Nilipotea! Part 4 - Sehemu ya D
Akabaki
bibi Cote na Net akiwa ameshachanganyikiwa. Maya naye akasogea. “Amesemaje?”
Maya akauliza. Kimya. “Net?” Bibi yake naye akamuuliza. Mbali na salamu, na
maneno machache sana ya kiswahili ni kweli yule bibi hakujua kiswahili kingi.
Net alimtisha tu Tunda kumwambia asimtete bibi yake.
“Amekwambia
nini?” Bibi yake akauliza tena kwa msisitizo. “Ameongea mambo mengi mabaya na
kunitisha, Nana. Ila amesema nikimuoa Tunda leo, ndio mwisho wa yeye kuitwa
Cote, na..” Net akashindwa kujizuia na kuficha ukweli lakini si kwa undani sana.
“Sidhani
kama tatizo ni kutokuambiwa mapema. Tatizo ni yeye kutokuwa tayari kushiriki
ufamle wake na Tunda.” Bibi yake alijibu hivyo. “Nitafanyaje Nana? Nimeingiwa
na hofu.” “Siwezi kukwambia nini chakufanya Net. Yeye ni mama yako, na unaishi
maisha yako. Uamuzi ni wako. Nimeishi maisha yangu kwa miaka 80 sasa. Unafikiri
najali wapi nitalala usiku wa leo?” Net akavuta pumzi.
“And
for me, I support you 100% Net. Kile utakachoamua, nitakuwa nyuma yako kaka
yangu. I love you and I have never doubt your decisions.” Maya akamtia moyo
kaka yake. “Thanks Maya.” Akamgeukia
bibi yake. “I love Tunda, Nana.” “Basi muoe.” Bibi yake akampa huo ushauri.
“Itakuaje
kuhusu mama?” “Huwezi kutatua matatizo yote sasa hivi hapa tuliposimama na
Tunda yupo ndani ya gari akisubiri. Ni aidha uende ukamwambie unaaihirisha
harusi mpaka wewe na mama yako mtakapowekana sawa, au mfunge ndoa kisha mtajua
kitu chakufanya baada ya hapo. Lakini kama alivyosema Maya, hata mimi sijawahi
kutilia mashaka maamuzi yako. Na nitakuwa na wewe katika kila maamuzi
utakayochukua. Lakini lazima uamue sasa hivi, kwa sababu Tunda hatakusubiri
milele.” Bibi Cote alimaliza kwa maneno hayo, akarudi kukaa sehemu ambayo
iliandaliwa sababu ya harusi. Maya akamfuata bibi yake nyuma wakamuacha Net
amesimama.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Net
akajua ndio amepewa nafasi ya kuamua mwenyewe. Akamkumbuka Gabriel
anavyomsubiria Tunda kwa hamu. Akajua akiahirisha yeye siku hiyo au kushindwa
kwake kumuoa Tunda siku hiyo ndio kumfikisha Tunda kwenye ndoa na mwanaume
mwingine, hasa Gabriel ambaye ameshakuwa na mahusiano ya karibu sana na Tunda.
Na asipomuoa Tunda siku hiyo, atamuoa lini?
Mama yake amemkataa Tunda kabisa. Si wakumkubali kesho wala kesho kutwa. Hakuna
jinsi atakuja kumkubali Tunda. Na ameshampa shutuma za wizi. Kisheria ni kweli
japo nyumba ilikuwa yake. Amchague nani, Tunda au mama? Net akabaki akiwaza
palepale alipoachwa amesimama.
“Lakini atanifanya nini hata nikimuoa Tunda
leo? Nitakuja kumbembeleza wakati mwingine. Nitamuacha hata kwa mwaka mzima,
halafu nitamtafuta. Nikishamuoa Tunda, tutahamia nchini Canada, nitarudi
kuzungumza na mama wakati mwingine. Hata iweje, hawezi kuja kunishitaki kwa
kosa la wizi” Net akafikia maamuzi hayo akijiaminisha kwa
umbali aliofika na mama yake. Aliacha mengi maishani kwa ajili ya mama yake. Amemfanyia
mengi makubwa. Akajiaminisha hawezi kumtenda vibaya. Watayamaliza tu.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Aliponyanyua
kichwa, akakuta kila mtu anamtizama yeye pale aliposimama. Ilishafika saa 11
kasoro jioni. Mchungaji akamsogelea. “Kila kitu kipo sawa, Net?” “Kila kitu
kitakuwa sawa. Naomba tuanze.” “Unauhakika Net? Maana tunaweza kuahirisha ili
uweke mambo ya familia sawa.” “Familia ni hii ninayotaka kuianzisha leo, baba
Penny. Nisipomuoa Tunda leo kwa hili, najuaje kesho?” Net akauliza, lakini
akionekana ametingwa kweli. “Sawa.” Wakarudi pale sehemu waliyokuwa
wameandaliwa kufungishiwa harusi, baba Penny akampigia simu mkewe kuwa wanaweza
kuingia.
Nyimbo
zilizoanza kupigwa, zikaanza kumtuliza Net. Wakaingia hao watoto wa kike
wakimwaga maua. Penny alionekana amechangamka sana, akaja mama yake Tunda. Tom
alikuwa amesimama na yeye mbele na mchungaji, pamoja na bwana harusi na yule
mfungisha ndoa wa serikali. Akaingia Tunda na mama Penny akimsaidia kuweka sawa
shela yake. Kulikuwa na wachukua video na wa piga picha. Macho ya bibi Cote
yakarudi kwa Net, akamuona anatoa tabasamu baada yakumuona Tunda. Wakamuona
anajifuta machozi mara kadhaa. Bibi yake akamuhurumia sana Net. “She loves her
so much.” Maya akasikika akisema ni kweli kaka yake anampenda sana Tunda.
Tunda
alipofika karibu na ile sehemu yakufungia harusi, Net akashuka pale na
kumpokea. Akamshika mkono. Akaubusu. Tunda akacheka. “Nakupenda Tunda.”
Alijikuta akiongea Net bila kujizuia au kwa sauti ya chini. Aliongea kwa wazi
kabisa. “Na mimi nakupenda Net.” Naye
Tunda ndani ya shela akajibu taratibu na tabasamu usoni. Net akataka kama
kumbusu, akajirudi. Watu wakacheka.
Ilikuwa
harusi ndogo. Watu wachache na tulivu. Kule kumuona Tunda kulimfanya asahau
kila kitu hata kama mama yake alitoka hapo na vitisho, Net hakuwa akikumbuka.
Mabusu kwa Tunda hayakuwa yanaisha. “Naona muondoke tu.” Bibi yake alifanya
kila mtu acheke. Na kweli. Hawakukaa hapo muda mrefu. Baada ya kukata tu keki,
Net akacheza mziki na bibi yake, wakaagana moja kwa moja kwa makubaliano yakuja
kuonana tena nchini Canada. Net na Tunda wakaondoka.
Honeymoon
ya Tunda na Net. Kwenye Resort ya nguvu jijini.
H |
awakwenda mbali sana kwenye
mapumziko yao. Kutoka hapo Salasala ilipokuwa nyumba ya Net, wakaelekea kwenye
hiyo Resort ambayo Net alichagua. Tunda alifurahia sana yale madhari. Alikuwa
ameandaa nguo za mapumziko ya juma nzima.
Tunda
alikusudia kupumzika haswa. Alifanya kazi mfululizo kuanzia anatua jijini
kutokea jijini Arusha. Miaka miwili bila mapumziko, mfululizo. Kama si kupamba
kwenye kumbi basi yupo ofisini kwake au kanisani. Hata hiyo week ya harusi pia
alikuwa na kazi mbili. Hakuziacha hizo za katikati ya juma. Alifanya ili
kutimiza lengo alilokuwa nalo. Kupata pesa kamili ya kumkamilishia mama yake
kodi ya nyumba ili atoke hapo hotelini siku ya jumapili.
Mama
Penny alikubali kuendelea kumfundisha kazi mama yake kama alivyomfundisha Tunda
mpaka atakapojua na kuendelea na biashara ya Tunda. Alipata nyumba mitaa
ya Kurasini. Tunda alihakikisha
anamkabidhi mama yake pesa ya kulipa kodi ya mwaka mzima ili asisumbuke na
watoto. Ni kweli Tunda alikuwa amechoka, maana hiyo siku ya alhamisi asubuhi,
alikwenda kupamba ukumbi wa kitchen party, akaenda saluni ndipo akaenda kwa
baba yake.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Net
aliingiza mizigo yao hapo ndani chumbani. Tunda alikuwa ameshabadilisha nguo
aliyokuwa amevaa ya harusi. Chumbani kwa Net, nyumbani kwao Salasala, wakati
Net anaagana na Maya na bibi yake. Kwahiyo alifika hapo hotelini na nguo za
kawaida tu, sio shela. “Natamani tu kulala.” Tunda aliongea wakati anatoa viatu
vyake. Net akamsogelea. “I wanna make love to you Tunda.” Net akamwambia kwa
upendo.
“Nataka
kukukumbatia, na kufanya mapenzi na wewe mpaka niridhike. Unajua nilikuwa
nakusubiria?” Tunda hakuwa akiamini. “Kweli Net!?” Tunda akasimama kwa
mshangao, asiamini. “Oooh yeah! Sasa unafikiri ni kwa nini nilikuoa?” Tunda
akacheka na kujificha usoni. Akahisi mikono ya Net mwilini mwake.
Midomo
akasikia shingoni, akaendelea kumbusu. Akamkumbatia akitegemea mabusu yaendelee
wakiwa wamesimama vile vile, akahisi gauni lake likipandishwa taratibu, mwisho
akalitoa kabisa. Midomo ikaendelea kumnyonya shingoni mpaka akafika juu ya
matiti yaliyokuwepo kwenye sidiria. “Leo
napata yakizungu.” Aliwaza Tunda.
Ile
mikono ya Net, ikafika kwenye vishikizo vya sidiria alipitisha vidole mara
kadhaa huko mgongoni huku midomo yake ikiwa shingoni, masikioni kwa Tunda mpaka
akili za Tunda zikatulia pale kwa mumewe, na yeye Net akaridhika kuwa Tunda
yupo pale kiakili.
Aliendelea
kumpapasa ndipo akamtoa ile sidiria. Tunda aliyezoea kutumikia wanaume, usiku
huo ukawa usiku wake, Net hakutaka afanye chochote kwenye mwili wake. Kila
Tunda alipotaka kujitoa ili amchezee yeye, alihakikisha anamrudisha kule
alipotaka kumfikisha akiwa ametulia. Alimnyanyua mpaka ukutani akamnyanyua kwa
mkono mmoja. Alitua kifuani kwa Tunda, mapenzi mapya na mageni kwa Tunda usiku
ule yakaanza.
Mapenzi
ya kunyanyuliwa, midomo shingoni huku mtoto huyo wakizungu akifanya naye
mapenzi! Tunda alishakuwa amechanganyikiwa. Mwili huo ulipapaswa vilivyo, kwa
mara ya kwanza Tunda akajisikia pumziko kwenye mikono salama ya Net.
Alimtoa
ukutani hapo na kumuweka juu ya meza iliyokuwepo hapo pembeni, Net akaendeleza
mchezo kwa muda mrefu, nakuhakikisha mpaka Tunda anaridhika. Waliingia kuoga
wakarudi kujilaza kitandani. Kimya kwa muda. Akiendelea kumchezea vinyweleo vya
pembeni ya kichwa. Mara kadhaa alimbusu huku akiendelea kumpapasa.
“Asante Net.” Tunda alijikuta akiongea na machozi. “Kwa
ajili ya nini?” Akauliza huku akimfuta machozi na kumbusu. “Sikuwahi kufikiria kama unaweza kunitazama, kunishika na
kufanya mapenzi na mimi kama hivi, hasa baada…” Net akaanza kumbusu
tena. Nakuufanya usiku ule uwe wa tofauti na siku zote Tunda alizokuwa
akiwahudumia wanaume wote kitandani.
Tokea
alipokuwa akifanya mapenzi na baba Tom bila kondom, akitumiwa mwili wake,
akatoka hapo na kuanzisha biashara kama hiyo, lakini akitumia kondom.
Akihangaika kuwaridhisha ili kudumu kwenye soko. Usiku huo kwa mara ya kwanza,
anafanya mapenzi ya kweli. Kwa hiari, akibembelezwa vilivyo, tena na mumewe!
Bila kondom. Huru. Hakuna wakati Net alimgusa, asifike tena kwa furaha. Ulikuwa
usiku wa kihistoria kwa Tunda.
Jumamosi ya Fungate!
Waliamshwa
na kifungua kinywa kizuri kilichokuwa kimeletwa na muhudumu wa hapo hapo
hotelini. “Kwani uliwaambia walete?” Tunda akauliza huku akitupia zabibu
nyekundu mdomoni aliyokuwa ameitoa kwenye kijisinia alicholetewa na Net hapo
hapo kitandani. “Nililipia huduma ya fungate. Tungeweza kwenda kula chini
mgahawani. Lakini nilitaka kutumia muda huu hapa kitandani na wewe. Sikutaka
tutoke kabisa, mpaka siku tunayoondoka hapa.” Tunda akacheka na kujifunika mto
usoni.
“Unafurahia?”
Akauliza Tunda huku akimchungulia pembeni ya ule mto. “Sana.” Akajibu Net na
busu la kipanda uso. Tunda akacheka akiashiria kuridhishwa na hilo jibu.
“Net!”
Net alikuwa amerudi kwenye kigari kilichokuwa na chakula, akageuka. “Jana
umeufanya ni usiku wangu tu. Na mimi leo nataka kukufurahisha.” Net akacheka
tu, na kugeuka. Akachukua na yeye chakula chake akasogea pale kitandani. “Chakwanza
nataka ujue jana haukuwa usiku wako tu. Na mimi ulikuwa usiku wangu. Mbali
yakukufurahia, ujue furaha yangu imekamilika kuona ulifurahia wakati wote.”
“Umejuaje kama nilifurahia?” “Huwa najua ninapo danganywa.” Net akajibu na
kumbusu tena. Safari hii alimbusu kwa muda kidogo. Akambusu tena na tena.
Hawakujua
ni saa ngapi waliweka chakula pembeni, nakujikuta wamezama katika ulimwengu
wao. Tunda akigugumia raha aliyokuwa akiipata kutoka kwa Net. Alimkumbatia
Tunda huku akifanya naye mapenzi kwa kutulia bila papara. Aliweza kuhisi ile
raha anayoipata hata Net mwenyewe. Hata Tunda mwenyewe alijua hadanganywi, ni
kweli Net naye anamfurahia.
Net
alitawala mchezo na siku hiyo karibia yote. Mwishowe Tunda akahisi labda
anataka kumpumzisha na shuruba alizokuwa akizipata kuhudumia wanaume. Ni kama
alitaka kumuonyesha kwa wakati ule hakuwa kazini, ila kwenye ndoa.
Usiku
wakiwa wamejilaza kwenye sinki la kuogea, Net akiwa mbele ya Tunda, amempa
mgongo, Tunda akimchezea nywele zake taratibu, akamuona anageuka. “Tunda!”
Akamwita. “Unapenda watoto wangapi?” “Sijafikiria Net. Unakumbuka nilikwambia
hata sijui kama nina uwezo wakuzaa?” “Nakumbuka. Lakini kama ikitokea Mungu
akakujalia uzazi, ungependa kuwa na watoto wa ngapi?” Tunda akafikiria kidogo. “Nitajua
nikishapata wa kwanza na wa pili.” Net akacheka na kumbusu. “Na wewe?” Tunda
akamuuliza. “Natamani wasiwe chini ya wawili.” Tunda akacheka huku akifikiria.
Net akajiweka sawa, nakuanza kumbusu tena.
“Twende
tukaanze kutafuta wa kwanza basi.” Net alimfanya Tunda acheke. “Tusipofanikiwa?”
“Ndio itakuwa hatujafanikiwa.” Tunda alibaki akifikiria. “Umeshafikiria kama
tukifanikiwa?” Net akauliza. “Nahisi bado ninahofu na hilo Net.” “Naomba utulie
kabisa, tumuachie Mungu. Ila naomba tukifanikiwa tukapata mtoto wa kiume,
tumwite Cote Junior Cote.” Tunda akashangaa.
“Net!
Umeshafikiria mpaka jina!” Net akacheka. “Unaniogopesha bwana!” “Nimekwambia
usiogope. Mwembe ni mwembe tu, hata usipozaa maembe ni mwembe.” “Wewe ni mzungu
gani unajua Kiswahili hivyo!?” Net alicheka sana.
“Usiogope
bwana. Naamini tutakuwa tu sawa. Twende tukamtengeneze Cote.” Tunda akacheka. “Ndio
tunafanyaje?” “Nitakufundisha style nzuri.” Tunda akazidi kushangaa. “Net
wewe!” Net akazidi kucheka. “Twende mke wa Net!” Tunda alijisikia vizuri sana.
Akacheka. “Nimefurahi ulivyoniita hivyo.” “Ndivyo ulivyo.” “Siamini mwenzio
kama nimeolewa na mimi!” “Hata mimi siamini kama nimekuoa Tunda. Nilianza
kuingiwa na wasiwasi, nikahisi watanzania watanipora hivihivi najiona.” Tunda
alicheka sana.
Jumapili.
Mazito & Machungu kwa
Net & Tunda.
W |
akiwa kwenye usingizi mzito
sana, wakasikia mlango wao ukigongwa. Lakini safari hii uligongwa kwa nguvu sio
kama jana yake walipokuwa wakiletewa chakula. Wote wakashtuka. Net akatoka kwa
haraka. Akavaa rob nakusogelea mlangoni
akiwa na hasira kidogo kwa nini mgongaji amegonga kwa fujo kiasi kile!
Akafungua.
“Wewe ni
Nethaniel Cote?” Walikuwa wanaume wanne hapo mlangoni wakamshtua sana Net. “Ndiyo.”
Net akajibu. “Upo na Tunda?” Tunda aliyekuwa pale kitandani kama alivyozaliwa,
akajifunika vizuri huku hofu ikianza kumuingia. Net akajua tayari mambo
yameharibika.
“Kuna
nini? Kwa nini mnamuulizia mke wangu?” “Kisheria sio mkeo, sababu hukukamilisha
taratibu ili kuweza kuoa hapa nchini. Kwa hiyo hata ndoa mliyofunga siku ya
ijumaa, haitambuliwi popote kisheria. Ulioa bila kukamilisha taratibu. Pili,
wewe na yeye wote mpo chini ya ulinzi kwa tuhuma zakuibia kampuni ya Cote.
Mmechukua nyumba ya kampuni uliyokuwa umeajiriwa, wewe kama mfanyakazi,
ukammilikisha Tunda bila idhini ya mmiliki mwenyewe ambaye ni mjane Bi Ritha Cote.”
Mwili mzima wa Net na Tunda ulikuwa ukitetemeka. Wale watu wakaingia ndani.
Bado Tunda alikuwa amekaa kitandani.
“Mpo
chini ya ulinzi. Vaeni, twendeni kituoni.” “Naomba mnichukue mimi. Tunda
hausiki. Kama ni nyumba, mimi ndiye nimemuuzia.” Net akajaribu kumtetea. “Tunda
anayo makosa yake. Anatumia biashara ya ngono kujiingizia kipato. Ushahidi wa
jinsi alivyokuwa akipokea pesa kwa biashara hiyo ya ukahaba, upo. Na wapo watu
ambao wapo tayari kutoa ushahidi wao, kuonyesha jinsi Tunda alivyotumia ngono
kama biashara. Safari hii tunamkamata hapa sisi wenyewe tukiwa mashahidi. Yupo
na wewe hapo, wote mkiwa uchi akiidhinisha kukaa kwako nchini kinyume na
taratibu kwa kukupa ndoa ya uongo ili tu, kujinufaisha.” Tunda na Net
wakashangaa sana.
“Sio
kweli kabisa. Tunda hajawahi kunishawishi kwa lolote na hajanidanganya! Nipo
hapa kwa ridhaa yangu mwenyewe. Kama ni makosa ni yangu sio Tunda. Huo ni uongo
wa mama kwa sababu anataka kuniadhibu mimi kwa...” Net akataka kuendelea
kumtetea Tunda. “Naomba mvae. Mtapata nafasi yakujitetea mbele ya hakimu. Sio
hapa. Sisi tuna kazi moja tu, yakuwafikisha chini ya vyombo vya usalama.” Ilimbidi
Tunda kuvaa palepale wakiwa wamewasimamiwa. Wakatolewa pale kwenye chumba chao
chafungate na pingu mkononi.
Walikuwa
wamekodi chumba cha juu kabisa. Wale askari kanzu walitumia lift kuwashusha
mpaka chini. Waliwatoa pale wageni wote waliokuwepo pale eneo la mapokezi na
mgahawa wa pale hotelini wakipata kifungua kinywa, walibaki wakiwashangaa wao jinsi
wanavyo vutwa tena wakiwa na pingu mkononi. Walitolewa kama wahalifu haswa.
Wakivutwa mpaka nje kabisa sehemu yakuegeshea magari, wakaingizwa kwenye gari
ya hao askari kanzu. Tunda alikuwa akilia sana. Net alijaribu kumtuliza huku
yeye mwenyewe akitetemeka hapo ndani ya
gari.
Ritha Awatenda Bila Huruma!
Mara
mlango wa nyuma wa gari walipokuwa wamewekwa, ukafunguliwa. Alikuwa mama Cote. “Naamini
mmesomewa mashitaka yenu.” “Umefanya nini mama? Kwa nini unamwadhibu Tunda bila
kosa? Naomba unifanyie mimi chochote, umwache mke wangu aondoke zake. Tunda
hafahamu chochote juu ya ile nyumba!” “Basi. Aweke saini hapa, kuonyesha
ameirudisha ile nyumba kwa jina la kampuni, ili kesho niende ofisi za Aridhi
kuzuia hati.” “Sawa.” Net akakubali kwa haraka sana.
“Bado
Net.” “Unataka nini tena mama?” “Msaini karatasi za talaka.” “Haiwezekani
mama!” Net akabisha. “Hivi unajua kosa linalokukabili wewe Net? Umeoa kimakosa.
Tena ukiwa upo hapa nchini bila kibali.” “Unaongea nini mama!?” “Kampuni ya
Cote inaonyesha ilishakufukuza kazi miezi mitatu iliyopita. Kwa hiyo upo hapa
nchini zaidi ya siku 90 ukiwa huna kazi.” “Mama!” Net akashangaa sana.
“Mbona
barua yako yakufukuzwa kazi ipo kwenye faili ya wafanyakazi wa kampuni
ikionyesha ulishafukuzwa kazi! Na ushahidi ninao.” Net hakuwa akiamini. “Ila
kwa muda wote huo umekuwa ukijilipa mshahara wewe mwenyewe. Uliiba hundi zangu
ukawa unaniibia kila mwezi.” “Kweli mama!?” Net
aliumia, akaona machozi yakimtoka bila kujua.
“Unakumbuka
mimi kukuandikia hundi ya kukulipa mshahara?” “Si kwa kuwa mimi ndiye
niliyekuwa nikilipa wafanyakazi mshahara?” “Kwa hiyo ndio hapo na wewe ukatumia
mbinu hizo hizo kuniibia?” Ritha alimgeuka mtoto wake, kama hamfahamu.
Tunda
alikuwa akilia sana nakushindwa hata kumwangalia mama Cote. “Wewe ni mwizi, na
umesaidiana na huyu malaya kuniibia. Kosa la pili upo hapa nchini zaidi ya muda
uliotakiwa kuwepo. Tatu, umedanganya serikali ya Tanzania kwa kutoa
vithibitisho vya uongo ili kukufanikisha kufunga ndoa.” “Naomba unifunge mimi muache Tunda. Hana hatia.” Net
alijitahidi kumtetea Tenda.
“Kwani
hujaambiwa makosa yake huyo malaya?” “Naomba usimwite hivyo. Ni mke wangu.
Tafadhali mama.” “Mke wako au tapeli uliyekubali akuibie mchana kweupe?! Una
nini wewe unachoshindwa kuelewa? Tunda anakabiliwa na kosa lakufanya biashara
ya ngono hapa nchini. Vidhibitisho vipo polisi. Wameprint historia za simu zake
zote jinsi alivyokuwa akipokea pesa za biashara zake. Na mashahidi wapo. Makosa
mengine ni kama niliyokutajia hapo juu. Kuingia naye njama za kuniibia, ili
umpe yeye mali zangu kwa kukufundisha wewe jinsi ya kumuoa ili upate kibali chakuwepo
hapa nchini. Kwa hiyo amekurubuni kwa ndoa yeye kama raia ili umpe mali zangu.
Usitegemee huyo malaya wako atatoka jela leo wala kesho. Watamfunga mpaka kifo
chake.” Tunda aliendelea kulia tu.
“Mkitaka
msaini haya makaratasi, ili nifute kesi ila kama hamtaki basi, mtakutana na
vyombo vya sheria.” Akataka kuondoka. “Naomba karatasi ya nyumba nisaini.” Net
akamuwahi kabla hajafunga mlango. “Kwa hiyo unaenda kufuta kesi?” Net akauliza.
“Si ndivyo nilivyokwambia? Okoa muda hawa maaskari wanataka kuondoka na
nyinyi.” “Wanifungue sasa! Nitasaini vipi na pingu?” Mama Cote bila hata
wasiwasi akaenda kumwita mmoja wa askari, akaja kuwafungua pingu Net na mkewe.
Net
akasaini zile karatasi baada yakusoma na kuona hajategwa tena. Akampa na Tunda.
“Naomba utulie uweke saini Tunda, haya mambo yaishe. Na samahani nimekuingiza
matatizoni.” “Huyo malaya alikuwa kwenye matatizo kabla hata hujamuokota.
Asijidai kulia. Weka saini urudishe mali zangu.” Mama Cote aliongea na
kufyonza.
Tunda
akafuta machozi na kuweka saini. “Bado ya talaka.” “Ni
nini mama? Nyumba yangu nimekupa. Tena kwa maandishi kabisa. Endelea na maisha
yako niachie mke wangu. Hayakuhusu tena. Umetaka nisikutafute, sitakutafuta.
Naomba utuache.” “Sitakubali Tunda akuharibie maisha yako Net. Hata kama
sasa hivi utanichukia, nichukie tu. Hii ndoa nitafanya kila niwezalo, ife. Yeye
ameshaishi maisha yake yote hapa duniani, anataka amalizie na wewe! Sitakubali.
Hata kama itanigarimu mtengane kwa kuishi jela. Potelea mbali.” Net akainama
kama anafikiria huku akilia kama mtoto.
“Basi
mtakachoamua, mtamwambia hakimu. Mimi nakwenda kupumzika.” “Naomba usibiri kidogo. Naomba muda na Tunda.” “Ili
akutapeli kwa maneno yake yenye sumu! Hata kidogo. Nikifunga huu mlango hapa,
mjue kujitetea kwenu ni mbele ya hakimu.” “Mama
please!” Net akajikuta akibembeleza karibia kupiga magoti kwa hofu. “Sikukusudia kudanganya swala la ndoa. Yule mwanasheria
aliniambia amefuatilia kila kitu na kukamilisha. Tunaweza kufunga ndoa.”
“Usinitanie
Net. Ujue unazungumza na mimi? Nakujua sana wewe sio mjinga, mtu wakudanganywa
kama mtoto mdogo. Ulikusudia kufumbia macho sheria, sasa hivi ndio unajidai
hukujua sababu unabanwa! Mimi naondoka. Sina jinsi yakukusaidia tena.
Nilikuonya juu ya huyo malaya, ona alipokufikisha!” “Tunda
hajanifikisha hapa mama, wewe ndio umenifikisha hapa.” “Unaendeleza
kiburi tu, kwa nini unashindwa kujifunza!?” Mama Cote akauliza kwa kushangaa.
“Anawalisha
nini huyu Tunda kitu kinachowafanya muwe kama wajinga!? Afadhali mwenzako Meto
amefunguka macho na ameamua kumshitaki huyo Tunda.” “Haiwezekani
kama umeweza kumshawishi hata na yule mzee mpaka akakubali kuingia kwenye hila
zako! Ni nini mama?” “Mungu amemfungua nakumjua Tunda kwa hila. Kuwa
ameingia kanisani kumaliza na wakanisani. Waduniani amewamaliza wote, sasa hivi
ndio anaharibu kanisa! Sasa hapa kwa Cote ndio aandike maumivu. Na ninakuapia
Net, usipo saini hiyo talaka, utayaona maisha ni machungu.” “Mimi naomba nisaini, ili nimuache huru Net.”
Kwa mara ya kwanza Tunda akaongea.
“Nipe mimi hizo karatasi.” Tunda akasisitiza, Net akazidi kulia. “Sasa
kwa kuwa ulishaingia kwenye hiyo ndoa feki, nataka na uandike kabisa. Umeamua
kumuacha Net, bila kutaka akupe kitu chochote. Mali ulizomkuta nazo Net,
zitabakia ni za Net, na wewe hutaki kitu chochote kutoka kwake.” “Mama! Yaani akili zako ziko kwenye pesa tu?” Mama Cote hakutaka kumjibu Net, akampa zile
karatasi Tunda. Akasaini na kuandika kama alivyoambiwa na mama Cote.
Akamkabidhi.
“Haya,
na pete zote ulizovalishwa na Net, naziomba hapa.” Mama Cote akanyoosha mkono
kwa Tunda. “Haiwezekani mama. Hizi pete za ndoa ni
jasho langu. Nimetengeneza kwa pesa nyingi sana na hiyo pete ya uchumba ni ya
bibi! Naomba muachie mke wangu avae.” “Ni nini usichoelewa Net? Unataka
kuzidi kunipandisha hasira? Bado unamwita huyu malaya ni mke wako! Nipe hizo
pete Tunda kabla sijakukata hicho kidole.” Tunda akavua zile pete na kumkabidhi Mama Cote. Akaziweka kwenye pochi yake, akatoka
na kumwita askari.
Yule
askari akafika pale. “Huyo mwanamke nishamalizana naye. Mnaweza kuendelea
naye.” “Hapana mama. Umeahidi Tunda akisaini
ndio anakuwa huru.” “Hayo ni juu yake yeye na sheria za Tanzania. Ataenda
kujitetea juu ya biashara ya ngono aliyokuwa akifanya. Huko sihusiki. Nahusika
na kumdhibiti kwenye himaya yangu.” Bila hata kupoteza muda, wakamvuta Tunda
kumtoa pale kwenye gari.
Net
alimsukuma mama yake kwa nguvu pale mlangoni alipokuwa amemsimamia, akataka
kwenda kwa Tunda huku akipiga kelele, askari mwingine alimkamata Net, Tunda
akaingizwa kwenye gari nyingine huku akilia, wakaondoka.
Kwa Net!
Baada ya
Tunda kuondolewa pale, Ritha akamgeukia mwanae. “Sasa hapa nchini huwezi kukaa
hata lisaa.” Mama Cote akiwa na askari wawili, akamwambia Net. “Unamakosa
ambayo ukifikishwa kituoni, hutakaa utoke leo wala kesho. Kwa usalama wako tu,
heri uondoke. Watu wa uhamiaji wameanza kukusaka tokea ijumaa. Ni vile jumamosi
na jumapili hawafanyi kazi. Lakini kesho ujue nilazima utakamatwa. Gabriel naye
amekushitaki kwa makosa yake. Yaani kwa kifupi, hapo ulipo Net, ni mhamiaji
haramu. Na mbaya zaidi, unaonekana ulikuwa hapa nchini ukiwa huna kazi ila wizi
tu.” Net alikuwa akilia huku ameweka mikono kichwani asiamini.
Mama Cote
alihakikisha anamtisha Net vilivyo. Akamtajia tena makosa mengi sana huku
akimsingizia kwa kazi ambazo alikuwa akimtuma yeye mwenyewe. Na ushahidi
alimwambia anao. Net alikuwa anashindwa hata kujitetea. Alijuta kumpeleka Tunda
kanisani kutubu. Alijuta kumkutanisha na mama yake. Alibaki akimuomba Mungu
msamaha bila yakumjibu kitu mama yake. “Mungu wangu naomba unisamehe! Tunda nisamehe. Mungu
wangu nisamehe! Tunda nisamehe!” Net alisikika akiomboleza bila
kuchoka wala kumjibu mama yake.
“Nimekukatia
tiketi ya ndege ya Emirates. Hawa polisi watakufikisha uwanja wa ndege na
kuhakikisha unaondoka hapa nchini mchana huu wa leo. Ukithubutu kuwatoroka kwa
namna yeyote ile ukidhani bibi yako atakuja kukutoa kesho yake, ujue utaangukia
mikononi kwa Gabriel. Anahasira na wewe yakupitiliza kwa kumsaliti. Umemuoa
mwanamke wake akiwa ameshakuonya. Kwa kifupi na yeye anakusaka kama alumuasi.”
Mama Cote akaendelea.
“Tangia
siku ya ijumaa aliposikia unamuoa Tunda, alianza kupita humo kwenye mahoteli
akikusaka. Mimi mwenyewe wamekubali kunipa namba ya chumba ulichopo ni kwa kuwa
nimeonyesha kitambulisho kuwa ni mama yako, na hawa ni polisi. Ndipo nikajua
kama upo chumba gani. Sasa ni aidha uondoke sasa hivi, au akukamate Gabriel
uliyemsaliti kwa kumuoa mwanamke wake, au ukamatwe na serikali ya Tanzania,
ufungwe jela na kujiharibia kabisa.”
“Na ujue
kwa kuwa ni wewe Nathaniel Cote, kesi yako itanguruma ulimwengu mzima. Habari
zitafikishwa mpaka Canada, hakuna atakayekuamini tena kwa makosa uliyojiingiza
kijinga hapa nchini. Na ujue wazi, hata hizo mali ulizotakiwa kukabidhiwa na
bibi yako hutaweza kumiliki tena kwa kuwa unaweza kujikuta unaishia jela. Na
utaua jina la Cote kote ulimwenguni. Hata kule alikokuwa akipita bibi yako,
hataweza tena.” Net aliendelea kulia tu.
“Tiketi
na hati yako yakusafikiria hiyo hapo.” Akamrushia pale alipokuwa amesimama. “Uamuzi
ni wako. Kwenda au kubaki, ukawe mali ya wanaume wenzako huko jela. Na hayo
macho na hiyo rangi, nakuhakikishia hutakaa jela ya hapa hata siku mbili bila
kulawitiwa, na utatoka na UKIMWI. Wewe wapelekee hiyo sura nzuri ya kizungu hao
wanaume wa jela wenye njaa za miaka na miaka za wanawake, halafu uone kama
hujanikumbuka zaidi.” Mama Cote akaondoka bila hata kugeuka nyuma.
Na wale
askari hawakusubiri Net aamue. Walimfunga pingu. Wakaokota ile hati yake
yakusafiria na tiketi, wakamwingiza Net kwenye gari mpaka uwanja wa ndege wa
kimataifa wa Mwalimu JK Nyerere, Dar. Aliingizwa kwenye ndege kama mfungwa,
wakahakikisha ndege inaondoka, ndipo wale askari nao wakaondoka. Nao walilipwa
ili kukamilisha hilo.
Kwa mama Cote.
Wakati
mama Cote akifanya hayo yote, Bethy hakuwa mbali. Alikuwa ndani ya gari yake
akisubiria aone mwisho wake ili kuhakikisha mama Cote hamdanganyi. Ugomvi wa
Bethy na mama Cote ni kutowatenganisha Net na Tunda. Bethy alisema wafanye
chochote kile, lakini Tunda asije akawa huru kurudi kwa Gabriel. Ndipo mama
Cote akatumia akili ya haraka kumtuliza kuwa, atamtenganisha Tunda na Net, na
hawatakaa wakaonana daima.
Wasiwasi
ulimwingia mama Cote pale alipoitwa na Net, siku ya harusi ya Tunda na Net. Mtu
mwenye akili ya haraka na ambaye atamuelewa kwa haraka akamfikiria nakumpata
Bethy. Lakini akakumbuka Bethy nia yake ilikuwa nikutaka Tunda na Net wawe
pamoja. Inamaana mama Cote hatashinda. Akamfikiria Gabriel. Akajua wote wawili
yeye na mkewe watamfaa kwa namna yake.
Akawapigia
simu mara tu alipotoka kuzungumza na Net pale nyumbani kwake siku ya ijumaa, ya
harusi. Aliwaambia kinachoendelea, ila akawasihi wasubiri mpaka kesho yake
ambapo bibi Cote anaondoka nchini na ulinzi wote uliokuwa ukimsubiria, ndipo
watekeleze. Ila kwa wakati ule, wakutane na washauriane nini chakufanya.
Bila
kuchelewa wakafika kila mmoja kwa wakati aliopangiwa na Ritha, lakini hakutaka
wawe wote watatu pamoja. Kila mmoja alikutana na Ritha akiwa na lake kichwani.
Gabriel akiwa na hasira yakusalitiwa, Bethy akiwa na furaha ya ndoa ya Net na
Tunda.
Ili
kumuweka sawa Bethy akamueleza kwa kumrubuni Bethy kuwa Net hawezi akawa
amemuoa kihalali Tunda. Akamueleza utaratibu wa sheria za Tanzania, kuolewa na
mgeni. Maana na yeye aliolewa na baba yake Net. Anajua mambo yote. Akamuhakikishia
hata yeye hayupo salama, kwani endapo ndoa hiyo ikitenguliwa tu, basi
akamuhakikishia Bethy kuwa, Tunda atarudi kwa mumewe.
Na
akamwambia tena, hata kama ndoa yao haitatenguliwa, basi, kwa kuwa Tunda ni
malaya sana, kitendo cha kuolewa na rafiki ya mumewe, ni kama kumkaribisha fisi
dukani. Lazima atamzunguka tu na kuishia kuwa na mahusniano na wote wawili.
Gabriel na Net. Hapo Bethy akakubali kwenda kikaoni kupanga mikakati mipya.
Maana mwanzoni alikataa hata kukutana na mama Cote. Alimwambia mama Cote ni
kama kazi yake yeye imeisha. Ameshamtoa Tunda kwa mumewe anaolewa na Net.
Kwa
Gabriel, akaweka mikakati rahisi tu. Kwa kuwa ni kama wao wawili malengo yao
yanafanana. Kuwatenganisha kabisa Net na Tunda. Kikao chao wao wawili kikaenda
vizuri wakiongea lugha moja, lakini akimficha mwisho wa Tunda. Wakaweka
mikakati ya mwanzoni pamoja. Gabriel akitaka watengane, ndipo apate nafasi
yakujirudi kwa Tunda, aombe msamaha, warudiane.
Mama yake akajua kabisa atakuwa amemtumia
mwanasheria wa kampuni kumfanikishia mambo yake ya ndoa, kwa kuwa aliona ule
ukaribu ulioanza ghafla kati ya Net na yule mwanasheria. Akampigia simu yeye
moja kwa moja na kumuuliza maswali ya kumtega, bila kujua akijua anamsaidia
mama yake Net, yule mwanasheria akamwelekeza kirahisi tu kwa yule mwanasheria
mwingine aliyemuelekeza Net, kwake. Alimpa na namba za zimu za yule mwanasheri.
Sasa kwa
kuwa mama Cote alijua sheria ya Tanzania kwa maswala ya ndoa, akaanza kumbana
yule mwanasheria kwa maswali magumu, mpaka akakiri kuwa alimtapeli tu Net.
Hakuwa amepeleka vitu vyote vilivyokuwa vikihitajika kwenye ofisi husika. Hapo
wote wakafurahi sana. Wakawa wamemkamata Net. Sasa ili kuwatenganisha, ndio
wakapanga kumsingizia makosa mengi ili akiondoka nchini, asiweze hata kurudi
tena. Hapo wakafikia sehemu nzuri, kila mmoja na furaha.
Ndipo
sasa siku ya jumamosi asubuhi wakiwa wamejawa furaha ya kupata habari zote,
wakakutana sasa wote watatu. Swali likaja kutoka kwa Bethy, sasa Net
akishaondoka, Tunda je? Kwa upande wa Gabriel alishaonya kabisa kuwa Tunda
aachwe, wasifikirie hata kumdhuru. Mkewe alipinga wazo la kuondolewa Net
nchini, na kuachwa Tunda bila ndoa. Ugomvi ukaanza hapo. Gabriel na mkewe.
Mwishowe mama Cote akamshika mkono Bethy, akamwambia aende naye chooni,
akatulie ndipo warudi kuzungumza akiwa ametulia.
Mama
cote kama kawaida yake akatumia akili za haraka. Wakiwa kulekule chooni
akamuweka sawa Bethy. “Mimi sio mjinga Bethy. Tatizo lako unaruhusu hasira
zikutawale na kushindwa kufikiria.” Mama Cote akiwa na Bethy chooni akaendelea.
“Tukiwa na Gabriel, muonyeshe huna shida na Tunda. Lakini mimi na wewe tutajua
jinsi yakumuangamiza Tunda.” “Tutafanyaje?” Kidogo Bethy akawa ameingia kwenye
mstari. Akasikika akiuliza akiwa ameanza kutulia.
“Hayo
ndio maneno! Sio matusi na fujo. Haya mambo yanahitaji kufanyika kwa akili.
Katika kila hatua tunamuhitaji Gab ili kutufanikishia. Gabriel anapendwa sana
na polisi kwa ukaribu aliojitengenezea na hicho chombo cha usalama. Mwache
atusaidie. Tukifika mwisho tutaendelea wenyewe. Jifanye mjinga.” Mama Cote
aliongea na tabasamu lakumtuliza.
“Hapo
sawa, sio vinginevyo. Ndio tunafanyaje sasa?” “Nikumpachika makosa ambayo
hawezi kutoka jela leo wala kesho.” “Makosa gani?” Bethy akahoji tena. “Kwanza
wewe unajua umalaya aliokuwa akifanya Tunda tunaweza kumshitaki kama ni
biashara ya ngono ambayo kwa sheria ya Tanzania ni kosa?” Bethy akacheka na
kugonga. “Unaakili wewe!” Bethy akamsifia asijue hata yeye anachezewa.
“Ndio
maana nakwambia tulia tupange.” “Haya, nipe mambo. Lakini hilo kosa, si anaweza
kutolewa hata kwa dhamana?” “Kwani tunampa kosa moja? Tunamshitaki kwa kosa la
kununua ile nyumba. Tunamshitaki kwa wizi pia. Kuwa alitumia rushwa ya ngono,
kumshawishi mfanyakazi wangu kumpa moja ya nyumba ya kampuni kwa ahadi nyingine
yakumpa uraia hapa nchini kwa kumtengenezea makaratasi ya uongo. Amemrubuni
Net.” Bethy alicheka sana. “Nimekukubali mama Cote!” “Mjini shule. Kula kwa
akili. Lasivyo tusingekuwa hapa?” Wakagonga.
“Gabriel
yeye atatusaidia kumtoa Net hapa nchini, wakati sisi tunamfunga Tunda. Akija
kutoka huko na wewe umetulia na mumeo.” Wakagonga tena. “Sasa kwa furaha hii,
sithubutu kurudi kwa Gab. Atanishtukia. Wewe nenda kanichukulie funguo zangu za
gari na pochi. Mwambie Bethy amekasirika sana, ameamua kuondoka.” “Umeona jinsi
ukitulia ulivyo na akili?” Wakabadilishana mawazo wakapanga mambo yao. Mama
Cote akafanya kama walivyopanga. Akaenda kumchukulia pochi na funguo zake za
gari, Bethy akaondoka na kumuacha mama Cote na Gabriel.
Walibaki
wawili hao wakipanga jinsi yakumtoa Net nchini. Na kwa kuwa Gabriel alikuwa mtu
wakuonekana akisaidia watu huko kwenye vyombo vya habari, ashajenga vituo vya
polisi zaidi ya vitano nchini ili kuimarisha ulinzi mpaka vijiji vilivyokuwa na
uhitaji huo. Alikuwa mtu wakutoa misaada mbali mbali kwenye vituo vya polisi.
Basi alifahamika na kuheshimika sana. Ritha alijua Gabriel atamfaa kumtoa mtoto
wake pale nchini.
“Hilo
halina shida mama Cote. Ila naomba kukuonya juu ya Tunda. Mwanao alinisababisha
nikamuacha Tunda akiwa kwenye shida, wakati mimi alikuwa akinisaidia sana.
Huwezi kujua ni shida kiasi gani ninapitia kwenye ndoa yangu. Kwa mabaya yeyote
yale mtakayomsema nayo Tunda, kwangu alikuwa mwema sana. Net ndiye
aliyenidanganya nikamtelekeza mwanamke aliyenipenda na kunithamini kwa dhati.
Sitakubali tena chochote kibaya kimpate Tunda. Kwa gharama yeyote ile, na kwa
yeyote yule, lakini sio Tunda. Naomba hapo tuwekane sawa kabla hatujaendelea.”
Gabriel alionekana wazi katika hilo hana ubiya na mtu.
“Mimi
nakuelewa Gabriel. Najua maumivu yakusalitiwa. Tusaidiane kutengeneza kisa
kizuri chakumuondoa Net hapa nchini. Zungumza na polisi watakao tusaidia kumtoa
hapa bila jina lake kuingizwa kwenye vyombo vya sheria. Najua ni ujinga tu,
nataka kumfundisha lakini sio kuyaharibu maisha yake kabisa.” Hapo Ritha akawa
upande mmoja na Gabriel.
“Lini
umeanza kunitilia mashaka Gabriel? Usiwe na wasiwasi.” Mama Cote alizungumza
akicheka kama kutaka kumzuga Gabriel. “Mimi sina wasiwasi. Ila nataka Net ndio
awe na wasiwasi ili asirudi tena hapa nchini kwetu. Wapo wanawake wengi tu huko
kwao, kwa nini aje kuchukua wake zetu huku? Ila kama wewe hutaweza, niachie
mimi hiyo kazi nimtengeneze vizuri, nimshikishe adabu.”
“Naona
tugawane tu majukumu. Wewe zungumza na
mkuu wa kituo cha polisi kirafiki, mimi nitaandaa vitu vyote na wewe
nitakupa.” “Hapo sawa. Jioni tukutane tena hapa ukiwa umekamilisha kila kitu.
Na mimi nitakuja na jibu la uhakika.” Bila kusubiri jibu, Gabriel akasimama na
kuondoka akamuacha mama Cote pagumu.
Wote
watatu walikutana hiyo hiyo siku ya jumamosi jioni. Wakawekana sawa.
Wakaonyeshana hili na lile. Gabriel akawapa mwendelezo wa kile walichozungumza
na mkuu wa kituo cha polisi. “Ameahidi kutupa askari wa nne bila shida. Tupo
naye karibu sana. Nimemueleza hatari ya kumuweka Net hapa nchini kwetu. Akataka
tumfungulie mashitaka kabisa. Ahukumiwe hapahapa nchini au hata akirudishwa
nchini kwao, arudi na pingu.” Mama Cote akashtuka sana, akajikaza kusikiliza
mpaka mwisho.
“Lakini
nikamweleza mahusiano tuliyo nayo na wewe mama yake, akanielewa. Lakini ametoa
agizo kuwa ifikapo jumatatu, Net asiwepo hapa nchini lasivyo wao watamkamata na
kumshitaki.” Hapo mama Cote akameza mate.
Wakaendelea
kuzungumza na kupanga, Gabriel akiwa hajui mpango kando wakufungwa kwa Tunda
kwa tuhuma nzito. Zile zile alizomshitakia Net kwa mkuu wa kituo cha Kawe,
kumbe ndizo hizo hizo mama Cote na Bethy wamezibadili tu jina na kusema Tunda
ndiye amezifanya kwa kutumia rushwa ya ngono.
Hiyo Jumapili Sasa.
Ndio
hiyo siku ya jumapili sasa wakafanikisha kukamatwa wote. Wale polisi
walimtaarifu Gabriel aliyewalipa pesa pembeni, wamjulishe pindi Net
atakapopanda ndege. Walimpigia simu Gabriel na kumtaarifu kuwa ndege ya Net,
imeshaondoka kwenye viwanja vya mwalimu Nyerere, Dar-es-salaam. Na yeye
akampigia simu mama Cote akiwa na furaha sana. Asijue mama Cote alikuwa na
Bethy kwenye hoteli ileile wakijipongeza kumtoa Tunda kwenye maisha yao.
Jumapili
hiyo ikawa na taarifa alizokuwa akizisubiri kwa hamu Gabriel. Kuondoka kwa Net
nchini. Tena baada yakusaini talaka. “Ameniachia
Tunda wangu. Sasa tupo huru. Kilichobaki nikurudi kwa Tunda, nakumuomba msamaha. Maisha yetu
yaendelee. Talaka ya Bethy naanza kuishugulikia kwa haraka sana.” Aliwaza
Gabriel na tabasamu usoni.
Kwa Tunda!
T |
unda alifikishwa kituo cha
polisi cha Kawe ilikuwa tayari ni saa tano asubuhi ya siku hiyo ya jumapili.
Alifunguliwa kesi ya makosa matatu makubwa, na aliambiwa hawezi kutolewa kwa
dhamana mpaka hukumu yake itoke. Gafla ikawa kama anakosa la jinahi! Hata hivyo
alijua hakuna anayejua alipo kwa wakati ule. Nani atamtolea dhamana! Akabaki
akilia tu asiamini kama fungate limebadilika kuwa kifungo.
Aliachana
na Net nje ya hoteli. Hakujua Net alipopelekwa na wala Net hakujua alipopelekwa
Tunda. Aliondoka nchini akilia bila chochote mkononi ila hati yake yakusafiria
tu. Na kama walimfanyia makusudi, asiwasiliane na yeyote yule mpaka anaondoka
nchini. Walimbana, hawakumpa hata nafasi ya peke yake akapiga simu. Mtoto huyo
wa kiume wakizungu, aliondoka nchini akilia kama mtoto mdogo aliyekatwa kidole
akiwa na hati yakusafiria tu, na tiketi yake ya ndege.
Tunda
alilala usiku huo, siku ya jumatatu yeye na mahabusu wengine wakahamishiwa
gereza la Keko. Tunda hakuwa akiamini. Wakati waliohudhuria kwenye harusi yao
wakidhani wapo wakifurahia fungate, kumbe maharusi hao ambao ndoa yao ilidumu
kwa masaa 42 tu, walikuwa kwenye shida isiyoweza kusimulika. Na mbaya zaidi,
makosa yote ni kweli Tunda alihusika moja kwa moja au kuhusishwa na Net.
Kwenye
mashitaka au kosa alilotuhumiwa la nyumba. Yeye alifanya akiambiwa kila kitu
kipo sawa kisheria, aweke tu saini. Sasa anakataa vipi wakati aliweka saini
kwenye karatasi zilizoonyesha amenunua nyumba kutoka kampuni ya Cote, wakati
mwenye kampuni amekataa kuwa hajamuuzia! Net alishaanza kushugulikia hati ya
nyumba ziwe kwa jina la Tunda. Fomu zote zipo tayari ofisi za wizara ya Aridhi, yeye Tunda akiwa ameweka
saini na majina yake yote yalikuwa yakionekana kwenye hati hiyo!
Mbaya
zaidi hakuwa na habari kamili juu ya maswala ya hiyo nyumba wala hati. Ni mambo
aliyokuwa akifanya Net mwenyewe na mwanasheria. Yeye alikuwa ni muweka saini na
mtoa taarifa zake kamili. Kama jina na mwaka wake wa kuzaliwa. Na sehemu ya
kuweka saini aliletewa hizo fomu na kuweka saini bila hata kusoma, akimwamini mpenzi
wake. Hakujua chochote. Ila alipokea milioni 3 taslimu na kuandika hundi yenye
jina lake kamili, kutoka kwenye akaunti yake, Tunda akilipa kampuni ya Cote,
kuonyesha yeye Tunda ndiye amenunua hiyo nyumba kwa milioni tatu tu. Wapi
kunakouzwa nyumba kwa milioni tatu kama sio alitoa na rushwa ya ngono!
Kwenye
kosa la maswala ya vyeti vya ndoa, hapo Tunda hawezi kukana pia. Picha zake na
saini kwenye kuomba kufungishwa ndoa na serikali vipo kwa yule mwanasheria.
Mama Cote alishamuogopesha na kumpanga yule mwanasheria vizuri, mpaka akakubali
kumgeuzia Tunda makosa yote. Kuwa yeye Tunda ndiye aliyetumia uraia wake
kuolewa na mtu ambaye asiye raia, kwa kumdanganya kuwa ameweka kila kitu sawa
ili aolewe.
Tunda
aliendelea kuwaza nakushindwa hata kuwatafuta kina mama Penny kuogopa
kuwaingiza na wao matatizoni. Hakujua ni umbali gani Ritha na Bethy wako tayari
kwenda kumuangamiza yeye na yeyote aliye karibu naye.
“Nikimtafuta mama Penny, anahasira sana. Anaweza kuwavaa wale
kina mama. Akaishia kubambikiziwa makosa na yeye.” Tunda
akaendelea kuwaza akiwa mahabusu. “Wakimkamata mama
Penny, ndio mama naye atakuwa amekwama. Hatakuwa na chakufanya. Tom na Aneti
watageuka kuwa watoto wa mtaani kama sio kufungiwa na mama yao na kushindwa
kwenda hata shule.” Tunda akaendelea kujiwekea vikwazo vizito wakati
akifikiria nani wakumpigia simu ili kumtaarifu kuwa amekamatwa.
“Mwishoe nitajikuta nakwamisha kila mtu mpaka huduma ya baba
Penny.”
Tunda akaendelea kuona ugumu. “Net inawezekana na
yeye amefungwa au amerudi nchini kwao! Mama Penny na mumewe wakikamatwa, na
baba naye atakuwa hana mtetezi.” Hapo Tunda akaona atulie kabisa hata
mama Penny hakutaka ajue mpaka ajue hatima yake yeye mwenyewe.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Ikawa
mchana, ikawa usiku siku ya kwanza. Ikawa jumatatu, ikawa jumapili, juma la
kwanza. Kimya. Hakuna aliyemsikia Tunda wala Net. Kwa kina mchungaji hawakuwa
na wasiwasi na wala hawakutaka kuwapigia simu kuwasumbua wanandoa hao wachanga,
wakaona wawape muda, mpaka wawatafute wenyewe. Maisha yakaendelea.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Kwa Net!
N |
et alitua nchini Canada akiwa na
hali mbaya. Kwanza aliondoka akiwa amevaa tu t-sheti na jinsi. Hakuwa hata na
sweta au simu. Mbali na tiketi na ile hati aliyopewa yakusafiria na mama yake,
hakuwa na simu wala pesa. Barafu ilikuwa ikimwagika nchini hapo pale Net
alipotuwa uwanja wa ndege ya Halifax Stanfield katika mji wa Nova Scotia karibu
kabisa na anapoishi bibi yake na Maya. Au nyumbani kwao nchini hapo.
Net
alipata panic attack, vichomi kama aliyebanwa na pumu. Akiwa kwenye kuhangaika
ili kutafuta taksii impeleke nyumbani kwao, kusini mwa Halifax kwenye mtaa wa
Beaufort, nje ya uwanja wa ndege kwenye baridi kali, akaanguka na kupoteza
fahamu. Gari ya wagonjwa ilimchukua mara moja na kukimbizwa hospitalini huku
wakijaribu kupandisha joto la mwili wake lililokuwa limeshuka sana.
Kwa
bahati mbaya sana pale alipoanguka, aliangusha na hati yake yakusafiria mbayo
ilikuwa na jina lake kamili na anuani ya nyumbani kwao. Walimpokea hospitalini
hata hawafahamu jina lake na yeye alikuwa hana fahamu. Siku tatu zikawa
zinaisha bila ndugu yeyote wa Net kumtafuta na yeye bado alikuwa na hali mbaya.
Kwa
matatizo ya kubanwa mapafu, Net akaanza kutumia mashine za kupumulia na
alishapata pneumonia. Alisafiri kwa masaa yote hayo zadi ya 15 kutoka Tanzania
mpaka Canada, bila sweta wala shati zito. Aliingia baridi yakupitiliza. Ni kama
alikuwa kwenye friji kwa masaa hayo yote.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Kwa hakika Tunda yu matatizoni. Tena matatizo makubwa sana. Anajitoa
vipi? Nani wakumtetea? Baba yake yupo gereza la Segerea, yeye yupo mahabusu
Keko.
Je, mama Penny na mumewe
watakubali kujiingiza doa kwa Tunda mwenye shutuma nzito na za kweli za
uchangudoa au umalaya kama anavyomwita mama Cote? Tena waliyekutana hata miaka
mitano haijafika, na wao wanakanisa la watu wanao wachunga na kuwaongoza?
Wanajibu vipi shutuma nzito
za wao kama wachungaji kushiriki ndoa ya serikali, tena kama vifichoni?
Walikuwa na haraka gani waliyoshindwa kuwashawishi kondoo hao kusubiri
kutangazwa kwa ndoa hiyo mara tatu tu ndipo waoane? Nini walichoficha na
kushirikiana na muhalifu huyo Tunda, kutomshauri kufuata taratibu nyingine kama
wanazowahubiria washirika wengine, kanisani!
Usikose kifuatilia
kitakachoendelea kwa Tunda huko mahabusu na Net mahututi hospitalini, nchini
kwao, Canada!
Ø Nini kitatokea kwa Gabriel baada ya juhudi zake
zote kugonga mwamba, na kuju kujua amegeukwa na mama Cote/Ritha?
Ø Pumziko alilokuwa akihangaikia Bethy, atalipata?
Ø Mali alizohangaikia kuzilinda Ritha, kwa kiasi
kikubwa hicho mpaka kufikia kutumia siri za nyumbani mwa Mungu, na kutengeneza
jeshi kubwa kinyume na Tunda, kumfanikishia mipango yake aliyopanga kwa akili
kiasi hicho, atafaidi kwa amani na utulivu?
Ø Bibi Cote atafanya nini?
Ø Nani wakulaumiwa?
Mengi mazito na
yakusisimua yatafichuliwa mbeleni.
Usikose....
0 comments: