NILIPOTEA! PART 5 - SEHEMU YA ‘E’.
“Mimi mwenyewe.” Net akajibu. “Nampenda Tunda jamani.” “Hilo tunajua. Wala hatujawahi kulitilia mashaka.” Akajibu mchungaji. “Mimi sijawahi kuoa na wala sijawahi kuona mama akifanya anayoyafanya. Nimejifunza kutokana na makosa.” Net akaendelea. “Sasa hivi hata nana, yupo makini na mama kwa kuwa tumejua kuwa ni mtu hatari. Ila tabia ya kuhakikisha anapanga mipango kwa makini mpaka kufanikiwa, hilo kila mtu anamjua. Anaakili sana yakupanga mambo yake. Popote nitakapokuwa na Tunda, nitaongeza umakini. Nitahakikisha Tunda hana kosa kisheria.” “Utafanyaje?” Mama Penny akauliza kwa haraka.
“Nyumba ya hapa, ipo chini yake.
Namaanisha ni ya Tunda. Hata leo akiniacha, nyumba ni yake kwa jina lake
kabisa. Sitamtoa Tunda hapa, nikaenda kuishi naye kule bila kibali maalumu.
Nitahakikisha nakamilisha kibali cha ‘Permanent resindence’ ili aweze kuishi kule na kuwa na uwezo
wa kuwa huku bila shida.”
“Atakuwa akifanya kazi na mimi, sio
kuwa namchukua tu hapa ili akawe mama wa nyumbani au kumfungia mahali. Hapana.
Ataishi maisha ya uhuru sio kama mfungwa. Akiwa huru kuchagua na kufanya kile
anachokipenda. Akiona hapapendi au haridhiki na mazingira ya kule, atakuwa huru
kuchagua kile anachokipenda.” Net akaendelea.
“Kujibu swali lako baba Penny. Nakwenda
kuishi na bibi. Pale ndio nyumbani kwetu au kwangu. Bibi yangu ni mtu mzima,
sina jinsi yakumuacha na kwenda kuishi sehemu nyingine, na hilo nilimwambia
Tunda. Bibi au nana kama nilivyozoea kumwita, anajua na anaelewa kuwa nina
familia, au alijua nitakuwa na familia. Anapoishi ndipo nitakapokuwa nikiishi.
Ndio maana kabla ya ndoa yetu, alitaka kupata muda na Tunda. Walizungumza nini,
mimi sijui.”
“Lakini nana alimpenda sana Tunda.
Anahistoria nzima ya Tunda, na bado alinitia moyo na kuniambia kama nataka kuwa
na maisha yenye amani hapa duniani, basi niwe na Tunda. Akatoa baraka zake
zote. Na yeye akiwa kama mmiliki mwenye kampuni ninayofanya kazi kwa sasa,
ananiruhusu kuwa na Tunda hapa, huku nikiwa na majukumu mazito ambayo
inamlazimu kuajiri mtu wa pili kufanya kazi yangu.”
“Hayo yote anafanya kwa ajili ya Tunda.
Nana anampenda Tunda na ndio maana alirudi nchini kumpigania kisheria,
kuhakikisha makosa yake yanafutwa. Tukafanikiwa mawili, moja kumbe Bethy
alificha ushahidi. Yote hayo nana amefanya kwa pesa zake ikiwa imemgarimu
mamilioni ya pesa.” Net akaendelea.
“Tutakuwa pia tukiishi na mdogo wangu,
Maya. Lakini Maya pia anampenda sana Tunda, hata Tunda anajua. Tuliishi wote
watatu Arusha. Tunda ndiye aliyemfanya Maya arudi shule. Hilo analisema Maya
kwa kila mtu, na familia yetu hawasahau hilo. Anamsubiri Tunda kwa hamu sana,
na kila wakati anauliza ni lini tutakwenda. Hao watu wawili waliobaki kwenye
maisha yangu, ndio wamuhimu, na ndio watakaoishi na Tunda na watoto wangu.
Mengine nitajua mbele ya safari.” Kimya.
“Narudia
tena. Sijawahi kuoa, wala kuwa na mama wa namna hii. Nikisema nina mipango
fulani makini dhidi ya mama yangu, nitakuwa nawafurahisha tu na kuwadanganya.
Sasa hivi yupo kimya. Sijui anawaza nini na anamipango gani mingine. Sijui
natakiwa kujipanga dhidi ya nini! Ila nimeshajua au tumeelewa kuwa nia yake
nikunitenga na Tunda, basi nikuongeza umakini.”
“Sasa
hivi hata nikisema nimuache Tunda hapa kwenu, itasaidia nini? Na kwa muda gani?
Itakuwa ndoa ya namna gani hiyo? Tunda amekubali kuambata na mimi, naombeni
mtutie moyo. Halafu Canada sio mbali jamani. Milango ya nyumbani kwetu ipo
wazi. Muda na wakati wowote, mje kututembelea, na mtushauri.” Kidogo mama Penny
akaridhika.
“Eti mama Penny?” Mama Penny akacheka kidogo. “Hapo
sawa Net. Naomba muongeze umakini tu. Tafadhali sana. Najua mnapokuwa kwenye
mapenzi machanga, mnakubaliana mambo ambayo hamfikirii madhara ya mbeleni. Sisi
tumeishi kwenye ndoa, ndio maana mnaona tupo kama tunawabana.” “Binafsi
nashukuru, japo unakuwa mkali sana kwangu mama Penny!” Net alilalamika kidogo,
wakacheka. “Hata kwangu Net. Sio wewe tu.” Tunda
akaingilia.
“Kwa kuwa nawapenda. Sitaki mkapotea, au watu
wakamfanya Tunda kama mpira wakuchezea na kuutupa popote. Hapana. Na sijui kwa
nini! Moyo wangu umefungamana na Tunda, siwezi kuhema wala kujisaidia.” “Na
hilo analolisema mama Penny sio uongo. Tumepoteza washirika wengi sana.” Akaongeza mchungaji.
“Nimeona, nikataka kuuliza kuna nini!?” Net
akaingilia. “Penny huyo! Mimi nikiwaambia naenda kumtoa sadaka, hamuamini. Heri
anyamaze tu.” Tunda akacheka na kumwangalia. “Mfunikeni jamani Penny wangu!
Pale baridi inampiga.” Tunda akamwita dada. “Naomba mfunike Penny wangu,
jamani! Ona alivyojikunja!” “Ujanja wote umemwisha!” Dada yao aliongeza huku
akienda kumchukua na kumpeleka kitandani.
“Mtoto huyu jamani! Sijui namfanyaje?” Wote
wakacheka wakati anatolewa pale kwenye kochi. “Kwani alifanyaje?” Tunda
akauliza. “Ila ujue mwanangu sio muongo.” Baba yake akamteta. “Ni mkweli
wakupitiliza Penny jamani! Na hana hofu hata!” Wote wakacheka.
“Nilimuona anamsuta mama Vero pale kanisani!” Tunda
aliwafanya waanze kucheka tena. “Na usifikiri ule ndio mwanzo. Hata yule mama
kumuona pale tena ni muujiza tu.” “Ila sidhani kama na yeye atarudi tena. Kwa
nilivyosimuliwa baada ya ibada ya leo!” Mumewe akaongeza.
“Hawezi kurudi kama wenzake.” Mama Penny
akamalizia. “Yote hayo ni Penny?” Tunda akauliza. “Dhambi zao bwana. Waache
kumsingizia mwanangu.” Mchungaji akamalizia, kisha akaanza kucheka. “Tena Pendo
nitamchapa! Anamwambia Penny anakipilipili kama changu!” Mkewe na kina Tunda
wakaanza kucheka tena mpaka machozi.
“Pendo amenishauri nichague mtoto wa kizungu, asiwe
na nywele kama za Penny, anakipilipili kama cha dad wake. Sasa sijui nachaguaje
na mtoto yupo tumboni.” Tunda aliongea huku akisugua tumbo taratibu kama
alivyomuona Net akifanya.
“Nitamtandika tu, ngoja aamke.” Baba yao aliongeza.
“Watoto hawa, naona niwagawe tu jamani!” Mama Penny aliongeza huku akifikiria. “Niambie
walifanyaje tena!” Tunda akauliza. “Si unajua mambo yako ndio yalijaa
mtandaoni?” “Askari wa pale mahabusu, Keko, walikuwa wakinionyesha na
kuniambia.”
“Basi, ukawa gumzo. Kila mtu anaongea lake. Lakini
ni kama Net akawa hayupo kwenye picha sana. Ni wewe, Gabriel na Bethy. Sasa
watu wakawa wanasema Net alikukimbia. Maana si alikuvalisha pete ya uchumba
hadharani?” “Nilipokuwa jela, niliona picha zangu mtandaoni za siku Net
akinivalisha pete ya uchumba. Nikajiuliza watu walijuaje?” “Itakuwa ni watu wa
palepale kanisani tu, ndio walianza kuzisambaza baada ya lile tukio la Gabriel
na mkewe.” Mchungaji akajibu.
“Au hata marafiki zangu na washirika wa kanisani
kwetu niliokuwa nimewaalika siku ile.” Net akaongeza huku akifikiria. “Labda.
Basi, habari ikawa hiyo kwenye mitandao. Tunda! Tunda! Sasa si Penny akawakuta
kina mama Vero na wenzie wanaangalia huku wakikusema? Penny akawasikiliza mpaka
akaridhika mwenyewe na kichwa chake. Acha aanze kuwasuta. Akawaambia Tunda ni
anti yake yeye. Ni kama mama yake wa pili. Anamjua anti Tunda, na wao ni waongo
wanamsingizia sababu ya wivu wao. Acha bwana yule mtoto awaseme wale kina
mama!”
“Akawaambia mzungu wa anti Tunda alimuoa, wala
hajamkimbia. Na yeye amesimamia harusi.” “Mama Penny!” Tunda akashangaa. “Kwani
ni madogo? Akawaambia na dad alikuwepo, yeye na Pendo walimwaga maua. Ilikuwa
harusi ya kizungu, wamefungia kwenye maua.” Wakaanza kucheka.
“Msicheke! Mtoto yule aliyaongea yote bila kuacha
hata neno. Yeye na mdogo wake walivalishwa nguo mpya, wakapanda limozini.”
“Yaani Penny!” Tunda alishika kichwa. “Akawasuta hapo na kuwaambia anaenda
kuwasemea kwa dad wake, na ibada ikianza atawatangaza kuwa wao ni wasengenyaji.
Si wakadhani anadanganya?” “Usiniambie alitangaza!?” Tunda akashtuka sana.
“Wewe si unamjua Penny? Sasa kipindi cha ushuhuda
kikaanza. Mchungaji kakaribisha watu kama leo vile. Hatujui kinachoendelea,
Penny kanyosha mkono. Baba yake akamkaribisha pale mbele tukijua ni mambo yake
ya kawaida. Acha mtoto aongee pale mbele. Niliomba Mungu ashushe unyakua siku
ile. Mtoto aliwasema vibaya yule, huku akiwashitakia kwa Mungu kuwa wao
wanadhambi kuliko shetani. Akawataja kwa majina yao wote pale mbele. Akieleza
baba yake na mama yeke ni mashahidi wa harusi ya anti wake, na wao walisimamia wala
mzungu wa anti yake hajamkimbia.” Tunda akatoa macho.
“Jamani Penny nyinyi!” “Akasema yeye anataka
watubu.” Tunda akaanza kucheka mpaka machozi. “Sasa baba Penny kwa nini
hukumpokonya kipaza sauti?” “Hivi wewe umemsahau Penny!? Mimi mwenyewe nilikuwa
kwenye mshtuko. Nilishinda kujua naendelezaje ile ibada. Maana ni kama na sisi
alitushitaki. Wachungaji, tunasimamia harusi za vichochoroni! Mambo yalianza
kanisani, kwa nini tulimalizia vichochoroni? Halafu na zile kashfa zote,
mwanangu anasema sisi tunajua. Alimsikia anti Tunda akitubu mbele ya Mungu na
dad wake. Na akasema hiyo ilikuwa mara ya pili. Alishasikia anti wake alienda
hata kutubu kwenye kanisa la mzungu wake.” Net alibaki akitingisha kichwa.
“Inamaana sisi tulikuwa tukijua yote kabla ya tukio
zima la Gabriel na mkewe halijatokea, ila tulificha au kufunika. Sijui kama
mnaelewa Tunda?” Mchungaji akauliza. “Mungu wangu Penny wangu!” “Lakini nia
yake ilikuwa nzuri, kukutetea. Yeye alisema anti Tunda alishasamehewa na Mungu
kwa kuwa alishatubu mbele ya mchungaji na Mungu. Lakini sasa watu walilaumu
sana. Wengine walisema tulikutetea ili utuletee mzungu kanisani kwetu.” “Sisi
wanafiki.” Mkewe akaongeza.
“Jamani poleni.” “Pole kubwa tu, maana kuanzia hapo
watu wakaacha kufika kanisani.” “Wala hawakuchukua muda mama Penny. Jumapili
inayofuata, nusu ya kanisa hawakufika.” Mchungaji akamalizia.
“Poleni sana jamani. Poleni na samahanini.” Tunda
alifikiria tena kidogo. “Sijui kwa nini, lakini nilijua tu, anguko langu mimi,
haliwezi kuwaacha nyinyi salama. Ndio maana sikutaka mjihusishe na sisi.” “Mama
Penny asingeweza. Alikuwa kama amechanganyikiwa. Heri ungetoka labda
ungemtuliza. Na usifikiri Penny alipoongea vile ndio ikawa basi? Na yeye
akaenda kuwaongezea.” “Mama Penny!” Tunda akashangaa sana.
“Aii! Mimi ujinga huwa siwezi. Anayetaka kuondoka
ataondoka na anaetaka kubaki abaki.” “Kabakiwa na vijana wake tu wanao mpenda.”
Mumewe akaongeza wakaanza kucheka. “Yaani mama Penny jamani!” “Na aliwawashia
moto kweli kweli.” “Sasa wewe ukasemaje?” Tunda akauliza huku akicheka.
“Ndio nilijua kibarua changu anakiotesha majani!
Nikajua washirika wote wataondoka, maana alifanya kuwapa na ushauri kabisa.
Asiyeweza kuendana na maono ya pale, yakupokea na kulea wenye dhambi, aondoke
wala hatazuiliwa.” “Mama Penny wewe!” Tunda aliendelea kushangaa huku akicheka.
Waliendelea kuzungumza hili na lile, Net na Tunda wakaondoka.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Tunda
alikuwa kimya njia nzima. Net alimuona ametulia zaidi ya kawaida yake. Akaamua
kumuacha. Walifika hotelini, akapitiliza kuoga, nakurudi kujitupa kitandani
moja kwa moja. Bado hakuwa amezungumza kitu. Hofu ya kumkuta mama Cote huko
waendako ikaanza kumsumbua. “Nini
atanizulia safari hii?” Tunda aliendelea kuwaza. “Akinifunga huko, nani atalea mtoto wangu?” Tunda akaendelea
kuwaza, asijue Net anamtizama muda wote. Na lile ombi lakutaka kusumbuliwa
kabla ya kulala pia akatupilia mbali. Akabaki amejilaza akiwaza.
Akajigeuza
kulia na kushoto akapotelea usingizini bila hata kuzungumza lolote. Alimsikia
asubuhi ameamka. Akafungua macho, alimkuta ameshavaa tayari. Alibeba bakuli la
ndizi walilopewa jana yake usiku nyumbani kwa mama Penny, akamuona anatoka. Akajua
ameenda kupasha moto. Lakini hakurudi kwa muda mrefu tu mpaka Net akaamua
kumfuata. Alimkuta amekaa nje, sehemu ya bustani akila. Akamsogelea, lakini
alikuwa akikizungusha tu kile chakula.
Net akavuta kiti mbele yake, akakaa.
Tunda akashtuka kidogo. “Sikutaka kula pale chumbani, nilijua ningekuamsha.”
“Sasa chakula sikitakuwa kimepoa?” “Hata hivyo nimeshiba. Mama Penny alikiweka
kingi. Nataka nikajiandae, niende hospitalini.” Net akabaki akimwangalia. Tunda
akajirudi. “Ungependa twende wote?” “Huo ndio ulikuwa mpango wetu. Lakini naona
umeamka na mipango mingine!” Tunda akainama na kuendelea kukoroga chakula
chake.
“Niambie kile ulichoamua Tunda.”
“Sijaamua chochote Net. Ila nikwambie ukweli tu, nimeingiwa na hofu. Maisha ya
jela sio maisha mtu yeyote angetamani kuishi. Wakati ule ilikuwa afadhali,
lakini safari hii nina mtoto! Itakuaje aje anizushie jambo jingine nifungwe?
Itakuaje kwa mtoto wangu? Mama yako anaakili sana Net. Sana. Hujui safari hii
atakuja na kitu gani. Najua unanipenda, lakini mapenzi peke yake hayawezi
kunilinda na mama yako. Tulijaribu, wewe mwenyewe uliona. Niliishia jela.” “Kwa
hiyo unataka kusema nini?” Net akauliza akiwa ameshabadilika rangi kabisa.
“Mama yako hawezi kubadilika. Atabakia
mama yako daima. Hata ufanye nini. Kama vile alivyokuwa mama yangu. Hata
nifanyeje, bado ni mama yangu tu.” “Kwa maana nyingine, wewe unaweza
kubadilika?” Tunda akanyamaza. “Ulipoapa ni katika shida na raha utakuwa na
mimi, ulimaanisha nini?” “Hapana dalili ya raha Net. Labda mama yako apate kile
anachokitaka, kwa mimi kuwa mbali na wewe. Lasivyo mimi nitabakiwa kuwa muhanga
daima. Sitaki kurudia kupita nilikopita Net, hasa sasa hivi ambapo nina mtoto
atakayekuwa akinitegemea.” Tunda alimuona mishipa ya kichwani ikisimama.
“Hapa nyumbani ndio utakuwa salama?” “Sijui
Net! Lakini angalau kwa hapa ni nyumbani na wewe unaweza kuingia na kutoka
utakavyo. Unaweza kuja kumuona mtoto wakati wowote utakao, bila shida. Naomba
mimi nibaki Net. Acha mimi nibaki tu.” “Na kuhusu sisi?” Net akauliza.
“Naomba uwe huru kuendelea na maisha
yako, ukipata mwanamke mwingine…” “Nyamza Tunda. Usimalizie. Tafadhali nyamaza
tu.” “Kweli Net.” “No. Unaniumiza tu Tunda. Naomba unyamaze tu.” Net alifikicha
macho. Akavuta pumzi kwa nguvu. “Naomba tujiandae twende hospitalini.” Net
akasimama na kurudi chumbani kwao, hapakuwa mbali.
Tunda alimuhurumia sana, lakini hakujua
chakufanya. Akasimama na kumfuta. Alimkuta bafuni akioga. Akavua nguo zake zote
akaingia bafuni alipo. Alimkuta amesimama katikati ya bomba anaangalia ukuta.
Tunda akamshika mgongoni taratibu. Akageuka. “Nakupenda Net.” “Sidhani Tunda.
Sidhani hata kama ulishawahi kunipenda.” Tunda alishtuka sana.
“Unawezaje kusema hivyo Net?” “Hivi
unajua sababu kubwa yakugombana na Gabriel, rafiki niliyekuwa naye tokea mtoto,
ilikuwa ni wewe? Ilikuwa ni heri nigombane na Gabriel kuliko kumuona hata
amekugusa. Lakini wewe upo tayari kuniona naoa!? Unawezaje hata kunifikiria
nipo na mwanamke mwingine na ukawa sawa tu!?” “Kwa sababu nakupenda Net. Sitaki
kukuona unateseka.” “Kweli Tunda!?” “Ni heri mimi niumie, kuliko kukuona
unateseka Net. Na ninajua kuwa na mimi nikujitesa tu. Ni heri uendelee na
maisha yako.”
“Naendeleaje Tunda? Niambie.
Naendeleaje? Eti unasema nikuachie mtoto wangu huku, niwe nakuja kumtembelea
kama nakwenda kutizama vivutio fulani hivi! Sijui hayo maisha Tunda. Najua
kupambana. Na ndoto zangu zote ni mimi kuhangaika kwa ajili yakumtunza mke wangu
na watoto.”
“Jana
uliniahidi tutakuwa wote, huwezi kuiachia bahati ya kuwa na mimi. Leo
umenishauri nini tena?” Tunda aliishiwa nguvu, akajiegemeza kwenye ukuta. “Nataka
kujua ukweli Tunda, unamaanisha ulichoniambia au ni hofu tu?” Tunda akabaki
kimya.
“Niambie tu ukweli. Ukweli ni upi unao
umaanisha? Ni jana au leo?” “Nimeingiwa na hofu
Net.” “Ukweli ni upi Tunda?” “Natamani kama
ingekuwa tofauti Net. Natamani tungekutana kwenye mazingira tofauti. Na wazazi
tofauti.” “Nisingekuwa ni mimi. Wapo wengi tu huko nje, wenye wazazi
tofauti. Lakini Net huyu ndiye aliyezaliwa na Ritha aliyekufunga, Tunda. Sina
jinsi yakubadili hilo.” Tunda alilia sana, hakujua ajibu nini. Net akajisuuza,
nakutoka.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Alikaa pale bafuni, mwishowe akaamua
kuoga tu. Akaoga na kutoka. Alimkuta Net alishavaa. “Itabidi leo tukatafute
nguo zako tukitoka hospitalini.” Tunda hakujibu. Alichukua lotion yake akakaa
kitandani nakuanza kujipaka taratibu, kimya kimya.
Net alifunga laptop yake akamfuata pale
kitandani. “Lete nikusaidie miguuni.” Tunda akanyamaza bila hata kumuangalia.
Net akavuta ile chupa ya lotion, akajiwekea mkononi, akaanza kumsugua taratibu
miguuni. Kuanzia mapajani mpaka kwenye nyayo. Akamuona anajilaza kwenye mto.
Akamfanyia hivyo kwa muda, akibadili
mguu mmoja kwenda mwingine. Akamuona ametulia kabisa, mpaka akahisi analala.
Akaona amshtue “Ni saa nne Tunda. Jikaze twende. Utakuja kulala ukirudi.”
Akajitoa pale kitandani, akavaa gauni jingine alilokuwa ameletewa na mama
Penny. Lilimuingia bila shida, Net akamsaidia kufunga nyuma, baada yakumbusu
mgongoni. Tunda alilisikia lile busu mwili mzima. Akafunga macho na kuvuta
pumzi taratibu na kuzishusha.
Net & Tunda hospitalini. Wajua na jinsia ya
mtoto.
Net alishauri waende wakatafute daktari
atakayewapa matibabu ya haraka. Hawakwenda mbali sana na pale hotelini
walipokuwa. Wakaanzia TMJ hospitali tena. Wakasogea mapokezi, wakamuuliza
muhudumu waliyemkuta pale na kumwambia, wanataka kuonana na daktari wa kawaida
tu kwanza. Yeyote, hawachagui. Kwa kuwa watu hawakuwa wengi sana na walitaka
daktari yeyote, wakaambiwa haitachukua muda mrefu. Net akaandikisha jina la
Tunda, wakati Tunda amesimama pembeni yake.
Walipomaliza
wakaelekezwa kwenye chumba kidogo ambacho waliambiwa Tunda atafanyiwa vipimo vya awali kabla ya
kuingia kwa daktari. Maelekezo hayo alikuwa akipewa Net. Akamgeukia Tunda
nakumshika mkono. “Twende.” Wakaongozana mpaka hapo kwenye hicho chumba. Kwa
kuwa hawakumkuta mtu nje, wakaingia moja kwa moja, wakamkuta nesi hapo ndani.
Wakamsalimia,
baada ya maswali machache tu, akaanza vipimo. Alipimwa kwanza uzito, akaja
pressure na kuangalia sukari yake. “Vipi?” Net akamsogelea nesi aliyekuwa
akimpima Tunda. “Sio mbaya sana. Umekula?” Akamuuliza Tunda. “Nimekula.” Tunda
akajibu kwa upole. “Umekula nini?” “Ndizi za kupikwa.” “Umekunywa chai?”
“Hapana. Kwani vipi?” Tunda akauliza. “Sukari ipo chini. Lakini usiwe na
wasiwasi. Jitahidi kula vitu vya sukari au niseme kula vizuri. Hata uzito wako
upo chini kwa mimba ya miezi hiyo sita karibu saba kama ulivyoniambia! Sio
uzito mzuri. Kwani unatapika?” Yule nesi akamuuliza tena.
“Sasa
hivi sitapiki sana. Ni mara chache sana kama harufu ikinikera au kuna vyakula
nimegundua nikila ndio natapika.” “Umeanza kliniki?” “Bado.” Tunda akajibu,
akamuona yule nesi ameshangaa kidogo. Hakutaka kumpa maelezo mengi. Akanyamaza.
“Muhimu kuanza. Na ukifika kwa daktari atawashauri zaidi.” Tunda akashusha
mikono ya gauni lake vizuri, akatulia. “Mnaweza kwenda kumsubiria zamu yenu
hapo nje, nesi mwingine ataita jina lako.” “Asante.” Tunda na Net wakashukuru
kwa pamoja nakutoka.
“Ungependa
nikuletee Fanta Orange? Itakusaidia.” “Nitashukuru.” Net akatoka. Tunda akabaki
amejiinamia akifikiria. Wakati ameinama akasikia wanawake waliokuwa wamekaa
kiti cha nyuma pembeni yake wakimteta. “Ni yeye.” “Hapana bwana. Wanasema Tunda
mwenyewe yupo jela.” Tunda alihamisha mawazo kwao. Kutoka kwenye kile
alichokuwa akikifikiria, akarudisha mawazo kwao, akabaki ameinama
akiwasikiliza.
“Mzungu
waliyesema kamuacha si ndie huyu aliyetoka hapa sasa hivi au siye!?” “Sijui
shoga! Nilivyosikia, alimkimbia. Ila sasa tujiulize mimi na wewe. Mimba hiyo
kaipataje na yeye alikuwa jela!? Hata kama umalaya jamani, umalaya huo umezidi!
Mpaka maafande?” Wakacheka taratibu.
“Mjini
kuishi kwa akili. Unawapa watakacho na wao wanakupunguzia adhabu.” Wakacheka. “Kwa
hiyo kwenye kupunguziwa adhabu ndio huko?” Mwenzie akamuuliza akicheka. “Kumbe!
Ndio na mimba tena! Unatoka na mtoto wa afande.” “Tatu mwehu wewe!” “Mjini
shule!” Tunda alibaki kimya akiwasikiliza.
“Mzungu
wake anarudi. Huyo! Inama kama hutujamuona.” Net akawapita, na kwenda upande wa
pili, kiti cha mbele alichokuwa amekaa Tunda. “Nimepata ya baridi.” “Asante.
Itanifaa.” Net akakaa nakuanza kumpapasa mgongoni. Tunda akamwangalia baada ya
kunywa pafu la kwanza. Macho yakagongana.
“Vipi?”
“Asante.” Tunda akashukuru. Ni kweli alimaanisha shukurani yake kutokea moyoni.
Angeficha wapi uso wake angetoka na tumbo lisilo na baba? Inamaana kile
alichokisikia pale ndio ingekuwa maneno mengine ya mtaani.
“Asante hii ni ya soda?” Net akamuuliza
kwa kumnong’oneza. “Kwa kunipenda.” Net
mwenyewe hakutegemea. Alibaki akimtizama. Tunda akajifuta machozi, akaina. Net
akambusu begani. Akamuegemea begani na kumbusu tena. Wakabaki kimya.
“Tunda Cote.”
Akasikia jina lake likitajwa hivyo. Akamgeukia Net kama anamshangaa kidogo.
Yeye ndiye aliyemuandikisha hilo jina. Akamsaidia kusimama akiwa amembebea
pochi yake na ile soda. “Twende.” Wakaongozana mlango waliosika jina lake
likitajwa.
Walimkuta daktari amekaa, Net akamvutia
kiti cha mbele ya meza hiyo ya daktari. Tunda akakaa. Net alimueleza yule
daktari mambo mengi akitaka Tunda apimwe kila kitu na kama inawezekana wajue
jinsia ya mtoto. Aliwaandikia vipimo
huku akiwaelekeza sehemu wanayoweza kufanyiwa ultrasound bila kuweka
appointment.
Tunda alifanyiwa vipimo vingi, karibu
kila kitu kwenye mwili wake. Walizunguka huku na kule, akatolewa damu na
kupeleka mkojo wakatoka kusubiria. Baada ya lisaa wakasikia tena wakiitwa
kurudi kwa daktari. Wakaambiwa hakukuwa na tatizo lolote, ila tu upungufu wa
damu na uzito upo chini sana. Wakaandikiwa dawa, wakatoka kwenda sehemu ya
kununua dawa. Net akatoa kile kikaratasi cha dawa, wakakaa nje wakisubiria.
Mama Penny akampigia Net.
Wakasalimiana. “Ndio tupo hapa hospitalini. Wamempima karibia kila
kitu, hamna ugonjwa wowote ila upungufu wa damu tu.” “Afadhali. Na mimi
nimetoka kukutana na mama anayeuza virutubisho vya GNL, ninamzigo wenu hapa.
Mkitoka hapo mpitie mchukue. Anatakiwa aanze leo, wala si kesho.” “Sawa. Lakini
tuna kituo kimoja kabla ya kuja kwako.” “Sawa.” Wakaagana, na kukata
simu.
“Mama Penny huyo!” “Nimemsikia.
Ananipenda huyo mama, zaidi ninavyostahili.” Tunda aliongea huku akifikicha
mikono yake taratibu. “Unabahati yakupendwa Tunda.” Tunda akamtizama na kuinama
akiendelea kufikiria. “Lakini lazima tumlipe. Itakuwa imemgharimu.” Tunda
hakujibu akabaki kimya. Walichukua dawa, wakatoka pale wakielekea Moroco,
kwenye sehemu waliyoelekezwa ya Ultrasaound.
Jinsia ya mtoto wao.
Walifika tena pale, Net ndiye
aliyeandikisha na kulipia. Haikuwa hospitali au sehemu kubwa. Ila garama
aliyosikia wakimtajia Net, ilikuwa juu. Tunda alitulia kimya. Wala mawazo
hayakuwa kwenye jinsia ya huyo mtoto. Binafsi hakujali. Alijiambia atakayekuja
ndio huyo huyo.
Akashtuliwa na mikono ya Net tumboni
kwake. Akamwangalia akakuta na yeye akimwangalia. “Njaa inauma?” “Naona ile
soda imenisaidia, japo natamani kula.” “Unataka kula nini?” “Nikikwambia
utamwambia mama Penny, halafu ataanza kunisema.” Wakacheka.
“Basi ngoja nikisie.” “Huwezi kupatia.”
Net akakunja uso huku akifikiria. “Mkate?” “Mikate ipo mingi. Wa aina gani?”
“Acha kunipoteza Tunda. Kwanza niambie nimepatia?” Tunda akacheka. “Maliza
jibu.” “Okay. Mkate mkavu kabisa.” “Haiwezekani Net!” Net akacheka sana.
“Usifanye mchezo na mimi.” “Hapana
bwana! Au nilikwambia?” “Wakati hutaki kuniongelesha?” “Sio kwamba sitaki, ila
sijui niseme nini Net!” “Niambie kuwa umenichagua mimi dhidi ya hofu inayo
kukabili. Hilo ndilo natamani kusikia Tunda.” Tunda akabaki kimya.
“Najua unaogopa, na mimi sijui jinsi ya
kukutuliza Tunda, kwa kuwa sijui ni nini kinatukabili mbeleni. Ila najua mimi
na wewe tutakuwa sawa, mke wangu.” Ile kuitwa mke wangu ilimfariji sana Tunda.
“Huku unakotaka kujificha, wala hutakuwa
salama bila mimi. Utamkimbia mama yangu, utakutana na mtu mwingine.
Utafanyaje?” Tunda akavuta pumzi. “Tupange kuwa pamoja na kupambana pamoja. Sio
kutengana. Ninauhakika hutaki watoto wetu wakue na mzazi mmoja. Sio kitu
kizuri. Tutatesa watoto sana.” “Hata mimi nitateseka kuwa mbali na wewe Net.”
Net akajisikia vizuri sana.
Akamsogelea karibu na kuanza kumbusu.
Kwa Tunda ilikuwa kitu cha ajabu, lakini sio Net. Alimbusu na kumbusu palepale
walipokuwa wamekaa mbele ya watu.
“Basi tusitengane. Nahitajika kazini
Tunda. Hapa ninapokwambia mambo mengi nakwamisha sababu ya kuwa hapa.” “Pole
Net, na ninakushukuru. Najua ingekuwa ngumu bila wewe.” “Na mimi najua. Na ndio
maana nipo hapa. Nimemsihi nana anivumilie.”
“Basi nenda mpaka visa yangu itoke.
Usisubirie hapa. Mama Penny yupo na mimi.” Net akainama kama anayefikiria. “Naomba
uwe na amani, Net. Kukitokea tatizo lolote, unajua mama Penny nilazima
atakupigia.” Wakacheka.
“Kweli Tunda? Unauhakika niwaache?”
“Kabisa Net. Tafadhali fanya lile unaloweza kufanya kwa sasa. Hata mwanao
atajua dad anamajukumu. Japo atamiss hiyo sauti yako.” Net akarudisha mikono
yake tumboni.
“Najisikia uzito!” “Najua. Na
ninakuelewa mpenzi wangu. Lakini huku hupotezi. Jua tunakusubiri, na tukipata
tu Visa, tutakufuata. Hata mimi naona shida kuishi bila wewe. Naisubiria hiyo
Visa kwa hamu sana.” Net akaanza kumbusu tena, mkono tumboni.
“Tunda Cote.”
Wakasikia wakiitwa. Wakasimama kwa
haraka. Safari hii wakiwa wanacheka sio kimya kimya. Wakaingia ndani na kuelezwa
kitu chakufanya na dada waliyemkuta pale kama muuguzi. Tunda akafuata maelekezo
na kupanda kitandani, ndipo mama wa kiasia akaingia. Alikuwa mchangamfu sana.
Akamtania kidogo Net, akakaa.
“Ni mtoto wenu wa kwanza?” “Ndiyo.”
Wote wakajibu. “Mnataka mtoto gani?”
Akawauliza huku akicheka. “Wakiume.” Net akajibu yeye wa kwanza tena kwa
haraka. Tunda akacheka. “Mimi yeyote. Sijali.” Tunda akajibu.
“Yeyote awe wa pili. Lakini wa kwanza
awe wakiume, Tunda.” “Wewe shauri yako kujiwekea mipaka. Utakosa raha bure
akiwa wakike.” “Hata kidogo. Tena huyo atakuwa kipenzi cha dad. Japo akianza
kaka yake sio mbaya.” Yule mama alikuwa akiwasikiliza huku akicheka.
Aliwasimulia stori ya mtoto wake wa
kwanza na wa pili, huku akimpaka jelly Tunda, tumboni. Akaanza kumtizama mtoto.
Net akasimama.
“Mnamuona anavyocheza?” Yule mama
akawauliza. “Atakuwa amesikia hiyo baridi ndio maana ameamka. Dad yake
alimbembeleza, akalala tukiwa TMJ.” “Basi ameamka. Tena ananyonya kidole.”
Wakacheka huku wakimwangalia mtoto wao.
“Atakuwa na njaa ya mkate mkavu na chai
ya rangi.” “Ngoja tumpigie mama Penny.” “Nimekwambia mtoto, Net. Sio mimi.”
Wakaendelea kucheka.
“Nani amesema anataka wakike nani
wakiume?” Yule mama akawauliza. “Mimi nimesema yeyote, dad amesema anataka
wakiume.” Wakamuona anacheka.
“Basi dad ameshinda.” Net aliruka
akishangilia. “Subiri kwanza Net. Unauhakika wa asilimia ngapi?” Tunda
akauliza. “Asilimia 97” Akajibu kwa uhakika na kuzidi kumfurahisha Net.
“Mungu wangu ni wa ajabu! Usifanye
mchezo.” Net akajisifia, Tunda akaguna. “Mnajina lake tayari?” “Nakwambia kabla
mimba haijatungwa, alishapewa jina kamili huyu mtoto.” Tunda akajibu.
Wakacheka.
Walipotoka tu, Net akampigia simu bibi
yake na Maya. Alikuwa na furaha, aliongea na bibi yake karibu njia nzima,
akifurahia. Wakampongeza Tunda na kumuuliza lini anakwenda. “Nataka huyo mtoto azaliwe kwenye hospitali aliyozaliwa babu yake na
baba yake.” Bibi Cote alisikika. “Ndio ukazane kuomba Mungu ili
Visa itoke mapema.” Net aliingilia, Tunda akacheka tu.
“Hakuna jinsi yakulipia ili
iwahi kutoka?” Akauliza bibi Cote. “Labda uende ofisi za uhamiaji
ukawaombe, uwaambie ni muhimu Tunda awepo hapo mwezi huu.”
Net alikuwa akimchokoza tu bibi yake, lakini bibi yake akachukua hilo wazo.
“Kesho nitakwenda.” “Nana!
Nakutania bwana.” “Unajuaje kama haitasaidia kuharakisha visa yao?”
Net na Tunda wakaangaliana. “Kweli utakwenda Nana!?” “Oooh
yeah! Why not? Nitamwambia Logan apige simu ubalozini sasa hivi. Ili aulizie
kama nahitaji kuweka appointment kwao au ofisi za uhamiaji.”
Hata bibi Cote alisikika amehamasika.
“Asante Nana! That’s why I love
you so much.” “I know son. Talk to you tomorrow.” Wakakata, Net akapiga
yowe. “Tunaondoka wote Tunda.” “Unajuaje?” “Namfahamu Nana. Akikusudia jambo!
Nakwambia kesho watakupigia simu ukachukue visa. Huwa hajui jibu la ‘hapana’. Na akisema atafanya kitu, ujue
atafanya tu. Subiri uone.” Tunda akacheka na kubaki akifikiria.
“Tunda
huyu anaenda kuzaa kwa wazungu!!” Tunda hakuwa akiamini. Akacheka. “Unacheka
nini?” “Siamini!” Net akajua na yeye amehamasika.
“Tonight, we gonna make love alllll
night!” Tunda alicheka sana kumsikia Net akisema watafanya mapenzi usiku kuchwa.
“Net! Kwa nini sasa!?” “Kumsherehekea Cote.” Tunda aliendelea kucheka.
Siku hiyo ilijaa furaha kwa Net,
alikuwa hawezi kutulia. Kila mtu aliambiwa Cote atazaliwa. Walikwenda kula.
Wakaenda kununua nguo za Tunda, ndipo wakaenda kwa mama Penny.
Alishampigia simu mama Penny na kumpa
taarifa za ujio wa Cote. Tunda alikuwa akicheka tu. Walikaa hapo nyumbani kwa
mama Penny wakiongea na kucheka mpaka usiku wa saa mbili, wakaondoka na
virutubisho vya Tunda. Wakarudi hotelini.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Ulikuwa usiku uliojaa furaha kwa Net,
Tunda alibaki akimwangalia tu. Kwake si kumpata tu mtoto wa kiume, bali hata
kwa Tunda kukubali kwenda naye. Tunda hakuwa akielewa umuhimu wake. Ni kwa nini
anamng’ania kwa kiasi kile! Kwa lipi? Tunda alijifikiria na kujiangalia mara kadhaa
na kushindwa kuelewa.
Kwa uzuri aliokuwa nao Net, uwezo wa
kifedha anaojua kwa sehemu anao, angeweza kuoa mtu yeyote yule, hata mtu wa
kwao, akapumzika. Kwa nini yeye? Tunda aliendelea kuwaza huku akimtizama Net.
Ukweli hakujua kucheza nyimbo za
kiswahili japo alielewa maneno, kwa hiyo alimfanya Tunda acheke katika kila
mziki wa nyimbo za kiswahili aliokuwa akicheza. Alicheza vibaya bila hata
kufuata mlio wa mziki. Ilikuwa fujo lakini ilimradi alicheza.
“Sasa furaha hiyo ni ya Cote au ni nini
Net?” “Nimepata uhakika wa kustaafu mapema.” Akaendelea kucheza, Tunda akakunja
uso. “Bwana tulia unieleweshe?” Net akambusu, na kukaa pembeni yake.
“Nilikwambia nina biashara ambayo familia tunarisishana.
Kutoka kwa mababu na mababu. Sasa imefika kwangu, ndio mimi.” “Kwani angezaliwa
wa kike si angeendeleza tu?” “Si kwa jina la Cote. Akiwa wakiume, jina
litabakia la Cote, daima.” “Net!?” Tunda akamshangaa mumewe.
“Wewe sasa hivi si unaitwa Tunda Cote?”
“Kwani lazima kubadilisha? Si angeweza kubakia kuitwa Cote tu!?” “Sisi
tumekuzwa traditional. Huku mnasema kama watu wa zamani. Bado kuna mambo
tunashikilia na kuyaamini, japo yanaonekana yamepitwa na wakati.” Tunda akabaki
akimshangaa.
“Basi kazi ipo!” “Usiogope. Ni mambo ya
kawaida sana. Utayaelewa na kuyazoea tu.” Net akambusu. “Mimi naenda kuoga
nilale Net. Upunguze fujo.” Tunda akasimama, Net akacheka.
“Sasa na lile ombi langu?” “Lipi tena
Net?” Net akasimama nakumfuata pale alipokuwa akivua nguo, akaanza kumpandisha
kigauni alichovaa taratibu huku akimbusu mgongoni.
“Net! Mimi na tumbo hili mapenzi ya
usiku kuchwa siyawezi bwana! Umeambiwa na daktari nipumzike.” “Basi twende wote
kuoga. Unipe ‘agaist the wall’, kidogo tu, tumfurahie mtoto.” “Wakati hapo ushaanza kunichokoza!” Net
alicheka sana.
Akamgeuza taratibu akaanza kumbusu
midomo yake taratibu. Alishakuwa amemtoa gauni lake, mikono ikitembea kwenye
mwili wa Tunda. Alishuka mpaka kifuani huku akimbusu shingoni na masikioni. “Asante.”
Tunda alimsikia akinong’ona masikioni. “Asante ya kuamua kuwa na mimi daima.”
Tunda akacheka. Akahisi mikono ya Net kiunoni akimpapasa juu chini, juu chini
taratibu huku akimbusu.
Akashuka kifuani kwenye matiti. Tunda alianza
kuchezesha miguu. Mikono ya Net ilitua sehemu ambayo Tunda mwenyewe alijilaza
pale sakafuni. Net akavuta mto, akamuwekea chini ya kichwa. Alimchezea mpaka
aliporidhika kuwa anaweza kuingia bila kumuumiza mkewe. Alimnyanyua miguu, hata
hakutumia muda mrefu pale chini, Tunda akamaliza.
Mikono yake ilikuwa huru kupita mbele
kwenye matiti, uke wake, na alifika kwenye hips zake pia. Alicheza na huo
mwili, akihakikisha akili za Tunda zinabaki naye pale bafuni na yeye. Mara
kadhaa alimbusu katikati ya mgongo ili kumsisimua zaidi. Na kwa kuwa Tunda
alikuwa akisimama tu, hakuwa akichoka kwa haraka, kwa hiyo Net alikuwa akitumia
muda wake atakavyo, mpaka afanikishe kwa wote.
Walitoka hapo bafuni, akamsaidia
kumkausha, wakajikuta wote wanataka tena. Ila hawakuliongelea hilo. Wakati
amekaa kwenye kochi wote wakiwa wametulia, Tunda akilipaka tumbo lake mafuta
maalumu kupunguza kupasuka au alama za michirizi inayosababishwa na kupanuka
kwa tumbo hilo kwa ujauzito, akaanza kujutia kumwambia Net anataka kuwahi
kulala. Ni kama usingizi ulipaa kwa mchezo wa bafuni.
Alijisugua taratibu kuzunguka tumbo
zima. Pembeni, chini, juu, taratibu tu huku akifikiria. Akamuona Net amepiga
magoti mbele yake, akiwa ametoa taulo alilokuwa amejifunga tokea bafuni. Tunda
akacheka taratibu. Alijua kinachofuata. Ni mtindo alioupenda sana Tunda. Kwani
hakuwa akitumia nguvu yeyote ila kufurahia tu. Net alipenda kumfanyia hivyo
zaidi alipotoka kifungoni. Ili tu kumfurahisha mkewe akiwa hatumii nguvu
yeyote.
Akamvuta kiuno mbele taratibu huku
akinyonya ulimi wake kwa kuufurahia bila papara akiwa yeye Net amepiga magoti
mbele yake, katikati ya mapaja ya Tunda. Atakapoinama hapo Net, hatatoka mpaka
mkewe awe ameridhika. Atampa ‘non penetration’ mpaka afike kileleni akiwa amejilaza nyuma, ameegemea kochi
akimpa uhuru wote Net. Na yeye alijua mikono ipite wapi na midomo ili tu
kumfurahisha mkewe.
Taratibu huku Tunda akinung’unika taratibu na vidole vya Net
vikiongeza ladha ya tendo zima, Tunda hakuchukua muda, akakamilisha hiyo
safari, ndipo akamuinamisha ili kupata, ‘rear entry.’
Hapo Net alikuwa akiingia taratibu akiwa amemuinamisha mkewe, amemshikilia kwa
upendo. Aliingia na kutoka kwa hisia zote, taratibu kuhakikisha hamuumizi ili
asimtoe kwenye furaha aliyompatia muda mfupi uliopita.
Ulikuwa usiku wa namna yake kwa wote wawili. Hawakukesha, lakini walilala wote wakiwa wameridhika. Furaha ndiyo iliyowapoteza kwenye ulimwingu huu na kuwapeleka kwenye ulimwengu wa usingizini.
Viza ya Tunda
Ilishakuwa saa 9 za mchana nchini
Canada, wakati simu ya Net ikiita nchini Tanzania saa moja asubuhi. Net
akashtuka kutoka usingizini, akaimbilia pale alipokuwa ameiacha mezani ili
asimuamshe Tunda. Ile shtuka ya pale kitandani, hata kabla hajafikia hiyo simu
yenyewe, Tunda alishtuka akakaa.
“Net bwana! Tulisema tuwe tunazima
simu.” “Pole, pole.” Net alinong’ona. “Sasa unanong’ona nini wakati
umeshaniamsha!?” Net akacheka na kupokea. Namba ilikuwa ngeni kwake. “Nethaniel Cote!” Akaanza Net. “Tunataka kuzungumza na Tunda.”
Ilisikika sauti ya mwanamke aliyezungumza kwa lugha ya kigeni. Net aliweza
kugundua lafudhi ya nyumbani kwao. Akacheka huku akimsogelea Tunda. “Just a minute.” Akajibu
Net.
“Ongea nao Tunda.” “Mimi!?” Tunda
akashangaa kwa woga. “Itakuwa ubalozi wa Canada. Ongea, usiogope.” Tunda
akachukua simu. “Tunda Cote.” Tunda alianza hivyo kama Net na
kumfurahisha sana Net. “See!” “Shhhh!” Tunda akamnyamazisha Net huku akicheka.
Alisikia wakimuuliza Tunda maswali
kadhaa, naye akijibu akisikika ametulia. Mwishowe akaambiwa akachukue Visa.
Tunda hakuamini. Akashukuru na kukata simu. “Mungu wangu Net! Wamenipa Viza.”
“Huyo ni Nana tu. Nilijua tu atafuatilia.” Net alifurahi sana.
Akachukua simu kutoka kwa Tunda, na
kumpigia simu bibi yake bila kupoteza muda. Akapokea huku akicheka. “Nilijua tu utanipigia.” “Asante Nana. You are the best!” “Sijasikia
Net. Umesemaje?” Net akaanza kucheka. “Usinifanye nirudie bwana. Najua umenisikia.”
Wakataniana na bibi yake hapo.
“Sasa juhudi zangu zote, ni
Tunda afike huku mapema. Aonane na daktari wa wakina mama. Tufanye vipimo vya
uhakika.” “Tunataka twende honeymoon kwanza, Nana!” “Hapana Net. Hospitalini
kwanza. Wakiona kila kitu kipo sawa, mtakuwa huru kwenda popote.” Bibi
Cote akaweka msisitizo.
“Tunda na mtoto walikuwa kifungoni kwa miezi
sita! Hatujui kwa hakika mtoto ana hali gani. Hatuwezi kuzembea halafu tuje
kusema, ‘tungejua’. Sitakubali uzembe wowote
utokee, Net. Lazima kujiridhisha kuwa Tunda yupo salama na anauwezo wa kumbeba
huyo mtoto mpaka mwisho, na Cote mwenyewe azaliwe salama.”
Kwa ile furaha ya kuondoka na mkewe, Net alikubali kila kitu.
Tunda naye akapata nafasi ya kushukuru.
Akamuuliza maswali waliyomuuliza watu wa ubalozi, Tunda akawa anamwambia
maswali na vile alivyojibu. “Lakini maswali mengine nilikuwa
sina majibu yake, niliwajibu sifahamu.” “Swali gani?”
Akauliza bibi Cote.
“Kama mji ambao nategemea
kuishi. Sikuwa na jibu.” Akamsikia akicheka. “Nilishawaambia utakuwa hufahamu mambo mengi, lakini niliwaambia Net
atakuwa na wewe safarini.” Wakazungumza tena kidogo. Tena kwa
urahisi tu, bibi yule akimuhakikishia hata asingewajibu chochote zaidi ya
kutaja jina lake pia wangempa hiyo Viza. Wakacheka kidogo na kuagana.
Tunda akabaki akijiuliza familia hiyo ni familia gani
inayoweza kuamuru mambo kama hayo na kutokea! “Huyu Net ni nani haswa!? Anatoka kwenye ukoo wa namna gani!?”
Tunda akajiuliza. Safari hii akimtizama Net kwa jicho la pili.
Ni jana yake tu Net ndipo alipomwambia
bibi yake labda aende ubalozini. Tena kwa utani. Kesho yake anapigiwa simu na
kufanyiwa usahili na ubalozi wa Canada akiwa kitandani kwake! “Mmmh!” Tunda akaguna mawazoni.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Net ndiye aliyekuwa na hati ya
kusafiria ya Tunda. Walitoka hapo. Wakaenda kulipia na kupeleka hiyo hati
kwenye ofisi za ubalozi wa Canada, wakaambiwa wafuate baada ya siku mbili.
Wakaacha hapo hiyo hati, wao wakaondoka. Hapo hapo Tunda akampigia simu mama
Penny nakumuelezea kila kitu.
Gafla hofu wote iliwaisha, ikawa ni
furaha tupu. “Tutakuja kuwaaga vizuri nyumbani. Acha nikuage kwa
sasa, ili nimpigie simu baba, nimuage.” “Utakuwa umefanya vizuri. Kwani mnaondoka
lini?”
Mama Penny akauliza. “Sijui Net. Lakini bibi yake ametaka iwe mapema, ili
nikaonane na daktari wa wakina mama.” “Nakwambia umeukata Tunda! Unaenda
kuzalia uzunguni!” Tunda alicheka sana.
“Mimi mwenyewe siamini dada
yangu. Hilo swali nilishajiuliza. Kama utani!” “Hongera mdogo wangu. Hongera
sana.” “Ninafuraha yakupita kiasi mama Penny.” “Nakusikia.” “Tutaongea zaidi
baadaye. Acha nimtafute baba. Natamani aje huku anione kabla sijaondoka.” “Muombe.”
“Eti eeh?” Tunda akaona ni wazo zuri.
“Kabisa. Baba yako ni mtu mzuri
sana Tunda. Ni hivyo nahofia kusafiri kwako, ningekushauri umfuate huko alipo
ukamuage. Upo dhaifu sana kwa kusafiri safari ya Kigoma. Ni muhimu muonane
kabla hamjaondoka. Mwambie ungetamani kwenda lakini daktari amekushauri
mapumziko, unamuomba yeye ndio aje?” Mama
penny akampa hilo wazo. “Nashukuru. Basi ngoja nimpigie.”
Wakaagana.
“Nataka kumpigia simu baba.” Akamgeukia Net. “Nimesikia.
Mwambia tutamtumia tiketi ya ndege ili aje huku muagane.” “Kwani ulitaka
tuondoke lini?” “Kwa kuwa tumeshapata uhakika wa Viza, naomba tusisubiri Tunda.
Tuondoke tu niwahi kazini kidogo. Niweke mambo sawa wakati daktari akishugulikia
mambo yako na mtoto, kisha ndipo twende mapumzikoni.” “Ndio lini sasa?”
“Tukipata hiyo Visa asubuhi, tuondoke
na ndege ya usiku wake. Nitawapigia simu, niwaambie watukatie tiketi yakuondoka
hapa usiku ili kusiwe na kuchelewa ndege.” Tunda akakunja uso. “Nani Tena?”
“Yupo mtu ofisini ambaye anashugulikia safari zetu. Usiwe na wasiwasi. Wewe jua
kesho kutwa tunaondoka.” Tunda akatulia kidogo akifikiria hili na lile juu ya
maisha hayo mapya anayokaribia kuanza kuyaishi. Kidogo akawa kama haamini kama
ni yeye.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Akaamua kumpigia simu baba yake. Iliita
mara moja tu, akapokea. “Ni mimi baba.” “Hospitalini wamekwambiaje?” “Kila
kitu kipo sawa. Nimejua jinsia ya mtoto wangu.” “Wetu Tunda! Mbona
hivyo?” Net akaingilia. Akamsikia baba yake akicheka.
Net akampokonya simu, “Mtoto ni wakiume. Anaitwa Cote Junior Cote au CJ Cote the 4th.
Shikamoo.” Akarudisha simu kwa Tunda. “Nakwambia Net
amefurahi huyo! Kila saa anacheka.” “Namsikia! Naona na majina yote kwa kirefu
na kifupi pia anayo huyo mtoto!” Baba yake akajibu. Tunda akacheka na
kuongeza. “Alikuwa nayo hayo majina hata kabla mimba yake
haijatungwa!”
“Hongereni sana. Nawaombea mtoto
akue vizuri na wewe uwe na afya njema.” “Asante baba. Lakini tunaondoka.
Tunaenda kuishi na Net. Canada.”
Kimya. “Baba!” Tunda akaangalia simu yake. “Nipo mama. Nakusikiliza.” “Nilitaka tuonane kabla sijaondoka.
Angalau nikuone. Net amesema atakukatia tiketi ya ndege uje hata kesho, maana
tunaweza kuondoka kesho kutwa usiku.” “Napanda ndege mama!?”
Tunda akacheka.
“Nitafurahi kukuona kabla
sijaondoka baba.” “Sawa. Tena kwa ndege ndio itakuwa rahisi. Nitawahi kuja
kuwaona kabla hamjaondoka.” Wakazungumza wakipeana mipango ya hapa
na pale, wakaagana.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
“Mbona sasa ni kama umekosa raha?” “Sio
mimi. Baba anaonekana kukosa raha. Hakufurahia kusikia ninataka kuondoka.”
“Nisikilize Tunda. Watu wote wanaokuzunguka bado wanakumbuka kilichokupata,
hasa akiwa aliyesababisha ni mama yangu mimi.”
“Kitendo chakuondoka hapa nchini, mama
akiwa hajulikani alipo, kila mtu anakuhofia ni kama unaenda kuyafuata
matatizo.” Tunda akainama akifikiria. “Natamani kukuahidi mambo mengi ili tu
kukufariji, lakini naomba unipe nafasi nyingine. Sitaki kukwambia mengi, lakini
naomba uniamini hata mimi nimeongeza umakini. Sijui kinachotukabili mbeleni,
ila naamini kile alichoniambia hata bibi yangu na kile ninachojisikia. Maisha
yangu hapa duniani, nitayafurahia nikiwa na wewe.” Tunda akamwangalia.
“Naomba wewe utulize mawazo. Tupokee
siku moja hadi nyingine kwa shukurani bila hofu ili tusiishi maisha yasiyo na
maana. Naamini tukishikamana, kila kitu kitakwenda vizuri. Sawa?” Tunda
akatingisha kichwa kukubali.
“Naomba unijibu Tunda.” “Sawa.” “Mbona
huongezi neno?” “Kwa kuwa naogopa Net! Sijui ni nini kitanikabili huko ugenini!
Nimekubali kukufuata, kwa kuwa tu najua siwezi kuwa na furaha mbali na wewe.”Tunda
akajiweka sawa kuweka msisitizo.
“Tafadhali usije kusahau hilo.
Nakufuata wewe. Usije ukafika huko, ukapata watoto, ukanisahau mimi.” “Siwezi
Tunda. Sitaki watoto bila wewe.” “Basi naomba hilo usije ukalisahau tafadhali.
Nikumbuke kila wakati na kwa kila utakalofanya. Jua Tunda yupo na wewe kwa kuwa
nakuhitaji wewe. Naomba nikose kila kitu, ila niwe na wewe. Siku
nitakayokukosa, ujue ndio umenimaliza Net.” “Mungu atanisaidia Tunda. Nakuahidi
siwezi kukuacha.” Tunda akavuta pumzi kwa nguvu, nakujiweka sawa pale kitini
akageukia dirishani.
Gafla ile furaha waliyokuwa wameamka nayo asubuhi, ikapotea
kwa simu moja tu aliyozungumza na baba yake. Na yeye akamtia hofu kama ya mama
Penny na mumewe. Akabaki akiwaza lakini alishaamua atayavulia maji nguo.
Baada ya ya miaka Mingi, Tunda & Baba yake
Uraiani .
Yohana alimuacha binti yake hospitalini
akiwa mgonjwa, akafungwa. Tunda akamuacha baba yake akiwa mgonjwa gerezani,
akisubiri atoke, na yeye akafungwa.
Baada ya miaka mingi tokea wawe pamoja
uraini. Tena wakikutanishwa na matatizo tu. Sasa hivi wote wakiwa huru,
hatimaye maisha yanawapa fulsa nyingine ya kukutana, lakini kwa ajili ya
kuagana tena. Siku inayofuata baada ya kuzungumza na baba yake kwenye simu,
nakupanga hiyo safari, Net alimsindikiza mkewe uwanja wa ndege kumpokea baba
yake.
Walikuwa wamemchukulia chumba palepale
hotelini. Yule mzee alishtuka sana kumuona Tunda. “Unakula kweli!?” Akamuuliza
Tunda. “Hapa nina nafuu baba. Muulize Net. Nilitoka nikiwa nimechoka zaidi ya
hivi.” “Mmmh! Umebaki tumbo tu! Huyo mtoto utambebaje kwa hali hiyo!?”
“Najitahidi kula, baba. Pole na safari.” “Asante. Nimepanda ndege, wala
sijachoka.” Tunda akacheka. Net naye akasogea akamsalimia.
“Mbona mzigo ni wa samaki tu?” “Sina
kingine.” “Si utakuwa huku mpaka niondoke?” “Ndiyo.” Tunda hakuwa ameelewa,
lakini akaona hilo alinyamazie. “Twende kwenye gari. Umekula?” “Hapana.” Baba
yake akamjibu huku akimwangalia kama ambaye haridhishwi kabisa na afya ya
mwanae. “Nitakuwa sawa baba. Usiwe na wasiwasi. Huu mwili utarudi tu. Ndio
nimetoka jela hata mwezi sijamaliza!”
“Na huo ndio wasiwasi wangu. Unakwenda
ugenini huko, unaanza vyakula vyakigeni. Hujui kama utapenda au la! Mwili
wenyewe hamna! Mpaka uzoee, unatakiwa ujifungue. Utaweza kweli?” Tunda kimya
huku wakielekea kwenye gari.
Gafla wakamuona anakimbilia pembeni
nakuanza kutapika. Net akamsogelea. “Vipi?” Alitapika mpaka akakaa chini. “Vipi!?”
Baba yake naye akamuuliza. “Nahisi ni hao samaki. Harufu imenichefua.” Wote
wakaangalia lile boksi lililofungwa vizuri la samaki.
“Unataka tuwatupe?” Baba yake
akamuuliza. “Tumpelee mama Penny. Atafurahi sana. Kwanza anakupikia chakula.
Anataka nikupitishe kwake ukale kwanza.” Tunda alimaliza kuongea vile huku
akijaribu kusimama. Net akamsaidia.
“Pole. Bado tu kutapika?” “Sio kila
siku na kuna harufu na harufu huwa zinanikera. Naomba nyinyi mtangulie na gari
mimi nitawafuata na taksii.” Net akatoa macho. “Kweli Net. Nitatapika njia
nzima. Naomba niwafuate kwa nyuma. Mkifika mwambie mama Penny awafungie kwenye
friji mpaka nitakapoondoka.”
“Siwezi kukuacha hapa Tunda!” “Huniachi
Net. Nawafuata na taksii. Wewe mpeleke baba.” Tunda akageuza palepale akielekea
sehemu zilipo taksii, akawaacha Net na baba yake wakishangaa.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
“Hili wazo lakumchukua Tunda akiwa na
hali hii, linatoka kwake au kwako?” Lilikuwa swali la kwanza alilolirusha baba
yake Tunda mara baada yakuingia kwenye gari. Net alitulia kidogo akifikiria
jibu sahihi kwa huyo mzee kijana. Alikuwa mkimya kama mwanae Tunda. Na
walifanana, hapakuwa na swali.
Net alisafisha koo mara kadhaa,
akajiweka sawa huku akiendelea kutafuta njia yakumtoa kwenye sehemu zakuegeshea
magari pale uwanja wa ndege. Walisogea mpaka sehemu yakulipia, akalipia bila
kujibu swali.
Waliona taksii iliyombeba Tunda mbele
yao. Net akamtizama baba yake Tunda baada yakupokea risiti ya pesa aliyolipia
yakuegeshea gari pale uwanja wa ndege. Akavuta pumzi mara kadhaa huku
akifikiria.
“Tunda ni mke wangu.” Alianza kujieleza
Net. “Maisha yangu yapo Canada. Siwezi kumuacha hapa yeye na mtoto. Lazima niwe
naye karibu.” “Unajua mama yako alipo?” Swali lililofuata lilimfanya Net abaki
kimya nakushindwa kujibu. Hapakuwa na maongezi yeyote humo ndani ya gari lao.
Net akanyamaza, na baba yake Tunda akanyamaza.
Walipofika mataa ya Buguruni kutokea
Tazara, yule mzee akamgeukia Net. “Watu wanajua ipo jela. Lakini hawajui
kinachoendelea humo ndani. Hata kama wakijua, ni kwa kusimuliwa, lakini sio
kuishi. Aliyeishi gerezani ana habari tofauti na aliyeishi mahabusu. Huwa
havilingani.” Akaendelea taratibu tu.
“Ni maisha ambayo kama una roho ya
kawaida kama Mungu alivyokusudia kwa mwanadamu yeyote awe na aina hiyo ya roho
ya kibinadamu, basi, usingependa mtu yeyote yule aishi huko. Na wengi wakitoka
humo, huwa hawatamani kuja kurudi tena gerezani.” Akamaliza baba yake Tunda, na
yeye akanyamaza.
Walifika kwa mama Penny, akawaambia
Tunda yupo chooni akitapika. Bila kujibu, Net akaelekea kwa haraka ilikokuwa
ikitokea sauti ya kutapika kwa Tunda huko chooni. Baba yake alikwenda kukaa sebuleni
bila hata salamu ya kueleweka. Maana sauti ya Tunda ilisikika nyumba nzima.
Baada ya muda yeye na Net wakatoka
chooni. “Wakati nyinyi mnakula, naona mimi nikajilaze hapo kwenye kitanda cha
Penny. Nasikia mbavu zinauma!” “Utataka kula nini ukimka?” Mama Penny akamuuliza. “Labda uji. Chakula
kabisa, naona hakitapita.” “Basi uji ukiiva, nitakuja kukuamsha.” Mama Penny
akarudi jikoni.
“Baba, nakwenda kupumzika kidogo.
Nikiamka, tutapata muda wa kuzungumza kidogo.” “Sawa.” Baba yake akajibu, kisha
akabaki kimya bila yakuongeza neno. Net akamsindikiza chumbani.
“Pole.” Tunda akacheka. “Muone sura
yake. Umepooza!” “Nilikuwa sijawahi kukuona unavyopata shida!” Tunda akacheka
huku akijiweka sawa pale kitandani kwa Penny. “Acha nilale kidogo.” “Pole.” Net
akarudia tena. Tunda akajua ameingiwa hofu.
“Nitakuwa sawa tu. Wewe nenda kale.”
“Nataka kukaa hapa na wewe.” “We Net! Acha woga bwana! Nenda kale. Mimi nipo
sawa.” “Unauhakika?” “Kabisa. Mimi nitakuja huko sebuleni muda si mrefu.”
Akambusu nakutoka.
Baada ya kama lisaa, Tunda akaamka.
Alimkuta Net amekaa pembeni ya kitanda ameinamia simu yake. “Net!”
“Unajisikiaje?” “Njaa. Sasa hivi natamani kunywa uji.” “Mama Penny alishapika,
ila nilimuomba akuache upumzike kidogo.” “Afadhali. Baba yuko wapi?” “Yupo hapo
sebuleni. Twende.” Wakatoka.
“Vipi?” “Sasa hivi nasikia njaa.
Umekula?” “Mama Penny ametulisha hapa, nasinzia kwa shibe.” Akacheka na kwenda
kukaa pembeni ya baba yake. “Jitahidi kula.” “Nikipata kitu ninachokipenda,
huwa nakula sana tu. Hata leo asubuhi nilikula vizuri.” Baba yake akabaki
kimya. “Nitakuwa sawa baba.” Alimwangalia akanyamaza.
“Vipi biashara?” Tunda akaendelea
kumuhoji taratibu. “Mwanzo mgumu. Ndio mara ya kwanza naanza biashara. Kuna
kukosea kwingi, lakini naamini baada ya muda mambo yatakaa sawa. Nitakuwa
mzoefu. Halafu pia ndio kama naanza maisha. Kwa hiyo bado.” “Utafanikiwa baba.”
“Naamini hivyo.” Tunda na baba yake walikuwa wakizungumza taratibu wakiwa wamekaa peke yao pale sebuleni.
Net akatoka jikoni na bakuli la uji. “Huu
uji unanukia vizuri, itabidi tubebe. Asante mama Penny.” “Afadhali kama
umeupenda. Nakuja sasa hivi, nawaandalia kina Penny chakula, ili wakitoka
shule, wale.” Tunda akaanza kucheka.
“Unacheka nini?” Mama Penny akamuuliza
akiwa jikoni. “Penny wangu anaendeleaje? Ameacha maneno?” Akamsikia mama Penny
akicheka, kisha akawafuata pale sebuleni.
“Kafanya nini tena!?” Tunda aliuliza
huku akiendelea kucheka. Alimjua Penny kwa vituko. “Mbona alitukomesha!” “Nini
tena?” Tunda akauliza huku akinywa uji. “Siku ile ya jumapili mlimuacha hapa
kalala, akaamshwa jioni, akaoga akarudi kukaa palepale. Kimya. Basi sisi
tukamshukuru Mungu, somo limeeleweka. Sasa shuguli ilitupata usiku.
Hatukulala.” “Kwa nini tena?” “Ndoto!” Tunda na Net wakaanza kucheka.
“Jamani Penny alilia yule mtoto! Mbona
nyumba nzima tuliamka! Eti anaota watu wanamla nyama, wengine wanamnyonya damu.
Haya, mimi na baba yake tukamuhamishia chumbani kwetu, ikaanza kazi
yakubembeleza.” Mama Penny akaguna.
“Na kubembelezwa huko ni amepakatwa na
baba yake. Anamlilia baba yake anamwambia yeye alifikiri anampenda, lakini
kumbe anataka kwenda kumtoa sadaka! Hapo analia kwelikweli! Anamwambia eti
ingekuwa yeye asingemtoa baba yake sadaka.” Walizidi kucheka, mpaka Tunda
akaweka bakuli la uji chini.
“Basi, ndio ikabidi baba yake amwambie
ukweli kuwa tulikuwa tunamuogopesha tu, hata iweje, hawezi kumgawa. Mtoto
alifurahi huyo!” Wakazidi kucheka. “Karudia hali yake ileile. Tena sasa hivi
usemi wake ni baba yake amemwambia anampenda sana, hata iweje, hamtoi sadaka.
Na dad wake anampenda kwa kuwa anongea ukweli. Anamtangazia kila mtu eti hata
umpe dad wake mamilioni ya pesa za kimarekani, hakuuzii Penny wake.” Tunda na
Net walizidi kucheka.
“Basi imekuwa shida! Huna
utakalomwambia akanyamaza. Anakuja sasa hivi. Utapata habari za tokea anatoka
hapo getini asubuhi mpaka anarudi hapa.” Mama Penny akarudi jikoni akawaacha wakicheka.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Wakiwa njiani Tunda akamgeukia baba
yake. “Tumekuchukulia chumba pale tunapoishi kwa sasa.” “Asante.” “Sasa utavaa
nini?” Akatulia. “Ulisahau nguo?” Tunda akauliza tena. “Nilipotoka jela,
nilikuta mama Chale amegawa na kuuza nguo zangu zote na viatu. Nikajinunulia
baadhi tu, ambazo zimegeuka za kazi huko nilipo. Kwa kuwa sina pakwenda
isipokuwa kazini tu. Zisingefaa kuja nazo huku.” Alijibu huyo mzee taratibu tu.
“Basi twende tupitie madukani ununue.”
“Twende mpaka huko hotelini, nitawaacha mimi nitoke nikajinunulie.” “Kwa nini?
Nataka muda na wewe baba.” Tunda alimgeukia baba yake. “Naona umedhoofu sana.
Unahitaji kupumzika, Tunda.” “Mimi nipo sawa baba. Twende tu. Nitapumzika
usiku.” Wakatoka hapo na kuelekea madukani.
Baada ya kupata nguo zake, na Tunda
kuridhika, ndipo wakarudi hotelini. Ilishakuwa jioni, kila mmoja wao alisema
ameshiba, ila Tunda alisema atakunywa uji wake akisikia njaa tena. Kwa hiyo
hawakuona sababu ya kwenda kula tena kwa kuwa Tunda alikuwa na chakula chake,
ikawa inatosha.
Baba yake alipoingia chumbani kwake na
Tunda pamoja na Net wakaingia chumbani kwao. Tunda alioga kwa haraka bila Net,
akamwambia anataka kwenda kuzungumza na baba yake kabla hajalala. Net
akaridhia.
Alifika kwenye chumba alichokuwepo baba
yake, akagonga. Baba yake akafungua akionekana na yeye ameoga na kuvaa t-shert
moja wapo aliyomnunulia Tunda. Nyeupe. Tunda
akacheka wakati anaingia. “Umependeza.” “Nakushukuru.” Tunda akaenda kukaa.
“Biashara yako na wewe inaendaje?” Akamuuliza Tunda. “Mama aliichukua.” Baba
yake akakunja uso. “Kivipi tena!?” “Kabla ya kwenda jela, nilimtambulisha
kwenye ile biashara. Nikamwambia kwa sababu alifukuzwa kazi, anaweza kuwa
akiifanya ile biashara ya kupamba. Basi nikaanza kwenda naye kazini, lakini
sikufanya naye muda mrefu ndio nikakamatwa nikiwa nimemuonyesha ofisi na
kumtambulisha pale kama mama yangu. Kwa hiyo nilipofungwa, yeye ndio akawa
mmiliki badala yangu.”
“Mama Penny anasema alibadili jina la
kampuni yangu ikawa kwa jina lake. Akatafuta mpangaji pale kwenye ofisi yangu
nilipokodisha, nasikia walimlipa pesa, akahamisha ofisi. Sijamsikia kwa muda
wote nilipokuwa jela, na mpaka nimetoka. Anavyo vyombo vyote na mapambo yote.”
Baba yake akainama.
“Ndio maana umeamua kuondoka hapa
nchini?” Baada ya muda baba yake akauliza. “Sio kwa sababu hiyo baba. Tokea
mwanzo nilitaka kumuachia kwa kuwa tulipanga baada ya kufunga ndoa mimi na Net,
niondoke naye, tukaishi pamoja Canada.”
“Wala huna haja yakumtetea mama yako.
Namfahamu vizuri sana zaidi ya unavyomfahamu wewe. Linapokuja swala la pesa,
huwa hana undugu.” “Simtetei baba. Nakumbuka hata wewe nilikwambia wakati ule
kuwa nitaondoka na Net. Labda umesahau kwa kuwa ni kipindi kile ulipokuwa
mgonjwa kule gerezani.” “Nakumbuka sana tu.” Baba yake akajibu.
“Nampenda Net, baba. Hakuna mtu ataweza
kunipenda, kuniheshimu na kunijali kama Net, baba yangu. Kwa sifa zote mbaya
nilizonazo, bado ananing’ang’ania!” Baba yake akamtizama.
“Halafu kumbuka makuzi yangu. Nimekuwa
kwa kutangatanga. Mara leo niishi kwako. Kesho nihamishiwe kwa mama! Na kote
mambo hayakuniendea vizuri mpaka kuishia jela. Sitaki mtoto wangu aje awe mtu
wa kutanga tanga. Nimejiambia japokuwa naogopa kwenda, lakini kwa ajili ya
mwanangu, heri niitumie hii nafasi yakuwa na baba yake. Mtoto wangu apate
familia yakueleweka, kitu nilichokosa mimi.” Tunda akaendelea kujitetea kwa
baba yake, taratibu tu. Baba yake kimya akimsikiliza.
“Hata hivyo kwa sasa sina jinsi baba.
Nina mtoto wake. Mimi sina kazi wala uwezo wakulea huyu mtoto, namtegemea yeye
ambaye ana kazi huko Canada.” “Na mama yake?” Baba yake akamuuliza.
“Ni wapi nitakapoishi nitakuwa salama,
baba? Nilikuwa hapa nchini, nyumbani kwetu, na bado yule mama alinikamata na
kuniweka jela. Wapi najificha nitakapokuwa salama? Ni aidha nijifiche niishi
kwa shida, au nikaishi na Net kwa furaha hata kama itakuwa ya muda mfupi.”
“Umezingatia afya yako lakini? Kwa nini
usisubiri mpaka ujifungue, upate nguvu, ndipo mfuate? Itakuaje ufike huko
halafu mazingira yakawa mabaya? Ukakutana na watu watakao kunyanyasa?”
“Net hawezi kuruhusu mtu aninyanyase na
yeye akiwepo. Halafu kama nikiona mambo sio mazuri, nitarudi baba. Sidhani kama
watakuwa wakinifungia. Tutakuwa tukiwasiliana. Ukiona kimya hata kwa siku tatu
tu, naomba uchukue hatua.” “Labda hivyo. Nakuhofia Tunda!”
“Naomba katika hili uniunge mkono baba
yangu. Namuhitaji Net sasa hivi kuliko
zamani. Nahisi nitachanganyikiwa akiondoka na kuniacha hapa. Ananipenda na
kunithamaini jinsi nilivyo.” Baba yake akavuta pumzi kwa nguvu na kujivuta
nyuma, akaegemea kochi.
“Utakuja kuniona?” Baba yake akacheka. “Ndege
yenyewe ndio nimepanda leo!” Tunda akacheka. “Hata passport sina!” “Naomba
uanze kushugulikia baba. Siwezi kuwa huko ugenini peke yangu wakati wote.”
“Kwani hurudi tena?” “Sidhani kama
itakuwa kwa haraka. Kumbuka nitakuwa na mtoto. Net hawezi kukubali nianze
kumzungusha mtoto huku na kule akiwa mdogo. Nilikuwa nikimsikia akimwambia
mchungaji kurudi huku ni mpaka angalau mtoto akifikisha miaka 3 ndio tunaweza
kurudi kutembea kama hapatakuwa na dharula.” Baba yake akatulia.
“Mbona hujibu baba?” “Huko mbali Tunda.
Mambo yangu hayajakaa vizuri. Nimekuwa kama nina mkosi, sijui! Ile pesa
niliyolipwa, ni kama imepotea yote.” Tunda akashtuka sana, akamgeukia vizuri
baba yake.
“Kuna mtu aliniambia tufanye naye
biashara hiyo ya dagaa. Akaniambia itatulipa kama tukifanya sisi wenyewe. Yaani
tusimamie sisi wenyewe. Ikiwezekana twende hata sisi wenyewe ziwani. Akashauri
tununue ngalawa ya kisasa na vifaa vingi vya uvuvi, tena vya kisasa. Sasa
nikamwamini kwa kuwa ni mtu wa nyumbani, tumekua pamoja kabisa. Halafu yeye ni
kama alikuwa anauzoefu wa hiyo biashara. Kwa kuwa alishafanya hiyo biashara
zamani. Au niseme alikuwa na hiyo biashara zamani akakwama. Nilipomuuliza kwa
nini aliacha, akasema kilichomkwamisha ni pesa, mtaji ulikuwa mdogo, hakuwa na
mtaji mzuri.” Baba yake akajicheka.
“Ikawaje?” Tunda akauliza. “Ndio
nikampa pesa yote aliyotaka ili akanunue hivyo vifaa ili tuanze hiyo biashara.
Baada ya siku tatu akarudi akaniambia ametapeliwa pesa yote. Labda nimpe pesa
nyingine. Akaniapia safari hiyo atakuwa mwangalifu. Na ujue mwanzoni nilikuwa
nimempa pesa nyingi tu. Basi, kwa kumuamini nikampa tena pesa yote niliyokuwa
nimebakiwa nayo.”
“Mbaya zaidi, nilimkabidhi bila
kuandikishana wala shahidi. Kwa hiyo akawa anayo pesa yangu yote. Akaondoka.
Kukawa kimya. Baada ya mwezi na siku kadhaa, naambiwa na watu ameanza au
amerudia biashara ileile, ila safari hii kwa hali ya juu.”
“Hivi hapa tunavyozungumza, ameshaanza
kuleta dagaa mpaka huku Dar. Kwa kifupi, amefanikiwa vizuri sana kwa pesa yangu
yote.” Tunda aliumia sana. Akajichukia kuona anafanana na baba yake mpaka tabia
za kuamini watu hovyo.
“Pole baba.” “Nahisi nina udhaifu ambao
natakiwa kuufanyia kazi. Na kazini ilikuwa hivyo hivyo. Nimeamini watu mpaka
wakanitia matatizoni. Isingekuwa wewe, mpaka sasa hivi ningekuwa jela kwa kosa
lakusingiziwa.”
“Hapa nimeanza biashara ingine kwa
kuuza kwa hasara gari aliyokuwa amenipa Net. Nilijaribu kuifanya taksii
kulekule Kigoma, nikaona sipati faida, inakuwa inanifilisi tu.” Tunda hakutaka
kuendeleza yale mazungumzo. Nitakuachia pesa ya kushugulikia hati ya kusafiria
baba. Naomba utengeneze hati, uwe nayo tu. Siku nikikuhitaji uje, kusiwe na
vipingamizi.” Kimya.
“Au hutaki kuja kuona mjukuu?” Baba
yake akacheka. “Wewe ndiye mtoto wa pekee niliyenaye kwa sasa. Ukinihitaji
nitakuja. Kwanza ni Canada, halafu napanda ndege!” Wakaanza kucheka. “Uzazi
mzuri.” Tunda alizidi kucheka.
“Nani alijua mtoto wa ujanani angenifaa
hivi!” Tunda alimwangalia nakuzidi kucheka. “Baba!” “Kweli mama. Unanipa
tumaini, ni vile hujui tu. Huko nimewaaga kwa kishindo kweli! Maana wananiona
mchovu mchovu. Kama nisiye na maana. Sasa nikawaambia mwanangu Tunda ananiita
Dar, tena nakwenda kwa ndege.” Tunda alizidi kucheka.
“Sasa subiri
safari ya Canada.” “Baba jamani!” Wakazidi kucheka. “Tena binti yangu kaolewa
na mzungu! Ni hivyo sina picha.” “Hii simu nakuachia baba yangu. Net anasema
huko hizi simu huwa hazifanyi kazi sijui, au sitahitaji. Kwa hiyo hii moja mpya
nakuachia wewe.”
“Niliinunua siku
chache kabla sijakamatwa, na hii ya zamani namwachia mama Penny. Sijui
atafanyaje nayo mwenyewe. Ila namwachia.” “Si unaona mambo hayo! Sasa uniachie
na picha humo humo ndani.” Tunda alizidi kucheka.
“Uzazi
mzuri!” “Hongera baba yangu.” “Na unipe hongera kweli! Maana ni wewe tu ndio
tumefanana. Wale wengine wamechukua kwa mama yao. Kwa hiyo nimeponea kwa mtoto
wa ujanani.” Tunda alikuwa akimwangalia baba yake huku akicheka.
“Ila
ujitahidi Tunda. Mwili umeisha huo. Kazana kula na kupumzika.” “Nitafanya
hivyo. Nitakuwa sawa baba, usiwe na wasiwasi.” “Wenyeji wako wanajua kama
unakwenda?” “Wanafuraha hao! Mpaka wananishangaza. Wanamsubiria mtoto kwa hamu!
Yule bibi kabla ya kulala, anapiga simu, anauliza habari za mtoto. Kama
amecheza, kama baba yake amezungumza naye. Haya mara aombe Net aweke simu
tumboni amsalimie. Yaani ni fujo ambazo mimi sijawahi ona.” Hapo baba yake
akapata faraja.
“Mdogo wake
Net, anaitwa Maya, ndio anasema ameshaanza kununua nguo. Naye kutwa ananipigia
kutaka kujua ninaendeleaje. Hivi tulikuwa tumepanga na Net twende tukamalizie
fungate ndio twende Canada, lakini bibi yake ameomba twende kwanza tukaangaliwe
afya. Mimi na mtoto. Daktari akiona nipo sawa, ndio twende kokote ninakotaka.”
Baba yake akacheka kwa furaha, akaonekana ameridhika.
“Utamuaga
mama yako?” “Hapana. Nimeamua kumuacha kabisa. Hajawahi kunipenda na wala
sidhani kama anampango wakuja kunipenda. Sijamtafuta tena.” Tunda akafikiria
kidogo.
“Unajua hata
hivyo ni mimi ndiye nilimtafuta kumuomba msamaha, ndipo nikamkuta kwenye
matatizo. Wala hakuniomba msaada, mimi mwenyewe ndiye niliyemtoa pale yeye na
watoto. Nilimkuta kwenye hali mbaya sana. Mtoto wake mdogo wa kike alikuwa
akibakwa na baba yake, akawa amemuambukiza gonorea. Alikuwa akiumwa, mama yake
hana pesa, wanafungiwa tu, wakati mama anaenda kukopa pesa mtaani.”
“Ndio
nikawahamishia hotelini kwa muda mpaka walipopata sehemu yakuishi huko
Kurasini. Nilichofanya nikumlipia kodi, na kumpa vitu vyangu vya ndani ili
aanze maisha, nakumtafutia mwanasheria.”
“Sikumbuki hata kukaa chini na
mimi kuzungumza. Ila alichoniambia au kuniuliza mara ya kwanza kuniona ni
kutaka kujua kama mumewe alikuwa akinibaka kama mwanae yule mdogo. Sikutaka
kumjibu kwa haraka kwa kuwa niliona ni kama anayo majibu mbele yake.” “Ungemjibu
tu ili ajue.” Tunda akavuta pumzi kwa nguvu.
“Alishambaka
msichana wa kazi karibu kumuua, baba. Mtoto wake ndio aliambukizwa mpaka gonjwa
la zinaa! Na Tom ananiambia pia alikuwa na mahusiano na msichana mwingine wa
kazi ambaye mama yake alimfukuza. Sasa kwangu alitegemea ilikuaje?”
“Kama
angetaka kuniamini, ataniamini tu, kama ni mtu ambaye hana imani na mimi, hata
ningemwambia nini, asingeniamini. Hata hivyo nilimkuta yupo kama
amechanganyikiwa. Alikuwa kama mwehu kwa matatizo.”
“Nisikilize
Tunda. Huwezi kuanza jambo ukaishia katikati. Kabla yakuondoka, lazima
uhakikishe unakaa naye chini, unamueleza upande wako wa stori.” “Baba!” Tunda
akashangaa kwa kusikitika sana. Hakutaka kumtafuta tena mama yake. “Kabisa. Na
mimi nitakupeleka. Aamini, asiamini, hiyo iwe juu yake mwenyewe. Lakini lazima
kuhakikisha anasikia kutoka kwako.”
“Upande wa
ndugu zake wote wanajua wewe ndio ulikuwa mbaya, wakati wao wawili au tuseme
sisi ndio tuliyaharibu maisha yako. Mpigie simu usiku huu huu, mwambie kesho
asubuhi unahitaji kwenda kuzungumza naye.” Tunda aliumia sana. Hakutaka kuonana
na mama yake tena.
“Atazidi
kuniumiza tu baba. Mama amehakikisha kwa maneno na vitendo, naelewa kuwa
hanipendi na wala hanitaki kwenye maisha yake. Sikutaka kuonana naye tena au
hata kuzungumza naye akazidi kuniumiza.”
“Unafikiri
mimi simfahamu Mandi? Namjua vizuri kuliko unavyomfahamu wewe. Hukuchagua
uzaliwe na sisi. Imetokea. Mandi ni mama yako hata ufanye nini. Lazima umalize
ulichoanza, ndipo utakuwa na amani. Huna haja yakumwambia utakapokuwepo au
utakapokuwa ukiishi.” “Kwanza hata sijui kama
anashida yakutaka kujua.” Tunda aliongea kwa hasira.
“Basi
mpigie. Mwambie kesho asubuhi unataka kuzungumza naye. Utamfuata popote alipo.”
Tunda akajifuta machozi huku akijifikiria jinsi hata yakuzungumza na mama yake.
Tunda na Mama yake!
Tunda
akachukua moja ya simu yake, akampigia mama yake. Ikaita mara kadhaa, ikakatwa.
Walifanya hivyo mara tatu. “Hapokei!” “Anayo namba yako?” “Hii hapa anayo. Ndio
nilikuwa nikiitumia sana zamani.” “Basi anakuonea haya kwa aliyokufanyia, na
hataki kukupa vitu vyako. Kamwite Net.” Tunda akasimama, nakutoka.
Baada ya
muda akarudi na Net. “Nataka kabla hamjaondoka, Tunda aachane na mama yake kwa
amani. Aliniambia alikwenda kumuomba msamaha, lakini hamkukuta mazingira
mazuri.” “Lakini ni kama ameshajua ukweli wote. Mtoto wake mdogo amepitishwa
alikopita Tunda.” Net akajibu.
“Hivyo
ndivyo unavyofikiria wewe, ukidhani na yeye angetakiwa kujua hivyo, lakini
hatujui kwenye moyo wake. Mama yake hajasikia ukweli kutoka kwa Tunda mwenyewe.
Unajuaje labda anadhani kuwa Tunda ndiye aliyemwanzishia hiyo tabia. Akapenda
mahusiano na watoto wadogo?” Hapo wote wakanyamaza.
“Kila mtu
anaufahamu wake. Na inategemea ni vipi mtu anamwamini mtu mwingine. Unayempenda
ndiye utamwazia vizuri. Sasa ninachoomba ni umpigie simu mama yake, umwamb...”
“Sasa asipopokea kama alivyofanya kwangu?” Tunda akamkatisha baba yake. “Amtumie
ujumbe, mwambie mnaondoka hapa nchini, mnataka kwenda kumuaga kesho asubuhi.
Namjua Mandi. Atawapigia yeye mwenyewe. Tena sasa hivi.” Hapo wakakubaliana.
Net
akampigia mara ya kwanza na ya pili. Simu zake yeye hazikukatwa, ila ziliita tu
mpaka mwisho. Ndipo Tunda akatuma ujumbe kama alivyoambiwa na baba yake. ‘Shikamoo mama. Mimi ni Tunda. Nilitaka
kuja kukuaga wewe na kina Tom. Nilitoka gerezani, tunahamia kuishi Canada kwa
kina Net.’ Tunda akamuonyesha baba yake ule
ujumbe, baba yake akaridhia, ndipo akautuma.
Mama Tom Amtapikia
vilivyo Tunda.
Wakabaki
wakisubiria. Wote kimya wakimwangalia baba yake Tunda aliyesema atapiga.
Zilipita dakika 6 tu, mama yake akapiga kwenye simu ya Tunda mwenyewe wala sio
Net. “Tom alikuwa akichezea simu yangu. Yeye
ndio alikuwa anakata hizo simu zenu. Hujambo?” Tunda akamtizama baba yake, akamuona anacheka huku akitingisha kichwa.
“Sijambo.
Naweza kuja kukuaga kesho?” “Nitafurahi sana. Tena Tom anashida na simu. Ndio
vizuri ukija umuachie hiyo simu yako. Kama ukumbusho. Si unakumbuka alivyokuwa
anaipenda?” Tunda aliumia sana.
“Nimeshampa
baba.” “Si baba yako umpe ile nyingine? Yeye mtu mzima bwana, anaweza
kujitafutia simu yake mwenyewe.” “lle nyingine yenye namba ya Tigo, ilipotea,
najua ile nyingine Tom hataipenda, nitaiacha kwa mama Penny.” Tunda akajaribu kujieleza taratibu.
“Sasa
kwa nini hiyo usimpe baba yako halafu hii ndio umpe Tom? Vijana ndio wana mambo
mengi au matumizi mengi na simu kuliko wazee. Mbali na kupiga na kupokea, hamna
matumizi mengine.” Net na baba
yake pia walikuwa wakisikiliza. “Unafikiri
kesho muda gani mzuri tunaweza kuja kukuona?” Tunda akaona arudi kwenye
alilompigia simu.
“Ningekuwa na gari,
ningesema tuje kukuaga. Lakini hatuna gari. Si unakumbuka gari yangu walichukua
ndugu wa baba Tom?” “Nakumbuka. Pole.” “Ndio hivyo. Lakini naona tupo vizuri
kwenye kesi yangu. Nitashinda tu.” Tunda
akabaki kimya.
“Au utuachie gari yako tutumie kwa muda mpaka nitakaporudishiwa gari
yangu.”
Tunda akachoka kabisa. “Namwachia baba. Atatusindikiza uwanja wa ndege,
kisha atabaki nayo.” Hapo Tunda akawa ameamsha kilichopo
ndani ya mama yake.
“Kwa hiyo kila kitu unamwachia
baba yako, aliyeshindwa kukulea!?” Akaanza Manda. “Alikuacha ukipigwa na mkewe kama mbwa, mimi nikakuchukua nikakuleta
nyumbani kwangu. Leo unashindwa kunipa chochote, unamwachia mpuuzi huyo gari,
simu na kila kitu chako!?” Tunda alishindwa hata kujibu, alibaki
akitokwa na machozi.
“Sasa hiyo kesho ulitaka kuniona
ili iweje?” “Kukuaga na kupata muda wakukupa upande wangu wa
stori juu ya baba Tom.” Tunda aliongea kwa shida. Hasira
zilishampanda. Alibaki akitetemeka midomo. “Ulitaka kusema nini ambacho ni
chatofauti? Sasa hivi amefungwa, na wala hatakaa akatoka jela kukanusha utakachokisema.” “Ungenisikiliza kwanza mama!” Tunda akazidi kuumia.
“Kuwa na wewe alikuwa
akikubaka!? Na kwamba hata ile safari uliyokuwa umetoka kwa bibi yako ukasema
unaenda kwa rafiki yako kumbe umejifungia hotelini na mume wangu, ukarudi
nyumbani nikakutoa mimba, nayo alikubaka kule Arusha ulikokuwa umemfuata?”
Tunda kimya.
“Wewe ndiye uliyemzoesha michezo
ya watoto. Ukamlemaza mume wangu, akaishia kutaka watoto tu. Umesababisha
mateso kwa familia yangu. Umesababisha ulemavu kwa yule binti aliyekuwa msichana
wangu wa kazi. Ukampa tatizo lakudumu mwanangu mdogo. Ukamuacha yeye
akimtumikia baba yake, wakati wewe unaendelea na kina baba wengine.”
“Leo nakuomba msaada, mshenzi
wewe, unaniambia unamwachia baba yako, mpuuzi huyo ambaye hakuna mwanadamu
anaweza kuishi naye!” Manda alicharuka haswa, akapata jukwaa.
“Na Mungu ameshaanza kukulipa
kwa ubaya uliotendea familia yangu. Hatakuacha Tunda. Na wewe atakutafutia
msaidizi kwenye ndoa yako.” Simu ikakatwa.
~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~~
Wanasema, ‘dua la kuku, halimpati
mwewe’. Manda si mwewe kwa Tunda. Mama
mzazi!
❖ Akiwa bado na hofu ya kuhamia
nchini Canada, mama yake anaongeza jambo jingine. Shutuma nzito, zinazoendana
na Ukweli. Na Laana juu! Tunda anaondokaje? Kweli
ameanza kulipwa?
❖ Ritha amekimbia nchi. Hakuna ajuaye alipo. Vita yake imeisha? Tena Tunda akionekana kama bado amemshinda. Amemfukuzisha nchi, amechukua familia yake. Net na Maya wapo upande wa Tunda. Na sasa yupo huru. Mipango yakumfuata alipo kimbilia ndio imepamba moto. Viza ya kwenda nchini Canada, Tunda ameipata kiurahisiii! Nini hatima ya safari yake?
❖
Yepi mengine yanamkabili Tunda?
❖
Kama litatokea jambo
jingine, je, safari hii Net ataweza kumlinda?
❖
Ipi hatima ya Tunda na mama
yake?
❖Nani aliyekuwa akivujisha
picha, siri na mambo yaliyokuwa yakiendelea Tanzania upande wa familia hiyo ya
Cote, Tunda & familia ya Gabriel, kwenye mitandao ya nchini Canada? Mwisho
wake nini? Anamkomoa nani?
Usikose Muendelezo...
0 comments: