnisimulie tu.” “Acha umbea wewe mtoto. Danny atakuja sasa hivi kukufuata. Sitaki mnijalie humu ndani kwangu, nataka kulala. Ondoka. Nanaa na wewe nenda kamalizie kujiandaa. Acha kupenda umbea. Kwanza mimi natoka mara moja. Narudi tena dukani, kuna kitu nimesahau kununua.” Nanaa alitoka huku akiendelea kucheka.
Grace akarudi chumbani kwao alipokuwepo mumewe na Fili wakicheza tv games. Fili alikuwa akishangilia anavyomfunga baba yake. Ilikuwa game ya mpira wa kandanda. Walikuwa wakicheza wawili tu hapo chumbani. Nanaa akaingia chumbani kwake. Mama G, na yeye akaondoka na gari yake. Kulikuwa kumetulia sana. Bado Geb hakuwa amerudi kutoka kazini. Nanaa akaanza kuwaza afungashe nini cha muhumu.
Mara wakasikia mlango wakuingilia ndani unafunguliwa. Sauti ya Liz na Geb. “Nimekwambia usiwe na wasiwasi Liz. Kwa nini unataka kujinyima raha bure?” “Kwanza kwa nini tuondoke na gari tusipande ndege? Mimi sipendi wala sijazoea usumbufu.” “Tukiondoka na ndege, tutatumia usafiri gani kutuzungusha tukifika huko Moshi? Tumekubaliana na Danny mara baada ya sendoff, tuzunguke kidogo. Hata tukiweza twende mpaka Arusha. Tutakuwa wengi, nina uhakika utafurahia tu.” “Hayo ndio yanayonichosha. Watu wengi kila mahali! Hamna sehemu ya utulivu ya kwetu sisi wenyewe! Kila mahali watu. Na leo tena unasema tutakuwa na watu humo kwenye gari. Hamna sehemu ya kupumzika jamani!? Watu kila mahali!” “Tunaondoka na hii SUV ya viti nane. Na tutakuwa watu wa humu humu ndani tu. Hatuwezi kubanana.” “Kila mtu anaharufu yake Geb. Tukichanganya harufu ya kila mtu humo ndani kwenye gari, na safari yenyewe mpaka Moshi! Nitatapika njia nzima.” Liz aliendelea kulalamika.
“Hivi mbona kama hujanielewa? Nimekupa suluhu ya tatizo lililokuwa likikukera. Tena kwa amani tu. Kwa nini unatafuta tatizo jingine? Kama hujaelewa chochote nilichosema tokea nimewafuata hapa, elewa hivi, sisi tutaendesha gari yetu. Mimi, Danny, Nanaa na Fili. Basi.” Grace alijaliwa sauti ya upole sana, japo ilisikika ya uvivu zaidi.
“Maana mnaweza msinielewe. Lakini mimi sijali.” Liz akaongeza. Grace hakusikika kujibu. “Kwanza nashangaa kwa kumbi zote zilizojaa hapa mjini eti mtu anaenda kufungia harusi au sijui sendoff huko milimani. Na sisi eti tunaenda! Kwa lipi hasa? Ndio maana nasema haya mambo yakuoa hujajiandaa kipesa sio mazuri. Harusi sio dharula. Ni kitu mtu anatakiwa kujipanga kabla. Sio kushikana mashati, eti mnachangishana!” Liz akaendelea.
“Watu wanawekeza mpaka kwenye misiba yao kabla hawajafa. Ili ukifa usisumbue watu na maiti yako. Sembuse harusi! Tena ya watu mnaokubaliana na kupanga tarehe! Panga harusi ukiwa na pesa yako sio unapanga harusi kwa pesa za watu wengina. Mtu akiwa na pesa yake si anatafuta ukumbi na hoteli sehemu za kueleweka? Kama ndugu zake wako mbali na mjini, anawaleta mjini na kuwaweka mahotelini. Harusi ikiisha kila mtu anarudi kwake, sio lazima kuendelea kufuatana nyuma. Hayo ndio maisha na hiyo ndio habari ya mjini. Sio mnafunga safari kufuata harusi ya kijijini! Kwa nini!? Mimi hata sielewei!” Nanaa alimsikia Liz akiendelea kulalamika. Aliongea kwa kutumia lugha ya kingereza kwa muda mrefu, huku akiweka maneno machache sana ya Kiswahili. Na kilikuwa kingereza kizuri. Maneno aliyatamka kifasaha kama mzawa wa huko nchini Uingereza. Nanaa akabaki akitamania.
Cha ajabu hakumsikia Geb, wala Grace wakijibu tena na wote walikuwa maeneo hayo hayo. Nanaa aliendelea kusikiliza maneno ya kingereza yanayotolewa kwa jazba. Mara akasikia hatua za Grace zikimfuata chumbani. “Nanaa!” Mlango ukafunguliwa. “Usiende kupika. Mama amesema atatuletea kitimoto na ndizi. Wewe endelea kujiandaa. Akirudi, nitakuja kukuita.” “Asante.” Nanaa akashukuru, Grace akatoka na sura yake tulivu. Akamsikia akiingia chumbani kwake. Kidogo wakasikia Geb na Liz nao wanaingia chumbani kwa Geb.
“Ujue wewe Fili nakusikia wewe! Na nisikuone kitandani kwangu tena. Ukalale huko huko unakomdanganya bibi yako.” Fili akaanza kucheka. “Basi bibi. Wewe tutalala wote kesho. Leo nalala na mama yangu.” “Kila siku habari ni hiyo hiyo. Mpaka ufukuzwe huko chumbani kwa watu, ndio kimbilio linakuwa mimi.” “Sasa si kwa sababu nakupenda wewe.” “Mmmh!” Bibi Fili akaguna tena.
“Nanaa yuko wapi? Mwiteni aje kula.” Aliposikia tu hivyo, akatoka haraka. “Halafu hii chupa mbona ina uji? Huyu Geb mbona hajanywa? Au hayupo? Lakini kama nimeona gari yake hapo nje!” “Yupo chumbani na Liz.” Grace alijibu huku akiandaa chakula. “Oooh!” Mama G akaitika. Nanaa akaingia. “Mbona sura imepooza tena, wakati nilikuacha na furaha?” Mama G alimuhoji Nanaa mara alipoingia pale jikoni. “Nimepata dharula mama. Naona sitaweza kwenda tena Marangu.” “Mmmh! Dharula hiyo dharula gani? Mbona gafla!? Nimekuacha hapa hata lisaa saa halijaisha, tayari umepata dharula!?” “Kweli mama. Natakiwa kwenda kuangalia chumba kesho. Dalali kanipigia simu sasa hivi. Kanipatia chumba.” Grace na mama yake wakabaki wakimwangalia Nanaa.
“Itabidi tu kwenda hiyo kesho. Lasivyo huyu dalali atakigawa chumba. Heri tu kesho nikifuatilie, nifunge mkataba kabisa.” Nanaa aliendelea kujitetea. Grace na mama yake wakaangaliana. “Basi kazi mtakuwa nayo huko njiani.” Mama G akasema. “Wala si kidogo.” Grace akajibu akikumbuka hasira za kaka yake, kama Nanaa asipokwenda. Lakini Nanaa hakuelewa ni nini wanachoongelea. Akanyamaza.
Danny akatoka. Wakaanza kula. Lakini kulikuwa na ukimya wa namna yake sio kama siku zote. Walikula kimya kimya mpaka wakamaliza. Kila mtu akaaga kuwa anakwenda kulala mapema tayari kwa safari kesho yake. “Msihangaike kuosha vyombo. Mimi nitaosha na kusafisha hapa. Nyinyi kawahini kulala. Mpumzike kwa safari kesho.” Nanaa aliongea huku akikusanya vyombo kurudisha jikoni. Danny na familia yake wakaondoka kuingia chumbani kwao. Bibi Fili naye akaingia chumbani kwake. Wakamuacha Nanaa.
Baada ya muda akasikia mlango wa jikoni unafunguliwa. “Nanaa!” Akageuka alikuwa Geb na uso uliopooza zaidi si kawaida yake. “Abee!” Nanaa aliitika kwa upole. “Mama ameniambia hutuendi wote tena.” “Nilimwambia kuwa dalali alinipigia simu akaniambia kesho nikaangalie chumba.” “Ni kweli?” Geb akauliza, Nanaa akabaki kama amepigwa na butwaa. “Nanaa?” “Hapana sio kweli.” Nanaa akajikuta anajisalimisha.
“Kwa sababu yeyote ile, naomba usiche kwenda na sisi kesho. Tafadhali sana.” “Sawa. Lakini mimi naomba niondoke na kina Grace.” Geb akatulia kwa muda. “Pia itakuwa vizuri nikiwa nao, nitawasaidia swala la mtoto njiani.” “Ok.” Geb alijibu na kutaka kutoka. “Hivi mimi nina wazimu gani jamani!?” Nanaa alijiuliza moyoni.
“Geb!” Nanaa akamwita kwa upole na sauti ya chini. Akarudi. “Hujala leo. Naomba usilale bila kula.” Geb akabaki pale mlangoni, akainama kama ametingwa na mawazo. “Naomba nikuwekee kidogo tu, ukale hata chumbani. Usilale hivyo.” Kimya. “Najua umechoka. Lakini naomba ujikaze kunywa hata uji tu. Usilale na tumbo tupu.” Nanaa akaendelea kusisitiza. “Nakushukuru Nanaa. Asante.” “Kwa hiyo umekubali kula?” Nanaa akauliza, Geb akacheka kidogo. “Uji, tafadhali.” “Yes!” Nanaa akafurahi sana mpaka Geb akajua. Akacheka.
Kwa haraka kama asimcheleweshe kurudi huko chumbani, akammiminia uji kwenye bakuli kubwa huku Geb akimwangalia. Akamuwekea kwenye sinia lake pamoja na maji na matunda. “Ukimaliza wewe weka hata nje ya mlango wenu. Usihangaike kurudisha huku. Mimi mwenyewe nitakuja kutoa.” Geb akamtizama. “Asante Nanaa. Nakushukuru. Ila nitarudisha tu mimi mwenyewe. Wewe nenda kapumzike.” Akamkabidhi. “Usiku mwema Nanaa.” “Na wewe pia, Geb.” Akamtizama kidogo, nakutoka.
“Mtoto mbaya wewe? Sasa kwa nini ukatae gari?” “Sio gari tu mama na wewe, na nyumba!” Nanaa akaongeza. “Gauni.” Mama G akaongeza. “Na viatu mama! Kwa raha zangu.” Nanaa alitembea mbele ya Mama G, huku anaringa kidogo. Yule mama akawa anacheka. “Nanaa wa dhahabu!” Mama G akaongeza. “Kumbe! Sasa hivi ningekuwa nimejaa madhahabu. Shingoni na mkononi.” Bibi Fili na Nanaa waliendelea kucheka pale jikoni mpaka wakaamsha kila mtu.
"Hivi nyinyi huwa mnacheka nini hakiishi jamani!? Mnajua saa hizi ni saa ngapi?” Grace aliingia pale jikoni. “Umbea wako ndio umekuamsha wala sio sisi. Usiye lala na mumeo ukatulia ndani ni nini?” “Kelele.” Grace akamjibu mama yake. “Mama huyo!” Nanaa akajitetea. “Aliye na kazi ya kucheka hapa jikoni ni nani kama sio wewe Nanaa? Acha kunisingizia bwana.” Grace alianza kusaidia kazi pale jikoni.
Mama G akaanza kucheka. “Si mama huyo!” “Alimuahidi yeye mwenyewe huyo Geb.” Mama G akaongeza. “Na ukimuahidi Geb kitu, lazima utimize. Ni heri kama huna uhakika, umkatalie tokea anakuomba. Anaumia sana ukija kubadilika baadaye. Na yupo hivyo tokea mtoto.” Grace aliongea kama mama yake. “Lakini nimemuomba tuondoke wote. Nipande gari yenu nyinyi.” Nanaa akaongeza. “Mmh! Mbona tena mnaendesha magari mawili wakati aliniambia mtaondoka na gari ile kubwa. Kwa nini kumkimbia mziwanda wangu!?” Grace na Nanaa wakaangaliana. Kisha wakanyamaza. “Nishaelewa.” Mama G, alijua tu baada ya Grace na Nanaa kuangaliana. Wakanyamaza.
“Mimi sipendi safari za jua kali. Hasa kama tunaendesha. Heri kama ingekuwa tuna fly na ndege.” Liz aliingia na kuingilia mazungumzo ya Geb na dada yake. “Basi nyinyi wahini. Tutakutana Moshi.” Grace akajibu kwa upole na kuondoka. “Tutaondoka pamoja. Tutawasubiri tu.” Geb alijibu akionekana kama na yeye amekasirika kidogo. “Geb! Nimesema sipendi jua.” “Nashauri uchukue ndege ya kesho utufuate Liz. Nitakuja kukupokea KIA. Itakusaidia kufika ukiwa umetulia. Sidhani kama upo tayari kwa safari ya gari.” Ukimya mkubwa ukatanda.
“Kwa hiyo hutaki kuendesha ukiwa na mimi?” “Tunakwenda kwenye jambo la furaha Liz. Sendoff ya mchumba wa Malii. Malii ni rafiki yetu wakaribu sana. Mimi, Zinda, James, Danny, Gozi na wengineo. Yupo kwenye maisha yetu tokea tupo sekondari. Kwakwe Marangu sio mbali, wala sio mlimani. Anakwenda kwa mwanamke anayempenda na ameomba tumsindikize tuungane naye katika furaha hii ya kwenda kukabidhiwa mke kimila. Kwa upande wa bibi Fili, Malii ni mtoto wake. Japokuwa anaumwa magoti, lakini amekubali kwenda kuungana naye. Sitaki sisi tufike pale tukionyesha sura za adhabu. Ni bora tusiende, au twende lakini tukiwa na furaha.” “Kwa hiyo unataka mimi nisiende?” Liz akauliza kishari.
“Hilo ni swali ambalo ukipenda, utanipa jibu baadaye kama uliamua kuja na ndege au la. Lakini mimi nitaondoka na gari kubwa, pamoja na kina Danny. Unanijua mimi huwa sio mtu wakubadilika badilika Liz. Nilipewa na Danny jukumu lakufanyia hiyo gari service ili iwe tayari kwa safari. Nimefanya hiyo kazi. Leo asubuhi siwezi kuamka eti nimwambie Danny apandishe familia yake kwenye gari ambalo halijafanyiwa service kwa safari ndefu, halafu eti mimi na wewe tunaendesha gari lenye viti nane! Tupo peke yetu njiani! Si sawa na sitafanya hivyo. Nashauri uje na ndege. Na kama utapata gari ya kukodisha pale uwanja wa ndege, uchukue utufuate Marangu au ukitaka mimi naweza kukufuata. Huna haraka ya kuamua. Utanijulisha kwa simu.” Watu wote walikuwa kimya.
Nanaa alipomsikia Geb ameweka tu kituo kwenye maongezi yake, akatoka pale jikoni kimya kimya, akarudi chumbani kwake akinyata. Mama yao alikuwa akiendelea kupika huku akitayarisha matunda. “We Geb! Hebu kaniletee ile cooler kutoka kwenye gari yako. Nataka niweke kila kitu tayari. Nisiwacheleweshe.” Mama yake akamtuma kwa kuamuru kidogo. Geb akajua ameshakasirika na yeye. Alisikika kwa sauti ya amri, wala si utani kama alivyokuwa na Nanaa pale jikoni. Geb akatoka. Wakasikia Liz anatoka na yeye.
Aliamka tena walipofika Chalinze. “Kuna anayetaka kujisaidia tusimame?” Geb akauliza. “Nanaa!” Grace akamwita. Sio kwamba hakuwa amesikia. Lakini aliamua anyamaze tu ndani ya mtandio wake. “Unataka kushuka?” “Mimi nipo sawa.” Nanaa akamjibu Grace taratibu kama kunong’ona. “Hata mimi nipo sawa tu.” Grace akaongeza. “Maadamu huyu amelala, kanyaga mafuta twende. Akiamka ndio tusimame acheze kidogo ndio tuondoke.” Danny na yeye alijibu huku akimwangalia mwanae aliyekuwa amelala kwenye kiti chake. “Ngoja aamke hapo, maneno yatakuwa mengi mpaka tufike. Kila kitu anajua yeye.” Mama yake aliongeza huku anamfunika vizuri.
“Dume la nguvu hilo. Limempita mbali sana Zinda.” Kila mtu alianza kucheka mpaka Nanaa. “Hovyo kweli Zinda. Sijui yukoje bwana!” “Nimemuona kapendeza kweli.” Grace akaongeza. “Jana kanunua nguo mpya eti kwa ajili yakuvaa leo na kesho ili Nanaa amuone. James anamwambia ajifunze kuongea kwanza. Anasema eti kizuri chajiuza. Atamfanyia action Nanaa mpaka amkubali mwenyewe.” Kila mtu alikuwa anacheka.
“Zinda ni chizi jamani! Sasa magauni na viatu vya Nanaa?” Grace aliuliza huku wote wanacheka. “Wewe utamuweza Zinda na fujo zake. Fujo tu. Alikuwa anasema kuanzia sasa, matendo yake yataongea. Hataki tena maneno mengi.” Waliendelea kuongea na kucheka mpaka walipofika Segera wakaamua wote wasimame.
Walio oa walikuja na wake zao. Kila mtu alikuwa anacheka. “Danny wewe tumetoka mbali sana ndugu yangu. Ukilikumbuka hilo, utanisaidia nimalize hii shuguli yote kwa haraka.” “Unataka nikutongozee Nanaa?” “Kwani mimi nachagua msaada kaka? Chochote tu napokea, ilimradi nimwingize Nanaa ndani.” Watu walizidi kucheka.
“Maua yenyewe hujapokelewa. Anza kwanza kwa kutoa maua. Tuanzie hapo. Usipige goti wala usiongee maneno mengi. Wewe mkabidhi maua kiume.” “Hilo mbona rahisi.” “Mpe sasa.” Zinda akajiweka sawa. Alikuwa amevaa suruali ya jinsi ya bluu, na shati la mikono mifupi. Akafunga na tai. Vyote vilionekana vipya. Na wala hakutisha. Nywele zilinyolewa vizuri. Wazi alionekana alikuwa saluni siku iliyopita.
“We Zinda! Nini bwana? Umeng’ang’ania maua kama wewe ndio umepewa?” “Danny naye hana subira! Acha nikusanye nguvu, kaka!” “Basi sisi tunaondoka. Hatuwezi kulala hapa Segera.” Kila mtu alikuwa anacheka. Walikuwa wametoka kwenye magari yao, wanaangalia vituko vya Zinda na Danny.
Danny akamsogelea akiwa bado amembeba mtoto wake, akampiga ngumi ya begani. Maana alibaki kama ameganda. “Zinda!” Danny akamwita kwa ukali. “Nanaa! Nanaa mama watoto..” Zinda akaanza tena. “Anaanza kuharibu tena!!” Danny alimkatisha. “Danny mbona huna subira kaka? Naanzia mbali. Subiri. Nitashika tu kasi.” “Sasa Nanaa mama watoto ndio nini Zinda? Mpe maua. Basi.” Kila mtu alikuwa akicheka sana.
"Mimi naona hili zoezi tuliahirishe. Mnamchosha dada yangu bure.” “Mimi si nilikwambia James? Akawa ananibishia, anasema nimeongeza. Sasa umeona mwenyewe?” “Kweli hii aibu ya mwaka!” “James! Mimi na wewe tumetoka mbali sana mtu wangu. Usininyime dada yako.” “Nanaa huyo hapo. Hujanyimwa chochote.” “Basi ngoja nikaongeze bia nyingine narudi sasa hivi.” Zinda akaondoka na maua yake mkononi. Watu walizidi kucheka.
“Umeyapenda mama watoto wangu? Eti Nanaa?” “Nimeyapenda ni mazuri.” Nanaa alijibu huku akiyaangalia yale maua. “Basi moyo wangu umefurahi sana. Nime..” “Aaaahhh.” Danny alikohoa kwa kumkataza. Zinda akatulia kidogo. “Au nihamie humu kwenye gari yenu ili niwe na Nanaa?” “Hapana Zinda. Ondoka. Hatukutaki humu ndani. Tena ondoka haraka kabla hujaharibu zaidi. Toka, rudi kwenye gari yenu.” “Sawa kaka.” Zinda akaondoka akaacha kila mtu akicheka huku wanachungulia kwenye magari yao. Wakaanza kushangilia. Zinda akawapungia mkono zaidi ya mara tatu. Akimuaga Nanaa. “Daah!” Danny alisikitika.
“Sasa maua kayapata wapi?” Grace aliuliza huku anacheka. “Nakwambia jana katuzungusha mjinga yule. Halafu sasa mbishi. Hataki tumshauri, huku anauliza.” Walizidi kucheka. Waliendelea kuongea mpaka simu ya Geb ilipoanza kuita.
is mine - ni Wangu! Part 1, Sehemu ya 14.
H
|
Japokuwa alikuwa akichelewa sana kurudi nyumbani, lakini alihakikisha anakula kabla ya kulala. Nanaa alimsikia akimwambia mama yake kuwa anatumia siku hizo chache za juma, jumatatu mpaka jumatano kuweka mambo ya kazini sawa kabla hajasafiri, kwa hiyo atakuwa anachelewa kurudi. Wakaelewa kuchelewa kwake.
Heka heka
kabla ya Safari ya Moshi kwenye harusi ya Malii.
Siku moja kabla ya safari, yaani siku ya jumatano,
Grace alimwambia Nanaa wawahi kutoka ili wakajitayarishe na safari. Mara baada
ya kufika tu nyumbani Nanaa aliingia chumbani kwa bibi Fili hakumkuta.
Akampigia simu. “Natafuta
vitu vya kula Geb njiani. Bila hivyo hatakula kitu ataishia kunywa maji tu. Na
safari yenyewe ndefu.” “Afadhali. Wewe si umeshaweka mizigo yako tayari? Maana
Grace amesema tunaondoka alfajiri sana.” “Mimi safari ndefu siziwezi, mwanangu.
Magoti yananisumbua. Nitawafuata na ndege ya ijumaa asubuhi.” “Mama wewe
jamani! Kwa nini hukuniambia?” “Nilijua nikikwambia utagairi kwenda na wenzio.
Nenda kajichanganye bwana.” Nanaa akanyamaza. “Utakuwa sawa. Narudi muda sio mrefu. Ninamalizia.
Nikija tutakuja kuzungumza vizuri.” “Usichelewe mama bwana. Kwanza nishakosa
raha.” Bibi Fili akacheka na kukata simu.
Bibi Fili akarudi. Nanaa akatoka chumbani kwake
haraka baada yakusikia sauti yake, akamfuata chumbani kwake. Akamkuta bibi Fili
anacheka mwenyewe chumbani kwake. “Ujue
ulichonifanyia sio vizuri mama wewe!” “Ningekwambia ungekataa kwenda. Lakini
kesho kutwa tu mbona tutakuwa wote na wewe!? Kachukue chumba cha watu wawili.
Mimi nikitua tu uwanja wa ndege, nakufuata tukae wote.” Nanaa akajitupa
kitanda cha jirani akionekana kuishiwa nguvu. Walishazoeana na Bibi Fili,
wakawa kama marafiki wa karibu sana. Kila alipotongwazwa huko, alimwambia bibi
Fili na kumtaka ushauri.
Bibi Fili kwa muonekana alikuwa kama Grace,
mkimya. Lakini kumbe akiamua kukuzoea, alikuwa mzungumzaji mzuri tu. “Acha
wasiwasi wewe. Ngoja nikusimulie habari ya Viola. Leo Grace kanikumbusha wakati
nipo kazini mchana, tukacheka sana.” “Alifanyaje?” “Alikuja hapa kusalimia.
Akampenda sana Geb. Akahangaika naye wee. Kama unavyomjua Geb. Akiamua
kukupuuza, utachoka tu mwenyewe. Kila akijaribu hivi, Geb kimya kama hajui.
Akaona Geb hana muelekeo, akahamia kwa Danny.” Bibi Fili akaanza kucheka
yeye mwenyewe, Nanaa akimwangalia.
“Sasa akili za Danny wewe si unazijua? Akawa
mwanzoni hajaelewa kama Viola anamtaka. Mimi kama unavyonijua, mtazamaji tu.
Nikawa namuona vile anavyohangaika na hawa wanaume wa humu ndani. Safari za
humu ndani hazimuishi. Kila siku anakuja hapa nyumbani kusalimia. Akaanza
urafiki na msichana wa kazi wa humu ndani ili apate sababu ya kuja kulala hapa.
Safari za kulala hapa zikaanza. Habanduki. Si mchana si usiku yupo humu.
Anamuwinda Danny na Geb. Lakini Geb akawa ameshamjua, akawa anamkwepa.”
Nana alijisikia vibaya sana.
“Usicheke bwana mama!” “Subiri sasa. Alipoona Danny haelewi, si akaamua kumwambia wazi wazi. Akamfuata Danny chumbani kwao. Asubuhi alipoona Grace katoka tu, yeye akaingia na khanga moja chumbani kwao. Akajua Grace kaenda kazini, Danny kabaki peke yake huko chumbani. Akamtongoza Danny pale pale, akavua ile khanga ndani yupo uchi, akapanda kitandani. Acha Danny aanze kupiga kelele kama mtoto mdogo. Akamvutia chooni kwao, akamfungia. Yeye akaendelea kupiga kelele. Tukakimbilia chumbani kwao tukajua kuna hatari. Kufika huko chumbani, eti Danny amepanda kitandani amesimama kabisa juu ya kitanda anapiga kelele.” “Mama!” Nanaa akabaki anashangaa.
“Kwani yalikuwa madogo! Alituacha mimi na Geb tumechanganyikiwa. Tunamuuliza kwani kulikoni? Anasema anataka James aitwe haraka sana. Geb akampigia simu James akamwambia afanye haraka aje pale nyumbani.” Mama G alikuwa akisimulia huku anacheka. “Hatujakaa sawa Grace naye akarudi. Kumbe hakwenda mbali, alienda kutafuta kitafunio. Hivi anavyokwambia Danny walikuwa wasichana wawili na hakuna chakula, ujue hatanii. Mnarudi kutoka kazini, mnaishia kula chakula cha kununua, au ndio tuingie jikoni tuanze kupika. Kikija kuiva ni saa 4 usiku wote tumechoka. Tunataka kulala tu.” “Mbona Grace huwa anapika vizuri tu?” Nanaa akauliza kwa kushangaa.
“Wewe hujachunguza vizuri. Danny hataki awepo nyumbani eti mkewe yupo jikoni masaa kwa masaa! Heri akanunue chips yai, au aje na nyama choma au rosti, mle kuliko mkewe ashinde jikoni wakati yeye yupo. Hathubutu. Au yale mambo ya mkewe amuache kitandani asubuhi kama wanawake wengine. Aamke, amuache kitandani ili amwandalie kifungua kinywa, hataki. Anataka alale na mkewe, waamke, waoge pamoja, ndio waende naye jikoni. Apike kidogo tu, atoke wakae wote. Na kitafunio cha haraka anachopikaga Grace ambacho anajua hakichukui muda mrefu huko jikoni ni chapati za maji tu. Sasa na zenyewe huwa zinachosha. Akipika kitu kigumu, ujue Danny yupo kazini. Basi apike haraka, akirudi amkute amekaa kama vile. Sio eti hajamuona mkewe siku nzima wakiwa kazini, halafu aje hapa mkewe yupo busy jikoni, hapo hamuwezi kuelewana hata kidogo na Danny.” Nanaa akacheka.
“Basi, turudi kwenye stori yangu. Grace anamuuliza mumewe umeona nyoka? Anasema hapana. Nakwambia Danny anapiga kelele kwelikweli anamtaka James aje pale haraka. Wote tukaingiwa na wasiwasi tukasema labda kapatwa na kichaa. Bahati nzuri ilikuwa siku ya sikukuu, watu hawaendi kazini, hakuna foleni. Kwa hiyo James akaja kwa haraka akamkuta bado yupo juu ya kitanda. James anamuuliza vipi? Akaanza kumuuliza James kama anakumbuka vile alivyohangaika kumpata Grace. Sasa James anamwambia anakumbuka, kwani vipi? Danny kakazana, eti James atuelezee shida alizopitia mpaka akakubaliwa na Grace. Basi James akasimulia kwa kifupi wakati huo bado kasimama juu ya kitanda kabisa, hataki kukaa. Watu wote tumetoa macho tunamwangalia. Grace amemletea maji ili anywe, hataki. James akamaliza kusimulia huku anamkatisha kila mara anamkumbusha hiki au kile. Anamwambia anasahau. Basi James akawa anarudia kueleza mpaka akamaliza. Wote tumesimama tunataka kujua mwisho wa yote ni nini kinaendelea? Maana habari za Danny na Grace kila mtu anajua.” Mama G akacheka tena.
“Sasa kwa nini alitaka kaka asimulie tena?” Nanaa akahoji. “Sikiliza sasa. Baada ya kuridhika, akamwambia afungue mlango wa bafuni. James si akamkuta dada yake yupo uchi huko bafuni. Akafunga mlango haraka kwa mshtuko. Sisi hatuelewi. Tunamuuliza James, kwani kuna nini huko bafuni? James kakaa kitandani ameinamisha kichwa kama mgonjwa. Grace akamuuliza tena Danny. Safari hii kwa ukali. Si ndio akaanza kusimulia kisa kizima kuwa Viola amemfuata hapo chumbani anamtaka kimapenzi.” Nanaa akakumbuka vile Viola na Vai walivyorudishwa nyumbani kwa haraka wakati Nanaa alivyokataliwa kuja nao huku jijini kipindi amemaliza kidato cha 6.
“Danny akaanza, ‘Huyu mtoto anakichaa kibaya sana. Grace mwenyewe wala sijamfaidi. Yaani yale matusi yakunikataa wakati namtongoza wala bado hayajaisha moyoni, eti na yeye anataka kunitoa humu ndani! Unataka kuniponza wewe?’ Yaani badala ya kusikitika, tukajikuta wote tunacheka mbavu hatuna. Vile anavyosimulia na anavyotetemeka, utafikiri amepigwa shoti ya umeme. Grace akamuuliza sasa kwa nini anaongelea juu ya kitanda? Anasema alikuwa anaweka msisitizo, ili James aje haraka, amchukue mdogo wake pale ndani, asimletee balaa.” “Maskini kaka yangu.” Nanaa akamuhurumia James.
“Nakwambia James alitia huruma. Akawa mwekundu kama nyanya. Ungemuhurumia. Alikuwa hawezi kumtizama mtu machoni. Alijisikia vibaya sana. Ungekuwepo, ungemuhurumia zaidi. Aliomba msamaha kwa Grace, mpaka akapiga magoti. Sasa Danny naye badala amfariji mwenzie James, amekazana kumshtumu eti yeye ndio amemtuma mdogo wake. Basi James yupo amepiga magoti anatubu huku anajitetea na Danny naye anaendelea kumlaumu tu. Mpaka Grace alipomgombeza Danny ndio akanyamaza. Sasa jioni yake ndio tulicheka mpaka machozi.” Nanaa akajifunika uso wake na mto.
“Aibu gani hii! Sasa wewe mama ulipomuona mwanzoni akiwa anahangaika na Geb, kwa nini hukumkataza?” “Mimi! Akaa. Nanyamaza kimya, ili kila mtu yakija kumshinda baadaye asije nilaumu. Najiangalizia kimyaa kama sipo.” “Sasa na kwa Danny? Kwa nini hukumwambia mkewe?” “Niambiwe mchonganishi, navunja ndoa za watu!? Tena na Grace mwenyewe aliniuliza hivyo hivyo. Nikamwambia kama yeye anajidai yupo busy haoni na anashindwa kumchunga mumewe, atajijua mwenyewe. Viapo alitoa yeye mwenyewe kanisani. Halafu aje ashindwe kuvitekeleza, atake watu wote tumchunge mumewe! Aku. Apunguze shuguli, amlinde mumewe.” Nanaa alikuwa anacheka nakujisahau kama watu wengine wanawasikiliza.
Waliendelea kucheka mpaka Grace naye akaingia. “Jamani mnacheka nini? Niambieni na mimi.” “Acha umbea wewe Grace. Nenda kalale na mumeo.” Mama yao alimjibu. “Si mnisimulie tu.” “Acha umbea wewe mtoto. Danny atakuja sasa hivi kukufuata. Sitaki mnijalie humu ndani kwangu, nataka kulala. Ondoka. Nanaa na wewe nenda kamalizie kujiandaa. Acha kupenda umbea. Kwanza mimi natoka mara moja. Narudi tena dukani, kuna kitu nimesahau kununua.” Nanaa alitoka huku akiendelea kucheka.
**************************************************
Grace akarudi chumbani kwao alipokuwepo mumewe na Fili wakicheza tv games. Fili alikuwa akishangilia anavyomfunga baba yake. Ilikuwa game ya mpira wa kandanda. Walikuwa wakicheza wawili tu hapo chumbani. Nanaa akaingia chumbani kwake. Mama G, na yeye akaondoka na gari yake. Kulikuwa kumetulia sana. Bado Geb hakuwa amerudi kutoka kazini. Nanaa akaanza kuwaza afungashe nini cha muhumu.
Mara wakasikia mlango wakuingilia ndani unafunguliwa. Sauti ya Liz na Geb. “Nimekwambia usiwe na wasiwasi Liz. Kwa nini unataka kujinyima raha bure?” “Kwanza kwa nini tuondoke na gari tusipande ndege? Mimi sipendi wala sijazoea usumbufu.” “Tukiondoka na ndege, tutatumia usafiri gani kutuzungusha tukifika huko Moshi? Tumekubaliana na Danny mara baada ya sendoff, tuzunguke kidogo. Hata tukiweza twende mpaka Arusha. Tutakuwa wengi, nina uhakika utafurahia tu.” “Hayo ndio yanayonichosha. Watu wengi kila mahali! Hamna sehemu ya utulivu ya kwetu sisi wenyewe! Kila mahali watu. Na leo tena unasema tutakuwa na watu humo kwenye gari. Hamna sehemu ya kupumzika jamani!? Watu kila mahali!” “Tunaondoka na hii SUV ya viti nane. Na tutakuwa watu wa humu humu ndani tu. Hatuwezi kubanana.” “Kila mtu anaharufu yake Geb. Tukichanganya harufu ya kila mtu humo ndani kwenye gari, na safari yenyewe mpaka Moshi! Nitatapika njia nzima.” Liz aliendelea kulalamika.
**************************************************
Nanaa aliyekuwa chumbani kwake aliweza kusikia
kila kitu. Hakujua Grace na mumewe kama na wenyewe wanasikiliza. Hamu ya safari
ikamwisha kabisaaa! Akaamua asiende. Akaacha kukusanya vitu vya safari. Akaamua
asubiri patulie, atoke akapike chakula cha kula nyumba nzima usiku huo. Kwanza
safari yenyewe ni ya Moshi. Hakutaka kwenda tena huko na kujiongezea matatizo.
Geb alimwambia ajiandae kwenda kuandika historia mpya. Lakini mpaka hapo,
akajua historia lazima itajirudia tu. Asiongeze idadi kwenye gari ya watu na
kuongeza harufu nyingine. Akajituliza.
**************************************************
Bado Liz aliendelea kulalamikia hili na lile.
Kila Geb alipompa suluhu la lile, aliongeza tatizo jingine. Mara Nanaa akasikia
mlango wa chumbani kwa kina Grace unafunguliwa. Akajiweka sawa kusikiliza kitakachoendelea.
Ukimya wa Geb na Liz ukazuka. “Samahani Geb na Liz. Naingilia mazungumzo
yenu. Kama harufu unazozungumzia wewe Liz ni ya hii familia yangu na Nanaa,
wala kusiwe na shida. Danny ameamua tuendeshe gari yetu tu. Kwa hiyo nyinyi
nendeni wawili tu.” “Hata mkinielewa vibaya ni poa tu.” “Wala hakuna
anayekuelewa vibaya Liz. Sisi tunaelewa. Na tuna amani.” “Mnaelewa nini sasa?”
Liz aliuliza kwa ushari.
“Hivi mbona kama hujanielewa? Nimekupa suluhu ya tatizo lililokuwa likikukera. Tena kwa amani tu. Kwa nini unatafuta tatizo jingine? Kama hujaelewa chochote nilichosema tokea nimewafuata hapa, elewa hivi, sisi tutaendesha gari yetu. Mimi, Danny, Nanaa na Fili. Basi.” Grace alijaliwa sauti ya upole sana, japo ilisikika ya uvivu zaidi.
“Maana mnaweza msinielewe. Lakini mimi sijali.” Liz akaongeza. Grace hakusikika kujibu. “Kwanza nashangaa kwa kumbi zote zilizojaa hapa mjini eti mtu anaenda kufungia harusi au sijui sendoff huko milimani. Na sisi eti tunaenda! Kwa lipi hasa? Ndio maana nasema haya mambo yakuoa hujajiandaa kipesa sio mazuri. Harusi sio dharula. Ni kitu mtu anatakiwa kujipanga kabla. Sio kushikana mashati, eti mnachangishana!” Liz akaendelea.
“Watu wanawekeza mpaka kwenye misiba yao kabla hawajafa. Ili ukifa usisumbue watu na maiti yako. Sembuse harusi! Tena ya watu mnaokubaliana na kupanga tarehe! Panga harusi ukiwa na pesa yako sio unapanga harusi kwa pesa za watu wengina. Mtu akiwa na pesa yake si anatafuta ukumbi na hoteli sehemu za kueleweka? Kama ndugu zake wako mbali na mjini, anawaleta mjini na kuwaweka mahotelini. Harusi ikiisha kila mtu anarudi kwake, sio lazima kuendelea kufuatana nyuma. Hayo ndio maisha na hiyo ndio habari ya mjini. Sio mnafunga safari kufuata harusi ya kijijini! Kwa nini!? Mimi hata sielewei!” Nanaa alimsikia Liz akiendelea kulalamika. Aliongea kwa kutumia lugha ya kingereza kwa muda mrefu, huku akiweka maneno machache sana ya Kiswahili. Na kilikuwa kingereza kizuri. Maneno aliyatamka kifasaha kama mzawa wa huko nchini Uingereza. Nanaa akabaki akitamania.
Cha ajabu hakumsikia Geb, wala Grace wakijibu tena na wote walikuwa maeneo hayo hayo. Nanaa aliendelea kusikiliza maneno ya kingereza yanayotolewa kwa jazba. Mara akasikia hatua za Grace zikimfuata chumbani. “Nanaa!” Mlango ukafunguliwa. “Usiende kupika. Mama amesema atatuletea kitimoto na ndizi. Wewe endelea kujiandaa. Akirudi, nitakuja kukuita.” “Asante.” Nanaa akashukuru, Grace akatoka na sura yake tulivu. Akamsikia akiingia chumbani kwake. Kidogo wakasikia Geb na Liz nao wanaingia chumbani kwa Geb.
**************************************************
Mara akasikia gari ya bibi Fili. Nusura aruke
pale alipokuwa amekaa. Akaona atulie kwanza kwani alimsikia Fili akiwa
amefungua mlango kwa haraka, anakimbia huku akiita bibi Fili. Bibi Fili
akaingia. “Umeniletea pipi yangu?” Fili aliuliza. “Nipokee kwanza.
Mbona hivyo Fili?” “Nataka kujua kwanza bibi.” “Nimeleta.” Bibi yake
akajibu. “Hivi nilikwambia kuwa
nakupenda?” Fili akamuuliza bibi yake. “Mmmh!” Nanaa akamsikia bibi
yake ameguna, akacheka peke yake pale chumbani. “Kweli tena bibi Fili. Mimi
nakupenda sana.” “Wewe mapenzi yako hayatabiriki bwana.” “Mimi nakupenda wakati
wote. Ni mama tu ndio huwa ananilazimisha kulala naye. Lakini mimi ningekuwa na
lala na wewe kila saa.” Grace akatoka.
“Ujue wewe Fili nakusikia wewe! Na nisikuone kitandani kwangu tena. Ukalale huko huko unakomdanganya bibi yako.” Fili akaanza kucheka. “Basi bibi. Wewe tutalala wote kesho. Leo nalala na mama yangu.” “Kila siku habari ni hiyo hiyo. Mpaka ufukuzwe huko chumbani kwa watu, ndio kimbilio linakuwa mimi.” “Sasa si kwa sababu nakupenda wewe.” “Mmmh!” Bibi Fili akaguna tena.
“Nanaa yuko wapi? Mwiteni aje kula.” Aliposikia tu hivyo, akatoka haraka. “Halafu hii chupa mbona ina uji? Huyu Geb mbona hajanywa? Au hayupo? Lakini kama nimeona gari yake hapo nje!” “Yupo chumbani na Liz.” Grace alijibu huku akiandaa chakula. “Oooh!” Mama G akaitika. Nanaa akaingia. “Mbona sura imepooza tena, wakati nilikuacha na furaha?” Mama G alimuhoji Nanaa mara alipoingia pale jikoni. “Nimepata dharula mama. Naona sitaweza kwenda tena Marangu.” “Mmmh! Dharula hiyo dharula gani? Mbona gafla!? Nimekuacha hapa hata lisaa saa halijaisha, tayari umepata dharula!?” “Kweli mama. Natakiwa kwenda kuangalia chumba kesho. Dalali kanipigia simu sasa hivi. Kanipatia chumba.” Grace na mama yake wakabaki wakimwangalia Nanaa.
“Itabidi tu kwenda hiyo kesho. Lasivyo huyu dalali atakigawa chumba. Heri tu kesho nikifuatilie, nifunge mkataba kabisa.” Nanaa aliendelea kujitetea. Grace na mama yake wakaangaliana. “Basi kazi mtakuwa nayo huko njiani.” Mama G akasema. “Wala si kidogo.” Grace akajibu akikumbuka hasira za kaka yake, kama Nanaa asipokwenda. Lakini Nanaa hakuelewa ni nini wanachoongelea. Akanyamaza.
Danny akatoka. Wakaanza kula. Lakini kulikuwa na ukimya wa namna yake sio kama siku zote. Walikula kimya kimya mpaka wakamaliza. Kila mtu akaaga kuwa anakwenda kulala mapema tayari kwa safari kesho yake. “Msihangaike kuosha vyombo. Mimi nitaosha na kusafisha hapa. Nyinyi kawahini kulala. Mpumzike kwa safari kesho.” Nanaa aliongea huku akikusanya vyombo kurudisha jikoni. Danny na familia yake wakaondoka kuingia chumbani kwao. Bibi Fili naye akaingia chumbani kwake. Wakamuacha Nanaa.
**************************************************
Wakati Nanaa yupo jikoni, Bibi Fili akamfuata. “Geb
anatatizo moja.” Nanaa akageuka kumwangalia. Alikuwa anatoa uchafu kwenye
vyombo vichache walivyolia chakula, ili avipange kwenye dishwasher, akaacha. “Tatizo
gani?” Nanaa akauliza. “Unapomuahidi kitu, anapenda utimize. Ni heri
usimuahidi kabisa. Yaani ukiona hutaweza kufanya jambo analokuomba, ni heri
usimkubalie tokea mwanzo. Anaumia vibaya sana, ukiahidi halafu usitimize.”
Yule mama aliongea kwa kifupi tu, akatoka pale jikoni akamuacha Nanaa.
**************************************************
Nanaa alibaki akiwaza pale jikoni. Alijua wazi
mama yule anampa yeye ule ujumbe. “Sasa mimi nina umuhimu gani wa
kwenda jamani!? Si atakuwa na ndugu zake na mpenzi wake!? Mimi ninaulazima
gani?” Nanaa aliendelea kujitetea mawazoni. Akasikia Geb ametoka na
kuita. “Mama!” “Nipo huku chumbani.” Geb akaenda chumbani kwa mama yake.
Nanaa akaendelea kusafisha.
Baada ya muda akasikia mlango wa jikoni unafunguliwa. “Nanaa!” Akageuka alikuwa Geb na uso uliopooza zaidi si kawaida yake. “Abee!” Nanaa aliitika kwa upole. “Mama ameniambia hutuendi wote tena.” “Nilimwambia kuwa dalali alinipigia simu akaniambia kesho nikaangalie chumba.” “Ni kweli?” Geb akauliza, Nanaa akabaki kama amepigwa na butwaa. “Nanaa?” “Hapana sio kweli.” Nanaa akajikuta anajisalimisha.
“Kwa sababu yeyote ile, naomba usiche kwenda na sisi kesho. Tafadhali sana.” “Sawa. Lakini mimi naomba niondoke na kina Grace.” Geb akatulia kwa muda. “Pia itakuwa vizuri nikiwa nao, nitawasaidia swala la mtoto njiani.” “Ok.” Geb alijibu na kutaka kutoka. “Hivi mimi nina wazimu gani jamani!?” Nanaa alijiuliza moyoni.
“Geb!” Nanaa akamwita kwa upole na sauti ya chini. Akarudi. “Hujala leo. Naomba usilale bila kula.” Geb akabaki pale mlangoni, akainama kama ametingwa na mawazo. “Naomba nikuwekee kidogo tu, ukale hata chumbani. Usilale hivyo.” Kimya. “Najua umechoka. Lakini naomba ujikaze kunywa hata uji tu. Usilale na tumbo tupu.” Nanaa akaendelea kusisitiza. “Nakushukuru Nanaa. Asante.” “Kwa hiyo umekubali kula?” Nanaa akauliza, Geb akacheka kidogo. “Uji, tafadhali.” “Yes!” Nanaa akafurahi sana mpaka Geb akajua. Akacheka.
Kwa haraka kama asimcheleweshe kurudi huko chumbani, akammiminia uji kwenye bakuli kubwa huku Geb akimwangalia. Akamuwekea kwenye sinia lake pamoja na maji na matunda. “Ukimaliza wewe weka hata nje ya mlango wenu. Usihangaike kurudisha huku. Mimi mwenyewe nitakuja kutoa.” Geb akamtizama. “Asante Nanaa. Nakushukuru. Ila nitarudisha tu mimi mwenyewe. Wewe nenda kapumzike.” Akamkabidhi. “Usiku mwema Nanaa.” “Na wewe pia, Geb.” Akamtizama kidogo, nakutoka.
**************************************************
Nanaa aliamka alifajiri sana. Akamkuta bibi Fili
jikoni. “Hivi mama wewe ukoje lakini!?” Wakaanza kucheka. “Kwani mimi
nimesemaje? Si nilimwambia tu kuwa huendi!” “Sasa kwa nini umwambie?” “Ulitaka
kufanyeje?” “Nilipanga asubuhi hii wakati watu wote washapanda ndani ya gari
ndio niseme.” “Halafu mwanangu asafiri bila raha? Aka mwenzangu! Ndio kiziwanda
changu huyo.” “Sasa mimi nina umuhimu gani huko kama sio kuongeza tu idadi!?”
“Bwana wee, wewe nenda bwana. Tena mumeo Zinda atakuwepo huko huko.”
Walianza kucheka mpaka wakajisahau.
“Mtoto mbaya wewe? Sasa kwa nini ukatae gari?” “Sio gari tu mama na wewe, na nyumba!” Nanaa akaongeza. “Gauni.” Mama G akaongeza. “Na viatu mama! Kwa raha zangu.” Nanaa alitembea mbele ya Mama G, huku anaringa kidogo. Yule mama akawa anacheka. “Nanaa wa dhahabu!” Mama G akaongeza. “Kumbe! Sasa hivi ningekuwa nimejaa madhahabu. Shingoni na mkononi.” Bibi Fili na Nanaa waliendelea kucheka pale jikoni mpaka wakaamsha kila mtu.
"Hivi nyinyi huwa mnacheka nini hakiishi jamani!? Mnajua saa hizi ni saa ngapi?” Grace aliingia pale jikoni. “Umbea wako ndio umekuamsha wala sio sisi. Usiye lala na mumeo ukatulia ndani ni nini?” “Kelele.” Grace akamjibu mama yake. “Mama huyo!” Nanaa akajitetea. “Aliye na kazi ya kucheka hapa jikoni ni nani kama sio wewe Nanaa? Acha kunisingizia bwana.” Grace alianza kusaidia kazi pale jikoni.
“Heri huyo Geb mumtengenezee uji mwingi.
Hatakula njia nzima.” Grace aliongeza. “Mama amemnunulia vitu vya kula
njiani. Karanga na korosho.” “Nitamtengenezea na fruits salad. Akale mbele ya
safari. Naomba msisitize. Unanisikia Grace? Lasivyo mtafika mmwage vyakula
vyote.” “Wewe mwekee kwenye cooler box na hotpot. Unamjua Geb. Akiwa na hasira
anaweza asile njia nzima. Akiwa anakupigia simu msisitize wewe mwenyewe. Mimi
anaweza hata asinijibu. Si unamjua mwenyewe?” “Bora viingie kwenye gari.
Nitakuwa nampigia mwenyewe nimkumbushe. Na wewe Nanaa naomba uwe unamkumbusha.”
“Kwani Nanaa anaenda tena!?” Grace akashangaa.
Mama G akaanza kucheka. “Si mama huyo!” “Alimuahidi yeye mwenyewe huyo Geb.” Mama G akaongeza. “Na ukimuahidi Geb kitu, lazima utimize. Ni heri kama huna uhakika, umkatalie tokea anakuomba. Anaumia sana ukija kubadilika baadaye. Na yupo hivyo tokea mtoto.” Grace aliongea kama mama yake. “Lakini nimemuomba tuondoke wote. Nipande gari yenu nyinyi.” Nanaa akaongeza. “Mmh! Mbona tena mnaendesha magari mawili wakati aliniambia mtaondoka na gari ile kubwa. Kwa nini kumkimbia mziwanda wangu!?” Grace na Nanaa wakaangaliana. Kisha wakanyamaza. “Nishaelewa.” Mama G, alijua tu baada ya Grace na Nanaa kuangaliana. Wakanyamaza.
**************************************************
Harufu ya manukato ya Liz ikaanza kuenea taratibu
pale ndani. Akatoka na funguo zake. “Nakwenda kuhamisha mizigo yangu kwenye
gari yako.” Walimsikia akimuaga Geb. “Sawa. Lakini si utarudi ndani ili
tunywe kwanza chai?” “Sio lazima.” Liz akajibu na kutoka nje. Geb akaingia.
“Shikamoo mama.” Akamsalimia mama yake. “Marahaba. Mlilala salama?”
“Ndiyo. Za asubuhi?” Akiwa anamaanisha salamu kwa Nanaa na Grace. “Kwetu
tumeamka salama.” Grace akajibu huku akitoka. “Ngoja nikamuamshe Fili,
tujiandae na sisi tuondoke.” “Si tutaongozana?” Geb akamuwahi dada yake. “Vyovyote
tu. Hamna shida. Ila ujue sisi bado. Mpaka huyu kaka aoge, tulazimishane kula,
na mimi nijiandae, tutawachelewesha.” Grace akajibu. “Hamna tunapowahi.
Vizuri tuondoke kwa pamoja.” Geb akajibu.
“Mimi sipendi safari za jua kali. Hasa kama tunaendesha. Heri kama ingekuwa tuna fly na ndege.” Liz aliingia na kuingilia mazungumzo ya Geb na dada yake. “Basi nyinyi wahini. Tutakutana Moshi.” Grace akajibu kwa upole na kuondoka. “Tutaondoka pamoja. Tutawasubiri tu.” Geb alijibu akionekana kama na yeye amekasirika kidogo. “Geb! Nimesema sipendi jua.” “Nashauri uchukue ndege ya kesho utufuate Liz. Nitakuja kukupokea KIA. Itakusaidia kufika ukiwa umetulia. Sidhani kama upo tayari kwa safari ya gari.” Ukimya mkubwa ukatanda.
“Kwa hiyo hutaki kuendesha ukiwa na mimi?” “Tunakwenda kwenye jambo la furaha Liz. Sendoff ya mchumba wa Malii. Malii ni rafiki yetu wakaribu sana. Mimi, Zinda, James, Danny, Gozi na wengineo. Yupo kwenye maisha yetu tokea tupo sekondari. Kwakwe Marangu sio mbali, wala sio mlimani. Anakwenda kwa mwanamke anayempenda na ameomba tumsindikize tuungane naye katika furaha hii ya kwenda kukabidhiwa mke kimila. Kwa upande wa bibi Fili, Malii ni mtoto wake. Japokuwa anaumwa magoti, lakini amekubali kwenda kuungana naye. Sitaki sisi tufike pale tukionyesha sura za adhabu. Ni bora tusiende, au twende lakini tukiwa na furaha.” “Kwa hiyo unataka mimi nisiende?” Liz akauliza kishari.
“Hilo ni swali ambalo ukipenda, utanipa jibu baadaye kama uliamua kuja na ndege au la. Lakini mimi nitaondoka na gari kubwa, pamoja na kina Danny. Unanijua mimi huwa sio mtu wakubadilika badilika Liz. Nilipewa na Danny jukumu lakufanyia hiyo gari service ili iwe tayari kwa safari. Nimefanya hiyo kazi. Leo asubuhi siwezi kuamka eti nimwambie Danny apandishe familia yake kwenye gari ambalo halijafanyiwa service kwa safari ndefu, halafu eti mimi na wewe tunaendesha gari lenye viti nane! Tupo peke yetu njiani! Si sawa na sitafanya hivyo. Nashauri uje na ndege. Na kama utapata gari ya kukodisha pale uwanja wa ndege, uchukue utufuate Marangu au ukitaka mimi naweza kukufuata. Huna haraka ya kuamua. Utanijulisha kwa simu.” Watu wote walikuwa kimya.
Nanaa alipomsikia Geb ameweka tu kituo kwenye maongezi yake, akatoka pale jikoni kimya kimya, akarudi chumbani kwake akinyata. Mama yao alikuwa akiendelea kupika huku akitayarisha matunda. “We Geb! Hebu kaniletee ile cooler kutoka kwenye gari yako. Nataka niweke kila kitu tayari. Nisiwacheleweshe.” Mama yake akamtuma kwa kuamuru kidogo. Geb akajua ameshakasirika na yeye. Alisikika kwa sauti ya amri, wala si utani kama alivyokuwa na Nanaa pale jikoni. Geb akatoka. Wakasikia Liz anatoka na yeye.
**************************************************
Nanaa akaingia kuoga haraka haraka akaanza kuvaa.
Wakati anamalizia, Geb akaingia. “Nimefuata mzigo wako. Umeshaweka kila
kitu?” “Nafikiri kila kitu kipo tayari.” Nanaa alijibu huku akiangaza kama
kuangalia kama amesahau kitu. “Nataka nikapange kwanza mizigo yote kwenye
gari.” “Umeshakula?” “Nitakula nikiridhika kila kitu kipo kwenye gari, hasa
mizigo yako wewe.” Nanaa akacheka. “Hukawii kubadili mawazo wewe!”
“Sibadiliki tena bwana.” “Wewe nipe mzigo nikaweke kwenye gari ndio tukae chini
tule.” Nanaa akamalizia kuweka vitu baadhi, akafunga sanduku hilo dogo, Geb
akatoka nalo.
Walikaa wote mezani, wakaanza kula. Kilikuwa
kifungua kinywa kikubwa kama chakula cha mchana. Nyama iliyokuwa imebakia jana
yake, ilipashwa moto. Kukawepo na chapati nzuri sana za kusukuma. Mchuzi wa
maharage na chai iliyowekwa viungo. Baadhi ya matunda aliyobakisha Mama G,
baada ya kumuwekea Geb ya kula safarini, aliyaweka hapo mezani. Geb alikunywa
uji wake kama kawaida yake. Mama yao akawaambia lazima waombe kabla ya safari.
Wakashikana mikono, bibi Fili akaomba. Safari ikaanza.
Safari ya
Moshi kwenye harusi ya Malii.
Alikuwa akiendesha Geb. Akakaa mbele yeye na
Danny. Nanaa na Grace walikaa kiti cha pili, Fili katikati yao. Kwa kuwa Liz
hakuwepo, wakalaza viti vya mwisho kabisa. Wakapanga mizigo yao humo nafasi
ikawepo tu yakutosha. Waliondoka jijini saa 11 asubuhi. Hakuna aliyeuliza alipo
Liz wala Geb hakutaka kuzungumzia hilo. Walipoanza kuliacha jiji la Dar,
wakaanza kupigiana simu na kukubaliana wasubiriane mjini Kibaha ndipo waendelee
na safari.
Walipofika Kibaha, wakatafuta mahali wakaegesha
magari yao. Nanaa alishangaa kuona magari zaidi ya nane yakiwa yanaongozana
kumsindikiza Malii kumchukua mke Marangu. Geb na Danny wao ndio walishuka
kwenye gari kuzungumza na wenzao. Baada muda mfupi sana wakarudi ndani ya gari
safari ikaanza tena. Nanaa alianza kusikia baridi. Geb aliwaomba radhi kwa kuwasha
AC kali. Akasema kila akiendesha anapenda kuwe na baridi kwenye gari, ili
asilale. Walimvalisha Fili sweta, Nanaa akajifunika mtandio wake, akalala.
Danny na Geb ndio walikuwa wakiongea njia nzima
huku wanacheka. Nanaa alishtuka kutoka usingizini baada ya Danny kucheka kwa
sauti. Akatoka ndani ya mtandio wake taratibu, akamkuta Grace ametulia kama
hayupo pale. “Mama alisema tumkumbushe Geb kula karanga au ndizi za kuiva.
Hakunywa uji mwingi.” Nanaa alinong’ona. “Nilisha sahau.” Grace
alijibu na tabasamu. Akachukua ndizi, akamenya kidogo akamgusa kaka yake
mgongoni. “Chukua hii ndizi ule.” Geb akapokea. “Asante. Nilifikiri
umelala.” “Nasinzia tu lakini usingizi hauji. Danny anacheka kwa sauti kweli!”
Grace alilalamika. “Mmmh! Wewe si mlalaji bwana. Mbona mwanangu kalala?”
“Nina usingizi sana. Lakini wewe ndio unaniamsha.” “Eti Nanaa?” Danny
alimchokoza Nanaa. Nanaa akabaki akicheka bila kujibu. Akajirudisha ndani ya
mtandio wake akarudi kulala.
Aliamka tena walipofika Chalinze. “Kuna anayetaka kujisaidia tusimame?” Geb akauliza. “Nanaa!” Grace akamwita. Sio kwamba hakuwa amesikia. Lakini aliamua anyamaze tu ndani ya mtandio wake. “Unataka kushuka?” “Mimi nipo sawa.” Nanaa akamjibu Grace taratibu kama kunong’ona. “Hata mimi nipo sawa tu.” Grace akaongeza. “Maadamu huyu amelala, kanyaga mafuta twende. Akiamka ndio tusimame acheze kidogo ndio tuondoke.” Danny na yeye alijibu huku akimwangalia mwanae aliyekuwa amelala kwenye kiti chake. “Ngoja aamke hapo, maneno yatakuwa mengi mpaka tufike. Kila kitu anajua yeye.” Mama yake aliongeza huku anamfunika vizuri.
“Dume la nguvu hilo. Limempita mbali sana Zinda.” Kila mtu alianza kucheka mpaka Nanaa. “Hovyo kweli Zinda. Sijui yukoje bwana!” “Nimemuona kapendeza kweli.” Grace akaongeza. “Jana kanunua nguo mpya eti kwa ajili yakuvaa leo na kesho ili Nanaa amuone. James anamwambia ajifunze kuongea kwanza. Anasema eti kizuri chajiuza. Atamfanyia action Nanaa mpaka amkubali mwenyewe.” Kila mtu alikuwa anacheka.
“Sasa ngoja tukaone fujo zake huko Moshi.”
“Wala hatutafika Moshi. Subiria tu, utamuona.” Danny alimjibu mkewe. “Katuzungusha
jana kama wendawazimu. Mpaka James akaamua atuache madukani. Eti anatuambia
tumwangalie kwa jicho la Nanaa. James anamwambia hatuwezi. Yeye achague nguo
anazotaka, tuondoke. Kanunua suti ya pesa kibao sababu ya Nanaa. James
anamuuliza atakula nini kama anatupa pesa yote hiyo kwenye suti? Akatuambia
hiyo ni pesa iliyokuwa imetengwa maalumu kwa ajili ya pombe kwa mwaka mzima.
Sasa ndio ameamua kuwekeza kwenye muonekano wake mpaka ahakikishe amemuweka
Nanaa ndani.” Walizidi kucheka.
“Zinda ni chizi jamani! Sasa magauni na viatu vya Nanaa?” Grace aliuliza huku wote wanacheka. “Wewe utamuweza Zinda na fujo zake. Fujo tu. Alikuwa anasema kuanzia sasa, matendo yake yataongea. Hataki tena maneno mengi.” Waliendelea kuongea na kucheka mpaka walipofika Segera wakaamua wote wasimame.
**************************************************
James na yeye alikuwa kwenye msafara. Alipanda
gari moja na Malii, Zinda, Kamali, na Jonas. Walifika Segera bado ni mapema tu.
Wengi wao wakataka wapate supu. “Utataka kula kitu?” Grace akamuuliza
Nanaa. “Bado najihisi tumbo limejaa.” “Hata mimi.” Grace aliongeza. “Tushukeni
tunyooshe miguu. Tumuamshe Fili ajisaidie kabisa.” Danny alishuka akaja
upande wa mkewe. “Shuka nikusaidie kumbeba huyo.” Grace akashuka
akampisha mumewe. Akamfungua mkanda mwanae, akamtoa pale kwenye kiti chake
akamuweka pembeni ili aamke. Fili akafungua macho. “Vipi?” Baba yake akamuuliza.
“Namtaka mama.” “Mama yako huyo hapo chini ya gari. Twende.” Fili
akachungulia kuhakikisha, akamuona mama yake ndipo akatulia.Wakaondoka Danny na
familia yake.
**************************************************
Wakabaki Geb na Nanaa mle ndani ya gari. “Twende
Nanaa.” Geb alizima gari akamgeukia. “Naona nyinyi nendeni tu,
mimi nitabaki humu humu ndani ya gari.” “Kwa nini?” Nanaa akakosa jibu. “Twende
tukakae na wenzetu. Usikae humu ndani peke yako.” “Nikuwekee matunda ule?”
Geb alifikiria kidogo. “Au nikupe korosho?” Nanaa akaongeza swali
jingine kabla Geb hajajibu. “Naomba korosho tafadhali.” Nanaa akafungua
mfuko maalumu aliotayarishwa na mama G, kwa ajili ya mwanae huyo anayesumbua
kula. Akatoa korosho, akampa. “Mbona nyingi?” Geb alilalamika kidogo huku
akipokea. “Unahitaji kula Geb. Hukunywa uji vizuri, na wewe unaendesha
safari ndefu. Utachoka. Kula tu, zikibaki nitarudisha. Chukua na hili kopo la
soda.” Geb alitoa tabasamu na kupokea. “Asante. Twende basi.” Geb
akasisitiza.
Geb akamwita wakati anafunga mfuko. “Nanaa!”“Abee!”
Nanaa akaitika na kumwangalia. “Nimefurahi umekuja.” Nanaa akainama huku
anacheka. “Twende.” Nanaa akashuka akawa anamfuata Geb kwa nyuma yake
kidogo.
**************************************************
Mara akasikia watu wanacheka. Akaangalia pembeni
akamuona Zinda anamsogelea na maua mkononi. Nanaa alitamani kugeuka upepo. Kila
mtu alikuwa anacheka huku wakiwaangalia. Akasimama, Zinda akamsogelea mpaka
pale. “Haya ni yako Nanaa.” “Acha kupiga goti kama mtoto wa kike Zinda! Wewe
ukoje bwana?” “Sijapiga goti bwana Danny.” Zinda akajitetea. “Umepiga
goti, wote tumekuona.” Kila mtu alimshambulia Zinda. “Tumekuona bwana,
acha ubishi Zinda. Magoti kama mtoto wa kike!” James alikuwa anacheka sana.
“Usicheke James. Anatia aibu kweli!” “Sikujua kama hali ni mbaya hivi! Na
hapo kanywa bia mbili za haraka haraka, akafunga na tai, ili aweze kutoa hayo
maua.” James aliongeza nakufanya watu wacheke upya, Danny akabaki
anatingisha kichwa.
“Sasa kutoa maua tu, unakunywa bia mbili na
kufunga tai. Siku ya kumkabidhi hilo gari si utafunga baa zote mjini?” Kila
mtu alikuwa anacheka. “Daah! Hapa kazi ipo.” Grace alikuwa anacheka
mpaka anafuta machozi. Nanaa akamtizama Geb. Akakuta anamwangalia kwa utulivu.
Macho yao yakagongana. Nanaa akainama.
Walio oa walikuja na wake zao. Kila mtu alikuwa anacheka. “Danny wewe tumetoka mbali sana ndugu yangu. Ukilikumbuka hilo, utanisaidia nimalize hii shuguli yote kwa haraka.” “Unataka nikutongozee Nanaa?” “Kwani mimi nachagua msaada kaka? Chochote tu napokea, ilimradi nimwingize Nanaa ndani.” Watu walizidi kucheka.
“Maua yenyewe hujapokelewa. Anza kwanza kwa kutoa maua. Tuanzie hapo. Usipige goti wala usiongee maneno mengi. Wewe mkabidhi maua kiume.” “Hilo mbona rahisi.” “Mpe sasa.” Zinda akajiweka sawa. Alikuwa amevaa suruali ya jinsi ya bluu, na shati la mikono mifupi. Akafunga na tai. Vyote vilionekana vipya. Na wala hakutisha. Nywele zilinyolewa vizuri. Wazi alionekana alikuwa saluni siku iliyopita.
“We Zinda! Nini bwana? Umeng’ang’ania maua kama wewe ndio umepewa?” “Danny naye hana subira! Acha nikusanye nguvu, kaka!” “Basi sisi tunaondoka. Hatuwezi kulala hapa Segera.” Kila mtu alikuwa anacheka. Walikuwa wametoka kwenye magari yao, wanaangalia vituko vya Zinda na Danny.
Danny akamsogelea akiwa bado amembeba mtoto wake, akampiga ngumi ya begani. Maana alibaki kama ameganda. “Zinda!” Danny akamwita kwa ukali. “Nanaa! Nanaa mama watoto..” Zinda akaanza tena. “Anaanza kuharibu tena!!” Danny alimkatisha. “Danny mbona huna subira kaka? Naanzia mbali. Subiri. Nitashika tu kasi.” “Sasa Nanaa mama watoto ndio nini Zinda? Mpe maua. Basi.” Kila mtu alikuwa akicheka sana.
"Mimi naona hili zoezi tuliahirishe. Mnamchosha dada yangu bure.” “Mimi si nilikwambia James? Akawa ananibishia, anasema nimeongeza. Sasa umeona mwenyewe?” “Kweli hii aibu ya mwaka!” “James! Mimi na wewe tumetoka mbali sana mtu wangu. Usininyime dada yako.” “Nanaa huyo hapo. Hujanyimwa chochote.” “Basi ngoja nikaongeze bia nyingine narudi sasa hivi.” Zinda akaondoka na maua yake mkononi. Watu walizidi kucheka.
Baada ya utani wa muda mrefu, huku Geb akicheza
mpira na Fili akiwa kama hayupo pale. Bila kuchangia neno lolote bali kumtizama
tu Nanaa, wakaamua waondoke tena. Wakati Geb anawasha gari Zinda akawakimbilia.
“Danny! Washikaji wameniambia kama haya maua hataondoka nayo Nanaa hapa,
basi mimi nipande tu basi niwafuate. Wamenishusha kwenye gari yangu bwana!”
“Sasa hapa kwangu unataka nini wakati Nanaa yupo hapo kiti cha nyuma? Wewe mpe
bwana tuondoke. Unatuchelewesha.” Wakasikia honi. Wakajua wanampigia Zinda.
Zinda akakohoa mara kadhaa. Akatoka pale kwenye
dirisha la mbele alilokuwepo Danny, akarudi dirisha la nyuma alilokuwepo Nanaa.
Akakohoa tena. “Sasa Nanaa, ni hivi. Moyo wangu umevutiwa sana na wewe.
Pokea maua haya, ishara ya upendo wangu kwako.” “Daah! Malii hana mistari
yakusema siku ya harusi yake.” Danny alifanya Geb na Grace waanze kucheka.
“Nanaa! Naomba pokea tu hayo maua. Lasivyo tutalala hapa.” Danny alimgeukia
na kumsihi. Nanaa akayapokea. “Asante Zinda.” Nanaa alishukuru huku
anacheka kwa aibu.
“Umeyapenda mama watoto wangu? Eti Nanaa?” “Nimeyapenda ni mazuri.” Nanaa alijibu huku akiyaangalia yale maua. “Basi moyo wangu umefurahi sana. Nime..” “Aaaahhh.” Danny alikohoa kwa kumkataza. Zinda akatulia kidogo. “Au nihamie humu kwenye gari yenu ili niwe na Nanaa?” “Hapana Zinda. Ondoka. Hatukutaki humu ndani. Tena ondoka haraka kabla hujaharibu zaidi. Toka, rudi kwenye gari yenu.” “Sawa kaka.” Zinda akaondoka akaacha kila mtu akicheka huku wanachungulia kwenye magari yao. Wakaanza kushangilia. Zinda akawapungia mkono zaidi ya mara tatu. Akimuaga Nanaa. “Daah!” Danny alisikitika.
“Sasa maua kayapata wapi?” Grace aliuliza huku anacheka. “Nakwambia jana katuzungusha mjinga yule. Halafu sasa mbishi. Hataki tumshauri, huku anauliza.” Walizidi kucheka. Waliendelea kuongea mpaka simu ya Geb ilipoanza kuita.
**************************************************
Ikaita tena, akapokea. “Nimepata
ndege. Naondoka mchana. Itabidi uje unipokee.” “Sisi bado tupo njiani Liz.”
“Mnategemea kufika saa ngapi?” Liz
akauliza. Geb akafikiria kidogo. “Geb!”
Liz akaita. “Sijui. Sina hakika.
Lakini nashauri kama utawahi kufika kabla yetu, chukua taksii ikupeleke mpaka
Marangu hoteli. Sisi wote tumekubaliana kukutana hapo. Ila sisi tukiwahi
kufika, nitawashusha hawa hotelini kisha nitakufuata uwanja wa ndege.”
“Ningependa wewe unifuate Geb.” Liz aliongeza. “Sawa. Nitajitahidi nisikuweke sana hapo. Uwe na safari njema utakapo
anza safari.” “Asante.” Liz akajibu, na
kukakata simu. Pakazuka ukimya. Nanaa akajirudisha ndani ya mtandio wake, akanyamaza.
**************************************************
Ndio kwanzaaaa mambo
yameanza. Je, historia mpya ya Marangu imeanza kuandikwa njiani?
v Geb anaeleza
furaha yake kwa Nanaa. Safari imeanza kwa utulivu, Nanaa akiwa nyuma yake. Je,
furaha hiyo itadumu? Atafanyaje na wanawake wawili kwenye hoteli moja huko
mjini Marangu?
v Zinda naye
amegaramia sana hiyo safari kwa ajili ya Nanaa. Mipango mingi aliyoipanga na
James kaka yake Nanaa, pamoja na Danny kwa ajili ya Nanaa tu. Ameanza kwa maua.
Huku muonekano ukikubali kumuuza. Je atafanikiwa?
v Baada ya
kuombwa na Danny, Nanaa ndio akapokea maua kutoka kwa Zinda, macho kwa Geb. Wanaume
wawili mbele yake. Zinda anayemuhangaikia na muwazi mpaka kwa kaka yake, au Geb
mpenzi wa Liz?
v Liz naye mwenye
mpenzi, yupo angani kumfuata mpenzi wake huko mjini Marangu. Hachezi mbali na
Geb. Amekaba kila mahali. Japo hafurahii kuwepo huko, lakini ameamua kwenda tu.
Je, nani ni
wa nani? Nani atammiliki nani huko waendako? Nini kitatokea?
Usikose Visa
na mikasa ya mjini Marangu kwenye Sehemu ya 15.
0 comments: